Haja kubwa iinatoka kama ya mbuzi

Kichwa Ngumu

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
1,726
312
Kwa muda mrefu sasa nimekuwa sijisikii hamu ya kula na hata nikila nakula kiasi kidogo sana na mara nyingi nikienda kupata haja kubwa mavi yanakuwa kama ya mbuzi.
Naomba ushauri
 
Kwa muda mrefu sasa nimekuwa sijisikii hamu ya kula na hata nikila nakula kiasi kidogo sana na mara nyingi nikienda kupata haja kubwa mavi yanakuwa kama ya mbuzi.
Naomba ushauri

Mkuu,

Usipate tabu sana ni dalili kuwa wewe unageuka mbuzi! Usijali,wala usiogope!

Hapo sehemu uliyopo kama unaweza kupata papai na ndizi mbivu(kama si mgonjwa wa kisukari) basi tumia vitu hivyo kabla ya kula chakula chengine chochote unapoamka. Lakini kwanza anza na maji moto, kunywa vikombe viwili vya maji moto, yasikuunguze lakini. baada ya dakika 10 kula ndizi mbivu moja,ile iliyovurugika kidogo sio ile ngumu, na papai. Papai bivu, kama utapata avocado (parachichi) ongezea, halafu nenda jogging kidogo kama 30mins utoke jasho, kama utakwenda mbali ukumbuke kuchukua mfuko wa plastiki akiba!

Natumai tatizo lako litatatuka,mkuu! Anza kesho.
 
Pole mkuu kwa tatizo.

Green tea ni nzuri pia. Pata pia mboga mboga za majani.
 
Nadhani ukila kidogo huwezi kupata haja kubwa (input = output) ila kula matunda yanasaidia constipation lakini in your case ni kwamba huna hamu ya kula jaribu appetisers
 
Kwa muda mrefu sasa nimekuwa sijisikii hamu ya kula na hata nikila nakula kiasi kidogo sana na mara nyingi nikienda kupata haja kubwa mavi yanakuwa kama ya mbuzi.
Naomba ushauri

Mkuu,

Kurudisha hamu ya kula.

Kama huna vidonda vya tumboni, basi pendelea kunywa mchanganyiko wa ndimu na limao, kamua mwenyewe, kama unapenda utamu ongeza sukari kidogo. pendelea kunywa at least mara tatu kwa siku hadi pale utakapoona hamu ya kula imerudi. Jikisie mwenyewe, sijui kama wewe ni motto(mtoto) au mtu mzima, ila ndimu moja na nusu limao kila unapotumia sio mbaya, usizimue mchanganyiko kwa maji mengi. Iwe (ndimu moja) na (nusu limao) kama utachanganya na maji isizidi nusu kikombe.

Acha coke, fanta, tumia maji moto,uvuguvugu kama maji ya kunywa.
 
Kwa muda mrefu sasa nimekuwa sijisikii hamu ya kula na hata nikila nakula kiasi kidogo sana na mara nyingi nikienda kupata haja kubwa mavi yanakuwa kama ya mbuzi.
Naomba ushauri

kunywa maji ya kutosha, isipungue lita mbili kwa siku...epuka vyakula vikavu kama vile mkate, muhogo wa kuchoma au vya aina hiyo...asilimia 60% ya chakula chako unachokula kila siku kiwe ni matunda na vegie ( majani ya salata na matango). inawezekana una maradhi yanayoitwa "irritable bowel disorder" au "irritable colon" .kwa kiswahili sijui yanaitwa vipi... kupoa kwake ni kufata taratibu nzuri za kula ...dawa za hospital zitakupa nafuu ya muda tu.
 
Kwa kukusaidia kwa haraka kunywa aloe vera ya forever living glass tatu kwa mara moja anagaloa kwa siku tatu kila asubuhi kabla ya kula kitu chochote.Matunda na mboga mboga iwe sehemu kubwa ya mlo wako kila siku.
 
Mkuu,

Usipate tabu sana ni dalili kuwa wewe unageuka mbuzi! Usijali,wala usiogope!

Hapo sehemu uliyopo kama unaweza kupata papai na ndizi mbivu(kama si mgonjwa wa kisukari) basi tumia vitu hivyo kabla ya kula chakula chengine chochote unapoamka. Lakini kwanza anza na maji moto, kunywa vikombe viwili vya maji moto, yasikuunguze lakini. baada ya dakika 10 kula ndizi mbivu moja,ile iliyovurugika kidogo sio ile ngumu, na papai. Papai bivu, kama utapata avocado (parachichi) ongezea, halafu nenda jogging kidogo kama 30mins utoke jasho, kama utakwenda mbali ukumbuke kuchukua mfuko wa plastiki akiba!

Natumai tatizo lako litatatuka,mkuu! Anza kesho.
kwa siku ngapi?
 
