Haileti maana kwa sisi waafrika kuendelea kumshangilia Trump.

Eberhard

JF-Expert Member
Dec 20, 2010
1,120
757
Sioni kama ni sahihi kwa sisi waafrika tunafanya kitu sahihi kumshangilia DonaldTrump. Hakuna maneno yake mengi yamejaa chuki na hayana uhalisia.

Ebu tuangalie mfano huu. Trump anasema sisi waafrika ni wazuri kwenye sex na yeye mwenye ameshaoa na kuacha mara tatu anatafuta nini? Mbaya zaidi mara ya mwisho( 2005)ameenda kuoa binti mdogo ambaye anawezae hata akamwita babu lakini bado anaona yeye siyo mpenda wa sex huku akendelea luxurious maneno makali sisi. Anatuhuma za kuwazalilisha wanawake kijinsia huko siyo kupenda sex?

Wakuu nimeamini aliyesema nyani hanoi..... hajakosea.

Wazungu wanazidi kutudhalilisha cha ajabu dada zetu wanapenda sana wafanane nap kwa kujichubua na kuvaa mawigi na manywele ya wafu huko Amerika na Ulaya.
 
Onyesha kwa ushahidi wa vyanzo vya kuaminika trump akitamka hayo maneno na madai uliyoyaandika.
 
Trump hajawahi kusema mambo hayo na hakuna ushahidi wowote kuwa alisema hivo.
Pia nchi karibu zote duniani zina fuatilia uchaguzi na siasa ya marekani, kwa hiyo kuanzia wachina , warusi wa mexico na kila taifa halikosi wanaotaka flani ashinde na huyu ashindwe na ndio ushabiki wenyewe huo.

Ila hakuna faida ya moja kwa moja kwa sisi tulioko Tandale kuwa tutafaidika na utawala wake.
 
Kuna moja niliipenda kutoka kwa Trump. Alisema kuwa viongozi wa nchi za Afrika wanakwapua fedha nyingi kutoka katika nchi zao na kuziweka nje kwenye mabenki Ulaya na Marekani, halafu haohao wanakwenda huko kuomba misaada ya maendeleo! Suluhisho lake likawa kwamba labda Wakoloni waje wawatawale tena!!!!
 
Hii ni kweli
 
Back
Top Bottom