Haikubaliki Jeshi la Polisi kugeuzwa kichaka cha wezi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Haikubaliki Jeshi la Polisi kugeuzwa kichaka cha wezi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Jan 29, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jan 29, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Maoni ya katuni


  Habari kwamba baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi wanahusika katika wizi wa shehena ya mahindi tani 600 ambayo yalikamatwa yakivushwa mpakani kwenda nchi jirani katika wilaya ya Longido, mkoani Arusha, ni za kushtua sana.

  Habari hizi ambazo tuliziandika kwa kina katika gazeti hili toleo la jana, zilisema kwamba shehena hiyo ilikuwa ni mkusanyiko wa mahindi ambayo yalikamatwa kutoka mikononi mwa wafanyabiashara waliokuwa wanafanya biashara ya magendo mpakani, nia ikiwa kwanza, kuzuia utoroshaji wa chakula nje ya nchi, lakini la muhimu kuwataka wananchi wajenge utamaduni wa kufanya biashara katika njia zinazokubalika kisheria.
  Kimsingi polisi ndicho chombo kikuu cha kulinda usalama wa raia na mali zao, lakini zaidi sana kuhakikisha kuwa sheria zote zilizopo kwa ajili ya nchi kujitawala zinafuatwa bila suluhu, ndiyo maana wanakamata mali za magendo na kuzitaifisha kwa manufaa ya umma; hizi aghalab hupigwa mnada au mara nyingine kutolewa kama msaada kwa taasisi za kijamii kama shule, hospitali za umma na kwingineko pale inapoonekana inafaa.
  Kadhalika zipo bidhaa nyingine zinapokamatwa ambazo hulazimika kuteketezwa kwa sababu ni hatari kwa uhai na usalama wa raia.
  Katika mazingira haya, unaposikia kuwa shehena ambayo ilikamatwa na polisi, ikawekwa chini ya himaya yao, ikahakikiwa, ikasafirishwa kwa maelekezo ya viongozi wa Jeshi hilo na viongozi wa kisiasa wa wilaya ili ikahifadhiwe kwenye maghala ya NMC ikisindikizwa na polisi, lakini haikufika ilikotakiwa bila kuwako kwa na taarifa zozote kwamba msafara wa shehena hiyo ulivamiwa labda na majambazi waliojihami kwa silaha nzito za kivita na hivyo kuwazidi nguvu polisi wetu, basi mshituko unakuwa mkubwa zaidi.

  Tunashtuka hivi kwa sababu kuna kila ishara kwamba mahindi haya yameibwa chini ya uangalizi wa polisi. Bila kumungÂ’unya maneno polisi wameshiriki wizi, hii ni aibu, fedheha na upakaji mkubwa matope Jeshi la Polisi. Ni jambo lisilokubalika kwa vyovyote vile.
  Itakumbukwa kwamba mwaka jana tulifuatilia kwa kina habari za kupotea kwa sehemu ya dawa za kulevya zilizokuwa zimekamatwa Tunduma, mpakani mwa Tanzania na Zambia. Sehemu ya dawa hizo ilipotea ikiwa mikononi mwa polisi, hadi leo hakuna taarifa yoyote ya maana imewahi kutolewa na Polisi juu kashfa hiyo.
  Kadhalika, kumekuwa na malalamiko mengi dhidi ya baadhi ya askari polisi kuwa wanashirikiana na wahalifu, wapo waliofikia hatua ya kukodishia wahalifu silaha kama tukio mojawapo lilitokea wilayani Siha mkoani Kilimanjaro ambalo mkuu wa kituo cha polisi alikamatwa kwa kosa la kukodishia majambazi silaha.
  Tunatambua Jeshi la Polisi ni taasisi muhimu kwa mustakabali wa taifa, lina dhima isiyopimika katika kuhakikisha usalama, ustawi na uhai wa raia unakuwapo. Wananchi wanalipa kodi ili pamoja na mambo mengine watumishi kama polisi waweze kutekeleza wajibu wao sawasawa, kwa hiyo habari kwamba baadhi ya askari wameshiriki uhalifu kama huu wa wizi wa mahindi, hazishtui tu raia bali zinaacha doa kubwa kwenye taasisi hii.
  Tumesikia msimamo wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo, kwamba hataki mchezo katika hili na amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Longido ambaye naye ni Mwenyekiti Kamati ya Ulinzi ya wilaya kumpata taarifa ya kina yaliko mahindi hayo ifikapo leo, Alhamisi Januari 26, 2012.
  Kila tukitafakari kwa kina wizi huu tunafikia hitimisho la kuamini kwamba walioshirikia uhalifu huu wana ujasiri wa kufanya uhalifu, inawezekana kabisa kwamba ni wazoefu, kwani hawakudokoa tu shehena hiyo na kuacha kiasi, waliichukua nzima nzima. Huu ni ujasiri wa kutisha.
  Tunachukua fursa hii kwa kweli kuwataka wote wenye wajibu wa kusimamia usalama mkoani Arusha kuchukua hatua kali na zinazofaa ambazo zitatoa funzo dhidi ya wote waliohusika na wizi huu. Ieleweke hapa hatuzungumzii tu polisi, pia tunagusa walionunua mzigo wa wizi, waliouficha, waliopata manufaa yoyote ya uhalifu huu. Tunapenda kuona hatua zikichukuliwa haraka iwezekanavyo.

  Tunajua Mkuu wa Mkoa amezungumza, Mkuu wa Wilaya naye pia kazungumza, lakini pia Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) naye amezungumza, tunajua pia yupo Kamanda wa Polisi wa Mkoa, hawa wote ni viongozi, hawa wote wapo kutumikia wananchi, lakini uhalifu huu unatokea kwenye maeneo yao kazi. Nini kifanyike?
  Umma unataka uwajibikaji sasa kwa kuwa Jeshi la Polisi kamwe haliwezi kuwa kichaka cha kulea wahalifu tena wanaovaa sare za jeshi hilo. Haikubaliki na haitakubalika asiliani.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. N

  Ndyali JF-Expert Member

  #2
  Jan 29, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,222
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Naogopa kuchangia hapa, hawa jamaa wamepewa uhuru na mkuu wa kaya kutupiga mabomu ya mchozi watavyo lol!:A S embarassed::A S embarassed:
   
 3. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #3
  Jan 29, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Polisi mbona ndo zao, ni vile wao hawana power ya kujiongezea posho so wanatumia means and ways!
   
 4. E

  ENGINE CONTROL Senior Member

  #4
  Jan 29, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 139
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hapo ndipo nichokapoo kabisaaa na serikali ya tanzania.Ukitaka kucheka na kuchanganyikiwa kabisaa watajifanya hawajui hio shehena imepoteldea wapi.

  1-OCD ndio awe wa kwanza kuwajibishwa maana yeye ndio anafaham ni vijana gani aliwatuma kwenye opresion hiyo.
  Kwa kuwa polisi ni kama mbwa aamrishwaye na mfugaji wake akiambiwa shika anashika bila kuuliza au kuhoji kwa sababu ipi au kwa kosa lipi unaweza kuona uhalifu huo kuna mkubwa anahusika.

  Sasa inamana gan ya kuwa na jeshi la polis ikiwa wao ndiyo wanaongoza kwa wizi??

  Sabubu walizo kamatia mahindi hayo yasiende kuuzwa nje mbona kwenye mali za uma kama madin,wanyamapor huwa hawazitumii?
   
Loading...