Haitakuwa busara kuiuza au kuivunja Ikulu ya Dar es Salaam

Wakuu hali zenu,
Najua mnajua kwamba tunakaribia kuhamia dodoma. Na baadhi ya vyanzo vya habari vinasema tukihama yale majengo ya serikali magogoni na mawizara tutayauza. Hili ndilo limenifanya niandike angalau kuweka mawazo yangu sawa.

Nashauri majengo ya Ikulu yabaki na tuyafanye makumbusho ambayo vizazi vyetu vitaendelea kujifunza historia endelevu ya taifa letu. Kwanza itaingiza kipato lakini pia itatoa fursa ya kulinda mandhari na heshima ya kitaifa. Nashukuru nimewahi kuishi uingereza na ufaransa kwa muda flan. wenzetu majengo kama haya huyahifadhi na kuyapa thamani zaidi. Tuweke uhai ndani ya majengo haya kwa kuonesha matukio gani au historia gani zilifanyika kwamfano rais gani alipenda kukaa na kufanya nini wapi? mikataba kadhaa ilisainiwa wapi au tukio gani lilifanyika wapi. ni muhimu, hatuhami nchi tunabadili makazi hakuna haja ya kuuza au kuvunja maana wapo ambao mawazo yao mafupi sana.

Msiweke mkuu wa mkoa mle kwani haya majengo hadhi na gharama zake ni kubwa sana. Mkuu wa mkoa aendelee kuishi anakoishi sasa. mnaweza kuweka ikawa ni ikulu ndogo ya raisi na ikatunzwa pia sio mbaya sana. Majengo ya wizara nakadhalika yakodishwe na sio kuuza. ukiuza unapata pesa once unatumia kujenga kolomije na zinaisha. ukiwekeza kwenye mambo mengine utaendelea kupata pango na umiliki wako utaendelea. tusiwe na mawazo ya kuharibu tu. tujifunze kwa wenzetu.

Nawasilisha kwa wenye akili walione,

Nangu mandokwa
Hata mimi nakubaliana na wewe; Ikulu isiuzwe wala kuvunjwa, bali ifanywe kuwa Makubusho. Tena mimi napendekeza ingefanywa kuwa makumbusho maaulumu ya kisiasa, itakayo kuwa inahifadhi/na kuonesha harakati za kisiasa za kabla ya uhuru, kipindi cha kuelekea uhuru, na za baada ya uhuru hadi hivi leo.
 
Ghorofa litaanza kubomoka jenyewe kabla ya kuguswa(Yaani litaanza kupumua kwa hofu kupitia expansion joints)...Naomba tusiyatishe majengo jamani.
 
Wakuu hali zenu,
Najua mnajua kwamba tunakaribia kuhamia dodoma. Na baadhi ya vyanzo vya habari vinasema tukihama yale majengo ya serikali magogoni na mawizara tutayauza. Hili ndilo limenifanya niandike angalau kuweka mawazo yangu sawa.

Nashauri majengo ya Ikulu yabaki na tuyafanye makumbusho ambayo vizazi vyetu vitaendelea kujifunza historia endelevu ya taifa letu. Kwanza itaingiza kipato lakini pia itatoa fursa ya kulinda mandhari na heshima ya kitaifa. Nashukuru nimewahi kuishi uingereza na ufaransa kwa muda flan. wenzetu majengo kama haya huyahifadhi na kuyapa thamani zaidi. Tuweke uhai ndani ya majengo haya kwa kuonesha matukio gani au historia gani zilifanyika kwamfano rais gani alipenda kukaa na kufanya nini wapi? mikataba kadhaa ilisainiwa wapi au tukio gani lilifanyika wapi. ni muhimu, hatuhami nchi tunabadili makazi hakuna haja ya kuuza au kuvunja maana wapo ambao mawazo yao mafupi sana.

Msiweke mkuu wa mkoa mle kwani haya majengo hadhi na gharama zake ni kubwa sana. Mkuu wa mkoa aendelee kuishi anakoishi sasa. mnaweza kuweka ikawa ni ikulu ndogo ya raisi na ikatunzwa pia sio mbaya sana. Majengo ya wizara nakadhalika yakodishwe na sio kuuza. ukiuza unapata pesa once unatumia kujenga kolomije na zinaisha. ukiwekeza kwenye mambo mengine utaendelea kupata pango na umiliki wako utaendelea. tusiwe na mawazo ya kuharibu tu. tujifunze kwa wenzetu.

Nawasilisha kwa wenye akili walione,

Nangu mandokwa

Tatizo ni moja serekali hii haipokei ushauri popote.
 
Hhh jamaa ni raisi wa ujenzi sio wa uchumi kila siku ye habari zake ni barabara na majengo tu maswala ya uchumi kwake hayajui

Ukitaka kuamini simamisha msafara wake alafu msikilize habari zake anazoongea utamsikia anaongea kujenga na kubomoa tu hhhhh
Kweli

Ova
 
Hata mimi nakubaliana na wewe; Ikulu isiuzwe wala kuvunjwa, bali ifanywe kuwa Makubusho. Tena mimi napendekeza ingefanywa kuwa makumbusho maaulumu ya kisiasa, itakayo kuwa inahifadhi/na kuonesha harakati za kisiasa za kabla ya uhuru, kipindi cha kuelekea uhuru, na za baada ya uhuru hadi hivi leo.

Automata ,

Mkuu, wao zuri sana.
Je, hiyo akili tunayo huko!?

Twiga kwenye ndege wanapanda kana kwamba Twiga anazo akili akiona ndege anaikimbilia anadandia.
Ngedere, tumbili , nyani , vyura , vipepeo .

Tembo, tunawamaliza tena viongozi wa vyama vyetu ivi hivi mifano ni mingi hadi waliokamatwa wa kule Mbeya wa chama tawala.

Madini wadhamini wa vyama vyetu ndiyo watoroshaji kwenda nje.
Mfano, Kesi ya jamaa wa juzi mwenyewe alibeba pesa ya zaidi ya mataifa 10+ (15) na dhahabu kilo 8.

Hiyo ni mifano michache sana kuwa bado tunayo majanga sana.

There's a need to reshuffle our institutions.
 
Tusirudie kosa tena. nyumba za Serikali zitunzwe zitumike kwa matumizi na manufaa ya Serikali.
 
Chris14,
Mkuu nilikuwa naota ,,, nawaza kwa sauti sasa. Awamu zijazo nazo zitaipeleka makao makuu Arusha au Mwanza.

Any way, wameamua hivyo ila binfsi naona awamu ya sita namba moja akiishi Dar kwenye ikulu ndogo halafu Dodoma ikawa ghofu.
 
Back
Top Bottom