Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,810
- 15,398
Hebu tuchukulie kwamba, umeoa hivi karibuni, kama miezi sita tu iliyopita. Lakini unapokea taarifa za kuaminika kwamba, huyo mkeo ni mke wa mtu. Unaambiwa kwamba, aliolewa na kukorofishana na mumewe, lakini hawajaachana na ndoa yao ilifungwa Bomani kwa mujibu wa sheria za nchi.
Taarifa zenyewe zinaonekana ni za kuaminika kuhusu jambo hilo, ingawa hujaletewa taarifa rasmi.
Hebu niambie kama ni wewe ungechukua hatua gani?
Najua The Boss atakuja na swali hapa kwamba, Je, Mume mpya alikuwa anajua kuwa mkewe aliwahi kuolewa hapo nyuma?
Jibu ni kwamba, Alimweleza mumewe mpya kuwa aliwahi kuolewa na kuachika huko nyuma, lakini hakuweka wazi kuwa kuachana huko kulikuwa kwa kufuata taratibu au la, na mume mpya hakuwa mdadisi ili kujiridhisha, alichukulia powa tu akafunga ndoa, na maisha yakaendelea.