Monica Mgeni
Member
- Oct 7, 2021
- 82
- 134
Na;
Tanzania Diaspora waishio Marekani (USA)
Yanayoitwa maandamano ya kudai katiba mpya katika mitandao ya kijamii kwamba yalifanywa na Watanzania waishio Marekani pindi Rais Samia akiendelea na Ziara yake nchini humo, ukweli ni kwamba kikundi hicho ni vijana wahuni (wasiozidi watu 15) wasio kuwa na ajira ambao wengi wao siyo Watanzania ambao wamelipwa na Wanaharakati na wapinzani waliopo nchini Tanzania ili kuchafua taswira ya nchi na serikali katika uso wa Dunia.
Ikumbukwe kuwa wakati wahuni hao wanafanya maandamo uchwara, Rais alikuwa akiwahutubia Watanzania waishio Marekani na kujadiliana nao juu ya masuala mbalimbali kwa maslahi mapana ya maendeleo ya Taifa letu huku wahuni hao wakiwa nje ya jengo wakipaza sauti zao ili kuwaridhisha wanaharakati na wapinzani ambao wamewapa ujira wa siku kwa ajili ya upuuzi huo.
Tanzania Diaspora in USA tunatambua jitihada zinazofanywa na Serikali kwa kushirikiana na wadau wa masuala ya siasa nchini Tanzania ikiwemo vyama vya upinzani kupitia Kikosi kazi cha Maridhiano ya Kisiasa kilichoundwa na Serikali kwa ajili ya kuleta muafaka wa kitaifa juu ya masuala mahususi ya kisiasa, kiuchumi na kijamii katika kuendelea kufanikisha maendeleo ya Taifa.
Hivyo, hatukubali kuona ajenda ya chama kimoja cha kisiasa cha upinzani ambacho kinashirikiana na wanaharakati wake kuzima Ndoto za viongozi wetu kwa maslahi yao ya kisiasa kuliko maslahi ya Taifa.
Tuwakatae mamluki!
Mungu Ibariki Tanzania 🇹🇿