Hadithi: Ulimwengu wa Siri

Six Man

JF-Expert Member
Dec 19, 2017
250
884
Sehemu ya kwanza

ILIKUWA ni majira ya saa nane na dakika kumi usiku. Mitaani, kulikuwa na giza la kutisha. Hali ya hewa ilikuwa ya baridi sana katika jiji la Birmingham nchini Uingereza.

Ni saa nne zilikuwa zimepita tangu kijana Alexander Norman apate usingizi katika nyumba yao ndogo iliyopo kaskazini mwa jiji la Birmingham.

Ilipofika saa nane na dakika kumi usiku, hali ya hewa ilibadilika, ulianza kuvuma upepo ambao ulikuwa unaongezeka kila sekunde zilivyokuwa zinayoyoma. Ndani ya dakika ishirini upepo huo wa ajabu haukukoma.

Saa nane na dakika thelathini usiku, upepo ulioshika hatamu ulisindikizwa na radi kali. Mishale mikale ya radi ilikuwa inamulika kwa sekunde chache anga la jiji la Birmingham na kufanya nje kuonekane kama mchana. Baada ya sekunde chache za mimuliko ya miale ya radi hali ya giza totoro ilirejea.

Katika chumba alipokuwa amelala Alexander kulikuwa patulivu sana. Ukiacha zile bughudha za upepo na radi zilizokuwa zinatokea huko nje, ndani ya chumba hiki kulikuwa patulivu.

Alexander alikuwa amelala fofofo juu ya kitanda cha futi sita kwa sita. Blanketi safi la rangi ya hudhurungi lilikuwa limemfunika juu yake. Alikuwa ametopea katika lindi la usingizi, usingizi uliokuja kirahisi tu kwakuwa alikuwa amechoka sana siku hiyo.

Saa nane na dakika thelathini na tano usiku, pembeni, katika kuta moja ya chumba hiko kati ya kuta nne zilizomo mle chumbani, ulitokea ufa mdogo. Ufa ulikuwa umeanzia chini kabisa karibu na sakafu hadi juu karibu na rinta. Ufa ule wa ajabu uliongezeka ukubwa kila sekunde, na kufikia ukubwa wa kuwezesha kupita mtu ingawa kwa shida. Mara, moshi mweupe ulitokea nje ya ufa ule na kuingia ndani ya chumba alicholala Alexander kupitia ule ufa. Kitendo hiko kilidumu kama dakika tano na ule moshi ulikoma. Ile kuta ilijiziba ukiuacha ule moshi mle chumbani.

Moshi ulisogea hadi katika kuta nyingine ya chumba cha Alexander. Ulizungukazunguka kama dakika tano zingine na kutengeneza umbo la mtu. Ulianza kusogea taratibu kuelekea pale kitandani alipolala Alexander. Ulisogea hadi upande wa kichwa cha Alexander. Kwa namna ya ajabu ulilifunua blanketi alilojifunika Alexander upande wa kichwa. Ule moshi uliinamia kichwa cha Alexander.

Na kutoa sauti.

"Alexander, nenda Milton Keynes, nyumba namba MK131402, kamuue Mr Robbin Thomas"

Baada ya ule moshi kusema maneno hayo, ulirejea kule ukutani ulipoingilia. Ukuta ulijitengeneza tena ufa kama awali na kuuruhusu moshi ule kupita. Baada ya moshi wote kutoka nje, ule ukuta ulijifunga kama awali.

Na dakika hiyohiyo kule nje upepo na radi zilizokuwa zimeshamiri zilikoma mara moja.

Je nini kitatokea?

Tukutane kesho hapahapa...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ULIMWENGU WA SIRI: Sehemu ya Pili


0652 212391

MR ROBIN Thomas alikuwa ni mwalimu wa sosholojia katika chuo kikuu cha Birmingham. Kila siku asubuhi ilimpasa kusafiri kutoka Milton Keynes hadi Birmingham, na jioni kurejea.

Umbali kutoka jiji la Birmingham hadi Milton Keynes ni maili 71. Kwa gari inakadiriwa kuchukua saa moja na dakika kumi na moja kutoka jiji la Birmingham hadi mji wa Milton Keynes.

Mr Robin Thomas alikuwa anaishi na mke wake na watoto wao wawili mapacha. Mke wa mwalimu Robin alikuwa anaitwa Glory Deen. Wazazi wa Glory walikuwa wamelowea kwa muda mrefu katika mji wa Milton Keynes, wakitokea katika nchi jirani ya Scotland.

Ilikuwa ni kawaida kwa Mr Robin kuamka saa kumi alfajiri. Na kuanza kujiandaa ili aelekee kazini kwake, Birmingham.

Alam aliyoitega Mr Robin ili imuamshe ilikuwa inaita kwa mara ya tatu sasa. Mara mbili za mwanzo bi Glory hakutaka kumuasha mumewe. Alijua atasikia na kuamka mwenyewe kama ilivyo ada yake. Lakini mwito huu wa tatu ulimfanya bi Glory kuamka na kufanya jitihada za kumuamsha muwewe. Lakini jitihada zake hazikuzaa matunda. Mr Robin Thomas hakuwa katika ulimwengu huu!

Bi Glory alimuamsha mumewe kwa takriban dakika tatu. Huku sasa sauti yake ikiingiwa na hofu juu ya kilichompata mumewe. Ilipotimu dakika ya nne ndipo alipogundua kwamba mwili wa mumewe ulikuwa wa baridi sana, tofauti kabisa na mwili wa kawaida. Fikra za kwamba mumewe amefariki zilianza kumea katika ubungo wake. Na hofu kuu ilishamiri moyoni mwake. Mumewe amefariki? Katu haikumuingia akilini mwake. Lakini kila alipomgusa mumewe, basi hisia kwamba mumewe amefariki zilipata nguvu kichwani mwake. Alijiona dhahiri alikuwa anaiamsha maiti!
Hapo ndipo yowe lilimtoka, huku akilia kwa nguvu na kuomboleza juu ya kifo cha mumewe.

Wanawe mapacha, Lilian na Irene, ambao walikuwa na umri wa miaka kumi na tisa walitoka mbio chumbani kwao na kukimbilia katika chumba cha wazazi wao. Walianza kugonga mlango ili waweze kufunguliwa mlango na kujua kulikoni?

Wakati huo Irene alipiga hatua moja mbele. Hisia zake zilimwambia kwamba kuna hatari, nao kama watoto wa kike alihisi pengine haitokuwa rahisi kukabiliana na kitu watakachoenda kukutana nao. Alimpigia simu binamu yake, Raul.

Bi Glory alilia sana kule chumbani. Kilio chake kilificha sauti za kina Lilian waliokuwa wanalia kule nje. Ndani ya nusu saa nyumba ilitawaliwa na vilio. Mama akilia ndani, watoto wakilia nje.

"Irene kuna nini? Mbona nyumba mzima mnalia?" Raul aliuliza akiwa nyundo mkononi.

"Mbona na nyundo Raul? Ya nini hiyo?" Irene aliuliza.

"Nimevunja milango yote kufika hapa. Nimegonga sana nikiwa nje, lakini hakukuwa na majibu. Imenipasa nitumie njia hii ili kufika hapa" Raul alisema.

Irene na Lilian walibaki na mshangao. Hakuna aliyesikia sauti ya Raul akivyowaita, wala sauti ya nyundo. Walijisukia wao wakilia, na ndani walimsikia mama yao akilia.

"Tusamehe kaka Raul, hatukukusikia gata kidogo waka.." Lilian alikuwa anaelezea jinsi alivyoingia ndani, lakini Raul alimkatisha.

