blackstarline
JF-Expert Member
- Sep 19, 2016
- 3,089
- 7,466
MAAJABU YALIYOWAPATA ALLAN QUATERMAIN NA WENZAKE
HADITHI YA UMSLOPAGAAS
SURA YA KWANZA
SIKU saba zilikuwa, zimepita tangu mwana wangu mpenzi alipozikwa na jioni ilipofika, nilikuwa Nikitembea huko na huko chumbani mwangu nikifikiri, mara mlango unabishwa, Nikaenda nikaufungua mlango mwenyewe, Kumbe rafiki zangu wa zamani Sir Henry Curts na Bwana John Good wapo nje.
Niliwakaribisha ndani wakaingiaa chumbani. Wakakaa mbele ya moto uliokuwa ukiwaka humo.
‘’Mmefanya vyema kuja kunitazama.’’
Hawakujibu neno, ila Sir Henry alishindilia tumbako katika kiko chake akakiwasha kwa kaa alilolitoa motoni, Alipokuwa akiinama mbele kufanya hivyo moto, uliwaka zaidi ukaangaza chumbani, nikafikiri jinsi alivyo mtu mzuri mno.
Uso wake mtulivu wenye nguvu, sura yake thabiti, macho yake makubwa ya kijivu ndevu na nywele zake rangi ya manjano.
Sura yake yote ilikuwa ya mtu aliye bora, tena umbo lake halikuwa kinyume cha uso wake, Sijapata kuona mabega mapana, zaidi wala kifua kinene kama chake.
Umbo la Sir Henry ni pana, ingawa ni mrefu wa futi sita na inchi mbili lakini haonekani kuwa mrefu nilipokuwa nikimtazama hivi, sikuweza kujizuia nisifiri namna mimi nilivyo mwembamba mfupi na namna nilivyohitilafiana na uso wake mzuri, na umbo lake bora.
Embu wazeni basi juu ya mtu mfupi aliyesinyaa, mwenye uso wa rangi ya manjano na umri wa miaka sitini na mitatu mwenye mikono membamba, macho makubwa ya kahawia, kichwa kimefunikwa na nywele zinazoingia mvi na kusimama wima kama brashi iliyotumika, kiasi uzani wake pamoja na mavazi aliyovaa ratili mia moja thelathini na mbili tu.
Basi hapo ndipo mtakapofahamu namna alivyo Allan Quatermain, ambaye kwa desturi huitwa Mwindaji Quatermain, na Waafrika humwita ‘’Makumazahn,’’ maana yake akeshaye usiku, yaani mtu mwerevu asiyedanganyika.
Tena, yupo Bwana Good ambaye hafanani na Sir Henry wala na mimi maana ni mfupi, mweusi kidogo, mnene mnene sana ana macho meusi yang’aayo na katika jicho moja siku zote huvaa rodi, yaani miwani ya jicho moja.
Nilisema yeye ni mnene, lakini neno hilo halitoshi kueleza namna alivyo mnene. Sir Henry humwambia ya kuwa amenenepa hivi kwa sababu yu mvivu, tena anakula sana, ingawa Bwana Good hapendezwi kwa maneno yake , lakini hawezi kuyakana.
Tulikaa kwa muda mfupi, kisha niilichuka kiberiti ili niiwashe taa, kwa sababu niiona giza linachosha, maana ndivyo inavyoelekea hasa ikiwa muda wa siku saba tu umepita tangu mtu alipozika tumaini la maisha yake.
Huku nyuma Sir Henry na Bwana Good walikuwa wamekaa kimya, wakiona nadhani, ya kuwa hawana la kusema linaloweza kunifariji, wakaridhika kunifariji kwa kuwapo kwao ni rambirambi zao za kimya.
Ni kweli ya kuwa twapata tumaini na faraja katika saa za majonzi kwa kuwapo wengine, wala si kwa maongezi yao ambayo huelekea kutuudhi tu. Wakakaa wakivuta tumbako, na mimi nilisimama mbele ya moto nikivuta tumbako pia na kuwaangalia.
Halafu kidogo nilisema, ‘’Je rafiki zangu wa zamani, tangu tuliporudi toka nchi ya Ukukuana hata leo, miaka mingapi imepita? ‘’Bwana Good akasema, ‘’Miaka mitatu. Kwa nini unauliza?’’.
Nikajibu, ‘’Nauliza kwa sababu nafikiri ya kuwa muda niiokaa pamoja na watu mijini umenitosha kabisa, Nitarudi mwituni tena.’’
Hapa Sir Henry alikipeleka nyuma kichwa chake, akacheka mcheko wake wa kindani, akasema, ‘’Ama ni ajabu sana, sivyo Good?’’
Bwana Good akaniangalia, na huku anacheka katika rodi yake, kama kwamba anaficha siri, akasema, ‘’Ndiyo, ajabu sana ajabu kweli kweli.’’
Mimi ni mtu asiyependa mafumbo na mambo ya sirisiri, basi niliwatazama mmoja mmoja, kishanikasema, ‘’Siwezi kufahamu vizuri,’’
Sir Henry akasema, ‘’Hufahamu? Basi, nitaeleza. Good na Mimi tulipokuwa tukija hapa tuliongea.’’
Nikayakatiza maneno yake kwa ukali kidogo, nikasema, ‘’Nadhali kama Good alikuwapo, hamkosi mliongea maana Good ni mtu apendaye sana maongezi. Je, mliongea habari gani?’’
Sir Henry, akauliza, ‘’Ee wafikiri tuliongea habari gani?’’
Nikatikisa kichwa changu.
Haiwezekani nikajua Good aliongea nini, maana mara nyingi huongea habari za mambo mengi.
Sir Henry akasema, ‘’Tuliongea juu ya shauri dogo nililoliwaza yaani kama wewe utakubali tutafunga mizigo yetu na kuiendea nchi ya Afrika kufanya safari nyingine,’’
Nilipoyasikia maneno yake, nilishtuka sana, nikasema, ‘’Ni kweli usemayo?’’ akajibu, ‘’Ni kweli, na Good naye amekubali pia, sivyo Good?’’
Na yeye akaitikia, ‘’Ndiyo.’’
Basi, Sir Henry akaendelea, na sauti yake ilionyesha namna anavyoona hamu, akasema, ‘’Nami pia nimechoka kukaa bure kiubwana katika nchi iliyokinai mabwana.
Kwa muda wa mwaka mzima na zaidi nimekuwa nikitukutika kama tembo mzee anusaye batari.
Kila mara ninaota ndoto za nchi ya Ukukuana, na bibi kichawi Gagula, na Mashimo ya Mfalme Sulemani. Nakuambia ya kuwa nimenaswa na hamu nisiyoweza kuieleza.