kalaghesye
Member
- Jan 16, 2012
- 79
- 11
- Thread starter
- #21
Kalaghesye hapa anajaribu kutuonesha mfumo wetu wa kimamlaka na kiutendaji ulivyo, na jinsi misuse of public resources ilivyo kubwa, kulingana na utafiti wake. Ni suala tu la kufanya utafiti linganifu na kuchallenge utafiti wake na si kusema ana wivu! Nadhani upande wa pili ndo una wivu na aibu kuona wanakula tu mishahara na posho wakati idara husika haina "majukumu linganifu na shughuli mama ya wizara". (Wanavuna wasichopanda)
Ndugu yangu Kingo, asant sana kwa mchango wako. Nilikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wanakataa kuwa ati humu ndani "Jamii Forum" kuna watu wapo kwa ajili ya kulinda maslahi yasiyo na tija kwa Taifa. Jamani tukumbuke kuwa tupo leo kwa sababu kuna watu walibakisha. Sasa sisi mbona tunakula bila kufikiria kuwa kuna watoto, wajukuu na vitukuu vyetu vinakuja.
Well, nina wivu wa kuiona nchi hii pamoja na wenye madaraka wana badilika. Naomba ieleweke kuwa mwanzo wa utafiti wangu sikulenga kukutana na matatizo. Nilikuwa nataka ku-prove a number of hypothesis za wenzetu waliotutangulia kuhusu miundo na mifumo ya taasisi .... nothing more.