Kasie
Platinum Member
- Dec 29, 2013
- 21,168
- 36,056
Habari za jumapili,
Natumai nyote ni wazima wa afya, vivyo hivyo Kasie. Leo ni jumapili na kuna mahali nilienda kuibadika, neno nililotoka nalo madhabahuni ni hiko kichwa cha huu uzi.
Tangu naingia shule ya jumapili aka Sunday School sikuwa nimeuelewa huu mstari au agizo kutoka kwenye kitabu cha Mungu. Miaka yotehiyo nilikuwa najua mwanamke hatakiwi kuvaa suruali, kaptura, kunyoa panki kama mwanaume na kuvaa viatu vya kiume kwa muonekano wa macho ya nyama.
Leo, leo hii ndio nimepata maana iliyo ndani yake. Ngoja nijaribu kuelezea kama nilivosikia.
Wamama na wanawake wengi leo wanapata shida kwenye mahusiano ya ndoa zao, na waume zao au wapenzi wao kwasababu wamevaa mavazi ya mwanaume. Matokeo yake wamemuacha mwanaume uchi......
Wamama na wanawake wa leo mambo yenu hayawaendei sawa kwenye familia na mahudiano sababu mmevaa mavazi yawapasayo wapenzi na waume zenu. Mmevaa mavazi ya kuwa vichwa kwenye familia aka being bread winner. Mmevaa mavazi ya kuibeba familia na ukoo kiasi kwamba ikitokea shida unatafutwa wewe mwanamke badala ya mwanamme kwenye familia. Uzuri Mungu aligawa majukumu kati ya mme na mke, na ambaye hakutimiza wajibu wake aliadhibiwa kwa nafasi yake na suluhisho halikuwa kuchukua jukumu la mwenzio ili maisha yaende bali kumkumbusha atimize wajibu wake ili nawe ufanye lako.
Kuna methali inasema mshika mawili moja humponyoka, najua wako wake wanaokaba kote Yaani kama baba na kama mamana amefaulu je ni wangapi? Wengi wao wamefeli na kujikuta wanabanwa na vazi la kiume ilhali wao ni wanawake.
Najua wapo wataosema huyo mhubiri anakumbatia mfumo dume, hizi zama za siku hizi mjumuiko wa majukumu ni kusaidiana....n.k n.k. Ila twende mbele turudi nyuma, mambo yamevurugika huko mitaani, familia zimekuwa tafrani. Aidha sababu wanaume waliacha kutimiza wajibu wao ikasababisha wanawake kuvaa mavazi yampasayo mwanaume na wao wanawake wakaacha mavazi yao hayana mtu na wengine yanavaliwa na dada wa matokeo familia inavurugika.....
Haikuwa sawa na madhara yake wamama wameacha kulea familia sasa wanaambatana na tabia za kianaume kutokana na kuvaa mavazi ya kiume.... Na nyingine wanaume waliacha kufanya yawapasayo kufanya baada ya kuona wanawake wamevaa mavazi yao, na wao walifanya kosa kuridhika, walitakiwa wavae mavazi yao ili mwanamke abaki kwenye nafasi yake maana madhara ya kuvaa mavazi ya kiume yana package yake.
Kutoka out usiku, kwenda gym jioni na alfajiri, kwenda safari za kirafiki weekend bila familia aidha na wafanyakazi wenzie au marafiki waliosoma wote sekondari hadi chuo hatimae kuacha jukumu kubwa la kuilea na kuiangalia familia... Madhara makubwa zaidi ni mtu kuanza kuona majukumu familia yake yanambana kufanya mambo yanayoambatana na mavazi ya mwanaume aliyoyavaa.... Hence kuchepuka... Kufumaniana... Kuachana....kuuana... Watoto wa mitaani...
Wanawake vueni hayo mavazi ya waume zenu ili nao waweze kukaa kwenye nafasi zao na kutimiza wajibu wao.
Nanyi wanaume, msibweteke sababu kuna wanawake viherehere wanavaa mavazi ya kiume na kufanya wajibu wa kiume. Vaeni mavazi yenu ya kiume familia ziende sawa.
Nawatakia jumapili njema nyote mlioenda ibadani leo,na ambao hamjaenda basi endeleeni kutafakuri ujumbe huu kutoka madhabahuni.
Love you people.
Kasinde.
NB: nimeongezea nyama kidogo hapo juu na kufafanua zaidi.