"Kuna tatizo gani?" Raul aliuliza.

"Mama!" Lilian na Irene walijikuta wakisema kwa pamoja huku wakiuonesha ule mlango wa chumba cha wazazi wao.

Ndipo hapo Raul alipotuliza akili, na kumsikia bi Glory akilia kwa kwikwi mle ndani.

"Amekuwa akilia kwa muda gani?" Raul aliuliza..

"Ni zaidi ya saa sasa" Irene alijibu..

"Tuuvunje mlango!" Raul alisema. Na alisema kweli maana hakutaka ushauri. Alitumia nyundo yake kuuvunja ule mlango.

Raul alifanya kama alivyofanya katika milango mingine ndani ya nyumba ile.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MWANAMKE SI RAFIKI
FRANK NA NESTO WAPO KANISANI...

Frank: Nesto Kwa Nini Mwanamke Yule Ananitazama Hivi?

Nesto:mwanamke Yupi?
Frank:yule Pale Kavaa Gauni Ya Bluu.
Nestor:usimtazame Kamwe achana nae.

Baada Ya Dakika Chache Frank Akasema Tena lakini Nesto Anani Konyezea Jicho!
Nesto: nimeshakwambia Usimtizame wewe sikiliza mahubiri.

Baada Ya Misa Frank Akapotea Na Nesto Akaja Kumuona Saa 5 Usiku.

Nesto: frank Ulipitia Wapi Tangu Mchana Saa 6 Mpaka Hivi?

Frank: Ndugu yangu Ni Story Ndefu Nimechoka sana hapa nilipo,yaani niko hoi!!!
Nesto: story Ndefu Kulikoni?

Frank: tulipotoka Kanisani Yule Mwanamke Akaniita Tukaongea vizuri tu halafu Tukaenda Kwake Tukala chakula Ila Alipotaka Kunikumbatia Tu Mumewe Askari Akaja Yule Mama Akasema Mumewe Ni Mkali Sana Ataniua Kwa Hiyo Akanipa Nguo Nyingi Sana Zilizo Kuwa Kabatini Nikajifanya Mpiga Pasi Nguo.

Nesto: yaan Toka Mchana Mpaka Hivi Saa 5 Usiku umekuwa unapiga Pasi Tu?

Frank: Ndio Kaka,na vyombo juu nimeosha na kusugua masufuria.

Nestor: Nilikwambia Usimuangalie Hukusikia Unatakiwa unisikilize ninapo Kwambia Kitu.
Unaona Zile Nguo Ulizo Piga Pasi Mimi Ndio Nilizifua Jumapili Iliyopita.
Na Mimi Kanifanyia Hivyo Hivyo Kaka na nimeambiwa ni mpango wao na mumewe ndio maana hawaajiri wafanyakazi wa ndani....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
HALFANI SUDY
ULIMWENGU WA SIRI
0652 212391

Sehemu ya Tatu

NI SAA moja na dakika kumi na mbili asubuhi. Wanafunzi walikuwa wamejaa chini ya bango moja kubwa sana lililodondoka. Yalikuwa ni maajabu na kweli. Bango kubwa lililoandikwa maandishi yakiyosomeka Birmingham University lilikuwa limedondoka chini.

Ilikuwa ajabu kwakuwa jinsi bango lile lilivyotengenezwa haikuwa jambo rahisi kuweza kudondoka. Lakini ilikuwa kweli kwakuwa bango lile lilikuwa chini.

Wakati wanafunzi wakilitazama bango hilo ndipo iloposambaa habari iliyomuacha mdomo wazi kila mmoja. Zilikuwa ni taarifa mbaya za kifo cha Mr Robin Thomas!

Hii ilikuwa taarifa mbaya sana kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Birmingham. Vilio vilitawala chuoni, simanzi ilimgubika kila mwanafunzi.

Nani alikuwa hamfahamu Mr Robin Thomas?

Likatoka tangazo la dharura, wanafunzi wote wakusanyike katika ukumbi wa chuo. Tangazo lilitekelezwa kwa haraka sana.

Wanafunzi walikuwa wamejaa ndani ya ukumbi wa chuo. Wengi wakiongea kwa kunong'ona juu ya kifo cha Mr Robin. Baada ya kama dakika kumi na tatu, ndipo mkuu wa chuo aliwasili ukumbini.

Uso wa mkuu wa chuo, tembea ya mkuu wa chuo na hata lugha yake ya mwili ilionesha kwamba kifo cha Mr Robin kilikuwa kimemsulubu bara'bara!

Alipoingia ukumbini, ukumbi wote ulikaa kimya. Macho na masikio ya watu wote ukumbini walimpa yeye.

Mshauri wa wanafunzi, Mr Yohane Smith alisimama mbele ya wanafunzi.

"Habari za asubuhi ndugu zangu. Najua nyote mmeshangazwa na mkutano huu wa ghafla. Kuna jambo zito limetokea hapa chuoni ndio maana mupo hapa. Mimi sitokuwa msemaji wa jambo hilo, namkaribisha Mr Daniel Schutter, mkuu wa chuo aje awaeleze kuhusu jambo hilo. Karibu mkuu wa chuo" Mshauri wa wanafunzi alisema.

"Habari zenu za asubuhi wanafunzi. Poleni sana na masomo.

Kama alivyosema mshauri wa wanafunzi. Kuna taarifa sio nzuri imetufikia hapa chuoni kwetu. Kwa kifupi tunasikitika kutangaza kifo cha mwalimu wetu wa Sosholojia, Mr Robin Thomas. Mr Robin amefariki alfajiri ya leo huko nyumbani kwake Milton Keynes" Mr Daniel Schutter alitulia kidogo huku akiwatazama wanafunzi wake. Wanafunzi walikuwa wamelowea katika majonzi makuu. Huku wanafunzi wengi wa kike wakishindwa kuyazuia machozi yao. Hii ilimpa simanzi sana mkuu wa chuo.

"Kifo cha Mr Robin kimekuwa ni pigo kubwa sana kwetu. Mr Robin alikuwa ni miongoni mwa walimu wetu waliodumu miaka mingi sana hapa. Amekuwa ni mwalimu mwandamizi katika somo la Sosholojia. Huwezi kutaja maaendeleo ya chuo chetu bila kumtaja Mr Robin. Kifo chake kimetokea wakati tunamuhitaji sana, tunahitaji sana taaluma yake iliyopo kichwani. Tunahitaji sana busara na hekima zake zilizosababisha chuo kikuu cha Birmingham kiwe ni miongoni mwa vyuo bora sana hapa Uingereza. Lakini pamoja na yote hayo hatuna jinsi, Mr Robin amemaliza safari yake iliyomleta hapa duniani. Mwendo ameumaliza, amepigana vyema sana vita vyake. Jukumu letu ni moja tu, kumuombea kwa mwenyezi Mungu ili amlaze mahali pema peponi...amiin" Mr Daniel Schutter alimaliza kutoa taarifa.

Mwisho wa taarifa hiyo ndio ulikuwa mwanzo wa vilio. Ukumbi wa chuo cha Birmingham ulijaa simanzi. Wanafunzi na walimu walilia na kulia. Lakini vilio vyao havikubadilisha kitu, Mr Robin Thomas alikuwa amefariki..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari mambo naitwa Mr Equator Nimeandika ujumbe huu kuku omba swala moja tu!
Mimi nimetengeza website ya ku share story ambayo ni EquatorStory
Je umekuwa ukipata tabu kupost story zako hapa?
Hili ndo suluhisho lako.
Mimi nataka nkupe nafasi ya kuwa mmoja wapo wa kwanza kutumia hii website
unda account yako na uweze kupost story yako mpya.
 

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom