Hadithi ya umslopagaas

SURA YA 21


Tulipofika juu ya mwinuko tulisimama kidogo ili farasi wetu wapumzike kidogo, tukageuka kutazama vita chini yetu. Miali mikali ya jua lililokuwa likishuka liliangaza pote ikapatia wekundu.


Mzee Umslopagaas akasema, ‘’Tumeshinda! Tazama jeshi la ‘Bibi wa Usiku’ linarudi nyuma kila upande, wala halina imani tena, linapindika kama chuma kilichoyeyuka, tena watu wake wanapigana kwa nusu ya mioyo tu.


Lakini, ole wetu, vita havitakwisha kwa kushinda upande huu wala huu, maana giza linaingia na vikosi havitaweza kufuatafuata na kuua!’’ Akatikisa kichwa chake kwa huzuni.

‘’Lakini nadhani askari zake hawatapigana tena, maana wamekwisha ona kuwa nguvu zetu ni nyingi. Ah! I vyema kuishi. Leo nimepata kuona vita vilivyostahili kupiganwa, nami nimeona vita vingi.’’

Basi, huku nyuma tulikuwa tumeianza safari yetu tena, na tulipokuwa tukifuatana kando kando nilimweleza kwa nini tunakwenda Milosis, na jinsi maisha yote yaliyopotea siku hii yatakavyo kuwa yamepotea bure ikiwa hatufanikiwi katika safari yetu, akasema, ‘’Ah!


Lazima tuende mwendo wa maili mia moja kabla hakujapambazuka hali tunao farasi wawili hawa tu! Haya basi, mbio! Mbio! Mwanadamu anaweza kujaribu tu, Makumazahn, na labda tutawahi kufika kwa wakati unaofaa na kumpasulia mbali kichwa Yule mchawi (yaani Agon).

Ndiye aliyetaka kutuchoma moto, Yule mganga wa kuleta mvua. Na sasa anataka kumtega mama yangu (Nyleptha). Haya, vyema! Hakika, kama mama yangu yu hai au kama amekufa, nitampasulia mbali kichwa mpaka ndevu zake.


Ndiyo, naapa kwa Chaka nitafanya hivi! Akatikisa Inkosikazi alipokuwa akienda. Sasa giza likawa linazidi kuingia, lakini kwa bahati mwezi ulipanda halafu, tena njia ni nzuri.


Basi, tuliendelea mbele, na wale farasi wawili wenye nguvu walituchukua vizuri kwa hatua ndefu zisizobadilika maili kufuata maili. Hatukusema, ila tuliinama mbele shingoni pa farasi wetu tukazisikiliza pumzi zao zinavyovutwa na kujaza mapafu yao makubwa, na vishindo vya kwato zao. Basi, vivi hivi saa baada ya saa.


Halafu niliona ya kuwa farasi mzuri niliyempanda anaanza kupotewa na nguvu. Nikaitazama saa yangu, ilikuwa karibu saa sita za usiku, na tulikuwa tumemaliza zaidi ya nusu ya safari yetu.


Juu ya mwinuko palikuwa na chemchem niliyoikumbuka nikamwashiria Umslopogaas asimame hapo, maana nilikusudia kuwapumzisha farasi zetu na sisi wenyewe muda wa dakika kumi.

Basi, alisimama, tukashuka katika farasi zetu farasi walisimama wanatweta wakisimama kwanza kwa mguu huu halafu huu, na huku jasho linawatoka na mvuke wao ulionekana kama ukungu katika hewa kimya cha usiku.


Basi nilimwacha Umslopogaas awashike farasi, nikajivuta karibu na chemchem nikanywa maji yake matamu. Kisha, nilijitia maji kichwani na mikononi nikarudi, na Yule Mzulu akaenda naye kunywa maji.

Kisha, tukawachukua farasi wakanywe maji kidogo tu, wala si zaidi lo! Tulishindana nao mno kuwavuta wayaache maji!

