HAI: DC Sabaya amewajia juu wafanyabiashara waliopandisha bei ya mafuta ya kula wilayani humo na kutoa saa 24 kujitafakari kabla hajazinguana nao

Mkuu wa wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro,Lengai Ole Sabaya amewaonya wafanyabiashara wa Maduka wilayani humo,wanaopandisha ovyo bei ya Mafuta ya kula na Nyama hasa Kwenye mfungo wa Ramadhani kuwa atawachukuliwa hatua Kali ikiwemo kufuta leseni zao za biashara .

Akipokea Kero za wananchi mapema Jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kituo Cha mabasi, boma Ng'ombe wilayani humo .

Amesema kitendo Cha baadhi ya wafanyabiashara wasiowaaminifu kupandisha bei ya Mafuta ya kula hakikubaliki, kwani kinawaumiza waislamu wasio na hatia ambao wamefunga kipindi hiki cha mwezi mtukufu.

Sabaya amemwagiza Mkurugenzi wa halimashauri hiyo ,Yohana Sintoo kuhakikisha anapata taarifa za manunuzi (Delivery Note ) za wafanyabiashara wote wakubwa ndani ya masaa 24 kabla hajachukua hatua.

Alisema upo ushahidi kwamba baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu wamekuwa wakipandisha bei ya mafuta kwa Maksudi kwa lengo la kukomoa walaji ,ambapo ameapa kuwashughilikia.

Amesema wapo wafanyabiashara waliopandisha mafuta ya kula hadi kufikia sh,35,000 kutoka sh,21,000 kwa dumu la Lita tano na wamekuwa wakiandika lisiti za uongo kwa wateja tofauti na bei aliyouzia.

"Nimefanya utafiti kwa kutumia wasaidizi wangu,nimegundua kuwa dumu la Lita tano wanauza hadi sh,35,000 badala ya sh,21000 hii haikubaliki kuanzia leo napiga marufuku kupandisha mafuta hasa kipindi hiki Cha mfungo wa ramadhani"amesema Sabaya

Awali Baadhi ya wananchi walieleza Kero mbalimbali ikiwemo ya kupanda kwa Bei ya Nyama na Mafuta na kumwomba mkuu huyo wa wilaya kuhakikisha anawasaidia kuwabana wafanyabiashara hao na kukomesha tabia hiyo inayofanyika kipindi hiki cha mfungo wa ramadhani.

Wakati huo huo Mkuu huyo wa wilaya amekemea hatua ya wafanyabiashara wa Nyama kupandisha bei ya kitoweo Cha Nyama kutoka sh, 6000 hadi kufikia sh,8000 akidai Jambo hilo halikubaliki na atawachukilia hatua wafanyabiashara wa nyama.

Awali wananchi walimweleza mkuu huyo juu ya kupanda maradufu kwa bidhaa mbalimbali ikiwemo Mafuta ya kula na Nyama wakidai tangu kuanza kwa mfungo wa ramadhani bidhaa hizo hazishikiki na wameshindwa kumudu gharama za manunuzi.

Ends...

IMG_20210420_143034_595.jpg
IMG_20210420_143054_023.jpg
 
Hivi huyu jamaa hajamsikia Rais kasema nini? kwani mafuta ya kula yanatumika wakati wa Ramdhan tu baada ya hapo sawa kupandisha. mafuta yameanza kupanda bei kabla ya Ramadhan na hakuna mtu anakulazimisha kununua kitu kwa bei ya juu duka hili limekushinda nenda duka jingine biashara yoyote ni demand and supply ndio ina control bei, acheni siasa katika biashara
 
Back
Top Bottom