Hadithi ya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri itaisha lini!? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hadithi ya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri itaisha lini!?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Feb 26, 2012.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,481
  Likes Received: 81,772
  Trophy Points: 280
  Mawaziri 13 kutupwa nje

  Na Jacob Daffi - Imechapwa 15 February 2012
  Mwanahalisi

  RAIS Jakaya Kikwete aweza kufanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri wakati wowote sasa, imefahamika.
  Taarifa kutoka ndani ya serikali zinasema mabadiliko ya baraza hilo yatafuatia kinachoelezwa kuwa ni "kuyumba kwa serikali."
  Mtoa taarifa anasema hatua ya kufanya mabadiliko makubwa au hata kuvunja baraza la mawaziri, inatokana hasa na serikali kushutumiwa mara kwa mara na wananchi kwa kutoonyesha kuwajibika.

  Mambo ambayo yanatajwa kuyumbisha serikali hivi sasa ni pamoja na migomo na maandamano ya kupinga unyimaji haki na stahiki nyingine.
  Mgomo wa madaktari uliochukua wiki tatu na kugharimu maisha ya wananchi, huku watendaji na wanasiasa wakiendeleza malumbano, ni moja ya sababu zinazotajwa.

  Migomo ya wanafunzi wa vyuo vikuu ambayo imeendelea bila ukomo na shinikizo mbalimbali kutoka kwa wapigania haki za binadamu, ni miongoni mwa mambo yanayohitaji "ubongo mpya," ameeleza mtoa taarifa ndani ya serikali.

  MwanaHALISI limeelezwa kuwa baraza la mawaziri linaweza kufanyiwa marekebisho au kuvunjwa na kuundwa upya kwa "lengo la kurejesha hadhi, ufanisi na uwajibikaji serikalini."
  Jingine ambalo linatajwa kuchangia kuwepo uwezekano wa kufanya mabadiliko, ni baadhi ya wizara kuwa na mawaziri ambao hawana afya nzuri na wanahitaji kupewa muda wa kujihudumia.

  Mahali pengine ni kule ambako mawaziri waliopo, ama wanapwaya kiutendaji kwa kutochukua hatua pale panapohusika, au wamejichimbia katika shughuli za binafsi kuliko za serikali.
  "Mnaadika kila siku kuwa Rais Kikwete ni dhaifu; lakini usisahau kuwa udhaifu wa rais si wake binafsi.

  Kwa hiyo akitaka kuuondoa sharti wengine waguswe; kama mawaziri na makatibu wakuu," ameeleza mtoa taarifa serikalini.
  Mabadiliko katika baraza la mawaziri yanaweza kwenda sambamba na mabadiliko katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambayo yalipitishwa na Halmashauri Kuu ya taifa wiki iliyopita.
  Kwa mujibu wa katiba, Rais Kikwete amebakiwa na miaka minne ya ngwe yake ya pili ya utawala.

  Baadhi ya wanaotarajiwa kukumbwa na mabadiliko hayo, ni Waziri wa Afya, Dk. Haji Mponda na naibu waziri, Dk. Lucy Nkya ambao wanadaiwa "kulea" mgomo wa madaktari hadi baadhi ya wananchi kupoteza maisha kwa kukosa tiba.

  Madaktari wanafunzi wapatao 100 walikomalia wizara kuwalipa posho zao ili wapate nauli, chakula na kugharamia makazi yao, lakini wizara ikabakia "njoo kesho" na bila maelezo mwanana.

  Kimya cha wahusika kilichofuatiwa na vitisho vya wizara, kilichochea madaktari wenzao kuunga mkono mgomo wa madaktari wanafunzi.
  Ukaidi wa wahusika na hatimaye vitisho vya waziri mkuu, kulifanya madaktari bingwa kujiunga na wenzao na kudai, siyo posho tu za Sh. 10,000 na 20,000, bali sasa mishahara yao na nyongeza.

  Kushindwa kumaliza mgomo ambao ungesitishwa katika hatua ya awali, kumeleta "jina baya kwa serikali, vifo kwa wananchi, ukosefu wa imani ya madaktari kwa serikali na kumeonyesha uzembe usiomithilika," ameeleza mtoa taarifa.

  "Katika mazingira haya, hata Waziri Mkuu Mizengo Pinda aweza kung'olewa kwa kuwa yote yalifanyika mbele yake; yalifanywa na mawaziri chini yake; na yeye alichochea hasira, ghadhabu na chuki ya madaktari kwa serikali pale alipowakemea huku wakidai stahiki sahihi," ameeleza mtoa taarifa.
  Naye Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja anaweza kuwekwa kando kutokana na kuandamwa na tuhuma kupitia bungeni ambazo zimekuwa ngumu kuzima.

  Ngeleja, pamoja na kutuhumiwa kukusanya na kutumia mamilioni ya shilingi kwa kushirikiana na katibu mkuu wake, David Jairo isivyo halali, wizara yake imekuwa goigoi katika kumaliza tatizo la nishati ya umeme nchini.
  Ripoti ya Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za umma iliyokuwa ikimkabili Jairo, imeonyesha jinsi Ngeleja na naibu wake, Adam Malima, walivyolipwa kiasi kikubwa cha fedha katika mazingira yenye mashaka.

  Wengine wanaotajwa kuwa kwenye mkumbo wa kuwekwa kando ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya, Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Cyrill Chami, na naibu waziri wa ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe.
  Mawaziri hawa wamekuwa wakihudhuria matibabu nchi za nje kwa kipindi kirefu sasa na mtoa taarifa ndani ya serikali anasema "…siyo busara kuendelea kuwaweka ofisini wakati utendaji wao ni mdogo."

  Prof. Mwandosya na Dk. Mwakyembe wamekuwa wakipata matibabu nchini India kwa kipindi kirefu. Naye Dk. Chami ameanza matibabu nchini humo.
  Mawaziri wengine ambao wanatajwa kuachwa iwapo rais atafanya mabadiliko makubwa ni Waziri wa Sheria na Katiba, Celina Kombani, waziri wa maendeleo ya Jamii, Wanawake na Watoto, Sophia Simba na waziri wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta.

  Kombani, Simba na Sitta wanaelezwa kuwa "hawaisaidii serikali." Mtoa taarifa hakueleza jinsi gani mawaziri hawa hawaisidii serikali, isipokuwa alisema "rais mwenyewe anajua."
  Mwingine anayeweza "kwenda na maji" ni waziri wa utawala bora, Mathias Chikawe. Hajajibu tuhuma za kujihusisha katika miradi binafsi kwa mgongo wa serikali.

  Mradi ambao unadaiwa kuwa mbioni kufanikishwa na Chikawe, ni biashara kubwa ya dawa za virutubishovya binadamu kwa wenyevirusi vya ukimwi iitwayo Secoment V.
  Naye Malima, hajajibu tuhuma zinazomkabili za kutaka kuingiza nchi kwenye mkataba tata wa uchimbaji madini ya shaba wilayani Mpanda, mkoa wa Rukwa.
  Mtoa taarifa anasema ni rais mwenyewe anayejua "nani hamfai hapa au pale, lakini watang'oka wengi ili kupata timu ya kumfikisha mwishoni mwa ngwe yake – 2015."

  "Mabadiliko hayo yanatarajiwa kufanyika kabla ya kumalizika mwezi au kama yamechelewa sana, itakuwa mwanzoni mwa Machi," ameeleza mtoa taarifa.
  Amesema, "Rais anahitaji timu mpya itakayokuwa na upya wa mawazo na msukumo katika kuleta mabadiliko haraka."
  "Hili jambo limekuwa likisemwa… hata baadhi ya viongozi, marafiki wa rais na wale wanaomtakia mema yeye na serikali yake, wamekuwa wakimshauri kuchukua uamuzi huo.

  Sasa wakati umefika wa kufanya hivyo," ameeleza waziri mwandamizi ndani ya serikali.
  Baadhi ya wanasiasa wametajwa kuwa huenda wakachukua nafasi zitakazoachwa wazi.
  Miongoni mwa wanaotajwa ni Prof. David Mwakyusa, mbunge wa Rungwe Magharibi, na mbunge wa
  Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi. Hii itakuwa kurejesha uwiano wa viongozi ikiwa Rais Kikwete atampumzisha Prof. Mwandosya na, au Dk. Mwakyembe.
   
 2. A

  August JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2012
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  tukisha pata Ushauri wa "Rose"
   
 3. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #3
  Feb 26, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hata kama akilivunja, hakuna mambo ya maana tutakayopata, kwa sababu tatizo sio balaza la mawazili, tatizo ni yeye mwenyewe chekacheka.
  Kama akiwa ni mzalendo, basi angeachia madaraka, ingekuwa jambo bora sana!
   
 4. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #4
  Feb 26, 2012
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 160
  Hapa kazi ipo ngoja tuone mwisho wake. Ila kiukweli hao Mwakyembe na Mwandosya wameugua mda mrefu sana wajameni mmmmhhh haya
   
 5. i

  iMind JF-Expert Member

  #5
  Feb 26, 2012
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 1,907
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  Sioni haja ya kuvunja baraza la mawaziri. Anaweza kujaza nafasi za hao wagonjwa bila kufanya pangua pangua. Pangua pangua ya mawaziri ni gharama kubwa na pia hurudisha nyuma kasi ya utekelezaji wa mipango mbalimbali, kwa sababu huchukua muda wa miezi 6 hadi mwaka waziri kuielewa wizara na kushiriki kikamilfu katika mipango.

  Bora awaache tu
   
 6. d

  dada jane JF-Expert Member

  #6
  Feb 26, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  iMind mawazo yako hujayafanyia utafiti wa kina.
   
 7. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #7
  Feb 26, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Yafaa mjiulize ana hun muda wa kuliandaa baraza jingine? Kusafiri atasafiri saa ngapi?
   
 8. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #8
  Feb 26, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,049
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  hii ya kupangua baraza la mawaziri imeshakuwa kama hadithi za 'paukwa pakawa' ... magazeti nayo yaache kum-preempt, labda ndio maana anasita kutangaza
   
 9. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #9
  Feb 26, 2012
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,784
  Likes Received: 6,269
  Trophy Points: 280
  Unless huyo ''mtoa taarifa'' ni Kikwete mwenyewe, huu utabaki kuwa uzushi na hisia tu. Sidhani kama Kikwete huwa anajadiliana na mtu wakati anataka kumtema Waziri
   
 10. i

  iMind JF-Expert Member

  #10
  Feb 26, 2012
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 1,907
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  Nimewahi kufanya kazi serikalini 8 years miaka 5 ya mwisho ya mkapa na 3 ya mwanzo ya kikwete. Sijawahi kuona mabadiliko ya mawaziri yenye tija zaidi ya kudisturb bajeti za wizara kwa kununua magari mapya, furnitures etc.

  Hebu niambie katika kipindi cha miaka 15 iliyopita, ni mabaraza mangapi yameendwa, na katika hayo ni mangapi yame perform hadi kufikia expectation za wananchi, na kwa nini unafikiri akifanya mabadiliko sasa hivi itaongeza tija?
   
 11. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #11
  Feb 26, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Mabadiliko ya baraza la mawaziri yatakuwa na tija if they are PARETO OPTIMAL!! Mkapa alijitahidi kufikia lengo hilo kwani yeye uteuzi wake mara nyingi haukufuata dini wala urafiki bali professionalism na wananchi hawakulalamika. Vigezo vya Kikwete vya kuteua ndugu zake na wale wa mkewe kuwa mawaziri hata pale wasipostahili haiwezekani kupata tija kwenye baraza kama hilo!!
   
Loading...