Haiwezekani Kwa Mapolisi wenye vyeti feki kuondolewa / Kutumbuliwa: Mkuu wa Kaya

Azarel

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
28,410
39,478
Habarini Wadau,

Mkiniuliza au Mkijiuliza kuwa nimepata wapi hili, nitawajibu kuwa ni katika kikao cha Mkuu wa kaya na jeshi la polisi nchini na nina uhakika na hili.

Mkuu wa kaya baada ya kushauriana na IGP mpya wameamua kutokuwatumbua maaskari wenye vyeti feki ila sababu zao ni za muhimu kweli kweli, nazo ni hizi zifuatazo:-

1) Kuwatumbua Mapolisi wenye vyeti feki kutapunguza idadi kubwa sana ya Mapolisi hasa wale walioajiriwa zamani. Hii ni kutokana na ukweli kwamba asilimia kubwa ya mapolisi wa zamani waliingia kazini kwa kutumia vyeti vya watu wengine ambao hawakuhitaji kuwa mapolisi.

2) Kutumbua mapolisi ni kuongeza UHALIFU nchini, Imagine polisi aliyeajiriwa kwa miaka mitano mpaka kumi iliyopita au ambaye tayari ana vyeo vingi huoni kama tayari anajua siri zote za jeshi la polisi? Hii inamaana anajua jinsi gani wanavyopambana na wahalifu, utumiaji wa silaha na mambo mengine mazito.

Mkuu wa jeshi hilo amesema kuwa kupunguza hata mapolisi watano tu ni hatari kubwa.

Hivyo busara imetumika kuwa hawa jamaa WAACHWE.

Nawasilisha.
 
Ila kupunguza madaktari vifo vya wagonjwa viongezeke ni sawa? Kufukuza walimu wanafunzi wasifundishwe ni sawa?

Kama aliona hizo athari angeangalia hata hao wafanyakazi wengine aliowafukuza maana wengine walikuwa wanategemewa na familia, na kwa wanasiasa nao wana athari gani?
 
Ofcourse Hilo wenye kusoma Alama za nyakat tulishalijua,polisi na jeshini operation vyeti feki haitafika.
 
Very well said Mkuu. Wengine wameshaanza kujiua.

Ila kupunguza madaktari vifo vya wagonjwa viongezeke ni sawa? Kufukuza walimu wanafunzi wasifundishwe ni sawa?

Kama aliona hizo athari angeangalia hata hao wafanyakazi wengine aliowafukuza maana wengine walikuwa wanategemewa na familia, na kwa wanasiasa nao wana athari gani?
 
Ila kupunguza madaktari vifo vya wagonjwa viongezeke ni sawa? Kufukuza walimu wanafunzi wasifundishwe ni sawa?

Kama aliona hizo athari angeangalia hata hao wafanyakazi wengine aliowafukuza maana wengine walikuwa wanategemewa na familia, na kwa wanasiasa nao wana athari gani?
Walimu hao fake watatumia ujuzi kwenye sector binafsi polisi au mwanajeshi wataajiriwa wapi na ujuzi wake wa mizinga au sniper?
 
Daah so sad kuna tcha wangu aliyefanya niijue HESABU nae katumbuliwa ilibaki miaka 4 tu ale kiinua magoti, Alisifka kata nzima na kutufanya tutoke na misonge ya namba leo hana chake yupo kazn cnc 90's if nt 80's pa1 na vyet fek bt wamelisaidia taifa hawa jamaa.
 
Ila kupunguza madaktari vifo vya wagonjwa viongezeke ni sawa? Kufukuza walimu wanafunzi wasifundishwe ni sawa?

Kama aliona hizo athari angeangalia hata hao wafanyakazi wengine aliowafukuza maana wengine walikuwa wanategemewa na familia, na kwa wanasiasa nao wana athari gani?
Mkuu nakupenda buureee unajibu kwa fact sanaaa sanaaa sanaaaa sanaaaa
 
Polisi bila kitambulisho na amri hawana athari zozote uraiani. Kumbe ndio maana siku moja nikamsikia akisena yeye anawapenda sana polisi tena toka moyoni.

Lakini ni vema ieleweke kuwa kuna kiwango hua Mungu havumilii.

Bado namkumbuka nesi mmoja MOI aliyemhudumia ndugu yangu kwa uweledi wa hali ya juu. Na hata nilipotaka kumpa soda akasema yeye anapata furaha akiona wagonjwa wanapata huduma na wanarejea kwenye majukumu yao. Sadly, ametumbuliwa. Hii kitu imeniuma sana.
 
Back
Top Bottom