Haiingii Akilini: Matokeo leo, Kuapishwa Kesho, Lakini Serikali Baada ya Wiki Mbili!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Haiingii Akilini: Matokeo leo, Kuapishwa Kesho, Lakini Serikali Baada ya Wiki Mbili!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mr. Zero, Nov 15, 2010.

 1. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #1
  Nov 15, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,496
  Likes Received: 2,742
  Trophy Points: 280
  Hivi hii imekaaje??

  Uchaguzi unafanyika siku moja, kura zinahesabiwa wiki nzima lakini rais anaapishwa siku mmoja tu baada ya matokeo tena mbele ya wageni waalikwa kutoka nchi mbalimbali including Presidents, halafu inachukuwa zaidi ya wiki mbili kuunda serikali!!!
   
 2. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #2
  Nov 15, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  SOMA KATIBA KILA KITU KIMEWEKEWA TIME FRAME YAKE, NDIO MAANA RAIS ALIMTEUA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI MAPEMA ZAIDI KWA KUWA ACCORDING TO THE TIME FRAME YA BUNGE KUITISHWA BAADA YA UCHAGUZI NI LAZIMA TANGAZO KUTOLEWA NDANI YA GAZETI LA SERIKALI. KILA KITU KINA WAKATI WAKE.

  My Take:- Ukitaka kumficha kitu Mtanzania kiweke katika maandishi. Hivyo naambatanisha nakala ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (iliyo in force lakini inahitaji marekebisho makubwa; pamoja Kanuni za kudumu za Bunge letu kwa taarifa yako na wengine.

   
 3. October

  October JF-Expert Member

  #3
  Nov 15, 2010
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 2,147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Bado anaendelea na zoezi la kuchakachua majina.
  Si unajua amezoea kuchakachua!!!:bowl:
   
 4. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #4
  Nov 15, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,496
  Likes Received: 2,742
  Trophy Points: 280
  Actually, sina tatizo na hiyo katiba ya mwaka 47!!! Ila ningefurahi sana kama katiba ingepanga na ratiba ya kutoa matokeo ili kufanya uchakachuaji uwe mgumu.

  Anyway, Ninachotaka kuhoji ni lini hao wageni walialikwa kuja kwenye sherehe za kuapishwa?? Kama kuna ushahidi walialikwa kabla ya matokeo kutangazwa then nani aliwaalika?? Na NEC walishakijulisha chama Tawala matokeo kabla ya kutangazwa siyo??
   
 5. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #5
  Nov 15, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Kutoa matokeo ni mambo ya utendaji zaidi huwezi kuwa na deadline kamili wewe,mbona kama kilaza sana?
   
 6. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #6
  Nov 15, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Walialikwa kumuapisha Rais wala siyo kumuapisha kikwete,yeyote angepita wangeamua wao
   
 7. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #7
  Nov 15, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Ameingia kwenye madaraka bila ridhaa ya watu waio wengi amechoka hata kabla ya kuanza kazi. Watanzania wamesha mshikisha adabu kwa kuwapiga chini vilaza wake, hivo anashindwa kuwatuuwa wachapakazi, yuko anaomboleza vilaza wake akina masha, Marmo, Batrida, Kamara na wengine.

  Anaogopa kuteua vichwa wasije kum-challenge kwenye utendaji.
   
 8. C

  Chesty JF-Expert Member

  #8
  Nov 15, 2010
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 2,348
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  Sina uhakika kama amepingana na katiba, ila anashangaa katiba kufanya hilo kwa timeframe ndefu hivyo.

  People need to get going very fast, we need to learn to quicken our pace.
   
 9. C

  Chesty JF-Expert Member

  #9
  Nov 15, 2010
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 2,348
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  Kwa standard za Tanzania, na tukifuata hizi standards unazoadvocate hapa hatutaweza kusonga mbele. Brazil they did the election today and the following day or so matokeo yakatoka.

  With that pace you set a deadline cos you know what you are doing.
   
 10. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #10
  Nov 15, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160

  HATA MIMI NILIPOONA ULE UGENI MZITO NILIJIULIZA SWALI HILO NA KUPATA JIBU KUWA KAMA JAKAYA KIKWETE ALIOULIZWA SWALI KUHUSU KUSHINDWA MARA TU BAADA YA KUPIGA KURA ALIJIBU "HAKUNA KUSHINDWA MBANO UNAULIZA ULIZA KUHUSU KUSHINDWA". LAKINI NIKAJUA HATA UKIHOJI UTAJIBIWA KUWA NI MARAIS RAFIKI WALIPATIWA TAARIFA IN SHORT NOTICE WAKAKABALI KUHUDHURIA KUTOKANA NA URAFIKI WAO. LAKINI UKICHUNGUZA KW AKINA WENMGI WA WALIOHUDHURIA AMA WAMEWAHI KUCHAKACHUA MATOKEO AU WA[PO NJIANI KUCHAKACHUA MATOKEO KAMA JACOB ZUMA.

  NASHAURI TUSIPOTEZE MUDA KUHOJI VITU VISIVYOKUWA NA TIJA TUJIULIZE TUTAFANYA NINI KUREKEBISHA HALI HII YA TANZANIA KUWA KATIBA YENYE MAPUNGUFU MAKUBWA NA TUEM ISIYO KUWA HURU YA UCHAGUZI.


  Tokea mwaka 1992 mfumo wa vyama ving ulipoanzishwa vyama vya upinzani vimekuwa na ajenda ya kudai mabadiliko ya Katiba ambayo yatawashirikisha wadau wote ikiwemo asasi za kiraia, madhehebu ya dini, asasi za kitaalamu, asasi za wakulima, wafanyakazi, vijana, akina mama, walemavu, wazee n.k.

  Baadhi ya vyama vya upinzani vilifikia hatua ya kuitisha maandamano juu ya suala hilo, lakini muitikio wa sisi watanzania ulikuwa ni mdogo sana kuweza kutuma ujumbe kwa Serikali na Jumuia ya Kimataifa kuwa watanzania wanahitaji mabadiliko ya katiba kwa njia za amani.

  Badala yake ccm yenye wananchama karibu ya milioni nne imekuwa ikisisitiza kuwa Katiba iliyopo haina tatizo lolote. Hivyo kwa kutumia wingi wa wananchama wake imekuwa ikikumbatia Katiba hii nyenye mapungufu makubwa, yenye kuweka Tume isiyo Huru ya Uchaguzi n.k.

  Kama watanzania tunataka katiba ifanyiwe mabadiliko ni lazima tuhakikishe kuwa tunaelimishana ili kila mmoja aweze kuhusisha umaskini na uduni wa maisha alionao na mapungufu yaliyopo kwenye Katiba yetu ili aweze kushiriki katika harakati za kudai Katiba mpya iwe ni kwa njia ya kuhudhuria mikutano, makongamano, semina, maandamano n.k

  Kwa bahati mabya Watanzania tulio wengi tumekuwa tukivitegemea vyama vya siasa kwa ajili ya kusukuma ajenda ya mabadailiko ya kudai Katiba mpya. Haya ni mapungufu makubwa. Ikiwa wananchi tutaweza kuanzisha mjadala mpana kwa maana ya kila Mtanzania kufikishiwa ujumbe na akatambua mapungufu yaliyoko katika Katiba yana uhusiano wa moja kwa moja na matatizo yanayomkabili, ni wazi kuwa mabadiliko ya Katiba itakuwani ajenda ya kila Mtanzania na vyama vya siasa kama CCM vitalazimika kutupendeza kwa kubadili katiba ili vipate kura zetu.

  Ili kufikia lengo hilo ni wazi kuwa ipo kazi kubwa ya kufanywa na wananchi ya kuelimishana wenyewe kwa wenyewe kuhusu mapungufu ya katiba yaliyopo na faida za kufanya mabadiliko ya Katiba mpya.

  Hatari iliyopo ya kutegemea vyama vya siasa kusukuma mabadiliko makubwa kama haya ni kuwa katiba iliyopo ni nzuri sana kwa mtawala yeyote awe CCM , CHADEMA, CUF n.k. Kutokana na kukerwa na chama kilichopo madarakani watanzania wanaweza kuiondoa CCM madarakani na kuingiza chama kingine huku katiba ikiwa bado na mapungufu yale yale kutokana na watanzania kutokujua kuwa mapungufu ya katiba ndio hasa chimbuko la matatizo yote tuliyonayo.

  Kutokana na mapungufu ya kibinadamu viongozi wa chama hicho kipya nao wanaweza kuing'ang'ania katiba hii mbovu kutokana na ujinga wa watanzania walio wengi na tukaendelea kuumia vile vile.

  Muarobaini wa Katiba mpya uko mikononi mwa watanzania wenyewe, vyama vya siasa vitaidaka ajenda hii kama watanzania walio wengi watakuwa wamelimishwa kudai katiba mpya.


   
 11. FarLeftist

  FarLeftist JF-Expert Member

  #11
  Nov 15, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 362
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Nani alikuwa na jukumu la kualika wageni? Je walialikwa kabla ya mshindi kujulikana?
   
 12. thereitis

  thereitis JF-Expert Member

  #12
  Nov 15, 2010
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 297
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Nakala ya katiba uliyoweka hapa imepitwa na wakati kwani inaonyesha ilifanyiwa marekebisho(amendment) mwaka 2000. Katiba sahihi ni ile iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2005. Bahati mbaya sina soft copy yake ningeiweka hapa.
   
 13. thereitis

  thereitis JF-Expert Member

  #13
  Nov 15, 2010
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 297
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Nakubaliana na wewe lakini nani atakayewaongoza hawa wananchi kudai katiba mpya?
   
 14. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #14
  Nov 15, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Asante kwa kutupatia katiba ya Tanzania
   
 15. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #15
  Nov 15, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,496
  Likes Received: 2,742
  Trophy Points: 280
  Nafikiri kilaza ni wewe usiyejua kusoma between the lines. Unasoma juu juu tu halafu unajifanya kuchangia pumba. I do not have time for you R*****h!!!
   
 16. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #16
  Nov 15, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Mkipindua nchi bure
   
Loading...