Haja ya kurekebisha baadhi ya sheria ili kuongeza ufanisi wa kupambana na magonjwa ya mlipuko

Lubengera

JF-Expert Member
Jun 21, 2019
808
1,291
Kama kichwa kinavyojieleza hapo juu.

Sio lazima kusubiri wengine wafanye nasi tuige, tunaweza kujitathmini na kufanya marekebisho kwa yale yanayoonekana kuwa tatizo katika mapmabano ya magonjwa ya mlipuko.

Kwa muktadha huo, nimejitahidi kupitia baadhi ya sheria mbali mbali za JMT, nikawa interested sana na sheria ya manunuzi, ambayo kimsimngi inahusisha manunuzi ya Dawa, Vifaa tiba na mambo mengine meengi sana. Kwa kutambua kuwa Dawa na Vifaa tiba hupatikana kwa manunuzi, nikaona isiwe tabu, kwanini nisiishauri Serikali yangu Sikivu kuangalia jambo hili.

1. Kupunguza mlolongo Mrefu wa manunuzi ya Dawa na Vifaa tiba
Sheria ya manunuzi imetamka bayana kuwa Hospital, Vituo vya Afya na Zahanati za umma, zinawajibu wa kununua dawa na Vifaa tiba kutoka Bohari ya taifa ya dawa (MSD), na kama zitakosekana, MSD watawajibika kutoa Certificate of non availability within One working day Reg 140 (5)and (6) ya 2013, ambapo kanuni hiyo imetoa idhini ya kuchagua njia nyingine itakayofaa kuendelea na mchakato wa manunuzi ya dawa na vifaa tiba.

Katika kanuni hii, mapungufu ninayo yaona ni pamoja na kanuni kushindwa kutambua uharaka wa upatikanaji wa dawa hasa inapotokea zimekosekana msd. Ukiangalia kwa makini karibia njia zote za manunuzi na hasa kwa rejea ya Jedwali la Saba (Seventh schedule) ya Kanuni ya Manunuzi ya Umma utaona kuwa manunuzi yote yanayoanzia Kiasi cha Tsh,. 10,00,000.00 mchakato wa muda mfupi zaidi huchukua zaidi ya Week 4 hadi 6 mpaka kumpata muuzaji (Supplier) Hii ni kwakuwa

a. Njia ya manunuzi lazima iidhinishwe na Bodi ya zabuni ya Taasis Husika ambapo idhini inaweza kuwa kwa Circular resolution au Kikao)- Hapa huchukua siku 3 au 4 kutoa taarifa kwa wajumbe
b. Mchakato wa kuwaita wazabuni kushiriki zabuni hiyo (inategemea na aina ya njia) kwa maelezo yangu nimetumia njia ya chini kabisa ambayo muda wa kuchukua zabubi hadi kurudisha huchukua siku 4.
c.Kufanya tathmini siku 1
d. Kuwasilisha taarifa ya PMU na Timu ya tathmini katika kikao cha bodi ya Zabuni nakadiria kuwa ndani ya siku 3
e. Kusubiri muda wa matazamio (Cool off period) siku 7, huu ni muda kwa ajili ya suppliers ambao hawakuridhika na mchakato wa manunuzi kukata rufaa ya mchakato ulivyoenda kama hawakuridhika
f. Kuandaa barua za award na kuwapatia supplier siku 3
g. Delivery withini siku 14

Kwahiyo kwa mlolongo huo, hakuna Acconting officer anaweza kukubali kuchukua muda mrefu, hivyo mara nyingi huishia kuvunja sheria na kanuni zake na hatma yake ni kukutana na hoja za Ukaguzi, kuzingishiwa kuiba, kutishiwa na kunyanyaswa hata kama alikuwa na nia njema ya kuokoa uhai wa watu na hasa kipindi kama hichi cha mlipuko wa COVID19​

Nini kifanyike
Serikali kupitia Bunge tukufu ipitie tena sheria hizi na hasa kwa manunuzi ya dawa na vifaa tiba, ili kupunguza muda unaotumika kununua dawa. Binafsi naona hakuna haja ya baada kukosa MSD kurudi kupata kibali cha Bodi ya Zabuni, lakini pia kusiwe na muda wa matazamio wa siku 7.​

Kwa leo nimeona tujadili hichi kipengele kimoja cha mlolongo mrefu wa manunuzi kwa dawa na vifaa tiba. Ambapo kunahaja ya kurekebisha na kuweka muda mfupi sana kadri itakavyowezekana.

Nitaendelea kusoma na kujifunza sheria hii kadri nitakapopata muda, na sitochoka kutoa ushauri hata kama kunaambao wataubeza.

Naandika haya kwa uchungu, kwakuwa sheria hii inasababisha ukosefu wa dawa,Oxygen na vifaa tiba huko mahospitalin kwa wakati

Nawasilisha.
 
Zipo sera ,sheria na kanuni zinazohitaji kupitiwa na Wizara ya afya na sheria ndogo za Halmashauri mbalimbali na NEMC ili ziendane na mazingira ya sasa ya ugonjwa huu unaoelekea kuwa endelevu.
 
Back
Top Bottom