Basi, kisha Umslopogaas alinisaidia nipande juu ya farasi na yeye mtu mwenye nguvu akarukia juu yake bila kuvigusa vikuku vya matandiko yake, tukaianza tena safari yetu. Kwanza taratibu mpaka farasi wakazoea, kisha mbio.

Basi, hivyo tulienda mwendo wa maili kumi tena, ndiyo tulipofika kwenye mwinuko wa mwendo wa maili sita au saba. Mara tatu farasi wangu alitaka kuanguka, lakini alipofika juu ya mwinuko alijikaza tena akaenda mbio kuteremka kwa hatua zilizokatika katika na huku anatweta sana.


Tulikwenda mwendo wa maili tatu nne zile mbio kuliko kwanza, lakini niliona ya kuwa ni juhudi ya mwisho ya farasi wangu.

Basi ghafla alishika sana hatamu katikati ya meno yake akaenda mbio sana kadiri ya yadi mia tatu nne, ndipo aliposita hatua mbili tatu akaanguka kichwakichwa, na mimi nilijitupa mbele yake kadiri nilivyoweza.

Nilifanya haraka kusimama nikamtazama farasi wangu, akanitazama kwa macho ya kusikitisha, kisha kichwa chake kikaanguka akaguna, akakata roho.

Moyo wake ulikuwa umepasuka. Umslopagaas alisimama, nikamtazama kwa fadhaa, maana hata sasa bado mwendo wa maili ishirini, tutafika namna gani kabla ya mapambazuko hali tuna farasi mmoja tu?

Ilikuwa kama haiwezekani, lakini nilikuwa nimesahau nguvu za kupiga mbio za Mzee Mzulu. Bila kusema neno akashuka katika farasi akanipandisha mimi.
Shukran mkuu blackstarline, wacha niifaidi kwa uzuri
 
SURA YA 24


Mwaka mzima umepita tangu rafiki yangu mpenzi Allan Quatermain alipoliandika neno lile ‘’Nimesema’’ mwisho wa taarifa ya mambo yaliyotupata.


Nisinge penda kuyaongeza maneno yake, lakini kwa namna ya ajabu ipo, njia ambayo kwayo labda maandiko yake yataweza kupelekwa Uingereza.

Kweli ni jambo la kubahatisha tu, lakini Bwana Good na mimi tunafikiri afadhali na tubaatishe, kwa muda wa miezi sita wameshughulika katika mipaka ya Zuvendi ili waone kwamba ziko njia nyingine za kutokea na kuingilia katika nchi hii, na moja imeonekana.


Njia hii ndiyo ile aliyopita Yule mtu maskini aliyefika kwa Bwana Mackenzie, nayo ilijulikana na makuhani wa nchi tu, wakaificha kabisa.

Sasa njia hii itazibwa kabisa, lakini kabla ya kuiziba tunapeleka tarishi ayachukue maandiko ya Bwana Allan Quatermain na barua kadha wa kadha toka kwa Bwana Good, kwa rafiki zake, na toka kwangu kwenda kwa ndugu yangu George Curtis.

Nasikitika sana ya kuwa sitamuona tena ndugu yangu, na katika barua yangu namwambia kwa kuwa yeye ni mrithi wangu, basi azichukue mali zangu zote.


Lakini sasa nataka kuongeza maneno kidogo juu ya mzee Quatermain. Alifariki asubuhi na mapema siku iliyofuata ile ambayo aliyaandika maneno ya mwisho ya sura iliyotangulia. Nyleptha, Bwana Good na mimi tulikuwapo alipofariki.


Saa moja kabla hakujapambazuka ilikuwa dhahiri ya kuwa anakufa, tukahuzunika mno.
Kulipopambazuka, aliomba ainuliwe aweze kulioa jua mara ya mwisho linavyotoka, akalitazama sana kwa muda, kisha akasema, ‘’Katika muda wa dakika chache nitakuwa nimekwisha ipita milango ile ya dhahabu.


