Haikuanza kwa Makonda miaka ya 1970 Rais Nyerere alimjia juu RC Rwegasira wa Dar es salaam kuwafukuza machangudoa

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,636
30,004
Miaka ya 1974 Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam wakati huo bwana Rwegasira, aliwafukuza wanawake wanaojiuza jijini Dar es salaam, na kuwapandisha magari wahaya waliojiuza kwenda Bukoba na mikoa mingine kama wachaga na wasukuma kwenda kwao,

Nyerere akiwa rais alimuita na kumhoji maswali yafuatayo

1.Unawafukuza umewahoji kujua matatizo yao?

2.Pili unapowafukuza unasababisha kukaribisha mazingira ya kubaka wake zenu,

3. Je kuwarudisha kwao ndo mazingira sahihi ya kuwafanya waache?

Nimeyapata kwenye gazeti Moja la Miaka ya 70 kwenye maktaba moja,

Nimejiuliza sana maswali mengi kumbe hajaanza makonda mambo haya

Nitaweka gazeti la serikali mwaka 1974 lililozungumzia habari hiyo soon

Britannica
 
Najiuliza hao waliokuwa wanajiuza enzi hizo miaka kede kede imepita je
1. Wanajisikiaje kwa sasa
2. Au ndio wale bibi wasio na staha kwa sasa
3. Walifikia lengo la utajiri?
Daah maisha haya, eti huyu bibi yako alikywa enzi hizo changu pale sudan temeke.....Amaizing
 
Kumbe hayo mambo yameanza zamani!
Watajwa wa hii biashara bado wanarithishana, wale wengine bado kama kawaida wanatega vichochoroni wengine kwenye mabaa Kama mabarmaid.
Wasukuma wameacha I think.
 
Nyerere alijijua. Alimkataza Kawawa kuzuia wasichana kuvaamini skirt. Akasema mitindo inakuja na kupita acha kuhangaika nayo. Baada ya mini skirt zikaja maxi. Sasa zimerudi tena mini skirt. Si unaona basi?
Nakumbuka ilikuwa 1974 mwalimu alikuwa nje ya nchi. Kurudi anakuta wanafunzi tulazimishwa kuvaa skirt ndefu shuleni. Baada ya wiki tuliambiwa ruksa. Tukaendelea na vimini vyetu. Je, kulikuwa na waliokuwa wanapata mimba shuleni? Jibu ni hapana.
 
Back
Top Bottom