Hadithi ya umslopagaas

SURA YA 24


Mwaka mzima umepita tangu rafiki yangu mpenzi Allan Quatermain alipoliandika neno lile ‘’Nimesema’’ mwisho wa taarifa ya mambo yaliyotupata.


Nisinge penda kuyaongeza maneno yake, lakini kwa namna ya ajabu ipo, njia ambayo kwayo labda maandiko yake yataweza kupelekwa Uingereza.

Kweli ni jambo la kubahatisha tu, lakini Bwana Good na mimi tunafikiri afadhali na tubaatishe, kwa muda wa miezi sita wameshughulika katika mipaka ya Zuvendi ili waone kwamba ziko njia nyingine za kutokea na kuingilia katika nchi hii, na moja imeonekana.


Njia hii ndiyo ile aliyopita Yule mtu maskini aliyefika kwa Bwana Mackenzie, nayo ilijulikana na makuhani wa nchi tu, wakaificha kabisa.

Sasa njia hii itazibwa kabisa, lakini kabla ya kuiziba tunapeleka tarishi ayachukue maandiko ya Bwana Allan Quatermain na barua kadha wa kadha toka kwa Bwana Good, kwa rafiki zake, na toka kwangu kwenda kwa ndugu yangu George Curtis.

Nasikitika sana ya kuwa sitamuona tena ndugu yangu, na katika barua yangu namwambia kwa kuwa yeye ni mrithi wangu, basi azichukue mali zangu zote.


Lakini sasa nataka kuongeza maneno kidogo juu ya mzee Quatermain. Alifariki asubuhi na mapema siku iliyofuata ile ambayo aliyaandika maneno ya mwisho ya sura iliyotangulia. Nyleptha, Bwana Good na mimi tulikuwapo alipofariki.


Saa moja kabla hakujapambazuka ilikuwa dhahiri ya kuwa anakufa, tukahuzunika mno.
Kulipopambazuka, aliomba ainuliwe aweze kulioa jua mara ya mwisho linavyotoka, akalitazama sana kwa muda, kisha akasema, ‘’Katika muda wa dakika chache nitakuwa nimekwisha ipita milango ile ya dhahabu.


Ninakwenda safari ya ajabu kupita zile zote tulizokwenda pamoja. Mungu awabariki, nitawangojea huko.’’ Akaugua, akalala, akafariki dunia.


Basi, hivyo ndivyo alivyo fariki mtu ambaye nadhani tabia yake ilikuwa nzuri kuliko tabia za watu wote niliopata kuonana nao. Bwana Good alisoma ibada ya kuzika wafu, na Nyleptha na mimi tulikuwapo.

Kisha kwa kuwa watu wote waliomba sana, maiti yake ilichukuliwa kwa sherehe nyingi na kuchomwa moto kama ilivyo desturi ya Wazuvendi.

Basi, dakika chache kabla ya kushuka jua, maiti iliwekwa juu ya milango ya shaba mbele ya madhabahu, tukasimama huko kuungojea mwali wa mwisho wa jua linaloshuka.


Halafu mwali wa mwisho ulipenya dirishani, ukauangazia uso wake kama mshale wa dhahabu, ukafanya kama taji ya dhahabu juu ya paji lake, ndipo panda zililia, na milango ilifunguka, na maiti ya rafiki yetu mpenzi ilianguka chini motoni .

Basi, huu ulikuwa mwisho wa maisha ya ajabu ya mwindaji Quatermain. Tangu mambo hayo yalipotokea, tumestawi sana.


Bwana Good anashughulika kuunda merikebu za vita za kusafiri katika ziwa la Milosis, na ziwa jingine, na kwa merikebu hizo tunatumaini kuzidisha biashara na kuwatuliza watu wengine wenye matata wanaokaa kando kando ya maziwa hayo.


Maskini Bwana Good! Mara nyingi huuzunika sana kwa kile kifo kibaya cha Malkia Sorais, maana alimpenda sana.


Lakini natumaini ipo siku machungu yake yataisha na kuhuzunika kwake kutaisha. Maana Nyleptha anamtafutia mke atakayemfaa. Na kwa habari zangu mimi, nadhani afadhali nisijaribu kuzisimulia, maana sijui nianzie wapi.

Cheo changu cha Kifalme kina madaraka makubwa sana, lakini natumaini kufanya mema siku zote, nami nimekusudia mambo mawili makubwa, yaani kuunganisha sehemu mbalimbali za wenyeji chini ya serikali yenye nguvu, na kuzipunguza sana nguvu za makuhani.

Na baadaye, Mungu akinijalia, natumaini kuweka tayari njia ya kuiondoa dini isiyo ya akili ya kuliabudu jua na kuingiza dini ya kweli ya Kikristo.

Kwa heri,

HENRY CURTIS.

Nilisahau kusema ya kuwa zamani za miezi sita, Nyleptha alijifungua mtoto mwanaume mzuri sana nadhani atakuwa mrithi wangu.

HC.


MAELEZOYA BWANA GEORGE CURTIS

Hati ya maandiko hayo yenye anwani yangu iliyoandikwa kwa mkono wa ndugu yangu mpenzi Henry Curtis ambaye nilifikiri kuwa amekwisha kufa, iliniwasili salama. Ilichukua muda wa miaka miwili kinifikia.

Nimeyasoma kwa ushangao, na ingawa sasa nimefarijika kujua kuwa yeye na Bwana Good wako hai, lakini kwa jinsi wanavyokaa katika nchi ile ya mbali naona ni kama kwamba wamekwisha kufa.

Wamejitenga na Uingereza na rafiki na jamaa zao milele.
Namna hati hii ilivyopata kunifikia sijui, lakini naona kwamba Yule tarishi aliyetumwa alimkabidhi bwana mmojawapo aliyeitia katika posta. Barua zile alizozitaja ndugu yangu hazikuniwasilia, na kwa hivi naona zimepotea njiani.


GEORGE CUTTIS.

MWISHO.
Shukrani sana mkuu, hakika umefanya kazi inayostahili pongezi
 

Similar Discussions

21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom