Hajenda period 2 month

[h=3]NINI KISABABISHACHO MWANAMKE KUKOSA HEDHI (AMENORRHEA)[/h]Amenorrhea husababishwa na nini?
Visababishi vya amenorrhea vyaweza kugawanywa katika makundi makuu matatu, vile vinavyohusisha matatizo katika mfumo wa homoni, vile vinavyohusisha matatizo ya kimaumbile katika njia ya uzazi ya mwanamke na vile vinavyohusisha mabadiliko katika mwili wa mwanamke.

1. Matatizo katika mfumo wa homoni: Matatizo katika mfumo wa homoni yanaweza kuwa katika tezi za hypothalamus, pituitary au ovary.

1. Matatizo katika Hypothalamus: Matatizo katika hypothalamus yanayoweza kusababisha mwanamke kukosa hedhi ni pamoja na
-Uvimbe katika ubongo karibu na tezi ya pituitary
-Ukosefu au upungufu wa homoni zinazochochea kukua na kufanya kazi kwa via vya uzazi. Ugonjwa huu hujulikana kama Kallmann syndrome
-Lishe duni na utapia mlo
-Uzito mdogo kuliko kawaida (kukonda kwa kupitiliza)

2. Matatizo katika tezi ya Pituitary: Vyanzo vinavyohusisha tezi ya pituitary ni pamoja na
- Kuwepo kwa kiwango kikubwa cha homoni ya prolactin katika damu au kwa kitaalamuProlactinemia. Prolactin ni homoni inayochochea uzalishaji wa maziwa wakati wa kunyonyesha. Hali ya kuwa na prolactin nyingi katika damu inaweza kutokea iwapo kuna uvimbe unaoitwa (prolactinoma) katika tezi ya pituitary.
-Kuwepo kwa uvimbe mwingine wowote katika tezi ya pituitary.
-Pituitary kushindwa kufanya kazi baada ya seli zake kufa, hususani iwapo mama alipoteza damu nyingi wakati wa kujifungua.
-Kuharibika kwa tezi ya pituitary baada ya seli zake kushambuliwa na mfumo wa kinga ya mwili.
-Kuwa na historia ya kupata tiba ya mionzi inayohusisha tezi ya pituitary.

3. Matatizo katika ovary: Vyanzo vinavyohusisha matatizo katika viwanda vya kuzalisha mayai ya kike yaani ovaries ni pamoja na
-Kutozalishwa kabisa kwa mayai (Anovulation)
-Kuwepo kwa kiwango kingi cha homoni za kiume katika damu (Hyperandrogenemia)
-Ovary kuwa na vifukovifuko (Polycystic ovarian syndrome) na kushindwa kufanya kazi zake vizuri. Haya ni matatizo ya homoni ambayo huwapata baadhi ya wanawake walio katika umri wa kuzaa
-Kufa na kushindwa kufanya kazi kwa ovary kabla ya muda wake
-Ugonjwa wa kuzaliwa unaoitwa Turner syndrome ambao humbatana na kukosekana kwa ovary au ovary kuwa changa kuliko kawaida, msichana kushindwa kuvunja ungo na msichana kuwa na kimo kifupi kuliko kawaida. Ugonjwa huu hutokana na matatizo ya kijenitikia (genetic disease)
-Ukosefu wa kimaumbile wa ovary ambao hutokea wakati wa ukuaji
-Kufa kwa ovary baada ya seli zake kushambuliwa na mfumo wa kinga ya mwili
-Historia ya kuwahi kupata tiba ya mionzi au madawa yanaathiri ovary
-Ugonjwa wa kurithi wa Galactosemia unaoambatana na kuwa na kiwango cha juu cha sukari aina ya galactose katika damu

2. Matatizo ya kimaumbile katika njia ya uzazi: Matatizo ya kimaumbile katika njia ya mfumo wa uzazi wa mwanamke yanayoweza kusababisha ukosefu wa hedhi ni pamoja na

1. Mwanamke/msichana kuzaliwa bila kuwa na uke, shingo ya uzazi au mji wa mimba (uterus)

2. Kuta za uterus zinazotazamana kujishikiza pamoja

3. Utando unaozunguka uke (hymen) kuziba kabisa na kukosekana kwa tundu la kupitishia damu ya hedhi (imperforate hymen)

4. Kuwepo kwa utando unaokatiza katika uke unaozuia damu ya hedhi kushindwa kutoka

3. Mabadiliko katika mwili wa mwanamke: Mambo yanayoweza kuathiri mwili wa mwanamke na kumfanya ashindwe kupata hedhi ni pamoja na

1. Kula kiasi kidogo sana cha chakula kuliko kawaida au kula kupita kiasi
2. Unene uliopitiliza au kupungua uzito/kukonda isivyo kawaida
3. Uwepo wa magonjwa sugu kama kifua kikuu
4. Utapiamlo
5. Msongo wa mawazo
6. Matumizi ya madawa ya kulevya
7. Matumizi ya baadhi ya madawa hususani baadhi ya dawa za kutibu magonjwa ya akili
8. Kuwa na hofu iliyopitiliza
9. Kufanya mazoezi ya mwili kupita kiasi

Dalili za Amenorrhea ni zipi?
Kukosa hedhi siyo ugonjwa bali ni dalili ya kuwepo kwa tatizo au ugonjwa fulani katika mwili. Kulingana na ugonjwa unaosababisha tatizo hili, kukosa hedhi kunaweza kuambatana pia na
• Matiti kutoa maziwa wakati mwanamke si mjamzito na wala hanyonyeshi, maumivu ya kichwa na matatizo katika kuona vitu ambavyo kwa pamoja vinaweza kuashiria uwepo wa uvimbe katika ubongo
• Mwanamke kuwa na nywele na vinyweleo vingi mwilini na kuota ndevu kama mwanaume hali inayoashiria kuwepo kwa wingi kwa homoni za kiume za androgen
• Ukavu katika uke, kutoka jasho sana wakati wa usiku, au mabadiliko katika kupata usingizi vinaweza kuashiria matatizo katika ovary
• Kuongezeka uzito kupita kiasi au kupungua kwa uzito isivyo kawaida
• Mwanamke kuwa na mhemko kuliko kawaida yaweza kuashiria kuwepo kwa matatizo ya kiakili na kisaikolojia

Je kukosa hedhi kunaweza kusababisha nisipate mtoto?
Ikumbukwe kuwa, kukosa hedhi si ugonjwa bali ni dalili ya kuwepo tatizo hivyo basi iwapo tatizo hilo lina uhusiano na kutunga mimba na kupata mtoto, uwezekano wa kupata mtoto utakuwa mdogo ikiwa tatizo hilo halitashughulikiwa.
 
Andaa nepi tu mkuu na vipampas vya kuanzia kama vya elfu hamsini. Kitu kishanasa hicho. Pia anza kudunduliza vijisent vya clinic za hapa pale teh teh
 
Kama periods zake ziko kawaida bila kuacha kwa mwezi au hata zaidi basi jipongeze kama Baba mtarajiwa.
 
Kama periods zake ziko kawaida bila kuacha kwa mwezi au hata zaidi basi jipongeze kama Baba mtarajiwa.

Huyu atakuwa ni wale ambao @lara1 anawaita free pumbu, sasa ili kumtoa pesa inabidi binti amdanganye kwamba ameanza kupata kichefu chefu na kutoona siku zake!
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom