haiwezekani kupenda kuliko kitu chochote! ...mnh?

Mbu

JF-Expert Member
Jan 11, 2007
12,753
7,839
usher-confession.jpg
...pamoja na kupendana saaaaaaana na mke/mume, binafsi nadhani kuna haja ya 'kuungama' kwa mwenza wako katika hatua za awali mfano;

"mwenzangu, pamoja na kukupenda saana mpaka usiku kucha silali, pia napenda pombe!"
au...

"ewe wa rohoni mwangu, usiponiona kwako...ujue barcelona na messi wameniteka akili!"

...au nyie mnaonaje wenzangu?...nyie mna confess vipi ili kuondosha 'kutokueleweka' kwa wapenzi wenu?
 
...the boss, bora umeungama leo hahaha..
Heri yako unayetazama tu ukaacha ende zake.
I hope hata wale wapenda ngono wata confess leo..
 
Wee Mbu Umewaza nini?? Yaaaaani Umenimaliza kwa kicheko.... Khaa!
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
...ashadii we cheka tu, hayajakukumba ee?

Hujawahi ona mtu anapenda kitu mbadala mpaka anajisahau
Ana mke/mume nyumbani?...it can be anything, watu wana myuti tu kuungama...
 
...ashadii we cheka tu, hayajakukumba ee?

Hujawahi ona mtu anapenda kitu mbadala mpaka anajisahau
Ana mke/mume nyumbani?...it can be anything, watu wana myuti tu kuungama...

No... kilichonichekesha ni kua kama Mzaha vile but so True.... Call a Man at his finals (watching) hata kama upo nude haoni kitu!
 
...ashadii we cheka tu, hayajakukumba ee?

Hujawahi ona mtu anapenda kitu mbadala mpaka anajisahau
Ana mke/mume nyumbani?...it can be anything, watu wana myuti tu kuungama...

mimi nina ndugu yangu yanga ikicheza popote pale,iwe morogoro,uganda au mbeya
lazima aende....na watu wote kwenye familia tumeshazoea kama kuna mechi ya yanga
na una shida nae unamfuata uwanjani lol
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
...mmeona ee? Yaani, kuna kitu piga ua wewe hata ukiwa na mpenzi wako pahala popote na wakati wowote, ukikumbukia tu..mawazo pia yanahama..

Iwe ni pombe, kamari, udaku na umbea, mpira, segere na mdundiko..etc
 
hahaa mbu vitu vingine acha watu waendelee kuungama kimoyomoyo
...mmeona ee? Yaani, kuna kitu piga ua wewe hata ukiwa na mpenzi wako pahala popote na wakati wowote, ukikumbukia tu..mawazo pia yanahama..

Iwe ni pombe, kamari, udaku na umbea, mpira, segere na mdundiko..etc
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
kuna vitu vya ku confess na vingine ni bora uviache kama vilivyo...lol

mfano nakupenda saana,but nikiona mdada mwenye wowowo kukuzidi...naishiwa nguvu kabisaaa....i cant help it...lol

Mhhhhhhhhh? sasa hapo the boss utaua band
 
Lol, chauro..hebu bana ..toa dokezo basi as if unamuongelea wifi wa jirani yake shemeji yako kwa mume wa binamu...aka mtu wa mbaaali..
 
Mi nadhani it boils down into knowing interests za kila mtu kabla hamjafanya uamuzi wowote 'mzito' ili kujua kama utaweza kucope

Kuna vitu vingine huwezi kuanza kusema tu kuwa ntafanya kama alivosema The Boss hapo

Ila kama napenda kuangalia mpira kwa mfano, au mtu wa club, au mtu wa kuwa na marafiki wengi, movies, au kusoma etc, ni kiasi cha kuangalia with time kama inaweza kukaa navyo au la.

nimeshuhudia baadhi yetu wanaume...wengine wanakuwa watoto wa 'mama' kiasi kuwa anampigia simu mama yake mara nyingi zaidi kuliko mpenzi/mke wake...mi kwangi haijakaa njema
 
kuna vitu vya ku confess na vingine ni bora uviache kama vilivyo...lol

mfano nakupenda saana,but nikiona mdada mwenye wowowo kukuzidi...naishiwa nguvu kabisaaa....i cant help it...lol

haaaa,nakupga kisu labda ukae mbal
 
...khaaa.. ya kaizari tumuachie kaizer...
Wenzetu 'wadhungu' wana maswali yao
Ambayo sina tafsiri ya kiswahili, mfano;

-what are your hobbies and interest?
-how do you spend your spare time?

...sasa kaiza ukinambia kuna mambo tuachie mapenzi yatuongoze, huoni ndio sababu baada ya mapenzi unayasikia malalamiko ya "siku hizi umebadilika"...?

...inatokana na "kutojuana" -mapepo- mapema..
 
Nakupenda sana lakini kuna kitu siwezi kukiacha!! Mh! Hii ni ngumu kumesa babaangu unless kiwe hakina ukwazo mkuuubwa kwa mpenzio. Mfano mpira. Lakini kama unapenda akina dada/kaka poa halafu unaconfess/ungama!!
 
Similar Discussions

4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom