Ikulu, Chamwino: Rais Samia Suluhu Hassan amwapisha Dkt. Philip Mpango kuwa Makamu wa Rais wa JMT

Elisha Sarikiel

JF-Expert Member
Aug 29, 2020
889
1,515
Mubashara:
Mhe.Dkt. Philip Isdori Mpango ameapishwa kuwa makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Jaji mkuu wa Tanzania mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma katika lkulu, Chamwino Mkoanii Dodoma na kushuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania, mhe. Samia Suluhu Hassan.

Update:
Anasubiriwa mhe. Samia Suluhu Hassan kuingia na kiapo kuanza.

mpango.jpg

Saa15:11- Mhe. Dkt. Mpango akiapa.


Saa 15:13 akienda kukalia kiti cha makamu wa Rais.

Mhe.Rais Samia Suluhu Samia, amempongeza mhe. Dkt. Mpango kwa kushika wadhifa huo wa makamu wa Rais na ameeleza kuwa baada ya kupitia majina mbalimbali ameona jina la Dkt. Isdori Mpango anafaa kushika wadhifa huo kutokana na historia ya uchapakazi wake, ucha Mungu na utulivu. Pia, kutokana na sifa hizo anatarajia pamoja na majukumu mengine, Dkt .Mpango amsaidia katika uchumi,udhibiti wa fedha za serikali kwa kuwa masuala ya Munngano yapo katika Ofisi yake atashughulikia ajenda iliyokwama ya uhusiano wa kifedha katika Muungano.

Naye Mhe. Dkt Mpango amemshukuru Mhe. Rais Samia kwa imani yake kwake na ameahidi kuwa atakuwa msaidizi mwaminifu na mtiifu kwa Mhe. Rais na nchi ya Tanzania. Ameongeza kuwa yupo tayari kuchapakazi mchana na usiku, kushirikiana na viongozi wengine na amesisitiza kuwa watanzania hawana hofu na uongozi wa Mhe. Rais Samia.

Salamu kuu za Rais Samia kwa umma kutangaza mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania







Viongozi mbalimbali waliohudhuria tukio hili ni Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hiussein Ali Mwinyi; Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe.Kassim Majaliwa; Makamu wa pili Rais wa Zanzibar, mhe. Hemed SuJeiman Abdulfa, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanznia,mhe. Job Yustino; Jaji mkuu wa Zanzibar mhe. Omar Othman Makungu; mawaziri na manaibu waziri na viongozi wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama. Viongozi wengine ni mawziri wakuu wastaafu mhe. John Samweli Malecela; mhe.Mizngo Pinda; makamu mwenyekiti wa CCM Bara Ndg. Philip Mangula, na wajumbe wa kamati Kuu ya CCM; Wabunge, na viongozi wa dini na viongozi wa taasisi mbalimbali.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Yustino Ndugai na Jaji na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma wamempongeza Mhe. Dkt. Mpango kwa kushika wadhifa huo na wameahidi kumpa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake
 
Back
Top Bottom