#COVID19 “Hadithi ya Miji Miwili” toleo la kisasa: michango ya China na Marekani katika kutoa chanjo dhidi ya COVID-19

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
VCG111334776648.jpg
Mwandishi wa riwaya wa Kiingereza Charles Dickens alifungua kitabu chake maarufu cha “Hadithi ya Miji Miwili” (A Tale of Two Cities) kwa kusema “ulikuwa ni wakati mzuri kabisa, pia ulikuwa ni wakati mbaya kabisa.” Sentensi hii inayojulikana sana pia inafaa kuelezea jinsi China na Marekani zinavyotoa chanjo dhidi ya COVID-19 kwa nchi zinazoendelea haswa nchi za Afrika.

Hivi sasa, nchi za Afrika zinajitahidi kutafuta na kupanua uagizaji chanjo kutoka nchi za nje, ili kukabiliana na wimbi kali la tatu la maambukizi na virusi vilivyobadilika vya Delta. Katika wikiendi iliyopita, ushirikiano kati ya China na Afrika ulipata habari nyingi nzuri. Ethiopia, Rwanda, Lesotho na Togo zilipata msaada wa chanjo kutoka kwa China; Kenya iliidhinisha matumizi ya chanjo ya Sinopharm ya China, na dozi milioni 2 zinatarajiwa kuwasili Nairobi mwezi ujao; na Wizara ya Afya ya Misri wiki hii itasambaza chanjo ya Sinovac ya China iliyotengenezwa nchini humo kwa kituo cha usambazaji wa chanjo cha taifa ili itolewe kwa umma, na uwezo wa uzalishaji wa chanjo hiyo nchini humo unaweza kufikia dozi milioni 15 hadi 18 kwa mwezi. Hivi sasa, China inaongoza duniani kwa kutoa chanjo kwa wingi zaidi kwa nchi za nje, idadi ambayo imezidi jumla ya chanjo zilizotolewa na nchi nyingine zote kwa nje. Kati ya nchi zilizopokea chanjo za China kama msaada, theluthi moja ni nchi za Afrika.

Lakini tofauti na China, wakati upatikanaji wa chanjo duniani unakosa usawa na kutokuwa na ushahidi wa kutosha wa kisayansi, nchi nyingi za magharibi zimetangaza kuwa zitatoa dozi ya ziada kwa wananchi ambao tayari wamemaliza kuchanjwa. Juu ya hilo, Shirika la Afya Duniani WHO wiki iliyopita lilifanya mkutano na waandishi wa habari likikosoa kitendo hicho linacholitaja kama ni la kukosa maadili. Mkurugenzi mkuu anayesimamia mipango ya dharura katika WHO Dkt Michael Ryan alisema, “wao wanapanga kuwapa njia za kujiokoa watu ambao tayari wana njia hizo, na wanawaacha mamilioni ya watu wasio na njia za kujiokoa wafe maji.”

Mapema mwezi Agosti, WHO iliwahi kutoa wito kwa nchi hizo kusitisha mpango wa kuongeza chanjo, lakini ilishindwa kuwazuia. Lakini swali ni kuwa dozi nyingi za chanjo namna hiyo zitazalishwa wapi? Hivi karibuni, makala moja iliyochapishwa kwenye Gazeti la The New York Times imefichua ukweli unaoumiza na kukasirisha watu, pengine chanjo itakayotolewa na nchi za magharibi kwa watu waliomaliza kuchanjwa inazalishwa barani Afrika ambako watu wengi hawajapata chanjo.

Makala hiyo inasema chanjo ya Johnson&Johnson ya Marekani inachukuliwa kama ni silaha muhimu ya Afrika kupambana na ugonjwa huo. Kampuni hiyo imezindua mlolongo wa uzalishaji nchini Afrika Kusini na kuahidi kutoa chanjo kwa theluthi moja ya watu wa Afrika. Lakini hili halitokei. Hatusemi ni Afrika, na hata Afrika Kusini, hadi sasa ilipata dozi milioni 2 tu ya chanjo ya Johnson&Johnson, kiasi ambacho ni kidogo sana ikilinganishwa na oda iliyosaini Afrika Kusini na kampuni hiyo ya Marekani.

Makala hiyo inasema kwa mujibu wa kumbukumbu iliyotolewa na maofisa waandamizi wa kampuni ya Johnson, kampuni ya chanjo ya Afrika Kusini Aspen Pharma na serikali ya Afrika Kusini inaonesha kuwa kampuni hiyo inauza mamilioni ya dozi za chanjo hiyo inayotengenezwa nchini Afrika Kusini kwa nchi za Ulaya.

Ni jambo la kawaida kuwa chanjo inayotengenezwa nchini Afrika Kusini ingetolewa kwanza kwa nchi maskini zilizoshiriki kwenye utengenezaji wake, lakini hali halisi ni kama nchi moja inaandaa chakula kwa dunia, lakini chakula chake kinapelekwa kwa sehemu zenye utajiri wa rasilimali, wakati wananchi wa nchi hiyo yenyewe wana njaa.

Inajulikana kuwa nchi nyingi za magharibi zimehodhi chanjo zilizotengenezwa ndani ya nchi hizo. Lakini kadri idadi ya watu wanaohitaji kuchanjwa inapungua, mamilioni ya dozi za chanjo zimepotezwa baada ya muda wake wa kazi kufika. Mtaalamu wa masuala ya mlolongo wa utoaji huduma za matibabu kutoka “Kituo cha Maendeleo Duniani” chenye makao makuu mjini Washington Prashant Yadav, ameviambia vyombo vya habari kuwa “hakuna mtu aliyefuatilia kwa makini kuna dozi ngapi za chanjo ambazo muda wale wa kazi umefika.” Naye mkurugenzi mwandamizi wa sera ya masuala ya afya na elimu duniani wa shirika lisilojipatia faida la Marekani One Campaign, Jenny Ottenhof, amekadiria kuwa katika wiki ama miezi kadhaa ijayo, kutakuwa na mamilioni ya dozi za chanzo ambazo muda wake utapita na kemikali ndani yake kubadilika, na jambo hili la kusikitisha haliwezi barani Afrika Kusini ambako ni asilimia 7 tu ya watu ambao wamemaliza kuchanjwa.

Kwa mujibu wa utafiti wa gazeti la The Times la Uingereza, mwaka huu serikali ya Afrika Kusini ilisaini mkataba usio wa kawaida na kampuni ya Johnson ya Marekani ambao unaitaka Afrika Kusini iache haki ya kuzuia uuzaji chanjo inazotengenezwa ndani ya nchi hiyo kwa nchi za nje. Msemaji wa Wizara ya Afya ya Afrika Kusini Popo Maja, alisema serikali hairidhiki na mkataba huo, lakini haina karata ya kukataa madai hayo. “Serikali haina chaguo lolote, kusaini mkataba ama kutokuwa na chanjo.” alisema katika taarifa moja. Hii imefichua umwamba wa nchi hizo za magharibi, na pia kuonesha hisia za kutokuwa na la kufanya na kukata tamaa kwa nchi hizo za Afrika.

Hali ya ukosefu wa chanjo nchini Afrika Kusini na hata Afrika nzima imeonesha ukosefu wa uwiao wa mamlaka kati ya nchi za magharibi, kampuni zake kubwa na nchi na bara lililokata tamaa. Meneja wa mpango wa kinga mwili na uendelezaji wa chanjo wa ofisi ya WHO kanda ya Afrika Dkt Richard Mihigo alisema, kama hakuna chanjo ya kutosha, asilimia 90 ya nchi za Afrika hazitaweza kutimiza lengo la kuwachanja asilimia 10 ya wananchi ifikapo mwezi Septemba mwaka huu. Amekiri kuwa “kabla ya kusambaza chanjo, kwanza tunatakiwa kuwa na chanjo.”

Tatizo la kukosa usawa katika kupata chanjo ni kikwazo kikubwa kwa dunia kumaliza janga la COVID-19 na kufufuka. Kama viongozi wa nchi za magharibi wanatoa chanjo kwa watu ambao tayari wamemaliza kuchanjwa badala ya kusambaza chanjo kwa nchi maskini, pengo la chanjo kati ya nchi zilizoendelea na zinazoendelea litazidi kuwa kubwa.
 
Back
Top Bottom