Haiti: Waziri Mkuu amtimua mwendesha mashtaka kwa kumtuhumu kuhusika na mauaji ya Rais Moise

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Waziri Mkuu wa Haiti Ariel Henry amemfuta kazi mwendesha mashtaka aliyekuwa anataka kumfungulia mashtaka kama mshukiwa katika mauaji ya Rais Jovenel Moise. Hatua hiyo imeitumbukiza Haiti katika mzozo mpya wa kisiasa.

Frantz Louis Juste, mwendesha mashtaka aliyesimamia kesi iliyohusisha vifo vya zaidi ya watoto 12 walioteketea katika kituo cha watoto yatima mjini Port-au-Prince mwaka jana, sasa ndiye mwendesha mashtaka mpya katika kesi hiyo.

Wiki iliyopita, mwendesha mashtaka katika kesi hiyo Bed-Ford Claude alisema, rekodi za simu zinaonyesha kwamba mtu anayeshukiwa kuwa mpangaji mkuu wa mauaji ya Moise, aliwasiliana na Waziri Mkuu Henry usiku ambao uhalifu huo ulifanyika. Kulingana na Claude, walizungumza mara mbili kwa kipindi cha dakika saba kila mara.

Mshukiwa huyo Joseph Baido ambaye alikuwa afisa katika wizara ya sheria na ambaye Henry amekuwa akimtetea, anadaiwa kutoroka na hajulikani alipo kwa sasa.
 
Back
Top Bottom