Hajazaliwa,Hajakulia,Hajasoma na Hajaishi Arumeru

Zamani issue hizi hazikuwa na uzito sana. Siku hizi kumbe tunagombea tulipozaliwa? Lazima niende ocean road kugombea Ubunge hata kama wapambe wa magogoni watanisogelea. Wengi ni wakuja!

No, Siyo hivyo brather Ndahani, siyo unagombea ulipo zaliwa, ila hua mtu anagombea alipojiandikisha, logic ni kwamba hata wakichakachua kura lazima na wewe upate kura moja ya kwako ukipata ziro uweze kusema ya kwangu iko wapi?Sasa ina maana Sioi akopata sifuri hawezi kabisa kujitetea.

 
Mh. Asumpta Mshama mbunge wa Nkenge alizaliwa BK akaolewa Dom lkn amerudi kugombea miaka 23 tangu ameacha kuwa mkazi wa nkenge na akamwangusha Mh.Kamala ambaye ni mzaliwa na ana mji wake jimboni nadhani kuna umuhimu wa katiba mpya kulijadili hili
 
Kuna mambo mengine tumeanza kuyafanya kama ni ya muhimu bila kujua athari zake. Hili la ukabila na la kuangalia tumezaliwa wapi na nani litatutafuna wenyewe
 
Kama ni data nyeti kweli mnazo wakuu!!!!!!!!!!

Hii inamaanisha halijui hata jimbo analogombea,kwanza aliliita mkoa,pili akaja akaliita Arumeru Magharibi na kumbe ni Mashariki.

Amezaliwa na kusoma Kenya,LLB kasoma uingereza na anaishi Mbezi,anatufaa kweli huyu? Mbaya zaidi hata jina lake halipo katika daftari la kudumu la mpiga kura,alijiandikishia Mbezi...

Ni uendawazimu kumpigia kura mtu ambaye hata yeye hata jipigia kura.
 
Back
Top Bottom