Haidar Gulamali akutwa amehifadhi tani 154 za Sukari huko Dodoma

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,691
149,912
Huyu nae amekutwa amehifadhi zaidi ya tani 154 za sukari kwenye ghala lake hapa Dodoma usiku wa kuamkia leo.

Polisi na TAKUKURU kwa maelezo yao wameshindwa kutoa conclusion kama sukari hiyo ilikuwa imefichwa au imehifadhiwa ila wameahidi kuchunguza swala hili.

Chanzo:ITV

Hivi katika hii biashara hamana wanasiasa ndani yake?

Changamoto kubwa hapa ninayoiona ambayo hata mahakamani inaweza kuwa ni tatizo kwa serikali, ni namna ya kuthibitisha kuwa tani hizi za sukari zilikuwa zimefichwa na si kuhifadhiwa iwapo kutakuwa na kupelekana mahakamani.

Ukweli ni kwamba, hata hizi tani za sukari zinazodaiwa kufichwa na wafanyabiashara zikiingia sokoni leo hii,hatua hii bado itakuwa ni temporary solution tu as long as viwanda vya ndani havikidhi mahitaji ya soko la ndani. Tusisahau viwanda ni vichache na vingine vinaripotiwa kufungwa kwa ajili ya matengenezo.

Alafu kama baadhi ya wafanyabiashara waliohifadhi sukari kwenye maghala yao wakawa na document za manunuzi zinazoonyesha kuwa walinunua sukari hiyo na kuhifadhi kabla ya serikali kuzuia uingiza wa sukari kutoka nje,serikali hapa itawabana kwa lipi?Hata mahakamani siwataibwaga tu serikali?

Serikali ikiri tu ilifanya makosa kuzuia uingizaji wa sukari kutoka nje.
 
Hivi kama ana kiwanda cha kutengeneza juice au bidhaa nyingine je?
Mkuu hupo sawa kabisa.

Inawezekana akawa na kiwanda cha Juice, biscuits au hata pipi au hata anaweza kuwa ni agent wa kiwanda/viwanda vingine.

Hili swala liliitaji dialogue na hao wafanyabiashara ili kufikia common understanding. Sasa hivi, serikali ni kama inavizia vizia tu.

#Dialogue matter.
 
Huyu nae amekamtwa na zaidi ya tani 154 za sukari kwenye ghala lake hapa Dodoma.

Hivi katika hii biashara hamana wanasiasa ndani yake?

Chanzo:ITV

Ukweli ni kwamba, hata hizi tani za sukari zinazodaiwa kufichwa na wafanyabiashara zikiingia sokoni,hatua hii itakuwa ni temporary solution tu as long as viwanda vya ndani havikizi soko la ndani.Tusisahau viwanda ni vichache na vingine vinaripotiwa kufungwa kwa ajili ya matengenezo.

Sawa, assuming serikali inakiri, kwa hiyo solution ni nini au hatua gani zichukuliwe?
 
Huyu nae amekamtwa na zaidi ya tani 154 za sukari kwenye ghala lake hapa Dodoma.

Hivi katika hii biashara hamana wanasiasa ndani yake?

Chanzo:ITV

Ukweli ni kwamba, hata hizi tani za sukari zinazodaiwa kufichwa na wafanyabiashara zikiingia sokoni,hatua hii itakuwa ni temporary solution tu as long as viwanda vya ndani havikizi soko la ndani.Tusisahau viwanda ni vichache na vingine vinaripotiwa kufungwa kwa ajili ya matengenezo.

Serikali ikiri tu ilifanya makosa kuzuia uingizaji wa sukari kutoka nje.

Upuuzi wa kukamata Mali/sukari ya Hawa watu huko mbele itatugharibu kodi zetu kuwalipa watu mabilioni wakishashinda kesi kwa unyanyasaji wanaofanyiwa bila msingi wowote.

Tutalipa gharama kubwa hata tutasahau kama kimizuka mizuka tuligawiwa sukari BURE.
 
Mkuu hupo sawa kabisa.

Inawezekana akawa na kiwanda cha Juice, biscuits au hata pipi au hata anaweza kuwa ni agent wa kiwanda/viwanda vingine.

Hili swala liliitaji dialogue na hao wafanyabiashara ili kufikia common understanding. Sasa hivi, serikali ni kama inavizia vizia tu.

#Dialogue matter.

Kama ana viwanda vya aina sioni tatizo lolote. Anaweza kujieleza na wakamwelewa kwa muda mfupi tu. Lakini tukumbuke sukari ya viwandani ya kutumia kwenye juice na vitu kama hivyo ni tofauti na hii ya mtumiaji wa nyumbani. Kakutwa na sukari ipi?
 
Hivi kama ana kiwanda cha kutengeneza juice au bidhaa nyingine je?
Na ndiyo sababu najiuliza hawa maafisa wa serikali wanapo kwenda kamata sukari ktk maghala ya wafanyabiashara wakubwa ambao wanafanya biashara ya sukari na uzalishaji wa bidhaa za sukari wanakamatwa kwa sababu zipi hasa?
 
Gulamali anazalisha bidhaa gani hapo Dodoma?? Hivi unamjua au ndiyo unadhani..
 
Hivi kama ana kiwanda cha kutengeneza juice au bidhaa nyingine je?
Kama ana kiwanda sheria haimbani lakini sukari ya kiwandani ni tofauti na ya kunywea chai kamamda
Hapa linakuja tatizo lingine,industria sugar inaingia kama malighafi kwa hiyo hakuna duty,wanaume wanaichanga na kidogo sana na sukari ya chai halafu wanaingiza mtaani,na kujipatia super profit
 
Hivi hivi vikosi vinataka vikute wafanyabiashara hawana stock kabisa au maana mfanyabiashara Wa sukari lazima awe Na sukari kwa akili ya wateja wake Na wafanyabiashara wengi wanakuwa Na stock ata ya mwezi kulingana Na mahitaji ya wateja wake Na eneo husika
 
Huyu nae amekutwa amehifadhi zaidi ya tani 154 za sukari kwenye ghala lake hapa Dodoma usiku wa kuamkia leo.

Polisi na TAKUKURU kwa maelezo yao wameshindwa kutoa conclusion kama sukari hiyo ilikuwa imefichwa au imehifadhiwa ila wameahidi kuchunguza swala hili.

Chanzo:ITV

Hivi katika hii biashara hamana wanasiasa ndani yake?

Changamoto kubwa hapa ninayoiona ambayo hata mahakamani inaweza kuwa ni tatizo kwa serikali, ni namna ya kuthibitisha kuwa tani hizi za sukari zilikuwa zimefichwa na si kuhifadhiwa iwapo kutakuwa na kupelekana mahakamani.

Ukweli ni kwamba, hata hizi tani za sukari zinazodaiwa kufichwa na wafanyabiashara zikiingia sokoni leo hii,hatua hii bado itakuwa ni temporary solution tu as long as viwanda vya ndani havikidhi mahitaji ya soko la ndani. Tusisahau viwanda ni vichache na vingine vinaripotiwa kufungwa kwa ajili ya matengenezo.

Serikali ikiri tu ilifanya makosa kuzuia uingizaji wa sukari kutoka nje.

Simple, unaposema sukari haipo maana yake, hakuna mtu yeyote atakuwa na stock kiasi hicho , kama haipo iwe haipo na hakuna yeyote mwenye stock.
 
Huyu nae amekutwa amehifadhi zaidi ya tani 154 za sukari kwenye ghala lake hapa Dodoma usiku wa kuamkia leo.

Polisi na TAKUKURU kwa maelezo yao wameshindwa kutoa conclusion kama sukari hiyo ilikuwa imefichwa au imehifadhiwa ila wameahidi kuchunguza swala hili.

Chanzo:ITV

Hivi katika hii biashara hamana wanasiasa ndani yake?

Changamoto kubwa hapa ninayoiona ambayo hata mahakamani inaweza kuwa ni tatizo kwa serikali, ni namna ya kuthibitisha kuwa tani hizi za sukari zilikuwa zimefichwa na si kuhifadhiwa iwapo kutakuwa na kupelekana mahakamani.

Ukweli ni kwamba, hata hizi tani za sukari zinazodaiwa kufichwa na wafanyabiashara zikiingia sokoni leo hii,hatua hii bado itakuwa ni temporary solution tu as long as viwanda vya ndani havikidhi mahitaji ya soko la ndani. Tusisahau viwanda ni vichache na vingine vinaripotiwa kufungwa kwa ajili ya matengenezo.

Serikali ikiri tu ilifanya makosa kuzuia uingizaji wa sukari kutoka nje.

Huyu ni mfanyabiashara wa jumla hapa Dodoma, Dodoma hatuna viwanda vya juice wala soda viwanda hapa ni wine na mafuta ya alizeti, huyu alikua ameficha 7bu ni mmoja kati ya wauzaji wa jumla wa sukari hapa Dodoma, nadhani wamepata kigugumizi ni mfadhili wa chama tawala na alijaribu ubunge ila aliangushwa kwenye kura za maoni, hapa Dodoma wiki ya pili tunanunua kilo 3500/- na tangu juzi sukari ilikua haipatikani madukani.
 
Back
Top Bottom