Haijakaa sawa kulipia huduma ya choo katika sehemu za huduma za jamii. Litazamwe upya

Acha ujinga wewe yaani ukaweke mimavi yako pale bure, usitumie maji etc na huyo atakayekuwa anakuflashia uchafu wako analipwa na nani na baadaye kinyesi chako kikijaa nani atagharamia kuzoa , muwe na akili wakati mwingine vinginevyo ungeenda kuishi porini huko na ngedere ukijiskia kuhara unahara tu popote hata usipotawaza safi tu eboh!
Duh! Si mchezo.
 
unadhani airport wanakwenda wale ndugu zako wanaokwenda hata kuoga kutokana na kukosa maji huko uswahilini
Heheh, although nakubali watu wanaotumia usafiri wa ndege kidogo Wana tofauti na wanaotumia usafiri wa basi, lakini haifanyi kwamba wote wanafanana kwa maana ya wote wanaopanda ndege kwamba nao ni wastaarabu au wanaopanda mabasi kwamba sio wastaarabu.

Binafsi kwa walei tunaosafiri kila siku aisee airport unaenda hata na ndala sio lazima uoge na upigilie nguo za Christmas mzee so mie naona kawaida hata kusafiri kwa basi stendi zimeboreshwa sana nimeona Ile ya kibamba na Dodoma na baadhi yake sioni tatizo kwa nini wasiweke watu wa usafi na mambo yakaendelea fresh tu mbona vyoo vya kwenye mahoteli ambayo mabasi husimama huwa vinakuwa visafi muda wote???

Unaposafisha kila muda hata wasio wastaarabu watastaarabika tu maana wataona noma mwishowe. Na ukimlipisha mtu asiye mstaarabu kutumia choo hachelewi kuacha kimba juu ya sinki la kunawia mikono anahisi Ile Mia mbili au Mia tano yake haijatumika kisawia.

Chukua mfano niliotoa wa vyoo vya mahotelini ambapo mabasi husimama kwa ajili ya chakula na kujisaidia. Pale magari yanakuwa mengi kwa wakati mmoja Ila wanahakikisha choo kisafi muda wote kinakuwa na mtu wa usafi, that's how it should be done kwa vyoo vya stendi pia. Kama wanakusanya mapato hivi wanashindwa kumuweka mtu wa usafi muda wote?

Waafrika tumefika sehemu hata kujisaidia kwenye public toilets inabidi kulipia sasa wapi inakuwepo huduma ya serikali kwa wananchi wake???

Hata mavi unalipia kuyamwaga kwenye choo Cha imma??? Sisemi wasiwepo wawekezaji wa mavi Ila hii ni aibu kama tunahimiza kampeni za kujenga vyoo halafu unaweka kunya kwa hela tena choo Cha imma na watu wanalipa ushuru sokoni au stendi na nauli zinainclude charges zote za huduma kadhaa zilizopo kwenye hiyo facility
 
Wanaposema umasikini ni pamoja na huduma ya choo kuilipia harafu vyoo vingi unakuta bado vochafu tuu inatakiwa kuwe na vyoo ambavyo viko chini ya majiji au halmashauri watu wanavitumia buree kabisa...mbona hamjiulizi kwa nini kwenye mall zote huwezi kukuta huduma ya choo ya kulipia hao wawekezaji huko walikotoka hiyo mambo haipo na vyoo vyao ni visafi kwa kuwa wapo watumishi kwa ajili ya hiyo tuu...
 
Wanaposema umasikini ni pamoja na huduma ya choo kuilipia harafu vyoo vingi unakuta bado vochafu tuu inatakiwa kuwe na vyoo ambavyo viko chini ya majiji au halmashauri watu wanavitumia buree kabisa...mbona hamjiulizi kwa nini kwenye mall zote huwezi kukuta huduma ya choo ya kulipia hao wawekezaji huko walikotoka hiyo mambo haipo na vyoo vyao ni visafi kwa kuwa wapo watumishi kwa ajili ya hiyo tuu...
This is what I'm talking about, angalia kwenye malls tena mhudumu anasafisha kila baada ya dakika kadhaa huwezi kukuta choo kichafu. Sasa public toilets unataka isafishwe Mara moja kwa siku hiyo haiweyhata nyumbani tu mkizidi watu watatu au zaidi lazima choo isafishwe Mara kadhaa kwa siku.

Sasa watu wanatia aibu kama hata public toilets iwe unalipia ingali kwenye malls na majengo ya kurent maofiai unaingia bure na vyoo visafi na mhudumu yupo mpaka muda wa kufunga maofisi.

Kiukweli ni lazima kujiuliza ni huduma gani serikali inatupatia free of charge japo tuenjoy kodi zetu tunapokata gogo???
 
Ni aibu sana kukata gogo au haha ndogo unalipia 😃😃 ishu ya uchafu hata uende wapi choo lazima isafishwe Mara kwa Mara especially public toilets lazima awepo mtu asafishe at least kila baada ya nusu saa.

Mbona kwenye mahoteli ya barabarani ambapo mabasi yanasimama huwa choo zao no Safi na Kuna mhudumu amesimama mlangoni anasafisha kila muda akiona kuna harufu mbaya au uchafu.

Kuhusu ustaarabu hii ni personal issue hata Ulaya wapo tu usipoweka mtu wa usafi utakuta choo imeziba tu.
 
Acha ujinga wewe yaani ukaweke mimavi yako pale bure, usitumie maji etc na huyo atakayekuwa anakuflashia uchafu wako analipwa na nani na baadaye kinyesi chako kikijaa nani atagharamia kuzoa , muwe na akili wakati mwingine vinginevyo ungeenda kuishi porini huko na ngedere ukijiskia kuhara unahara tu popote hata usipotawaza safi tu eboh!
Sina hakika kama umemuelewa mtoa mada.Chukulia mfano huu,Mtu ameenda kumpokea mgeni wake stendi,Akalipa shilingi mia tatu kuingia ndani ya stendi.Akiwa mle ndani akahitaji kwenda haja,ilitosha ile fedha aliyolipia mule ndani apate hiyo huduma bila kupazimika kulipia tena.

Ushuru wa kuingia ndani unaolipiwa kimantiki ni kwa ajili ya kufacilitate huduma
atakazozipata,choo ni sehemu ya huduma,Hivyo hakupaswa kulipia tena.

Utaratibu wa watoa huduma wenye ofisi zao katika maeneo hayo mfano wenye ofisi za mabasi stendi kulazimika kulipia kila anapohotaji kwenda chooni,unachangia kuongezeka kwa uchafu, maana watu wanalazimika kukojoa kwenye makopo na baadae yanatelekezwa maeneo mbalimbali.
 
Akili za kimasikini Sana hizi, Tsh 200-300 tunapiga kelele, ulimwengu wa kibepari hautaki kulia Lia, pambana tafuta hela
 
Akili za kimasikini Sana hizi, Tsh 200-300 tunapiga kelele, ulimwengu wa kibepari hautaki kulia Lia, pambana tafuta hela
Sasa hayo mawazo yako ndo ya kimasikini, unadhani mabepari ndo hela zao zinachezewa kirahisi!!?
Na kwa taarifa tu sehemu wanazomiliki mabepari ndio huduma za choo Ni bure na vyoo Ni visafi...

Elimu ya darasani uliikosa,Basi jaribu kupanga bajeti usafiri ujifunze elimu ya duniani....hakika mawazo yako yatabadilika
 
Lipa tu mkuu, kuna siku hapa tumebanwa na wife tukazama sehemu chooni kwenye mall ni buku 3 tulilipa.nikamtania tu buku tatu kunya alicheka mpaka akaanguka.
 
Acha ujinga wewe yaani ukaweke mimavi yako pale bure, usitumie maji etc na huyo atakayekuwa anakuflashia uchafu wako analipwa na nani na baadaye kinyesi chako kikijaa nani atagharamia kuzoa , muwe na akili wakati mwingine vinginevyo ungeenda kuishi porini huko na ngedere ukijiskia kuhara unahara tu popote hata usipotawaza safi tu eboh!
Hoja hujibiwa kwa hoja na sio kwa matusi; watu wanahitaji hoja
Amesema; hao watu wanakuwa wameshalipia kodi, hivyo hapo wanatozwa marambili
Mbona ukiingia kwenye mgahawa kula, ukienda chooni hulipii?
 
Tumekuwa na utaratibu wa kulipia huduma ya choo katika masoko yetu, stendi za mabasi nchini.
Mimi nimekuwa najiuliza saana kuhusu utaratibu huo.

Mbaya zaidi, ni pale hata wafanyabiashara au wenye ofisi maeneo hayo wanalazimika kulipia huduma hiyo.

Inafahamika Wenyee shughuli zao katika sehemu hizo wanalipia Kodi. Wanaopata huduma sehemu hizo wananunua na kukatwa Kodi, iwaje Tena watu haohao walipishwe huduma ya choo tena?

Ukifungua shule au Zahanati, au Mgahawa nk, usipokuwa na choo unafungiwa siyooo? Kwanini mantiki hiyohiyo isitumike katika sehemu za huduma.

Halmashauri, Miji na Majiji huku sio kutoza kitu kimoja Kodi zaidi ya moja kwenye huduma moja!.

Madiwani na watunga mipango liangalieni Hilo, linadhalilisha wasiokuwa nacho na linaongeza uchafu sehemu hizo.
Tembea na choo chako !! Mlitakiwa mjengewe vya kwenu visivyo na uangalizi, sidhani kama mngeingia kwa uchafu ambao mngeukuta huko. Piga picha huko nyuma kabla ya vyoo vya kulipia kuanzia hali ya usafi ilikuwaje.
 
hata kwenye dimba na Mkapa...ingefaa iwe kulipia pia.....binadamu viumbe vya ajabu sana....anakunya kwenye sinki then anaacha hapo anasepa zake....
 
Gharama ya usafi na maji atalipia nani?.
Tatizo sio kutoza pesa ndo vyoo vinakuwa visafi,la hasha ana maanisha unapoingia kwenye terminal pesa unayotoa kuingilia ndo inatakiwa kucover huduma km hzo za choo...
Ndo akatolea mfano unapoingia hotelini au kwenye mgahawa haulipishwi hela ya chooni...
Na haimaanishi kwakuwa haulipi Basi utakuta choo kichafu..
Tumeona kwenye mall vyoo Ni visafi na vya kisasa na muda wote wapo watu wanafanya usafi ,hakuna mtu anachangisha pesa ya choo na Ni visafi kuliko hata vya kulipia...
 
Ukienda katika masoko na standi utakuta kampuni za usafi na zinalipwa pia, kwanini wasihusike na vyooo!
Nionavyo mimi ni bora huduma ya vyoo ikitolewa na watu binafsi kama sasa - ili kuwe na unafuu katika usafi. Taasisi za umma zikiendesha vyoo yamkini kubwa ni kwamba usafi utakuwa janga.
 
Back
Top Bottom