imhotep
JF-Expert Member
- Oct 13, 2012
- 46,678
- 71,032
Soma acha kuupotosha umma.
Soma acha kuupotosha umma.
Hata Japan imepitia/hupitia majanga tele tu, tusihalalishe uzembe.Uhuru walipata 1801 mkuu matetemeko na vimbunga na ukimwi soma soma soma
kwa uongozi uliopo hawana exposure tusitegemee maendeleo yoyote zaidi ya kutawala kwa vitisho na kugandamiza demokrasiaKuna watu wanadhani kama wakiendesha utawala wa kubinya haki za raia na uonevu kwa wananchi kadri watakavyo basi maendeleo wanayofikiri wananchi wanapaswa kuwa nayo yatakuja na wananchi watafurahi.
Huko America ipo nchi inaitwa Haiti ambayo raia wake kwa zaidi ya 90% ni Waafrica wenzetu weusi. Kwa kipindi kirefu cha uhuru wake wa miaka zaidi 200 (Haiti imepata uhuru mwaka 1804, January 1) ikiwa ni nchi ya pili kuwa huru katika America baada ya USA iliyoitangulia kwa miaka 28 tu.
Pamoja na miaka mingi ya uhuru Haiti ni moja ya nchi masikini kabisa duniani. Ikiwa ndiyo kinara wa umasikini huko America. Hii yote imesababishwa na aina ya siasa ambazo wananchi wa Haiti wamejikuta wakikabilina nazo ambazo kwa kiasi kikubwa zinaendana na siasa za sasa za serikali ya Magufuli.
Haiti ni nchi yenye demokrasia ya maneno huku serikali ikiwa busy kubinya uhuru wa raia na kufanya mambo inavyopenda na siyo kadri raia wa nchi hiyo wanavyotaka. Lakini kwa sababu raia hawana cha kufanya imebidi waishi katika hali hiyo ambayo imewasababishia umasikini na unyonge kwa miaka 214.
America walipopata uhuru walichagua kuwa na siasa ya kistaarabu yenye kuheshimu haki za raia na uhuru wa kujieleza. Haiti wao ilikuwa kinyume chake na matokeo yake leo hii nchi hizi mbili za mwanzo kupata uhuru huko America moja wanaishi kama peponi (USA) na wengine wapo jehanum(Haiti)
Yanayotokea hapa nchini leo yananifanya nione kabisa nchi yetu imeamua kupita njia waliyopita/wanayopita Haiti. Kufail kwa Haiti imekuwa ni reference ya ujinga wa mtu mweusi. Kwamba hata ipite miaka mingapi hatuwezi kuendesha nchi ikaweza kuendelea.
Nawasihi viongozi wetu wabadilike na wakubali ukweli kuwa Watanzania siyo ng'ombe ambao wanaweza kuwaburuza kadri watakavyo. Waone umuhimu wa kuheshimu haki za raia na haki ya kuwa na mawazo tofauti. Mambo ya kusema mtu akiandamana ataenda msimulia baba yake au kuwa mtu akiandamana hata chumbani kwake watamkamata ni tabia za ki-Haiti na kama wataendelea hivyo basi wajue hata miaka 200 itapita na hakuna maendeleo yatakayokuwepo kama ilivyo Haiti.
Viongozi wetu waone aibu kusema uongo hadharani kama yule aliyesema wanaoandaa maandamano wanandaa risasi wajipige ili kuchafua sura ya nchi. Hata kama sisi Waafrica hususani Watanzania ni wajinga lakini tusioneshe ujinga wetu hadharani kama alivyofanya yule waziri wetu leo pale Singida. Waziri yule ni Dr. anapoamua kusema uongo hadharani kama alivyosema leo basi ajaribu hata kuufanya ili uonekane ni uongo uliotolewa na mtu mwenye PhD na siyo anaongopa kama kilaza wa darasa la nne.
Kumbe ipi mkuu Kenya raila kajiapisha bila bunduki kulia wamerudia uchaguzi hatukuona damu zikimwagwa vipi hayo yangetokea tzKenya ni mfano mbaya pia umekosa nchi ya kutufananisha nayo mkuu
Tupe wewe unaoijua.Huijui historia ya Haiti,soma vizuri ndio uilete hapa.
Mkuu tumegee unachokifahamiReal, Unafahamu historia ya Haiti mkuu, Kama unaongelea kile kisiwa cha makazi ya watumwa waliochoka basi mleta uzi nina kupinga nenda google au Wikipedia soma vizuri The Haitian development and its reform utajua kwanini Haiti ni maskini
Haiti na Tanzania ni nchi zilizoletwa kwa majaribio
Kwa nini wewe unayeijua usimrekebishe. Rubbish na weweHuijui historia ya Haiti,soma vizuri ndio uilete hapa.
Watu weusi wengine wanatoka bara lipi?"Huko America kuna nchi inaitwa Haiti ambayo asimia 90 ni WAAFRIKA wenzetu"
Sio kila mtu mweusi ni muafrica.
Anyway, naunga mkono hoja!
Kuna nchi zina majanga na bado zinapeta. Angalia majanga ya indonesiaHaiti ipo kwenye ukanda wa majanga. Kila ikijaribu kujiinua inaangushwa ama na matetemeko au vimbuka.
Kasome historia ya Singapore na nchi nyingine zote zilizo katika kile kijulikanacho kama 4 Asian Tigers ujue njia zilizopitia kutoka kuwa mataifa fukara hadi kuwa mataifa tajiri...tatizo la mwafrika sio kumpa uhuru, ni kumbadili utamaduni wake completely (Culture, attitude and mentality)
Hakuna nchi yenye utawala wa kibabe ambayo imefanikiwa kuwafanya wananchi wake kuwa na maendeleo.
Mifano mizuri linganisha Taifa la China lenye udikteta na tawala huru kama Taiwan, Hong Kong na nchi kama Singapore na Japan.
Mpaka leo nchi ya China kwa kipimo cha maendeleo ya raia, ni duni sana.