Haiwezekani Serikali nzima iwe inakusanya mapato; tutajenga taifa la watu maskini na fukara!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,806
141,710
Kimsingi kazi ya kukusanya na kusimamia mapato ya Serikali ni ya Wizara ya fedha na taasisi zake.

Lakini kwa sasa kila waziri amejigeuza kuwa mtoza ushuru au mkusanya tozo na kuacha majukumu yao muhimu ya kusimamia ustawi wa jamii katika sekta zao.

Jana nimemsikia Waziri wa Mawasiliano na Tehama Dkt. Ndugulile akisema halizishwi na mchango wa Tehama kwenye pato la taifa.

Kwamba mchango wa Tehama ni 0.5% tu wakati taasisi nyingi yakiwemo mabenki yanatumia mfumo huo na kwa hiyo unaweza kuchangia hadi 10% ya pato la taifa.

Tusisahau kuwa kodi na tozo zote anayekuja kulipa ni mtumiaji wa mwisho ambaye ni mwananchi wa kawaida.

Tusipokuwa makini tutamkumbuka ni yeye na kaulimbiu yake.

Maendeleo hayana vyama!
 
102011131.jpg
 
Umaskini unaupata wapi sasa. So mliambiwa muandamane kutetea maslahi yenu ya kuibiwa kura. Lissu alisisitiza sana kwamba haki haiji tu bali inapiganiwa mkaona maisha yenu ni Bora zaidi kuliko kupigania haki. Sasa unalalama Nini na Nani akusaidie zaidi ya wewe mwenyewe kujipigania.

Uganda wametuzidi angalia Bobi Wine watu walivyotayari kufa ili kupigania haki. Ila Tanzania mnakimbilia kwenye key board tu huku mmejificha. Acheni niendelee kunyanyaswa hamjawa tayari kupigania haki zenu
 
Kwani toka tumepata Uhuru, Kuna chama chochote kilishawahi kutawala na kukusanya ushuru?

Kiki za wapinzani hazipo tena,tutegemee Bungeni vioja vingi vitatokea.

Ndiyo maana mnawalazimisha Covid 19 waingie Bungeni kwa nguvu, ili muwe mnawaangushia jumba bovu ili Bungeni kuwe na kiki.
 
Hata mmoja haujaisha. Tufunge mikanda kama Ile ya wakati WA Vita vya Idd Amin Dada. Ilikuwa miezi 18.
 
Umaskini unaupata wapi sasa. So mliambiwa muandamane kutetea maslahi yenu ya kuibiwa kura. Lisu alisisitiza Sana kwamba haki haiji tu bali inapiganiwa mkaona maisha yenu ni Bora zaidi kuliko kupigania haki. Sasa unalalama Nini na Nani akusaidie zaidi ya wewe mwenyewe kujipigania.

Uganda wametuzidi angalia bobi wine watu walivyotayari kufa ili kupigania haki. Ila Tanzania mnakimbilia kwenye key board tu huku mmejificha. Acheni niendelee kunyanyaswa hamjawa tayari kupigania haki zenu
Huyo Tundu Lissu aliandamana?

Maalimu Seif aliandamana Zanzibar!
 
Kimsingi kazi ya kukusanya na kusimamia mapato ya serikali ni ya Wizara ya fedha na taasisi zake.

Lakini kwa sasa kila waziri amejigeuza kuwa mtoza ushuru au mkusanya tozo na kuacha majukumu yao muhimu ya kusimamia ustawi wa jamii katika sekta zao.

Jana nimemsikia Waziri wa Mawasiliano na Tehama Dr Ndugulile akisema halizishwi na mchango wa Tehama kwenye pato la taifa.

Kwamba mchango wa Tehama ni 0.5% tu wakati taasisi nyingi yakiwemo mabenki yanatumia mfumo huo na kwahiyo unaweza kuchangia hadi 10% ya pato la taifa.

Tusisahau kuwa kodi na tozo zote anayekuja kulipa ni mtumiaji wa mwisho ambaye ni mwananchi wa kawaida.

Tusipokuwa makini tutamkumbuka ni yeye na kaulimbiu yake.

Maendeleo hayana vyama!
Kwani Mara hii umeshamsahau niyeye? Endelea kumkumbuka hamna shida.
 
Wale wanakusaidieni hawana njaa kama unavyolialia wewe. Hata asipoandamana lakini ameplay apart kukuonesha kwamba haki zako zinadhulumiwa kwa hiyo ni kazi yako kutafuta haki. Yeye hana shida Sana Kama ulizonazo wewe. Achana na mawazo mgando
Tundu Lisu alijificha ubalozi wa Ujermani tofauti na yule mpambanaji wa ukweli wa Afrika mashariki Bob Wine!
 
Back
Top Bottom