Hai: Msako wa DC Ole Sabaya wamnasa Mfanyabiashara Alex Elibariki Swai, atuhumiwa kufanya biashara kinyume na Sheria

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,801
11,961
Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya ameongoza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Kilimanjaro pamoja na Maafisa kutoka Halmashauri kufanya operesheni maalum iliyopelekea kunaswa kwa shehena (Godown) lililokuwa likitumika kuhifadhi vileo feki na bidhaa zingine zikiwemo shehena za mbolea na saruji bila kuwa na vibali halali.

Msako huo uliofanyika kwa kushtukiza usiku wa manane umemnasa Alex Elibariki Swai na Mkewe wanaofanya biashara hizo bila kulipa kodi, huku stika maalum za TRA zikigundulika baadhi kutokuwa halali na zile halali kuwa katika bidhaa tofauti na zilizoidhinishwa awali na Mamlaka.

Wafanyabiashara hao ambao pia walikutwa na lita nyingi za Diesel kinyume na sheria pamoja na fedha kiasi kikubwa ndani wamekabidhiwa kwa vyombo vya dola huku DC Sabaya akiagiza kulindwa kwa eneo lote hilo hadi Mamlaka husika zitakapomaliza shughuli zake na kubainisha taarifa zote za muhimu kwa ajili ya hatua zaidi.

 
Ni vema watanzania tukajitahidi kuchapa Kazi Kihalali na kujipatia riziki zetu halali bila kuvunja Sheria za nchi.
Serikali Ina mkono mrefu.

Kazi na Sala.
Kwa nchi hii yenye urasimu na kodi/tozo/ushuru kibao kufanya kazi kwa uhalali100% hutoboi. Hata hao TRA hawaishi kwa mishahara yao wengi wajanja janja wa mjini. Wanasiasa ndo usiseme kabisa. Kama unataka kufukisika kabla hujaanza we fuatisha kila amri uone
 
Shida ya Sabaya anapenda sana makamera,yeye kila tukio,makamera!
Na hela sana rejea ishu ya wafanyabiashara wa hotel walivuokua wanalazimishwa kutoa hela....na hapk kwenye kiasi kikubwa cha fadha ndo zishaondoka hizo
 
Back
Top Bottom