Hai: Aliyekuwa Diwani wa CHADEMA aachiwa huru kwa tuhuma za kumbaka Mwanafunzi baada ya DNA kuonesha Mtoto aliyezaliwa sio wake

Kasomi au Kajinga? Vile kabisa tuseme hujui maana ya kubaka inapohusu watoto? Mtu chini ya miaka 18 ni mtoto. Anawaza, kunena na kutenda kitoto. Hata kama amekutongoza yeye umebaka!
Kwa dhana hiyo miaka 30 inakuhusu. Yule jamaa aliyesema majaji wetu wanakopi na kupeisti naye alikuwa mbumbumbu wa hiyo dhana. Isipokuwa kiaina. Fataki wale miaka jela. Mabinti wasirudi shule. Hasomeshi wazazi bure. Fataki alibaka kwa dhana ya mtoto. Mzazi wa mimba za utotoni alitaka mwenyewe kwa ujinga wa Kasomi! Hapo chacha(sio mura!).
Dah kweli kasomi ni kajinga mkuu
 
Je wewe unaamimi au una ushahidi wowote wa uhakika kuwa kweli huyo binti hajawahi kufanya mapenzi na mtu mwingine yeyote zaidi ya huyo mshtakiwa??!!
Mimi tena? Mimi nimesema hayo ili ku pointi kuwa huyo binti haaminiki na huyo anaesemwa alimpa mimba yawezekana hata hamjui
 
Siasa ilitufikisha pabaya sana kama taifa. Halafu yule mhalifu Ole Sabaya asiposhughulikiwa na mahakama za kidunia basi Mungu atashughulika nae.
Sawa Aikael Mbowe, Hivi kwenye Post zako Kila Sekunde Sebaya Sebaya kwani amekufanya nini? Au kushindwa Ubunge ndo sababu
 
Binti ana kesi ya kujibu. Baba tarajiwa imesthibika si yeye! Kaidanganya mahakama
Usikute alihusika, lakini matokeo ya DNA yamechezeshwa. Sijawahi kumwamini hakimu wala mkemia hata hata siku moja.

Kuna kisa kimoja cha kitambo kidogo. Binti mwanafunzi wa sekondari alitoa mimba kwa msaada wa daktari. Kwa bahati mbaya ilimharibu kiasi cha kupoteza maisha.

Kabla hajafa alihojiwa na polisi na akaeleza nazingira yote ya tukio na kumtaja mhusika. Mhusika alipokamatwa alikiri kosa na akaonyesha alipofanyia zoezi hilo. Taratibu za kisheria zikaanza. Kesi mahakamani na sample za dawa zilizokutwa eneo la tukio zilipelekwa mahakamani.

Amri ya mahakama ikatuma vitu hivyo kwa mkemia mkuu. Ripoti iliyorudi ilisema hakuna uhusiano kati ya sample hizo na utoaji mimba na binti hakufa kwa tukio la kutoa mimba bali ni kuvuja damu kupita kiasi akiwa siku zake za hedhi.

Kesi iliishia hapo na mtuhumiwa aliachiwa huru na kurudishwa kazini.
HII NDIYO DUNIA YA WENYE HELA NA MAMLAKA.
 
Huyu ni mmoja tu Wa watu wengi waliozushiwa mambo mengi katika kila sehemu iwe mtumishi wa umma ungesingiziwa wewe chadema ukaumizwa sana,au mfanya biashara ungepigiwa kodi kubwa kwa kweli watu wameumia sana.
 
Usikute alihusika, lakini matokeo ya DNA yamechezeshwa. Sijawahi kumwamini hakimu wala mkemia hata hata siku moja.

Kuna kisa kimoja cha kitambo kidogo. Binti mwanafunzi wa sekondari alitoa mimba kwa msaada wa daktari. Kwa bahati mbaya ilimharibu kiasi cha kupoteza maisha.

Kabla hajafa alihojiwa na polisi na akaeleza nazingira yote ya tukio na kumtaja mhusika. Mhusika alipokamatwa alikiri kosa na akaonyesha alipofanyia zoezi hilo. Taratibu za kisheria zikaanza. Kesi mahakamani na sample za dawa zilizokutwa eneo la tukio zilipelekwa mahakamani.

Amri ya mahakama ikatuma vitu hivyo kwa mkemia mkuu. Ripoti iliyorudi ilisema hakuna uhusiano kati ya sample hizo na utoaji mimba na binti hakufa kwa tukio la kutoa mimba bali ni kuvuja damu kupita kiasi akiwa siku zake za hedhi.

Kesi iliishia hapo na mtuhumiwa aliachiwa huru na kurudishwa kazini.
HII NDIYO DUNIA YA WENYE HELA NA MAMLAKA.
Mkuu kwahiyo wewe adhima yako ni kuona diwani anafungwa 60 years au? Mahaka imekanusha wewe unakuja na hadithi
 
Mahakama ya Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, imemwachia huru diwani wa zamani wa Masama Mashariki (CHADEMA), John Munisi, ambaye alikuwa akikabiliwa na kesi ya kubaka na kumpa ujauzito mwanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari Marire.

Akisoma hukumu hiyo Leo, Hakimu Mkazi wa Wilaya hiyo, Jasmin Abdul amesema mahakama hiyo haijamtia hatiani mshtakiwa huyo katika makosa mawili yanayomkabili, kwa kuwa vipimo vya sampuli za vinasaba (DNA), kuonyesha mtoto aliyezaliwa, hakuwa mtoto wa mshtakiwa.

Aidha, hakimu huyo amesema kwa kuwa mtoto aliyezaliwa si wa mshtakiwa, mahakama hiyo haioni sababu ya kuamini kwamba mshtakiwa alimbaka mwanafunzi huyo, hivyo inamwachia huru.

Awali, ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Lebulu Mbise, kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo kwa nyakati tofauti.

Anadaiwa alitenda kosa la kwanza katika Kijiji cha Ngira, Wilaya ya Hai, kwa kumbaka mwanafunzi huyo Aprili 4, mwaka 2019, kosa alilotenda akijua ni kinyume cha sheria.

Ilidaiwa kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo, kinyume na kifungu 130 (1) (2) na kifungu 131 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura 16 ya Sheria iliyofanyiwa Marejeo Mwaka 2000.

Aidha, ilidaiwa pia mahakamani hapo kwamba, mshtakiwa alitenda kosa la pili katika kijiji hicho hicho, kwa kumpa ujauzito mwanafunzi huyo Aprili, kinyume na Sheria ya Elimu, kifungu cha 60 (A) (2) na (3) iliyofanyiwa Marejeo Mwaka 2002.

Katika ushahidi wa shahidi muhimu wa kesi hiyo ambaye ni mwanafunzi, alidai mahakamani hapo wakati akitoa ushahidi wake kwamba, hakuwahi kufanya ngono na mtu mwingine yoyote maishani mwake, tofauti na mshtakiwa huyo.

Wakati mshtakiwa Munisi, akitoa utetezi wake akiongozwa na Wakili Elia Kiwia, alidai hakuwahi kuwa na uhusiano wowote wa kimapenzi na mwanafunzi huyo, wala hakuwahi kufanya ngono naye.

Mshtakiwa huyo alijitetea kwamba alibambikiziwa kesi hiyo, baada ya kiongozi mmoja, kumlazimisha ajiunge na Chama Cha Mapinduzi (CCM) alipokataa, ndipo akambambikizia kesi hiyo namba 127 ya mwaka 2019.

Chanzo: IPP MEDI

Chanzo: IPP MEDIA
Kazi ya Dc sabaya ya kubambikizia watu kesi
 
Pole Sana diwani kwa mkasa huo, ulikataa kufanywa bidhaaa, ulisimama na chadema, haukutaka kuwa msaliti.
Sasa kituo kinachofuata kafungue kesi mahakama kuu kudai fidia Ili huyo Mwanafunzi na waliomtuma wakulipe fidia.
 
MEKO afadhari amekufa,maana alikuwa ni kiongozi mkatili kuwahi kutokea katika historia ya Tanzania. Ashukuriwe Mungu wa mbinguni kwa uamuzi wake, maana sisi watanzania tulishashindwa .MATAGA wapo tu kimya wanaendelea kumlilia dikteta wao
 
NOMA SANA AISEEE,MAMBO YA AJABU KABISA,DIWANI ADAI FIDIA TU AJICHUKULIE MKWANJA WAKE KWA ULAINIII
 
Back
Top Bottom