Mkuu, ukiacha natural remedies ambazo zimeelezwa hapo juu kama kula papai and the like pia unaweza tumia mafuta ya nyonyo (Castor oil). Onyo ukitumia mafuta ya nyonyo hakikisha upo karibu na private house, otherwise unaweza kuwa kama umekunywa dengerua, mambo yote yatatoka bila break.
Kwa ushauri wa daktari kama hauna matatizo mengine ya tumbo for once to clean up intestine unaweza tumia vidonge vinavyoitwa dulcolax, hivi ni zaidi ya mafuta ya nyonyo. Baada ya hapo uendelee matunda kwa sana. Kama ikizidi ninakushauri kufanya barium meal test ili kujiridhisha kuwa hauna ulcers ambazo sometimes husababisha complecations katika digestion.
 
kwa siku ngapi?

Mkuu,

Kwa kawaida ikizidi siku tatu bila kupata mabadiliko yoyote basi waganga hushauri ubadilishe dawa. Ushauri niliokupa mimi ,kama utaufata kama nilivyokueleza basi within 2hrs tumbo lako litaanza kupata mawasiliano.

Na baada ya siku tatu tatizo liwe limeondoka, sasa basi kama utaona kuna mafanikio basi uendeleze tu kwani hayo matunda si makemikali ya viwandani,ni virutubisha mwili. Ukiona baada ya siku saba ni usumbufu, basi unaweza kuacha ila ujuwe kuwa uwezekano wa kurudia kiwanda cha "mbuzi" utakuwepo.

Angalizo, nimeona umepata ushauri kutoka kwa watu tofauti, ni vyema kujaribu moja moja, usichanganye yote kwa wakati mmoja, hasa ushauri wa aloe vera, (shubiri) na castor oil, Itakuwa story ya bata anapojisaidia.

Kama utatumia njia hii mkuu urudi hapa baada ya siku tatu ili utoe mlisho nyuma (feedback).
 
Ebwana heeee poleeee sana.

kaka ni kwamba wewe una vidonda vya tumbo halafu unakula vitu vikavu ndo maana kaka unatoa karanga za mbuzi.

unatakiwa usinywe vinywaji vyenye gas, vyakula vikavu na pia unywe maji mengi vyakula vya fibres na vyepesi kama mtori.

Pia zingatia muda wa kula kula kidogo kidogo mara kwa mara unaposikia njaa.....

na kwa mbia hivyo kwasababu nina mfano hai........

pooooooooooooooooooleeeeeeeeeeeeee sana
 
Asante
Ebwana heeee poleeee sana.

kaka ni kwamba wewe una vidonda vya tumbo halafu unakula vitu vikavu ndo maana kaka unatoa karanga za mbuzi.

unatakiwa usinywe vinywaji vyenye gas, vyakula vikavu na pia unywe maji mengi vyakula vya fibres na vyepesi kama mtori.

Pia zingatia muda wa kula kula kidogo kidogo mara kwa mara unaposikia njaa.....

na kwa mbia hivyo kwasababu nina mfano hai........

pooooooooooooooooooleeeeeeeeeeeeee sana
 
Kwa muda mrefu sasa nimekuwa sijisikii hamu ya kula na hata nikila nakula kiasi kidogo sana na mara nyingi nikienda kupata haja kubwa mavi yanakuwa kama ya mbuzi.
Naomba ushauri

Nenda kwenye maabara iliyo karibu na wewe ukapime choo au mkojo! Pengine kuna tatizo la germs au parasite fulani fulani na siyo lishe tu! Pole sana, humu kuna watu wengine ni wanasheria, wanasiasa, wachumi, mashushushu, wanaIT, wanadini, waganga wa jadi, mafisadi, vibaraka nk. Watakuchanganya tu!
 
Pamoja na ushauri tabibu uliopata hapo juu. Naongezea yafuatayo: Kwanza ijue fomula ya kunywa maji ni hii 0.04 x body weight= litres to be taken in 24 hours daily. Kama wewe una uzito wa kilo 90. Kiasi cha lita za maji kitakuwa 0.04x90= 3.6 lts. Pili kuondoa tatizo la constipation na kuhuisha cells za mwili wako ili kujenga kinga ya mwili ili kuepukana na magonjwa yote yasiyokuwa ya kimelea ni pamoja na kutumia maji yaliyohuishwa kupitia kifaa maalumu kilichotengenezwa kisayansi kiitwacho BIODISC. maji yaliyopitishiwa kwenye biodisc huhuisha maumbo ya maji (molecules) na kufanya ziwe thabiti kuwa hexagonal. ukitaka maelezo zaidi basi niambie tuwasiliane.
 
Tumia Juice ya ukwaju glass moja kila siku
Bila kuchanganya sukari ila unaweza weka
Asali kidogo.Pia zingantia ulaji wa chakula bora na
Maji kunjwa kwa wingi .ikikusaidia nijulishe
Tafadhali
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom