Hadithi ya umslopagaas

blackstarline

JF-Expert Member
Sep 19, 2016
3,091
7,468
MAAJABU YALIYOWAPATA ALLAN QUATERMAIN NA WENZAKE
HADITHI YA UMSLOPAGAAS

SURA YA KWANZA


SIKU saba zilikuwa, zimepita tangu mwana wangu mpenzi alipozikwa na jioni ilipofika, nilikuwa Nikitembea huko na huko chumbani mwangu nikifikiri, mara mlango unabishwa, Nikaenda nikaufungua mlango mwenyewe, Kumbe rafiki zangu wa zamani Sir Henry Curts na Bwana John Good wapo nje.

Niliwakaribisha ndani wakaingiaa chumbani. Wakakaa mbele ya moto uliokuwa ukiwaka humo.

‘’Mmefanya vyema kuja kunitazama.’’

Hawakujibu neno, ila Sir Henry alishindilia tumbako katika kiko chake akakiwasha kwa kaa alilolitoa motoni, Alipokuwa akiinama mbele kufanya hivyo moto, uliwaka zaidi ukaangaza chumbani, nikafikiri jinsi alivyo mtu mzuri mno.

Uso wake mtulivu wenye nguvu, sura yake thabiti, macho yake makubwa ya kijivu ndevu na nywele zake rangi ya manjano.

Sura yake yote ilikuwa ya mtu aliye bora, tena umbo lake halikuwa kinyume cha uso wake, Sijapata kuona mabega mapana, zaidi wala kifua kinene kama chake.

Umbo la Sir Henry ni pana, ingawa ni mrefu wa futi sita na inchi mbili lakini haonekani kuwa mrefu nilipokuwa nikimtazama hivi, sikuweza kujizuia nisifiri namna mimi nilivyo mwembamba mfupi na namna nilivyohitilafiana na uso wake mzuri, na umbo lake bora.

Embu wazeni basi juu ya mtu mfupi aliyesinyaa, mwenye uso wa rangi ya manjano na umri wa miaka sitini na mitatu mwenye mikono membamba, macho makubwa ya kahawia, kichwa kimefunikwa na nywele zinazoingia mvi na kusimama wima kama brashi iliyotumika, kiasi uzani wake pamoja na mavazi aliyovaa ratili mia moja thelathini na mbili tu.

Basi hapo ndipo mtakapofahamu namna alivyo Allan Quatermain, ambaye kwa desturi huitwa Mwindaji Quatermain, na Waafrika humwita ‘’Makumazahn,’’ maana yake akeshaye usiku, yaani mtu mwerevu asiyedanganyika.

Tena, yupo Bwana Good ambaye hafanani na Sir Henry wala na mimi maana ni mfupi, mweusi kidogo, mnene mnene sana ana macho meusi yang’aayo na katika jicho moja siku zote huvaa rodi, yaani miwani ya jicho moja.

Nilisema yeye ni mnene, lakini neno hilo halitoshi kueleza namna alivyo mnene. Sir Henry humwambia ya kuwa amenenepa hivi kwa sababu yu mvivu, tena anakula sana, ingawa Bwana Good hapendezwi kwa maneno yake , lakini hawezi kuyakana.

Tulikaa kwa muda mfupi, kisha niilichuka kiberiti ili niiwashe taa, kwa sababu niiona giza linachosha, maana ndivyo inavyoelekea hasa ikiwa muda wa siku saba tu umepita tangu mtu alipozika tumaini la maisha yake.

Huku nyuma Sir Henry na Bwana Good walikuwa wamekaa kimya, wakiona nadhani, ya kuwa hawana la kusema linaloweza kunifariji, wakaridhika kunifariji kwa kuwapo kwao ni rambirambi zao za kimya.

Ni kweli ya kuwa twapata tumaini na faraja katika saa za majonzi kwa kuwapo wengine, wala si kwa maongezi yao ambayo huelekea kutuudhi tu. Wakakaa wakivuta tumbako, na mimi nilisimama mbele ya moto nikivuta tumbako pia na kuwaangalia.

Halafu kidogo nilisema, ‘’Je rafiki zangu wa zamani, tangu tuliporudi toka nchi ya Ukukuana hata leo, miaka mingapi imepita? ‘’Bwana Good akasema, ‘’Miaka mitatu. Kwa nini unauliza?’’.

Nikajibu, ‘’Nauliza kwa sababu nafikiri ya kuwa muda niiokaa pamoja na watu mijini umenitosha kabisa, Nitarudi mwituni tena.’’

Hapa Sir Henry alikipeleka nyuma kichwa chake, akacheka mcheko wake wa kindani, akasema, ‘’Ama ni ajabu sana, sivyo Good?’’

Bwana Good akaniangalia, na huku anacheka katika rodi yake, kama kwamba anaficha siri, akasema, ‘’Ndiyo, ajabu sana ajabu kweli kweli.’’

Mimi ni mtu asiyependa mafumbo na mambo ya sirisiri, basi niliwatazama mmoja mmoja, kishanikasema, ‘’Siwezi kufahamu vizuri,’’

Sir Henry akasema, ‘’Hufahamu? Basi, nitaeleza. Good na Mimi tulipokuwa tukija hapa tuliongea.’’

Nikayakatiza maneno yake kwa ukali kidogo, nikasema, ‘’Nadhali kama Good alikuwapo, hamkosi mliongea maana Good ni mtu apendaye sana maongezi. Je, mliongea habari gani?’’

Sir Henry, akauliza, ‘’Ee wafikiri tuliongea habari gani?’’
Nikatikisa kichwa changu.

Haiwezekani nikajua Good aliongea nini, maana mara nyingi huongea habari za mambo mengi.

Sir Henry akasema, ‘’Tuliongea juu ya shauri dogo nililoliwaza yaani kama wewe utakubali tutafunga mizigo yetu na kuiendea nchi ya Afrika kufanya safari nyingine,’’

Nilipoyasikia maneno yake, nilishtuka sana, nikasema, ‘’Ni kweli usemayo?’’ akajibu, ‘’Ni kweli, na Good naye amekubali pia, sivyo Good?’’
Na yeye akaitikia, ‘’Ndiyo.’’

Basi, Sir Henry akaendelea, na sauti yake ilionyesha namna anavyoona hamu, akasema, ‘’Nami pia nimechoka kukaa bure kiubwana katika nchi iliyokinai mabwana.

Kwa muda wa mwaka mzima na zaidi nimekuwa nikitukutika kama tembo mzee anusaye batari.

Kila mara ninaota ndoto za nchi ya Ukukuana, na bibi kichawi Gagula, na Mashimo ya Mfalme Sulemani. Nakuambia ya kuwa nimenaswa na hamu nisiyoweza kuieleza.
 
Nimechoka kupiga kanga na kwale, na sasa nataka kuwinda wanyama wakubwa. Mwaka ule mmoja tuliokaa pamoja katika nchi ya Ukukuana huonekana kama kwamba thamani yake inapita thamani ya jumla ya miaka yote ya maisha yangu.

Labda ni mpumbavu kwa hamu ninayoiona, lakini sina nguvu kuishinda, natamani kwenda, tena sina budi kwenda.’’ Basi alisita kidogo, kisha akaendelea..

‘’Tena, kwa nini nisiende? Sina mke wala baba, wala mama, wala mtoto wakunizuia nisiende. Nikipatikana na ajali, cheo changu na Mali itarithiwa na ndugu yangu George na mwanawe, nao watairithi kwa vyovyote.

Mimi si kitu kwa mtu yeyote.’’ Akasema,
‘’Ah! Nilifikiri utasema hayo. Na wewe Good, mbona wewe unataka kusafiri, unayo sababu?’’

Bwana Good, akasema na huku anajizuia asicheke, ‘’Ndiyo, ninayo sababu. Mimi sifanyi neno bila kuwa na sababu. Lakini ukitaka kujua sababu ya kweli, nitakwambia, ingawa sipendi kukuambia. Ninaanza kuwa mnene zaidi!’’


Basi, nilitia moto kikoni, maana ulikuwa umezimika, ndipo niliposema tena, nikauliza, ‘’Ninyi mmepata kusikia habari za mlima Kenya?’’

Bwana Good akajibu, ‘’Sipajui mahali hapo.’’
Nikauliza tena, ‘’Mmepata kusikia habari za kisiwa kiitwacho Lamu?’’
Bwana Good akajibu, ‘’La.

Ngoja si mahali palipo kaskazini ya Unguja kadiri ya maili mia tatu?’’
Nikasema, ‘’Ndipo. Sikilizeni. Shauri langu ni hili.

Twendeni Lamu, na kutoka huko tutasafiri ndani ya nchi kadiri ya maili mia mbili na hamsini mpaka mlima Kenya. Kutoka mlima Kenya tuendelee mbele tena kusikia habari zake. Kumbuka Mashimo ya Mfalme Sulemani.’’


Kadiri ya majuma kumi na manne yamepita tangu tulipoongea hivyo, na sasa habari hizi zinatokea katika mahali pa namna nyingine kabisa.

Baada ya kufikiri na kuhojiana sana habari, tuliona ya kuwa itafaa kuianza safari yetu kuuendea mlima Kenya mahali karibu na mlango wa mto Tana, wala si Mombasa.

Basi, ikatokea ya kuwa tulipofika Lamu, tuliteremka pwani pamoja na vitu vyetu vyote, na kwa kuwa hatukujua mahali pa kwenda, tulikwenda moja kwa moja mpaka nyumbani kwa Bwana Balozi wa Serikali ya Kiingereza, tukapokewa kwa ukarimu.


Lamu ni mahali pageni kabisa, lakini mambo yanayodumu katika fikira zangu hata leo ni uchafu wake na uvundo wake. Hasa uvundo wake ni mno. Mbele ya jumba la Bwana Balozi ni pwani, au tuseme fungu la matope liitwalo pwani.


Maji ya bahari yapwaapo huacha nafasi wazi , ndipo mahali panapotupwa taka zote za mji. Pia, hapo wanawake huja wakafukia nazi katika matope na kuziacha humo mpaka makumbi yaoze, ndipo huja kuyafukua na kuzitumia nyuzinyuzi zake, yaani usumba, kutengenezea busati na vitu vinginevyo.


Kwa kuwa mambo hayo yameendelea kwa vizazi na vizazi, ni heri hali ya pwani hiyo ilivyo iwaziwe tu kuliko kuelezwa. Katika siku za maisha yangu nimepata kunusa harufu mbaya nyingi, lakini harufu kali iliyotoka pwani ya Lamu tulipokuwa tumekaa juu ya gorofa ya Bwana Balozi inazifanya zote ziwe kama si kitu kabisa.

Si ajabu ya kuwa watu hushikwa na homa Lamu. Lakini hata hivyo mahali hapo pana uzuri wa namna yake ingawa labda utamchosha mtu upesi.

Basi, tulipokwisha kula, tulikaa tukavuta tumbako, na rafiki yetu Balozi mkarimu aliuliza, ‘’Je, ninyi mabwana mnakwenda wapi?’’

Sir Henry akajibu, ‘’Tumekusudia kuuendea mlima Kenya, kisha, kuendelea mbele mpaka mlima Lekakisera. Quatermain amesikia hadithi ya kuwa liko taifa la watu weupe wanaokaa katika nchi za mbali zisizojulikana bado, kupita huko.’’

Bwana Balozi aliyatega masikio yake, akajibu ya kuwa hata na yeye amepata kusikia habari kama hizo.

Nikamuuliza, ‘’je, umesikia nini?’’ Akajibu, ‘’Si nyingi, ila najua ya kuwa zamani, kadiri ya mwaka mmoja, nilipata barua kwa Bwana Mackenzie, mtu wa misioni anayekaa mahali mwisho wa mto Tana panapofikiwa na mitumbwi, naye alitaja habari hizo.’’

Nikamuuliza, ‘’Je, unayo barua hiyo?’’

Akasema, ‘’La, niliitatua; lakini nakumbuka alisema ya kuwa mtu mmoja alifika kwake akasema kwamba alikwenda mbali kadiri ya safari ya miezi miwili kupita mlima Lekakisera, ambao hapana mtu mweupe aliyeufikia yaani kwa kadiri nijuavyo mimi akavumbua huko ziwa liitwalo Laga.

Kisha akaendelea upande wa mashariki ya kaskazi, safari ya mwezi mzima kuvuka jangwa na mbuga na milima mirefu, mpaka alipofika nchi wanapokaa watu weupe wakaao katika nyumba za mawe.

Huko alipokewa kwa ukarimu akakaa kwa muda, mpaka makuhani wa nchi ile walipo chochea habari ya kuwa yeye ni shetani, basi watu wakamfukuza, akasafiri muda wa miezi minane hata akafika mahali alipomkuta Bwana Meckenzie anakufa.
 
Blackstarline naomba nitumie jina lako nitumie pm nipate kukushukuru kwa kuniwezesha kupata simulizi ya mashimo ya selemani naitaji nipost simulizi iyo kwenye page yangu facebook nitakuwa natenda haki nikikutaja shukrani
 
Blackstarline naomba nitumie jina lako nitumie pm nipate kukushukuru kwa kuniwezesha kupata simulizi ya mashimo ya selemani naitaji nipost simulizi iyo kwenye page yangu facebook nitakuwa natenda haki nikikutaja shukrani
Hakuna shida wewe iweke tu popote unapoona pana faa, nadhani itakuwa faida kwa watu wote wanao penda Hadithi napia ni akiba kwa vizazi vijazo. But usiwe lagai ukauzia watu.
 
Huko alipokewa kwa ukarimu akakaa kwa muda, mpaka makuhani wa nchi ile walipo chochea habari ya kuwa yeye ni shetani, basi watu wakamfukuza, akasafiri muda wa miezi minane hata akafika mahali alipomkuta Bwana Meckenzie anakufa.
Inaendelea tulipo ishia..

Basi, hivyo ndivyo nilivyosikia, na hizo ndizo habari ninazozijua. Mimi nasadiki ya kuwa ni uwongo mtupu lakini ukitaka kujua habari zaidi, afadhali uufuate mto Tana mpaka mahali hapo anapokaa Bwana Mackenzie, ukamuulize yeye habari hizo.’’

Sir Henry na mimi tulitazamana, maana sasa tumekwisha pata habari za kuzithibitisha zile tulizokwishazisikia. Nikasema, ‘’Nadhani tutakwenda kwa Bwana Mackenzie.’’

Bwana Balozi akasema, ‘’Vyema, ni shauri linalowafaa zaidi, lakini nawaonya ya kuwa labda safari yenu itakuwa ya matata, maana nimesikia kuwa Wajivuni wanatembeatembea huko, nao kama mjuavyo si watu wapole.


Shauri litakalofaa zaidi ni kuchagua watu wachache wenye sifa nzuri wawe watumishi na wawindaji wenu na kuajiri wapagazi kuichukua mizigo yenu toka mji mpaka mji.

Jambo hli litawasumbua, lakini nadhani litakuwa shauri jema na rahisi kuliko kuajiri wapagazi kufuatana nanyi safari nzima, tena udhia wa wapagazi kutoroka utapungua.’’

Kwa bahati yetu, walikuwapo Lamu askari wa Kikazi wachache. Wakazi wamefanana na Wajivuni ni watu hodari wenye nguvu, wenye tabia nyingi njema kama zile za Wazulu, tena ni wawindaji hodari.

Watu hawa walikuwa wamekwenda safari ndefu pamoja na Mwingereza aliyetoka Mombasa akasafiri kuuzunguka mlima Kilimanjaro.


Mwingereza huyo maskini alikufa kwa ugonjwa wa homa wakati alipokuwa akirudi. Alikuwa amekwisha fika karibu na Mombasa ; ilibaki Safari ya siku moja tu.

Basi, wawindaji wake walimzika, kisha wakaja mpaka Lamu katika jahazi.
Rafiki yetu Bwana Balozi alitushauri afadhali tujaribu kuwaajiri watu hao, na kwa hivi asubuhi yake tulifuatana na mkalimani wetu tukaenda ili tujaribu kupatana nao.


Tuliwakuta katika nyumba mwisho wa mji. Watatu walikuwa wamekaa nje ya nyumba, nao walikuwa watu wazuri wanaonekana kama kwamba wanaweza kutumainiwa.


Tuliwaambia sababu tuliyowaendea, na kwanza hawakukubali hata kidogo. Walisema ya kuwa hawawezi kabisa kwenda pamoja nasi, ya kuwa wamechoka kabisa kwa safari ndefu, tena mioyo yao ni mizito kwa kufiwa na bwana wao. Walikusudia kurudi makwao wakapumzike kwa muda.


Nikawauliza wenzao wako wapi, maana niliambiwa ya kuwa wako sita, nahapo niwatatu tu. Mmoja wao akasema, ‘’Wamo ndani ya nyumba wamepumzika baada ya taabu waliyopata. Usingizi unawaelemea machoni ni bora walale usingizi, maana usingizi huleta usahaulifu.’’ Lakini walikubali kuwaamsha.


Baadaye kidogo wale watatu wengine walitoka nyumbani, wanapiga miayo watu wawili wa kwanza walikuwa wa kabila lile lile na namna ile ile ya wale tuliowakuta wamekaa nje ya nyumba, lakini Yule watatu alinifanya nishtuke mno.


Alikuwa mtu mrefu sana, nakisia urefu wake ulikuwa kadiri ya futi sita na inchi tatu, lakini mwembamba, na viungo vyake vilikuwa na nguvu kama nyuzi za chuma.

Mara nilipomtazama nilitambua ya kuwa huyu si Mkazi ni Mzulu halisi. Alitoka, na huku ameuweka mkono wake mwembamba mbele ya uso wake kukiziba kinywa chake alipokuwa akipiga miayo, nikaona ya kuwa ni mtu mzima, naye ana shimo lenye pembe tatu katika paji la uso wake.

Kisha, aliuondoa mkono wake, nikaona uso wa nguvu wa Kizulu, na kinywa cha ucheshi, na ndevu fupi zenye mvi kidogo, macho ya kahawia makali kama ya mwewe.


Nikamtambua mara ile, ingawa nilikuwa sijamwona kwa muda wa miaka kumi na miwili. Nikasema kwa sauti ndogo kwa lugha ya Kizulu, ‘Hujambo Umslopogaas?’’

Mtu huyo mrefu, ambaye hadithi zake nyingi zilisimuliwa katika nchi ya Wazulu, na ambaye katika watu wake huitwa ‘’Gogota,’’ na ‘’Mchinjaji’’ alishtuka, na shoka lake la vita lenye kipini kirefu lilikuwa karibu kumponyoka kwa mshangao.
 
Mara ile alinitambua akawa ananiamkia.
‘’Mkuu, mkuu wa zamani. Mkuu, mkuu! Baba! Makumazahn, mzee mwindaji, muuaji wa tembo, mla simba, mwerevu akeshaye! Hodari, mwepesi! Ambaye risasi zake kabisa hazikosi shabaha, apigaye shabaha ya kweli, rafiki mwaminifu.

Mkuu! Baba! Ile methali ya kikwetu isemayo ‘’Milima haikutani lakini wanadamu hukutana,’ ni ya kweli kabisa na yenye busara.

Tazama! Tarishi alikuja toka Natal, akalia, ‘Makumazahn amekufa! Nchi haitamwona Makumazahn tena.’ Haya yalitokea zamani sana.

Na sasa, tazama hapa katika nchi ngeni ya harufu mbaya namwona tena Makumazahn, rafiki yangu.

Ndiye bila shaka. Manyoya ya mzee mbweha yameingia mvi; lakini macho yake na meno yake ni makali kama zamani.

Ha! Ha! Makumazahn, unakumbuka namna ulivyoipeleka risasi katika jicho la nyati aliyekuwa akishambulia, unakumbuka?’’

Basi, nilikuwa nimemwacha aendelee hivyo, kwa sababu niliona ya kuwa wale Wakazi watano walionekana kwamba wanaweza kufahamu maneno mengine katika yale aliyosema, tena yanawatia fikira, lakini sasa niliona inafaa kumnyamazisha, maana hakuna kitu kinachonichukiza kuliko desturi ile ya Wazulu iitwayo kubonga, yaani kusifu kupita kiasi.


Nikasema, ‘’Nyamaza! Ala, maneno yako yenye kelele yamezibwa tokea tulipoachana, na hii ndiyo sababu yanabubujika na kutughalikisha hivi? Unafanya nini hapa pamoja na watu hawa, wewe ambaye tulipoachana ulikuwa mfalme katika nchi ya Wazulu?


Umekujaje hapa katika nchi iliyo mbali na kwenu, na kukaa pamoja na wageni?’’

Umslopogaas aliliegemea shoka lake refu la vita, ambalo kipini chake ni kipande kizuri cha pembe ya kifaru, na uso wake ulikuwa umejaa huzuni, kisha akawatazama wale Wakazi, akasema, ‘’Baba yangu, ninazo habari nitakazokuambia, lakini siwezi kusema mbele ya watu wanyonge hawa maneno yangu ni baina ya mimi na wewe tu..

Baba yangu, nitasema haya tu: Mwanamke alinihaini mauti, akalifunika jina langu kwa aibu, ndiyo, mke wangu mwenyewe, mwanamwali mwenye uso kama mwezi, alinihaini, lakini niliokoka na mauti, ndipo nilipoponyoka katika mikono ya wale waliokuja kuniua.


Nilipiga mapigo matatu tu kwa shoka langu hili Inkosikazi hakika baba yangu atalikumbuka moja upande wa kuume, moja upande wa kushoto, na moja mbele yangu, niliwaacha watu watatu wamekufa.


Kisha, nilikimbia, na kama baba yangu ajuavyo, ingawa mimi ni mzee, lakini miguu yangu ni mepesi kwenda mbio kama ile ya paa, wala hapana mtu anyeweza kunigusa tena nikisha mtoka mbavuni pake.

Mbele nilikimbia, na matarishi wa mauti waniandama nyuma, na sauti zao zilikuwa kama sauti za mbwa wanaowinda. Kutoka nyumbani kwangu nilikimbia, nikampita Yule aliyenihaini alikuwa akiteka maji kisimani.


Nilimpita upesi kama kivuli cha mauti, na nilipokuwa nikipita nilimpiga dharuba moja kwa shoka langu, tahamaki! Kichwa chake kilimtoka, kikaanguka kisimani. Kisha, nilikimbilia kaskazini.

Siku baada ya siku nilisafiri; kwa miezi mitatu nilisafiri, nisipumzike, nisisimame, ila nilizidi kukimbilia kwenye usahaulifu, mpaka nilipoonana na safari ya Yule mwindaji mweupe aliyekwisha kufa, nami nimekuja hapa pamoja na watumishi wake.


Wala sikuleta kitu pamoja nami. Mimi aliye mtoto wa watu, ndiyo, wa damu ya mfalme mkuu Chaka, mimi niliye mkuu mwenyewe, jemedari katika kikosi cha Nkomabakosi, sasa mimi ni mgaagaa, mtu asiye na nyumba.

Wala sikuleta kitu pamoja nami ila shoka hili langu, kwa nguvu zake ambazo kwazo niliwatawala watu wangu.

Wamegawanya ng’ombe zangu, watwaa wake zangu na watoto wangu hawautambui uso wangu tena. Hata hivyo, kwa shoka hili hili nitakata njia nyingine nifike mpaka kwenye usitawi. Nimesema! ‘’Basi, akalizungusha shoka lake kichwani likalialia lilipokuwa likiikata hewa.
 
Nilitikisa kichwa changu, nikasema, ‘’Umslopogaas, nimekujua tangu zamani.

Wewe siku zote ulitamani kupata nguvu na uwezo zaidi, tabia hii I katika damu yako, lakini naona ya kuwa umeshindwa safari hii.

Zamani ulipotaka kufanya shauri juu ya Kitswayo bin Mpande, nilikuonya, ukanisikiliza. Lakini nilipokuwa sipo karibu nawe kukuzuia mkono, ulichimba shimo kwa miguu yako mwenyewe kuliangukia sivyo?


Lakini yaliyotendeka yamekwisha tendeka. Na ni nani awezaye kufufua mti uliokwisha nyauka? au kuiangalia nuru iliyokuwako mwaka jana? Nani awezaye kurudisha neno lililokwisha semwa, au kurudisha roho za wale walioangamia? Yale yaliyomezwa na wakati hayarudi tena. Kisa chako na kisahauliwe basi!


‘’Na sasa, tazama, Umslopogaas, nakujua ya kuwa u mtu jasiri wa damu ya kifalme, mwaminifu mpaka kufa.

Hata katika nchi ya Wazulu ambako watu wote ni hodari, walikuita, ‘Mchinjaji,’ na wakati wa usiku walipokuwa wamekaa kuzunguka moto walisimulia hadithi za matendo yako na za nguvu zako.

Nisikilize basi, wamwona mtu mrefu huyu, rafiki yangu’’ nikamwelekezea kidole Sir Henry; ‘’yeye ni mtu jasiri pia kama ulivyo wewe, naye ana nguvu kama ulivyo nazo wewe, aweza kukutupa begani mwake. Jina lake ni Inkubu.


Tena, wamwona huyu; mwenye tumbo, na jicho linalong’aa, na sura ya kuchangamka? Jina lake ni Bougwan, kwa sababu ya rodi anayoivaa jichoni, naye ni mtu mwema mwaminifu.

‘’Basi, sisi watatu unaotuona tunataka kusafiri kupita Dongo Egere, ule mlima mrefu mweupe, na kuingia karibu nchi isiyojulikana.

Hatuna habari za mambo tutakayoona huko; tunakwenda kutafuta matendo ya ujasiri, na kuona mahali papya, kwa kuwa tumechoka kukaa bure na kuzungukwa na mambo yale yale siku zote.

Je, utafuatana nasi? Wewe utakuwa na amri juu ya watumishi wetu wote, lakini yatakayokupata siyajui kamwe.

Zamani sisi watatu tulisafiri pamoja, tukamchukua mtu kama wewe, jina lake Umbopa, tazama, tulipoagana naye alikuwa amekwisha kuwa mfalme wa nchi kubwa, ana majeshi ishirini ya askari, na kila jeshi lilikuwa na askari elfu tatu, waliokuwa wanamngojea kuzitimiza amri zake.

Mambo yatakayo kupata wewe siyajui; labda mauti inakungojea wewe na sisi pia. Je, utashirikiana nasi na kuandamana nasi na kubahatisha ajali, au unaogopa Umslopogaas?’’


Yule mkuu wa zamani alichekelea, akasema, ‘’Maneno yako yote ni ya kweli Makumazahn.

Kweli nimefanya mashauri mengi katika maisha yangu, lakini sikuangamia kwa kutafuta uwezo kupita kiasi; ila ni aibu juu yangu kusimulia kwamba ni uso mzuri wa mwanamke, ndiyo ulioniangusha.

Haya heri na tuyasahau. Basi, tutaona habari kama zile tulizoziona zamani Makumazahn, tulipofika na kuwinda katika nchi ya Wazulu, Ndiyo, nitaenda, kama ni kwa maisha, ama kama ni kwa mauti, ni sawa tu kwangu, mapigo yaanguke upesi na damu imwagike tu.


Ninazidi kuwa mzee na vita nilivyopigana havijanitosha! Nami ni mtu wa vita kuliko watu wa vita, tazama makovu yangu’’ akaonyesha makovu na alama za majeraha zisizo na hesabu, michomi, mikato, iliyokuwapo katika ngozi ya kifua na miguu na mikono yake.


Tazama shimo hili katika paji la uso wangu, ubongo, wangu ulitokeza humu, na hata hivyo nilimuua Yule aliyenipiga, nami ni hai, je, wajua watu wangapi niliowaua katika vita vilivyopiganwa mkono kwa mkono Makumazahn?


Tazama, hii ni hesabu yake’’. Alionyesha mstari mrefu wa michoro katika kipini cha shoka lake, ‘’Zihesabu Makumazahn mia moja na tatu nami sikuwahesabu ila wale niliowatumbua kama ilivyo desturi yetu, wala sikuwahesabu wale. Waliopigwa na mtu mwingine.’’

Basi, nilitambua kuwa anaanza kuona hamu, kumwaga damu, nikasema, ‘’Nyamaza, nyamaza. Unaitwa ‘Mchinjaji’ kwa haki.


Hatutaki kusikia habari zako za kumwaga damu. Kumbuka ya kuwa ukija pamoja nasi, sisi hatupigani isipokuwa kujitetea tu. Sisi tunahitaji watumishi, Wakazi. Hawa wamesema kuwa hawataki kuja pamoja nasi.’’

Umslopogaas akasema kwa sauti kuu, hawa! Yu wapi mbwa anayekataa kuja baba yangu? Wewe’’ akaruka mbele akawarukia wale Wakazi niliosema nao kwanza, akamshika mmoja mkononi akamkokota mbele yetu, akamtikisa hata Yule mtu alitishika sana, akasema.

‘’Wewe mbwa ulisema ya kuwa hutaki kufuatana na baba yangu? Sema maneno yale tena nami nitakukaba koo, wewe na wale walio pamoja nawe.’’

Vidole vyake virefu vilimkaba koo. Kisha akasema .. ‘’Je, umesahau jinsi nilivyomfanyia ndugu yako?’’

Yule mtu akatweta, akasema kwa kigugumizi, ‘’Basi! Basi! Tutafuatana na mtu mweupe huyu.’’

Umslopogaas akafanya kama amefura kwa hasira, akasema, ‘’mtu mweupe! Unamtaja nani mbwa mwenye ufidhuli?

Yule mkazi akajibu upesi, ‘’Basi! Basi! Tutafuatana na bwana mkubwa .’’
Basi, Umslopogaas akatuliza sauti yake, akamwacha Yule mtu akaanguka chini, akasema, ‘’Ndiyo, nafikiri ya kuwa mtafuatana nasi.’’
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom