HADITHI YA KUSISIMUWA MTEGEMEE MWENYEZI MUNGU TU PEKE YAKE USIMTEGEMEE BINADAMU

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,080
INASISIMUA NA KUTISHA ILA INAFUNDISHA

Katika kijiji cha Matare wilaya ya Mugumu
Serengeti, bwana Wambura alikamatwa kwa kesi
ya kusingiziwa na kuhukumiwa kwenda jela
miaka mitatu. Huku nyuma akiacha mke na

watoto wanne waliokuwa wanasoma. Hukumu
hiyo ilimtesa sana kichwa chake, alitamani kila
mtu anayemhisi kuwa ana makosa aingie katika

moyo wake na kuupata ukweli. Alilia na
umaskini wake, labda angepata wakili mzuri
angeweza kumtetea, kumkosa wakili

kukahalalisha kifungo hicho!! Alikwenda
gerezani huku akiumia sana rohoni. Aliyaanza
maisha mapya kwa shida sana, akawamnyonge
kila mara na mwili ukapoteza afya kiujumla.

Huko gerezani alifanikiwa kupata rafiki
aliyekuwa na cheo ama jukumu la uzikaji wa
wafungwa hasahasa ambao hawakuwa na ndugu
ama ambao ndugu zao huwa hawajitokezi pale

gerezani. Mzikaji alijaribu sana kumtia moyo
Wambura na kumwaminisha kuwa hiyo ilikuwa
hatua tu ya maisha

anapaswa kuizoea na siku moja ukweli
utajulikana tu! Bwana Wambura maneno ya
mzikaji hayakumuingia kabisa.. alizidi
kunyong’onyea. “Siwezi kuvumilia kukaa

gerezani miaka mitatu…..kama unajali kilio
changu nisaidie nitoroke kwa namna yoyote ile
ndugu yangu!!” Wambura alimsihi mzikaji.

SIKU MOJA mzikaji akamwambia Wambura kuwa
msaada umepatikana. Lakini yataka moyo!!

“Nipo tayari kwa lolote ilimradi tu nitoke
humu!!” alijibu kwa msisitizo huku akimtegea
sikio mzikaji. “Msaada pekee wa kukutorosha

humu ndani ni kwa njia ya jeneza… yaani
mfungwa akifa mimi nakuunganisha naye
kwenye jenerza…..” akashusha pumzi kisha
akaendelea “Wewe ukisikia kengele ya msiba,

njoo mara moja kwenye chumba cha maiti,
utakuta tayari sanduku liko katikati ya chumba
linakuwa halijafungwa, funua mfuniko ingia

ndani yake ulale pembeni ya maiti kwani
sanduku huwa kubwa la kutosha kila aina ya
maiti na hata miili miwili inaingia.

Kisha nitakuja na kulipigilia misumari. Baada ya
muda tutalipakia kwenye gari na kutoka kwenda
nje ya gereza makaburini nikiongozana na
baadhi ya wafungwa na maaskari magereza.

Tutakuzika huko lakini baada ya dakika 20 hadi
30 nitarudi kukufukua. Hautaweza kushindwa
kupumua kwa dakika hizo, utatoka ukiwa huru.”

JAPOKUWA wazo lilikuwa zuri lakini lilimtisha
sana Wambura. Hata hivyo akaona afadhali
afanye hivyo

kuliko kukaa gerezani miaka mitatu
bila kosa. Siku moja akasikia kengele ya msiba.

Akafanya kama alivyoelekezwa na mzikaji.
Akaenda na kuingia chumba cha maiti. Kweli
akalikuta sanduku, akiwa na hofu
kuu akaingia na kulala pembeni ya maiti
iliyokuwepo. Mara akasikia mtu ameingia na
kulipigilia msumari sanduku. Muda mfupi
baadaye sanduku likainuliwa na kuwekwa

kwenye gari. Gari likatoka nje ya gereza hadi
makaburini. Sanduku likashushwa
na kuwekwa kaburini na kuanza kufukiwa.

Wambura alijitahidi sana kuvumilia japo hofu
ilizidi kutanda. Alimtegemea sana mzikaji na
alianza kumuona mkombozi wa maisha yake.

Kama alivyoambiwa, akasubiri
dakika kumi, ishirini.. zikapita kimya!! Dakika
thelathini kimya. Joto nalo likazidi kuongezeka.

“Nitavumilia hadi afike…” alijisemea kisha
akajiongezea kauli ya ujasiri.

“Kama nilitakiwa kuishi gerezani miaka mitatu
kivipi dakika kadhaa za hapa kaburini

zinishinde” KWA kuwa alishakaa gerezani kwa
muda kiasi akatamani kujua aliyekufa ni nani…
ni kweli aliogopa kuitazama maiti lakini aliona
kama inatisha zaidi ikiwa

imefunikwa vile kuliko ikiwa wazi. Akaifunua
upande wa usoni… Kwa kuwa kulikuwa na giza
nene alikodoa sana macho kuitazama.

LAHAULA!!! MACHO YAKAKUTANA
NA SURA YA MZIKAJI!!!
MZIKAJI ALIKUWA AMEKUFA NA AMEZIKWA NA
AHADI ZAKE ZA UKOMBOZI!!
________________

FUNZO::
Usimtegemee sana mwanadamu katika maisha
yako, kwanza ni dhambi!! Pili mwanadamu
anakumbana na vikwazo kama unavyokumbana
navyo wewe hadi kumwendea yeye. Hivyo
kumpatia maisha yako ni kuzidi kuyaweka
hatarini zaidi!!
Umeonewa umesingiziwa unanyanyaswa…..
mwachie Mungu afanye maamuzi…
_______________
Haya mzikaji aliyetegemea atamfukua naye ni
maiti…… tazama mateso atakayoyapata hadi
kufa kwake…..Bila shaka atatamani kurudi
gerezani kwa miaka mingine kumi
lakini haitawezekana tena!!


JENEZA.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom