jingalao
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 35,053
- 28,245
Habari za asubuhi!
Kichwa cha habari kinajieleza vyema na kinajaribu kuamsha kumbukumbu na kuondoa hofu watoto wa miaka ya 92+.
Tunawasikia ndugu zetu wa upinzani wakilalamikia kasi ya CCM kuwanyakua wapinzani na hivyo kupelekea tishio la upinzani kupotea kabisa katika siasa zetu.
Kwa maoni yangu...Upinzani huu wa kitapeli ni bora na lazima ufe katika awamu hii ya ukweli,usawa na ufuataji sheria.
Upinzani huu wa hadaa ulipewa fursa kubwa sana awamu zilizopita ingawa wakatumia fursa hizo kwa maslahi binafsi na familia zao,upinzani ukageuka chaka la wakwepa kodi,wauza ngada na kimbilio la mafisadi waliofurushwa CCM.
Ni upinzani uliogeuka na kuwa watetezi wa wezi wa rasilimali zetu...
Ni upinzani uliodumaa kiakili kiasi kwamba imani yao imebakia kulilia misaada ya ughaibuni na kuamini miongozo ya ughaibuni(yaani hauna jipya kwa hisani ya watanzania)
Kwa muktadha huu wa upinzani mbovu hatuna budi kubakia na CCM iliyo imara na yenye kutoa fursa kwa wananchi wa strata mbalimbali za kiuchumi,kimaumbile,kabila na dini...
ni bora mara elfu moja tukabaki na utawala wa Chama kimoja kilichoboreshwa na kuwa na fikra mbalimbali kuliko kuendelea kuwa na mivyama inayotumia ruzuku kuneemesha wakwe,mashemeji na nyumba ndogo zao.
Kabla ya 1992 tulikuwa na CCM na maisha yalisonga ...sio aibu wala sio hatari kubakia na CCM kwa miaka hata 1000 ijayo.
POVU RUKSA ILA HOJA HUJIBIWA KWA HOJA!
"BUYUNGU -UMOJA NI USHINDI"
"UKONGA-WEMBE NI ULE ULE"
ARUMERU-2020 TENA