Haja ya kuwa na Madaktari na Maprofessor katika shule za Msingi na Sekondari


Kardo Joseph

Kardo Joseph

New Member
Joined
Oct 6, 2011
Messages
4
Likes
0
Points
0
Kardo Joseph

Kardo Joseph

New Member
Joined Oct 6, 2011
4 0 0
Kadri karne zinavyozidi kusogea kumekuwa na mporomoko mkubwa sana wa elimu ya Tanzania. Kuna shule za kata nyingi ambazo zimejengwa hazina walimu wenye sifa za kutosha pia hata mazingira yake kutokuwa kichocheo cha mwanafunzi kujifunza wala mwalimu kuishi na kuifurahia kazi. Tuendako na ukizingatia twaelekea kuwa kitongoji kimoja kwa nchi za Afrika Mashariki, kuna hatari ya watanzania waliopita shule kuja kuwa vibarua kwa ndugu zetu jirani tena ndani ya nchi yetu. Kuna haja ya kuwepo kwa mkakati wa makusudi wa kuboresha wawezeshaji wetu katika shule za msingi na sekondari kwamba walimu katika shule hizo watatlakiwa kuwa madaktari hata maprofessor waliobobea katika elimu ya shule za msingi na sekondari tena wanaofahamu vizuri njia sahihi za kumfundisha na kumshirikisha mwanafunzi katika tendo la kujifunza. Kwa kufanya hivyo pengine itasaidia kuinua kiwango cha elimu kwa Tanzania na kwamba mwanafunzi achaguliwapo kwenda chuo kikuu ataonekana kweli anafaa na ameiva ambaye ataweza kujitegemea kwa asilimia kubwa na siyo kumtegemea mhadhili wake, atakuwa yupo vizuri katika lugha ya kujifunzia, ataweza kuandika 'paper', atakuwa mdadisi wa mambo, atajitegemea akiwa ndani ya taasisi na nje ya taasisi na atashindana vizuri katika soko la ajira.
 

Forum statistics

Threads 1,235,341
Members 474,524
Posts 29,219,277