JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,308
- 5,455
Ndege ndogo imeanguka katika mtaa wenye watu wengi katika Jiji la Nchini Port-au-Prince Nchini Haiti, jana Aprili 20, 2022 na kuua watu sita akiwemo rubani wa ndege hiyo.
Ndege hiyo ilikuwa ikiruka kutoka Uwanja wa Ndege wa Port-au-Prince saa 9:44 Alasiri kuelekea katika Jiji lingine Nchini humo la Jacmel. Mamlaka za Usafiri wa Anga zimesema injini ilifeli na kusababisha ianguke saa 10:04 Jioni.
"Natoa pole kwa wafiwa na walioathiriwa kwa tukio hilo," aliandika Waziri Mkuu wa Haiti, Ariel Henry kupitia ukurasa wake wa Twitter
Meya wa Jiji ambapo ndege ilianguka, Jude Edouard Pierre amesema watu sita wamefariki, rubani akifariki wakati akiwa njiani kupelekwa hospitali.
Source: Usnews