Haitoshi kuziadhibu klabu kwa matukio ya kuharibiwa uwanja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Haitoshi kuziadhibu klabu kwa matukio ya kuharibiwa uwanja

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Mar 19, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 19, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Juzi, Serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ilielezea kwa mara nyingine tena masikitiko yake kuhusiana na vitendo vya hujuma za makusudi dhidi ya miundombinu ya Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

  Katika taarifa hiyo, Serikali ambayo ndiyo mmiliki wa Uwanja wa Taifa, ilieleza kwamba vitendo hivyo havivumiliki na kwamba sasa, adhabu ya uharibifu wa viti itapanda kutoka ya chini ya Sh. Milioni 5 na kuwa Sh. Milioni 10.

  Aidha, ilielezwa vilevile kwamba, kamwe serikali haitakuwa tayari kuruhusu uwanja huo kuendelea kutumiwa ikiwa uharibifu wa makusudi utaendelea kufanywa na baadhi ya mashabiki wa soka waliokosa ustaarabu.

  Taarifa hiyo ya serikali ilifuatia muendelezo wa matukio ya kuharibiwa kwa miundombinu ya uwanja.
  Awali, mashabiki waliodhaniwan kuwa ni wa klabu ya Simba walifanya vurugu na kusababisha uharibifu wa viti 152

  wakati wa mechi waliyoshinda 2-1 ya kuwania Kombe la Shirikisho dhidi ya Kiyovu ya Rwanda. Simba ilitozwa faini ya Sh. Milioni 5 kufidia uharibifu huo.

  Jumamosi iliyopita, uharibifu mwingine ukafanywa na mashabiki wanaodhaniwa kuwa wa Yanga wakati wa mechi ya ligi kuu ya Bara baina yao na Azam. Yanga walipoteza mechi hiyo baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-1. Hata hivyo,

  wakati mechi hiyo ikiendelea na hata baada ya kumalizika, baadhi ya mashabiki waliokuwa hawaridhishwi na uamuzi wa refa waling’oa viti na kuvitupa huku na huko. Baada ya tathmini, ilibainika kuwa viti 119 viliathiriwa.
  Kama ilivyokuwa kwa mahasimu wao Simba, Yanga pia wametakiwa kulipa Sh. Milioni 5 ili kufidia gharama za uharibifu huo.

  Sisi hatupingi hatua zinazochukuliwa hadi sasa katika kulinda miundombinu ya uwanja huo uliojengwa kwa mabilioni ya fedha. Klabu zinapaswa kuelimisha mashabiki wao kuwa vitendo vya uharibifu havifai kwani licha ya kuzigharimu klabu zao kwa kulipishwa fidia, pia huigharimu Serikali ambayo hulazimika kutumia rasilimali zake kukaribati uwanja huo badala

  ya kujihusisha na mambo mengine muhimu kama ya kuboresha huduma za maji, afya na elimu.
  Mashabiki wa soka wanapaswa kutambua kuwa serikali haina kwingine inakopata fedha kwa ajili ya matumizi yake

  isipokuwa ni kwa wananchi wenyewe, wakiwemo mashabiki hao wa soka, kupitia kodi zinazolipwa moja kwa moja na pia zinazokatwa kupitia manunuzi ya bidhaa na huduma mbalimbali.

  Hata hivyo, sisi tunadhani kwamba kuziadhibu klabu peke yake, kama ilivyokuwa katika matukio ya vurugu za Yanga na Simba hakuwezi kusaidia sana katika kukomesha vitendo hivi.
  Bali, tunadhani kwamba hatua kali zaidi zinapaswa pia kuchukuliwa dhidi ya watu wanaojihusisha moja kwa moja na uharibifu wa viwanja vyetu.

  Tunakumbushia jambo hili kutokana na ukweli kwamba kuziadhibu klabu peke yake kunawapa unafuu wahusika kwani laana na adhabu hutua jumla kwa timu nzima. Ikumbukwe vilevile kwamba sio mashabiki wote wanaokwenda uwanjani kutazama mechi ya klabu ‘A’ ni lazima wawe wa klabu hiyo.

  Mashabiki wa timu za Azam, Yanga na Mtibwa hawazuiwi kwenda kutazama mechi za Simba. Kwa adhabu zinazotolewa sasa, inaonekana kwamba mashabiki wa aina hii wanapofanya fujo na kuharibu miundombinu, bado hupata nafasi rahisi

  ya kusalimika kwani adhabu huzikuta timu wanazokwenda kuzitazama hata kama hawazishabikii, jambo ambalo tunadhani kwamba si sahihi hata kidogo.

  Katika mazingira kama hayo, tunadhani kwamba ni vyema Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) likashirikiana na vyombo vya usalama kuwanasa wahusika na kuwachukulia hatua kali ili iwe fundisho kwa wengine wote; badala ya ilivyo sasa ambapo klabu peke yake ndizo huadhibiwa na wahalifu wakiachwa huru bila kupewa somo la kujutia madhambi yao.

  Kama jitihada za kweli zikifanyika katika kukomesha madhambi haya, ni wazi kwamba wahusika mmoja baada ya mwingine watapatikana kwani hata katika matukio yaliyopita, baadhi ya watuhumiwa walikuwa wakionekana wazi

  kupitia marejeo ya picha za video. Askari wanaokuwepo uwanjani wasijishughulishe kutazama mpira na badala yake, washirikiane na raia wema kuwanasa waharibifu ili hatimaye wachukuliwe hatua kali za kisheria.

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #2
  Mar 19, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Ni kweli kupitia camera zilizofungwa uwanjani hawa jamaa watafutwe. Picha zao ziwekwe magazetini na nje ya viwanja vya michezo. Klabu nazo ziadhibiwe kwasababu hawa jamaa wanaofanya fujo wengi wanafahamika ktk klabu husika. Na mwisho ni aibu kwa Simba na Yanga kutokua na viwanja vyao. Hizi klabu miaka ya 70 zilikua na maendeleo makubwa,sasa hivi zimebakia majina tu!
   
Loading...