Hadithi ya mbwa wa ushuani na uswazi V/S Tafakuri ya siasa za Tanzania kwa sasa.

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
21,567
50,393
Siku moja mbwa wa uswazi akiwa kakonda na manyoya yamenyonyoka kwa kukosa matunzo, alianza kukatiza mitaa akitafuta msosi.

Mbwa huyo alizunguka sana ghafla akajikuta ushuani. Akamuona mbwa wa ushuani akiwa kanona kweli kweli. Shingo shongo na manyoya yake yana afya nzuri na masafi haswa lkn alikuwa na mnyoyororo shingoni ndani ya banda lililo ndani ya fensi.

Mbwa wa uswazi akamshangaa sana mbwa wa ushuani kwa yale maisha ya mnyororo anayoishi. Akamuuliza "kulikoni unashinda na mnyororo shingoni tena ndani ya banda na ndani ya fensi?" Mwenzako mm niko huru natembea bila masharti ndiyo maana niko huku natafuta chakula.

Na mbwa wa ushuani naye alimshangaa sana yule mbwa wa uswazi. Akamuuliza "kulikoni umekonda namna hii ---manyoya yako yamenyonyoka, mbavu zimetokeza na umefika hadi huku kwa kuhangaika kutafuta msosi?" Mwenzako mm naletewa msosi, natibiwa na kuogeshwa.

Tafakari hadithi hii kwa muktadha wa siasa za nchi yetu.
 
Mama anaupiga mwingi
giphy.gif
 
Back
Top Bottom