Wanabodi.
Radio Free Africa wanarusha kipindi cha sito sahau kila Jumapili saa nne na kuendelea.
Sasa hivi kuna hadithi ya jamaa anaye jiita Lwanda Magere! nimesikiliza hadithi yake kwa baadhi ya episode zake! Jamaa kiukweli kwa maneno yake mwenyewe, anakiri kuua watu wengi sana hasa kupitia ajali za Magari, na bahati mbaya amekuwa akitamka hadi ajali alizohusika.
Wito wangu! Management ya Radio Free Africa, haioni kama inaamsha uchungu kwa watu waliopoteza wapendwa wao katika ajali hizo? lakini pia haioni kama inahatarisha uhai wa huyo Lwanda Magere sababu watu wanaweza mfanyia kitu kibaya.
Hadithi ya Lwanda Magere inaweza kuwa na Fundisho au kutokuwa na umuhim kwa jamii yetu, story ime base kwenye mambo mabaya na machafu kuyasikia katika Radio Kubwa kama Radio Free Africa inayosikilizwa mpaka na watoto wadogo.
Rai yangu:
Kwakuwa hadithi imeonekana kuwa na mambo mengi kama kuua, umalaya, uzalilishaji, na hata ushirikina! ni wakati sasa hadithi hii ikarushwa usiku kuanzia labda saa nne usiku, ili kuepuka hawa watoto.
Na kwakuwa watu wanaifuatilia, hata mkiweka mida hiyo bado mtapata wateja wenu.
Nawasilisha.