Ninakwenda safari ya ajabu kupita zile zote tulizokwenda pamoja. Mungu awabariki, nitawangojea huko.’’ Akaugua, akalala, akafariki dunia.


Basi, hivyo ndivyo alivyo fariki mtu ambaye nadhani tabia yake ilikuwa nzuri kuliko tabia za watu wote niliopata kuonana nao. Bwana Good alisoma ibada ya kuzika wafu, na Nyleptha na mimi tulikuwapo.

Kisha kwa kuwa watu wote waliomba sana, maiti yake ilichukuliwa kwa sherehe nyingi na kuchomwa moto kama ilivyo desturi ya Wazuvendi.

Basi, dakika chache kabla ya kushuka jua, maiti iliwekwa juu ya milango ya shaba mbele ya madhabahu, tukasimama huko kuungojea mwali wa mwisho wa jua linaloshuka.


Halafu mwali wa mwisho ulipenya dirishani, ukauangazia uso wake kama mshale wa dhahabu, ukafanya kama taji ya dhahabu juu ya paji lake, ndipo panda zililia, na milango ilifunguka, na maiti ya rafiki yetu mpenzi ilianguka chini motoni .

Basi, huu ulikuwa mwisho wa maisha ya ajabu ya mwindaji Quatermain. Tangu mambo hayo yalipotokea, tumestawi sana.


Bwana Good anashughulika kuunda merikebu za vita za kusafiri katika ziwa la Milosis, na ziwa jingine, na kwa merikebu hizo tunatumaini kuzidisha biashara na kuwatuliza watu wengine wenye matata wanaokaa kando kando ya maziwa hayo.


Maskini Bwana Good! Mara nyingi huuzunika sana kwa kile kifo kibaya cha Malkia Sorais, maana alimpenda sana.


Lakini natumaini ipo siku machungu yake yataisha na kuhuzunika kwake kutaisha. Maana Nyleptha anamtafutia mke atakayemfaa. Na kwa habari zangu mimi, nadhani afadhali nisijaribu kuzisimulia, maana sijui nianzie wapi.

Cheo changu cha Kifalme kina madaraka makubwa sana, lakini natumaini kufanya mema siku zote, nami nimekusudia mambo mawili makubwa, yaani kuunganisha sehemu mbalimbali za wenyeji chini ya serikali yenye nguvu, na kuzipunguza sana nguvu za makuhani.

Na baadaye, Mungu akinijalia, natumaini kuweka tayari njia ya kuiondoa dini isiyo ya akili ya kuliabudu jua na kuingiza dini ya kweli ya Kikristo.

Kwa heri,

HENRY CURTIS.

Nilisahau kusema ya kuwa zamani za miezi sita, Nyleptha alijifungua mtoto mwanaume mzuri sana nadhani atakuwa mrithi wangu.

HC.


MAELEZOYA BWANA GEORGE CURTIS

Hati ya maandiko hayo yenye anwani yangu iliyoandikwa kwa mkono wa ndugu yangu mpenzi Henry Curtis ambaye nilifikiri kuwa amekwisha kufa, iliniwasili salama. Ilichukua muda wa miaka miwili kinifikia.

Nimeyasoma kwa ushangao, na ingawa sasa nimefarijika kujua kuwa yeye na Bwana Good wako hai, lakini kwa jinsi wanavyokaa katika nchi ile ya mbali naona ni kama kwamba wamekwisha kufa.


Wamejitenga na Uingereza na rafiki na jamaa zao milele.
Namna hati hii ilivyopata kunifikia sijui, lakini naona kwamba Yule tarishi aliyetumwa alimkabidhi bwana mmojawapo aliyeitia katika posta. Barua zile alizozitaja ndugu yangu hazikuniwasilia, na kwa hivi naona zimepotea njiani.


GEORGE CUTTIS.

MWISHO.
Wakuu

Sir Henry alikua anaandika aisee, daah. Nimebaki nimestaajabu
 

Similar Discussions

21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom