Hahaa

winston20

JF-Expert Member
Jun 21, 2020
1,117
2,256
Jamaa flani alikuwa amelala na mkewe. Mara akamuona mtu amesimama kitandani.
Jamaa akafoka, "Toka hapa, we ni nani mpaka unakuja kitandani mwangu?"
Yule mtu akajibu, "Mi ni malaika na hapa sio kitandani mwako uko mbinguni!"
Jamaa, "Huh! Inamaana nimekufa,mbona mi bado kijana… naomba nirudishwe!"
Malaika, "Inawezekana lakini siwezi kukurudisha kama mtu labda urudi kama mbwa ama kuku."
Jamaa akakumbuka mbwa wanavyopata taabu ya kulinda, akaonelea arudi kama kuku.
Malaika akamgeuza kuku, akamwambia ajifunze kutaga kabla hajapelekwa duniani.
Akachuchumaa na kuanza kujikamua; yai la kwanza likatoka. akajikamua tena, yai la pili likatoka. Akajikamua tena mara ya tatu.
Wakati yai la tatu linatoka… akashtukia amepigwa konde likifuatia na sauti ya hasira ya mkewe, "Pumbav*! Balaa gani hii…. unakuny* kitandani!!"
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom