Hadithi: Time Travel

MUDA

SEHEMU YA SITA.

“Basi mwanangu naomba upumzike kesho njoo utakuta nimeongea nae”
Baada ya maneno hayo Anitha alipangusa machozi na kusimama akisaidiwa na mama Nelson.

“Naomba unisindikize mama nimeacha gari kule barabarani,”
Waliongozana huku mama Nelson akimpa maneno ya kumfariji. Walipofika Anitha aliingia ndani ya gari na kutoa kiasi flani cha fedha na kumkabidhi mama Nelson.
“Simulizi langu linaitwa”
“ Mimi na wewe”
Vijana wawili walikutana kwenye ukumbi wa mziki msichana alipenda kunywa sana kileo ila mvulana alipenda tu kusikiliza mziki wali...........”
Inatosha Meneja alimkatisha yule kijana
“ Leo jioni njoo usimulie ila jaribu kuweka hisia si ulikuwa unamsikiliza mwenzako aliyeondoka”
Moyo wa Meneja ulikuwa na mashaka ila hakutaka kumuangusha mtu aliyempatia kiasi cha fedha.
“Endelea kufanya mazoezi nitakufuata baada ya kipindi”.
Aliongea yule mwanamme aliyekuwa mkuu wa shule ya akina Nelson.
“ Ndugu wasikilizaji leo tutaendelea na kipindi cha simulizi kila mtu aliisogelea Redio yake wengine waliweka spika zao za maskioni tayari kwa kusikiliza Anitha mwenyewe alikuwa amewasha Redio yake kupunguza hisia za maumivu cha ajabu kufika tu katikati mwa mda wa simulizi wengi walishasahau kama Redio imewashwa wengine walikuwa wakisonya.
Ni kama mtu amezoea kula wali maua gafla unaletewa bokoboko tena lililozidishiwa maji Anitha aliirudisha redio ile na kujigonga kwenye mguu wa meza na kuifanya izime bila kupenda. Mda wote Anitha alikuwa akiitazama saa yake iliyoko mezani kama kiwango cha mwendo wa muda .

Usingizi haukumjia mda wote alikuwa akiiwaza safari ya Mtoni Mtangoni. Saa kumi na moja alfajiri. Anitha alikuwa mezani kwake mbele ya kioo kikubwa kinachoilemba meza hiyo akijipodoa (kujilemba) kwa manukakato tofauti.
Baada ya kumaliza alichukua saa yake ya mkononi na kuivaa mkono wa kushoto aliitazama vyema wakati inasukuma mishale yake.
“Kati ya vitu unavyopaswa kutunza maishani mwako ni saa hii ninayokupatia”
aliikumbuka sauti ya daktari wake aliyeponesha maisha yake.
“Ukijua kuitumia vizuri saa hii maisha yako yatabadilika sana, maana utakuwa na uwezo wa kufanya chochote nje na ndani ya mda”.
Bado maneno ya daktari yaliendelea kumjia. Baada ya kumaliza alichukua funguo zake za gari na kufungua friji yake alitoa chupa moja ya mvinyo na kuiweka ndani ya gari, kisha aliwasha gari lake na safari mtangoni ilianza.
Alikuwa ameazimia moyoni mwake ikiwa Nelsoni atamkimbia tena atahakikisha anakunywa mvinyo yote hiyo ili asihisi maumivu yamtawale kama ilivyokuwa. Anita alipofika Mwenge alisimama na nkuanza kuzunguka huku na kule, alikuwa akitafuta batiki nzuri na yenye mwonekano mzuri, alitaka kumzawadia mama Nelson kama atamsaidia aweze kuongea naye.
Katika mzunguko wote hakuweza kupata, hivyo aliliwasha gari lake mpaka Kaliakoo. Aliweza kuipata batiki moja ilikuwa na mchanganyiko wa bluu na mawingu ya mvua, kusema kweli batiki ile ilpendeza sana. Hapo moyo waAnitha ulilidhika na aliingiza katika gari lake na kuondoka.
Nelson alikuwa amelala bado, akiwa kitandani aliendelea kuesabu mda wa dakika thelathini uliotosha kuaribu maisha yake.
“huu mda ni nini?”
Alionekana kujiuliza
“ Dakika tu chache mfumo mzima wa maisha unabadilika”
Hivi hakuna njia yoyote ya kubadili makosa uliyoyafanya bila kupoteza mda mwingine?.
Hivi nikibadili maisha yangu na kuyafanya yawe bora nitakuwa nimeondoa dosari ya awali? Naona hiyo itakuwa kama kuanza safari ya kwenda mji A. Napata changamoto ya usafiri badala ya kurekebisha unaamua kupanda mwingine unaokufikisha mji B. Eti kwa sababu yote ni miji hivi siwezi kufanya jambo lolote au ni.......”

Nelson aligunduliwa na mama yake mdogo aliyemuomba aje sebuleni ana shida naye kubwa.

Nelson alisonya kimoyo moyo kwani aliona mda wake unaendelea kupotea lakini alitambua kuwa yule ni sawa na mama yake mzazi hangekuwa na kibali cha kumkatalia jambo lolote lile. Alinyanyuka na kuelekea sebuleni ambako alimkuta Anitha akiwa amekaa huku chai ya kila aina ikiwa imetapakaa mezani.
“Njoo”
Mama yake alimwita kwa hisia.
Nelson alijivuta kwa unyonge na kukaa mahali pale. Moyoni mwa Anitha kulikuwa kunarindima hisia za shangwe. Mdomo wake ulianza kucheza cheza bila mpangilio.

“Nisamehe mwanangu mpendwa kuna hadithi mbaya kati yangu mimi na wewe ninaona hadi haibu ya kukusimulia hadithi hii”.
Alipotamka maneno hayo machozi yalianza kumtoka mfululizo.
“ Nelson mimi ndiye mama yako mzazi yule uliyekuwa unaishi nae ni mama mkubwa, yaani ni dada yangu mimi, nikiwa kidato cha pili nilipendana na mwalimu wangu wa masomo ya sayansi maana mimi pia nilikuwa napenda masomo hayo, alikuwa bado kijana tena ni mzuri kama wewe, kwa kuwa yule mwalimu alikuwa ni wa kujitolea aliitajika kwenda masomoni nje ya nchi.
Nilimwimiza tupime kabla ya yeye kuondoka ili kila mmoja ajue anabaki akiwa katika hali gani. Kumbe mimi nilitaka nijue afya yangu, maana nilikuwa sijielewi kabisa katika mwili wangu. Tulipopima niligundulika mjamzito mwalimu wangu aliogopa sana akawa anatetema tu bila kuongea chochote.
Nilienda nyumbani huku nimemuaidi mwalimu wangu atafakari jinsi ya kufanya, lakini kesho yake hakutokea aliamua kuondoka kimya kimya, hali niliyopitia ilikuwa ngumu sana nilifukuzwa shule na baba yangu aliwekwa ndani miezi miwili kwa kutonitunza vizuri.
Kwa kweli akili yangu ilivurugika kila nilipomuona mama yangu analia, toka siku hiyo niliapa nitatoa mimba yako au nitakutupa endapo ningefanikiwa kukuzaa.

Dada yangu aliujua huo mpango wangu, alinifungia ndani kwa uwangalizi wake mpaka nilipojifungua, alikuchukua na kuniambia niko tayari kufanya lolote ninalotaka kufanya.
Toka siku hiyo sijawahi kuonana na mwalimu wangu ambaye ndiye baba yako. Kwa kweli mpaka leo sijawahi kusikia taarifa yake yoyote.

Alitua kidogo na kuvuta pumzi nzito, alipokwisha kuitoa alisema
“wewe pia unataka kupitia hali yangu , usiruhusu hilo mwanangu, muhurumie Anitha pia”,

Alipomaliza kusema hayo Nelson alinyanyuka huku kilio cha kwikwi kikimuandama, alitoka nje na kuanza kupambana nayo. Anitha alimfuata naye alikuwa akilia kwa uchungu.
“Pole Nelson, mimi pia napitia hali kama yako”.
Alimtuliza huku akimpapasa mgongoni.
“Njoo mwanangu”.
Mama Nelson aliwaita.
Baada ya kukaa, waliongea mambo mengi na wote walionekana wakinywa chai kwa pamoja.
“Hizo saa mlinunua wapi?”
Aliuliza mama Nelson baada ya kuona saa zao zanafanana. Kila mmoja alinyanyua mkono na kuitazama saa yake zote zilihesabu saa sita kamili mchana, hata hivyo hakuna aliyejibu swali hilo zaidi ya wote kutabasamu kwa mshangao.

Anitha alinyanyuka haraka kama mtu anayefukuzwa na baada ya mda kidogoa alirudi na mzigo mkononi, alimkatia mama Nelson na kumwambia akajaribu huko ndani kwake.
“Acha wee! Mama lakee”
alitamka Nelson baada ya kumuona mama yake kapendeza na batiki limemkaa sawasawa katika mwili wake. Mama Nelson alianza kuruka ruka kwa staili ya tajiri wa kikongo maarufu pedejyee. Ni kama kumkuna anayewashwa, Anitha na mziki alikwisha ingia na kuanza kukatika.

Wakati hayo yakiendelea Nelson alikuwa akiukagua mda kuona ni matokeo gani na yanaweza kuchukua mda gani yanayoletwa na furaha. Baada ya staili hizo zisizo na hara yoyote ya mziki, wote walionekana kuwa wamoja katika mapatano.
Hapo Anitha alimuomba Nelson waende pamoja nyumbani kwake.
Kwa furaha waliyokuwa nayo Nelson asingependa kuikatiza alikubali mara moja. Na mama Nelson aliwasindikiza mpaka kwenye gari. Mama Nelson alirudi nyumbani huku moyo wake ukihisi furaha kubwa.
Wakati mama akisherehekea Anitha pia moyo wake ulikuwa mweupe kabisa. Aliliwasha gari lake na kuanza safari ya kuelekea Tegeta nyumbani kwake.
Alipofika Mtangoni kwa Azizi Ally, alikuta foreni ndogo na aliamua kufungua mziki huku mawazo yake yakimuona mama Nelson akicheza kwa staili yake. Kadiri mziki ulivyomuingia ndivyo Anitha alivyoanza kujitupatupa kwa mbwembwe.

Foleni iliruhusiwa na Anitha alikanyaga mafuta kwa fujo.
Ni Nelson aliyekuwa wa kwanza kumuona mtoto aliyekuwa anamkimbilia mama yake mzazi aliyekua ameishavuka bara bara.
“mama wee!”
Alitamka Anitha huku akikanyaga breki gafra.
“Sio kweli hii ni ndoto.”
TUKIO LA AJABU

Alijipiga piga kichwani kuakikisha kama amelala usingizi au ni mzima wa afya, ukweli ni kwamba ni mzima kabisa tena hana hata alama ya mchubuko.
Nelson hakuwa akijishangaa mwenyewe hapana, pia kundi la vijana waliokuwa wanacheza mpira walimzunga kwa mshangao wa aina yake.
“Wewe nani na umefikaje hapa?”
Alianza kapteni wa timu hiyo, kilichowashangaza wakati wanajiandaa kuanza mazoezi hakukua na mtu yeyote uwanja wote waliukagua.
Sasa imekuaje aonekane mtu katika eneo hilo?
Hayo maswali walijiuliza sana.
“Unaitwa nani?”
Mchezaji mmoja alimuuliza
“Mimi naitwa Nelson! Hapa niko wapi?”
Nelson nae aliuliza
“Unaitwa nani?
Alistaajabu yule kapteni, maana kila alipomtazama yule mtu alikuwa na sula ya baba yake, tofauti ni kwamba baba yake ni mkubwa kiumli ukilinganisha na mtu huyu.
“Umetoka wapi?”
Aliuliza yule kijana mchezaji wa mpila.
“Tumegonga mtoto na gari,nilikuwa na Anitha sijui yeye yuko wapi, tulikuwa Mtoni kwa Azizi Ally .
“Anitha?”
Kijana yule alioji kwa mshangao,
“Wewe ni Nelson,alafu ulikuwa na Anitha!”
Alizidi kuchanganyikiwa yule kijana .

“Mlikuwa mnatoka wapi?”
Alizidi kuhoji, Tunatoka Mtangoni kwa mama yangu mzazi.
“Kwa mama yako mzazi! Anaitwa nani?”
Kijana alizidi kuchanganyikiwa zaidi
“Joanita”
Alijibu kwa ufupi Nelson.

Yule Kijana alimsogelea na kumkaba kabali,
“Acha utani hebu nijibu ninachokuuliza”
Alionyesha kughadhabika.
Hata hivyo kijana mwingine alimshika na kumuondoa Nelson
“Wewe Robi mbona huna heshima hebu mtazame mtu huyu mbona anafanana na babayetu?”
Alihoji huyo kijana mwingine aliyekuwa amefanana sawasawa na Robi.
“Baba yenu yuko wapi?”
Aliuliza Nelson.
“Umesema unaitwa Nelson?”
Aliuliza yule kijana mwingine.
Mimi naitwa Fobi, huyu ni ndugu yangu pia Baba yetu anaitwa Nelson, mama yetu nae anaitwa Anitha, hata bibi yetu alikuwa anaitwa Joanitha ila amekufa miezi michache iliyopita.
Maelezo hayo yalimchanganya kichwa zaidi Nelson alianza kuwabembeleza wampeleke nyumbani kwao ili awaone hao wanaoitwa Nelson na Anitha.
Na kwakweli vijana wote waliweka mpira chini na kumpeleka Nelson nyumbani kwao.
Nelsoni Alistaajabu sana alimuona Anitha akiwa amepalalaizi miguu akiwa kwenye kiti cha kutembelea matairi, huku yeye mwenyewe akiwa anamkokota Anitha katika kigari hicho. Tofauti ni kwamba Nelson na Anitha walikuwa wanaelekea uzeeni.
“Wewe Mama ulikuwaje?”
Aliuliza Nelsoni, swali lililo wafanya Robi na Fobi kutikisa kichwa kwa pamoja kama ishara ya kusikitika.
“Gari letu lilimgonga Mtoto, alikuwa akivuka barabara wakati huo mke wangu Anitha ndiye aliyekuwa anaendesha Gari hilo, Mshtuko ule ndio uliomfanya hivi mke wangu”

Nelson alishtuka kisha akauliza
“ni eneo gani hilo?”
Pale vijana wanapochezea mpira kipindi hicho kulikuwa na Barabara ya raundi (Mzunguko)Lakini Rais mpya aliyeingia baada ya yule mama,
Alibadilisha barabara na kujenga Barabara za juu pale pembeni na zile za magari ya mwendo kasi. Baada ya kutamka maneno hayo Nelson alitambua jambo akanyoosha mkono uitazama Saa yake iliyokuwa mkononi na yule mzee pamoja na Anitha walisema kwa pamoja
“ Hizi si ndio Saa tulizowapa Robin a Fobi?”
“Hebu nizione Saa hizo”
Robi na Fobi waliingia chumbani na kuleta zile saa,
Saa zenyewe zilikuwa zimebonyea kidogo na upande wa mkanda zimechubuka,
Mzee akasema
“Hapo ni kwasababu ya lile tatizo la kugonga”
Story yetu kumbe imerudi

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
 
SEHEMU YA NANE
Aliuliza Dora huku akionesha woga “usijari mimi na huyu (akimuonesha kidore Anitha) Ni dada na kaka zake hawa Robin a Fobi , na hawa ni wazazi wetu ila kilichofanya tukuite hapa ni yule mama yetu unaona amepata matatizo na matatizo hayo yametokana na wewe, umekuwa ukiwachanganya ndugu hawa wawili, Sasa wamepigana na kuleta matatizo hapa nyumbani.”

Maneno hayo ya Nelson yalimfanya Dora kuchanganyikiwa alianza kutetemeka na kujikuta ameangukia magoti yake mbele ya watu wale “Naomba mnisamehe mimi sijui lolote lile namjua tu Fobi huyu mwingine simjui, ingawa nimekuwa nikigombana sana na Fobi kwa utani wake wa kuniigizia, mara namkuta uwanjani anacheza mpira, mara namkuta ukumbini akipiga mziki, yaani amekuwa akibadilika badilika kama kinyonga nae hakuwai kuniambia kama ana ndugu wanae fanana sana, Mungu wangu ninawezaje kufanya upumbavu huu kwa kudhamilia?
Siwezi siwezi nasema siwezi!
(Aliongea kwa uchungu huku machozi yakimtililika). Kaka !Tafadhari kaka, Mimi nimesema ukweli kwa mara ya kwanza nilikutana na Fobi katika Hoteli ya “Home spice”nilienda na Baba yangu kupata chakula cha jioni. Fobi alikuwa akitumbuiza katika Hoteli hiyo.
Kusema ukweli mimi ni mmoja wa wateja aliyeshindwa kuondoka eneo lile, Fobi alimaliza mawazo yangu yaliyokuwa yakiniangaisha mda mrefu kwa wimbo wake laini, bado naukumbuka wimbo huo mpaka leo hii. Ninaukumbuka vizuri Ulisema “ni Mda tu”Wimbo huo ulinifariji sana, ulionyesha makosa yangu, niliyokuwa nimeyafanya maishani mwangu.

Kupitia wimbo huo nilijiona kama nimezaliwa upya nilikuwa nimepoteza vitu vyenye thamani kwa kutojua thamani ya mda. Watu bora maishani mwangu nilikuwa nimewapoteza. Niliapa moyoni mwangu Fobi atakuwa mwalimu wa maisha yangu. Kumbe sikujua, nasema sikujua niliojua nilisisimka sana,Fobi aliponiambia “Hakuna mtu aliyemfanya aimbe vizuri wimbo ule kama mimi, maana aliziona Hisia zangu, aliniambia maneno hayo kwa njia iliyogusa sana moyo wangu.

Sasa ninawezaje kufanya ujinga huo?
Ni pale nilipoanza kuona mabadiliko ya Fobi ilikuwa imepita miezi miwili tukiwa kwenye mahusiano, Fobi alianza kunionyesha mapenzi yake katika michezo mingine, jambo lililokuwa tofauti na Fobi wangu wa kwanza.
Fobi alianza kupendezwa zaidi na mpira wa miguu kuliko mziki ulionivutia, Ila kwasababu nilikuwa nimejiapiza kuwa na Fobi milele, nilikubaliana na mabadiliko hayo.
Fobi alikuwa akihesabu mda wa kila alama ya nukta katika nziki wake , kitu kilichonivutia.
Nakumbuka siku anahojiwa kuhusu mbinu anayoitumia ili kuwa mwimbaji mzuri tena mwenye mvuto, alisema “Ninajua Mda na Eneo sahihi la kutua , hivyo kinanda changu huendana na mda ulioratibiwa.
Lakini hata baada ya Fobi kubadilika na mchezaji bora wa mpira wa miguu nilipatwa na wasi wasi sana, ila siku alipohojiwa kuhusu umakini wake wa kufunga na kutoa pasi zenye manufaa, nakumbuka alisema “Ninajua Mda sahihi wa kupiga pasi na mda sahihi wa kufunga goli tena kila mda umeratibiwa vyema.”
Maneno hayo ndiyo yaliyonifanya niseme Fobi ni yule yule kabadili tu mapendezi.
Maneno ya Dora yawafanya Nelson na Anitha, wanyanyue mikono yao na kuzitazama saa zilizokuwa pale mikononi. Kilchowashangaza Saa zile zile zilikuwa mikononi mwa Fobi na Robi.
“Robi kwa nini uliamua kufanya hivyo?”
Aliuliza Anitha aliyekuwa bado anaitazama Saa yake iliyokuwa ikionyesha mwanga wa Zambarau yenye mchanganyiko wa kahawa.”Mama alionyesha kutonipenda toka mwanzo Mda wote alimpendelea Fobi, ingawa Baba alinipendelea mimi, lakini hakuwa na wakati na mimi kama mama alivyo na mda na Fobi, Wao walicheka kwa furaha mda wote walicheza mziki pamoja kila siku, walitunga nyimbo pamoja hadi mimi nikawa sijisikii vizuri.

Baba yangu nilimuona mara moja kwa Juma ili nicheze nae mpira, kusema ukweli niliboreka sana.
Furaha iyohiyo niliiona wakati Fobi anamtambulisha Dora kwa mama yangu bila mimi kushirikishwa. Baba yangu hakuwa na Mda na mimi rafiki yangu wa karibu alikuwa kocha wangu.
Wakati huo nilianza kufanya vibaya uwanjani nilipomsimulia kocha wangu kilichokuwa kikiniangaisha, alinishauri nimpende, nifanye chochote ilimradi niweze kufanya vizuri uwanjani. Kusema kweli furaha yangu ilikuwa kumwalibia Fobi furaha yake.

Ilikuwa usiku, Fobi alikuwa amelala usingizi nilipochukua namba ya simu ya Dora katika simu ya Fobi. Nilimuandkia Dora ujumbe wa kumkaribisha katika hoteli ya “Home spice”iliyokuwa imeingia mkataba na Fobi wa kutumbuiza wateja wake kwa mwaka mzima.
Wao wenyewe hawakugundua utofauti wa mtu aliyetumbuiza siku hiyo, ni Dora pekee aliyegundua utofauti kidogo kwani ukaribu wangu ulivuka mipaka na Dora alianza kunifokea, huku akilalamika kuwa nimebadilika.

Nilijua atanigundua, maana siwezi kufanya kwa ubora uleule kama wa Fobi aliyekuwa akifanya mazoezi kila siku, Ndipo nilipoamua kumualika uwanjani ili anishuhudie nikisakata kandanda, ambacho ndicho kitu nilichokuwa nimechagua. Kwakweli umaarufu wangu ulianza kumvutia Dora na hapo alianza kuamini kuwa mimi ni Fobi.

Wakati mimi ninaonyesha mbwembwe zangu uwanjani Fobi alikuwa hotelini akitumbuiza kilichoniponza ni pale Fobi alipomuona Dora kwenye luninga akinipongeza kwakunikumbatia baada ya kuiwezesha timu yangu kuibuka na ushindi mnono.
Ugomvi wangu ulianzia hapo na Fobi.
Fobi alipanga kuniumbua siku yetu ya fainali aliingia uwanjani mapema, maana alijua Dora atakuja. Baada ya mimi kutambua hilo sikutokea uwanjani,Kocha wangu alimkamata Fobi akijua ni mimi alihisi labda nimetingwa na mawazo,hivyo alimlazimisha kuvaa jezi, Fobi alivaa jezi badala yangu. Mimi nilijitahidi kumtumia ujumbe Dora ili asiende uwanjani aje tukatumbuize hotelini lakini inaonekana Dora alikuwa ameanza kunogewa na mchezo wa kandanda.

Alielekea uwanjani na Baada ya kumuona Fobi alinitumia ujumbe akisema “Umeanza tena kunichezea?”Nilijua moja kwa moja ameishafika uwanjani na amemuona Fobi.
Niliumia sana baada ya kumuona Fobi akisakata kandanda kwa uwezo wa aina yake huku Dora akimshangilia sana kuliko alivyokuwa akinishangilia mimi.

Nilitamani kuvunja kioo cha luninga iliyokuwa pale hotelini.
Wakati Robi anasimulia hayo Wazazi wake walikuwa wakitokwa na machozi.
Mazungumzo yake yaliwahuzunisha wengi na Nelson na Anitha walibaki kinywa wazi.
Kabla Nelson hajauliza kama wote walifanya nae Ngono , Anitha alikuwa akiangaika kubonyeza kitufe cha Saa yake alikuwa ameamua kuuchezea Mda tena, alitaka arudi nyuma ili akarekebishe makosa ya Ujana wake yalikoanzia.
Nelson aliwahi na kumshika mkono “Unataka kufanya nini?”
Aliuliza Nelson kwa mshutuko.
“Sitavumilia kusikiliza haya acha nikayarekebishe haraka”
Alijibu Anitha kwa sauti.
Na wote walibaki wamemtazama.
Nelson alibaki amemshika mkono.
“Tafadhari tunakuja mara moja ngoja tukaongee hapo nje”Alitamka na kuuvuta mkono wa Anitha na kuelekea nje.
Baada ya kufika nje Nelson alikumbuka kitu na kurudi haraka ndani, alipofika alimkuta Robi akijaribu kuomba msamaha kwa Dora aliyekuwa akiendelea kulia, huku magoti yake yakizisugua Marumaru bila huruma.
“Tafadhari ndugu zangu, ni nani mwenye shilingi Elfu kumi hapo anionyeshe”
Fobi na Robi walichomoa kiasi hicho cha fedha kwa pamoja na kumuonyesha.
Nelson alitabasam na kurudi nyuma kinyume nyume mpaka alipoakikisha amezama kabisa mlangoni. Nimepata uhakika kuwa bado Hela inatumika hii tuliyo nayo, hivyo tunaweza kwenda. Alitamka Nelson huku akiushika mkono wa Anitha.

“Acha nifanye kitu Nelson jambo hili linafedhehesha”
Aliongezea Anitha huku akijaribu kuuchomoa mkono wake mkononi mwa Nelson.
Nisikilize Anitha hili alijatuleta huku, Tunahitaji kusafiri ili tukaonane na yule Daktari kule ndiko kuna chanzo cha matatizo, kuna mambo tunahitaji kuyafahamu vizuri, nina imani nikikutana na huyo Daktari kuna mambo mengi ya msingi nitayafahamu. “Anitha” Aliita Nelson huku akimkazia macho Anitha.
Nina maswali mengi kichwani mwangu lazima nikutane na huyo Daktari .
Alimaliza kuongea kilichomshangaza Nelson ni mwonekano wa Anitha,Anitha alikuwa akionyesha uso mlegevu Macho yake yalionyesha waziwazi kujawa na huba. “Anitha”Nelson aliita kwa mshangao.
Badala ya kuitika Anitha alimshika kwa nguvu Nelson na kumuuliza.
“Inamaana wewe utakuwa mme wangu?”
Na sisi tutazaa watoto wawili mapacha?
Baada ya maswali hayo alinyanyua macho na kumtazama Nelson
“Nijibu Nel Tafadhar!”
Aliongea kwa sauti ya kusihi.
Hata hivyo Nelson hakumjibu alimvuta mkono kwa nguvu na kumtaka waondoke eneo hilo.
Safari hiyo iliwapeleka moja kwa moja mpaka uwanja wa Ndege wa Mwlimu Julius Kambarage Nyerere. Wote walianza kustaajabu jinsi uwanja huo ulivyokuwa mkubwa na wa kisasa, ulitapakaa Ndege za kila aina tofauti na wakati walikotoka.

Walitafuta Ndege iliyokuwa ikielekea eneo walikotaka kwenda, Jambo linguine walilostaajabu ni kuona kila mkoa ulikuwa na Ndege zake na gharama zake zilikuwa nafuu sana kuliko hata nauli ya Mabasi waliyoacha katika wakati wao. Jambo hilo liliwafanya kutokazia mazungumzo yao ya awali na kujikuta wakijadili maendeleo waliyo nayo, na kitu kingine kilichowastaajabisha ni kuona mabango mengi ya matangazo yamejaa vivutio vya utalii badala ya picha za viongozi wanaotawala.

Haikuwachukua Mda mrefu walikuwa wakitua katika mkoa walikokuwa wakienda. Mkoa huo ulijulikana kwa uhaba wa usafiri wa uma, kwani watu wengi walimiriki magari ya kibinafsi,Na huo ndio uliokuwa wasiwasi mkubwa kwa Nelson akihofia kuchukua Mda mwingi kufika eneo hilo.
Baada ya Nelson kushuka katika Ndege alionekana kumshirikisha Anitha mshangao wake baada ya kuona magari ya mwendo kasi yakipishana kubeba abiria. “Huyu aliyeifikisha hapa Tanzania ni kiongozi kweli!”
Alitamka Anitha kwa mshangao, “Sio huyu sema au umesahau Katiba ya Tanzania, inasema mmoja ataishia miaka kumi? Hiyo inamaana watakuwa wamepita wawili”Aliongea huku akitabasamu, mazungumzo yao yenye bashasha yaliwafanya wasione umbali wa safari yao.
Nelson na Anitha walinyanyua mikono yao na kuzitazama saa zao, zote zilikuwa zikienda kwa mwendo waliouzoea, ingawa rangi ya mwanga tu ndio ilikuwa imebadilika kutoka Zambarau yenye ukahawia na kuonyesha rangi ya machungwa ya kufifia.
“Eneo lenyewe ni hili hapa”
Anitha alionyesha eneo ilikokuwa ile Hosptari alikopelekwa kulazwa.
Hakujua kama eneo hilo Nelson analifahamu vizuri na ndiye mtu aliyempeleka Hosipitarin hapo, ingawa waliona utofauti mkubwa sana wa eneo hilo , lakini hawakujari kwani walikuwa wameanza kuzoea mambo mapya kwao na yenye kustaajabisha.

Kipindi kile Eneo hili lilikuwa na Hospitali iliyofaa kuitwa Zahanati, kwani haikuwa na wataalamu wa kutosha pia Majengo yao yalikuwa machache na yasiyo bora, ila Nelson na Anitha walikuwa wakiitazama Hosptali kubwa sana iliyozungushiwa Miti mirefu na mizuri kwa mwonekano huku bango la kupendeza lenye maneno ya kiingereza “AFRICAN TRADITIONAL CLINIC”
Yakisomeka vizuri kwa kila mpita njia. Watu wengi walikuwa maeneo hayo jambo lililowafanya Nelson na Anitha kuhisi utofauti wa huduma zinazotolewa Eneo hilo, kwani mahari walipotoka, mikusanyiko kama hiyo huwa maeneo ya viongozi wakubwa wa kisiasa ama kidini.

Na mara nyingi wakati wa kampeini au Viongozi wa kidini wakiwa wanaondoa matatizo ya waumini wao. Baada ya kuona hivyo Nelson na Anitha walianza kupenya katikati mwa Watu hao ili kuingia ndani ya Hospitali hiyo. Kitendo hicho kiliwachukua mda mrefu kuingia ndani ya Hospitali kuliko Mda walioutumia kusafiri kufika Eneo hilo “Lakini kuna jambo la tofauti, mbona watu hawa wanalia?”
Aliuliza Anitha aliyekuwa karibu na mama mmoja, aliyekuwa amevimba macho huku wekundu wake ukiashilia hali tofauti katika eneo hilo. Na Nelson alianza kuyakagua macho ya watu wale kwa umakini.
“Ni kweli kuna jambo haliko sawa hapa!
Alitamka Nelson na kuanza kupambana ili apenye haraka katikati mwa Watu hao.
Anitha aliishika nguo ya Nelson kwa nyuma na Nelson alianza kusukuma Watu kwa mikono yake ili wampe njia ya kupita.
 
Duh

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
 
Huu utakuwa ufafanuzi rahisi was kitu ama Muda.

Je inawezekana kwenda miaka ya mbele ama kurudi nyuma kwa akina Yesu na Yuda Eskaroti?

Sasa hapa utapata ufafanuzi wa time travel.

Ipo ama haipo utapata majibu.

Hebu anza na hii

Mtunzi: Jonas Rututuka
Mwandishi: Nelson Ntimba.
Time travel

MUDA
“MUDA NI NINI? Ama niulize wakati ni nini?. Watu huupima wakati kwa kutumia vitu mbali mbali. Wapo wanaopima muda kupitia kifaa maalum kiitwacho saa.

Lakini nayo saa hupimwa kwa kutumia kifaa kingine kama satilaiti ama kifaa chochote cha kuhisi mijongeo ya mawimbi na hata kifaa kingine cha kiumeme.Ajabu ni kwamba na vifaa hivyo vinaendelea kuitegemea saa ili viwe sahii.

Ningeliweza kuuliza maswali mengi kuhusu muda ama wakati ila kulingana na wakati tulio nao ambao unatuongoza hapa, Acha nizungumzie umuhimu wa kutokupoteza wakati. Je unajua siku nzima ina muda wa saa24?.Kati ya saa hizo saa 8 watu huzitumia kuwa shuleni,ama katika kazi, Na saa 8 nyingine hushauriwa na wataalam ziwe ni za kulala ama kupumzika wakati wa usiku.

Hivyo kila mtu ana saa 8 za ziadakwa ajiri ya mambo yake binafsi. Kumbe watu wote walio fanikiwa walitambua muda huo wa ziada na kuutumia vizuri.Hapo ndipo walipo fanikisha ndoto zao kuzitimiza.

Je unajua kuwa ukizitumia saa hizo vibaya kila siku unakuwa umepoteza saa 56 kwa wikinzima?
Ama umepoteza saa 224 kwa mwezi ?. Ama nisema utakuwa umepoteza saa 2688 kwa mwaka?
Na hii ina maana kuwa hapa shuleni ukiupuuza muda huo utakuwa umepoteza jumla ya saa10752 amabao ni sawa na mwaka mmoja kasoromwezi mmoja na saa 4 tu.

Ukitafakari hili kwa uzito . Utagundua upotevu wa muda tunao ufanya kwa kuendekeza mambo yasiyo ya muhimu. Hivyo basi wanafu……….”

Kabla kijana Nelson ajamalizia mazungumzo yake yalisikika makofi ya mkuu wa shule yakitokea nyuma ya mstari wa wanafunzi. Wanafunzi wote walihamaki na kugeuza vichwa vyao ili macho yao yahakiki kile ambacho masikio yao yalikuwa yakiwaletea.

Wapo walio anza kujikagua kama wana makosa yanayo onekana wazi. Wengine walianza kutawaliwa na wivu wakitamani mazunguzo yale wangeliyawasilisha wao. Wakati kila mwanafunzi akiwaza jambo lake akilini, Mkuu wa shule alipaaza sauti yake yenye muungulumo.
“Safi saafi sana kijana umenikosha kwa mazungumzo mazuri ya asubuhi kama hayo yenye kujenga. Tafadhali kijana huyu kuanzia leo namuweka kuwa mtunza muda wa shule mpaka pale atakapo maliza shule ndipo tutakapo mchagua mtu mwingine”

Mkuu wa shule alitua kidogo na kumeza mate kwa mbwembwe. Kisha akaendelea kuipaaza sauti yake yenye muungurumo.

“Tena akitoka hapa namaanisha baada ya masomo haje ofisini kwangu kuchukua zawadi yake”

Kijana Nelson hakuhamini kilicho tokea, alikuwa ameyaandaa mazungumzo yake kwa njia ya kawaida sana. Lakini alishangaa matokeo yake kuwa makubwa kiasi hicho. Muda wa masomo ulipo isha kama lilivyo semwa agizo la Mkuu wa shule aliingia ofisini kwake. Nelson alikuwa apotezi muda hata dakika chache.
Wapo walio mtania kwa kumuita mzungu kwa njinsi alivyo kuwa akiujali wakati. Aliingia kwenye ofisi ya Mkuu wa shule bila kubisha hodi. Mkuu wa shule alishutuka na kukimbilia mlango ili aufunge haraka. Hata hivyo Nelson alikuwa amesha zamisha kichwa chake na kuchungulia ofisini.

Alimuona mwanafunzi mwenzake akiwa amepiga magoti kama mtu aliye katika nyumba ya ibada akiomba msamaha kwa Muumba wake tena akijaribu kusisitiza kwa msisitizo mkubwa ulio ambatana na kilio cha uchungu.
Mwanafunzi mwenyewe alikuwa ni wa kike. Haraka Nelson alichomoa kichwa chake hata hivyo macho yake yalikuwa yamesha tuma taarifa hiyo kwenye ubongo nao ubongo ulikuwa ukilichakata jambo hilo. Ingawa alijaribu kuulazimisha ubongo wake usifanya kazi yake lakini ilishindikana.

Mkuu wa shule alitoka ofisini kwake na kumkuta Nelson karibu na mlango wa ofisi yake.
Mkuu wa shule alikuwa na wasiwasi na rangi yake ya ngozi ilionyesha matonetone ya jasho.
Alianza kumsifia Nelson huku macho yake yakienda kulia na kushoto chini na juu bila mpangilio.
Nelson alitambua kuwa hali haiko sawa.

Aliinamisha kichwa chake na kuanza kumsikiliza Mkuu wa shule,Kwani alihisi akimtazama usoni macho yake yatamhukum na kumshuku Mkuu wa shule.

Mkuu huyo hakuwa na lolote la maana zaidi ya kumumiminia tu sifa nyingi kijana Nelson. Baada ya sifa hizo Nelson alitoka ofisini na kuwakuta wanafunzi wakimsubiria agonge kengele ili waweze kwenda nyumbani.

Nelson alijilaum sana kwani mada hii aliyo iwasilisha kwa wanafunzi asubuhi aliiandaa miakamiwili iliyo pita. Ikiwa angeliitoa muda huo huenda angeliipata nafasi hiyo mapema. Hata hivyo alijisemea
“Hakuna kilicho haribika”

Kisha alikwenda kugonga kengele na wanafunzi wote walikusanyika mstarini.
Nelson aliendelea kusifiwa kwani hakuwahi kupoteza hata therusi ya sekunde.

Aliizoelea ratiba hiyo ya muda hivi kwamba wakati mwingine halinyanyuka bila kuitaza mpaka ilipo kengere na akiangalia saa yake anakuta muda umefika ama unapungua tu sekunde chache.

Wanafunzi hawakuwa na shida ya kubadili nyakati za saa zao.Wao walitumia kengele iliyo kuwa ikigogwa na Nelson. Naye akibadili ya kwake kupitia saa za wenzake. Mzunguko huo hakuna aliye wahi kuugundua kamwe,Maana walijua saa zao ziko sahii na zinawapimia wakati kwa njia waliyo ihitaji. Ili mradi walitimiza mambo yao kwa wakati ulio pagwa.
Ilikuwa siku ya jumatatu saa nne na nusu asubuhi,ndivyo saa ya Nelson ilivyo onyesha maana ilikuwa na mlio fulani ulio kuwa ukimkumbusha pale alipo pitiwa.Nelson alinyanyuka haraka na kukimbia ilipo kengere,Aliingonga kwa nguvu hata hivyo alishangaa itikio la wanafunzi halikuwa kama la siku zote.

Hakuna aliye shanngilia wala kutoka darasani kama siku nyingine wafanyavyo. Nelson alirudi darasani haraka akihofia labda mwalimu aliingia darasani mara tu baada ya yeye kutoka. Alifika darasani kitu kilicho mshangaza watu wote walikuwa kimya.

Tena wasio tikisa hata kope zao. Aliwatazama kwa muda mara akanyanyua mkono wake kutazama saa iliyo kuwa mikoni mwake mishale yake yote ilikuwa imesimama. Alijaribu kuipiga piga akihisi imeharibika.
Lakini ghafula alisikia mwanafunzi mmoja akisema
“Shetani amepita”
mwingine alicheka na kusema.
“Hapana Mungu alikuwa anatuhesabu”
Hapo minongono ya wanafunzi ilisikika kwa vurugu kama kawaida yao.
Nelson akiwa kwenye mshangao wa nini kimetokea aligeuka na kuitazama saa yake tena.
Ilikuwa ikiendelea kama kawaida yake kuhesabu wakati.

“Muda bado jamani kengele ya uji mbona inachelewa”
Aliongea mwanafunzi mwingine akimtazama Nelson aliyekuwa amepigwa na butwaa. Hata hivyo Nelson alitoka nje na kwenda kungonga kengere kwa mara ya pili.

Hapo wanafunzii wote walipaaza sauti zao za vigelele na kukimbilia sehemu ya uji. Nelson alionyesha kuchanganyikiwa kwani kila mara alikuwa akijiuliza ni nini kilitokea mpaka hali ikawa namna hiyo?. Hata hivyo hakupata majibu kabisa.

Ingawa jambo hilo lilimkumbusha jambo fulani lilowahi kutokea linalo fanana na hilo.Wakati huo Nelson alikuwa kijana mdogo alikuawa ameenda sokoni na mama yake kununua mahitaji. Wakiwa sokoni wananua vitu, ilitokea hali kama hiyo watu wote walikuwa kimya kwa ghafula.

Tena yule mama aliyekuwa anawauzia mchicha alionekana kama amepigwa shoti ya umeme. Na tukio hilo pia lilionekana kwa mama Nelson tena wakati huo alikuwa ameshika pesa mkononi.
Nelson alichua pesa hiyo na kumuwekea mama muuza mchicha mkoni mwake. Kisha aliuchukua mchicha na kuuweka kwenye kikapu chao.

Wakati akitaka kuwashutua alishangaa kuona wanaendeleza mazungumzo kana kwamba hakuna kilicho tukia. Miziki yote ya sokoni ilianza upya kuunguruma. Ila kutokana na umri wake kuwa mdogo hakuweza kujiuliza maswali mengi zaidi.
Wacha nikwambie uko vizuri nakukaribisha unikosoe kwenye KISANGA na The Hidden Truth.

Kuna ninayojifunza toka kwako Kaka.
 
SEHEMU YA TISA
MUDA.
JONESS RUTUTUKA.
0656353765.

Kipindi kile Eneo hili lilikuwa na Hospitali iliyofaa kuitwa Zahanati, kwani haikuwa na wataalamu wa kutosha pia Majengo yao yalikuwa machache na yasiyo bora, ila Nelson na Anitha walikuwa wakiitazama Hosptali kubwa sana iliyozungushiwa Miti mirefu na mizuri kwa mwonekano huku bango la kupendeza lenye maneno ya kiingereza “AFRICAN TRADITIONAL CLINIC”

Yakisomeka vizuri kwa kila mpita njia. Watu wengi walikuwa maeneo hayo jambo lililowafanya Nelson na Anitha kuhisi utofauti wa huduma zinazotolewa Eneo hilo, kwani mahari walipotoka, mikusanyiko kama hiyo huwa maeneo ya viongozi wakubwa wa kisiasa ama kidini.

Na mara nyingi wakati wa kampeini au Viongozi wa kidini wakiwa wanaondoa matatizo ya waumini wao. Baada ya kuona hivyo Nelson na Anitha walianza kupenya katikati mwa Watu hao ili kuingia ndani ya Hospitali hiyo. Kitendo hicho kiliwachukua mda mrefu kuingia ndani ya Hospitali kuliko Mda walioutumia kusafiri kufika Eneo hilo “Lakini kuna jambo la tofauti, mbona watu hawa wanalia?”

Aliuliza Anitha aliyekuwa karibu na mama mmoja, aliyekuwa amevimba macho huku wekundu wake ukiashilia hali tofauti katika eneo hilo. Na Nelson alianza kuyakagua macho ya watu wale kwa umakini.

“Ni kweli kuna jambo haliko sawa hapa!

Alitamka Nelson na kuanza kupambana ili apenye haraka katikati mwa Watu hao.

Anitha aliishika nguo ya Nelson kwa nyuma na Nelson alianza kusukuma Watu kwa mikono yake ili wampe njia ya kupita.

Nelson alijitahidi mpaka akaukaribia Mlango wa Hospitali hiyo, Mlangoni kulikuwa kumefungwa kamba yenye maandishi,

“USIVUKE HAPA”

Nelson aliyasoma hata hivyo hakuyajari Aliinyanyua ile kamba ili apite chini yake kuingia mle ndani. Kabla hajaingiza Mwili mzima walitokea Wamaume Wawili waliovalia Suti Nyeusi walimsukuma na kumwambia

“SUBILI UTARATIBU WA MAZISHI MTAMUONA MTU WENU”

Maneno hayo yalimvuruga Nelson na wakati huo Anitha alikuwa akimnyanyua kutoka chini alikokuwa amedondoka. “Ni nani amekufa? Niambie Tafadhari!”

Alitamka Nelson kwa mchemko.

“Ni Dokta Mtabuzi! Dokta wetu mpendwa, Basi wangetuonyesha maiti yake turidhike”

Alitamka Mama mmoja aliyeonyesha kulia kwa Mda mrefu huku akimsaidia Anitha kumnyanyua Nelson.

Akili ya Nelson ilikuwa imeenda kwa kasi sana, Aligeuka na kumtazama Anitha Alinyanyua mkono wake na kuitazama Saa yake kitendo hicho kilimfanya Anitha amwige kwa kuitazama Saa yake pia.

“Ishirini Ishirini”

Alitamka Nelson na baada ya Maneno hayo hakuonekana mahari hapo, tena, wale Wanaume Wawili walitahamaki na kuonyesha kuchanganyikiwa.

Waliingia ndani kwa kukimbia, Walipofika ndani walikuta utaratibu wa kuandaa mwili wa Mtu aliyekufa ukiendelea , Dokta Mutabuzi alikuwa pembeni amefungwa kwa vifaa maalumu vilivyokuwa vimembana hivi kwamba hana uwezo wa kuongea wala kujitikisa labda macho yake tu ndiyo yaliyokuwa yakifanya kazi, huku Wanaume wale wakijitahidi kumvalisha maiti aliyekuwa amelala kitandani Sura iliyofanana Sawasawa na Dokta Mutabuzi.

Ujio wa wale wanaume wengine wawili waliokuwa nje wakijaribu kudumisha ulinzi uliwashtua wenzao.

“Kuna Tatizo nje”

Bwana mmoja aliongea kwa wasiwasi

“Tatizo Gani?”

Mwanaume mwingine aliyekuwa amevalia mavazi ya kidaktari aliuliza kwa kutumbua macho.

“Kuna kijana ana nywila zetu! Ametembea na Mda alikuwa akigangania kuingia humu tulipomzuia aliigusa Saa yake na hatujajua ameelekea Mwaka gani?”

Watu wale walionekana kuangaishwa na hari hiyo. Baada ya Dokta Mutabuzi kusikia taarifa hiyo macho yake yalianza kungaa huku mdomo wake ukishindwa kuonyesha Tabasamu lililokuwa moyoni mwake.

Anitha pia alikuwa amerudisha mshale wa Saa yake ilipo Namba Ishirini ishirini.

Mara moja alijikuta katika Hospitali hiyo iyo aligeuza macho yake na kuitazama picha ya Dokta Mutabuzi iliyokuwa imebandikwa mbele ya Hospitali hiyo.

Wakati akiendelea kuitazama picha hiyo, Alikuja mama mmoja na kumsarimia kwa shangwe.

Anitha aliitikia kwa upole, kama unamtafuta Dokta Mutabuzi subiri kidogo amepata mgeni Mda sio mrefu hata hivyo matatizo yako yote yatakwisha, ni Dokta mzuri mimi ni shuhuda wa jambo hilo.

Mama yule alitamka kwa hisia jambo lililomfanya Anitha aone ukweli wa maneno ya Mama huyo. Hata hivyo Anitha alipata jibu kwa nini Mama huyo alikuwa akilia sana katika Mwaka alikotoka inaonekana ni mnufaika mkubwa wa Dokta Mutabuzi

“Mgeni mwenyewe ni Kijana mwenye Saa kama hii?”

Anitha aliuliza

Baada ya kujibiwa kwa kuhakikishiwa kuwa ndiye aliomba kupelekwa sehemu walipo , kwani kuwa kwake hapo ni kwasababu ya Watu hao wawili, Mama huyo alimwelekeza vizuri sehemu walipo.

Anitha aliingia katika chumba kile alishangaa kumuona Dokta na Nelson wamekumbatiana kana kwamba wanafahamiana kwa Muda mrefu,

“Nilijua siku moja utafanya hivi sasa nina sababu ya kufurahi”

Dokta Mutabuzi maneno yalikuwa yakimtoka mfululizo huku Tabasamu za bashasha zikiufanya mdomo wake usitulie. “Na wewe Binti yangu! Njoo nikukumbatie.

Tafadhari Alitamka Dokta Mutabuzi huku akiipanua mikono yake ili imvae vyema Anitha aliyekuwa ameduwaa mlangoni.

Dokta mtabuzi alimbinya kwa shauku Anitha hadi Nelson alihisi wivu ukijikusanya kifuani pake.

Dokta MUtabuzi aliwakaribisha kwenye viti nae alikaa kana kwamba anataka kuwapatia ushauri wa kitiba.

“Niambieni sasa ni mambo gani mnayafahamu katika Suala hili la Muda”

Alitamka Dokta mutabuzi huku akiwadadisi kwa macho yake, Nelson alijipanga vizuri katika kiti chake , maneno ya Dokta mutabuzi yalikuwa yameamsha maswali yaliyokuwa akilini mwake.

Nelson alinyanyua mkono na kuitazama Saa iliyokuwa mkononi mwake, Jambo lililomfanya Anitha afanye hivyo pia. Dokta mutabuzi aliwatazama kwakutoa tabasamu isiyo wazi.

“Hizi Saa zina Tofauti gani na Saa nyingine ,na ilikuwaje tukawa nazo sisi peke yetu?” Aliuliza maswali mfululizo Nelson huku akiendelea kuitazama Saa yake iliyokuwa ikitua rangi tofauti na mwanga ukilinganisha na alivyozoea.

Anitha alikuwa ametega masikio kwa nguvu ili kusikia majibu ya Dokta, Dokta Mtabuzi naye alinyoosha mkono wake wa kushoto na kuvuta mkono wa vazi la kidokta uliokuwa umefika mwanzoni mwa kiganja chake baada ya kuvuta Saa yake ilionekana ilikuwa ya muundo kama wa zile Saa za Nelsoni na Anitha tofauti ilikuwa rangi peke yake.

Uligundua lini kuwa Saa yako ni tofauti na Saa zingine?

Dokta Mtabuzi aliuliza kwa upole.

Kuna jambo limekuwa likitokea na ninahisi ni wachache wamekuwa wakiona jambo hilo, vitu vyote kukoma katika utendaji wake , Yaani kila kitu kusimama tuli, hata liwe tone la maji ama ukungu, Tukio kama lilitukia siku kadhaa nikiwa kariakoo katika Duka la kuuza Saa na mikufu lakini Saa hii iliendelea na utendji wake. Lakini jambo lingine Saa zote huwa na mianga (mwanga) ila mwanga wa Saa hizi (Nelson akiionesha kwa kidole Saa yake) hubadilikana kulingana na mazingira pia kutokana na watu ulio nao ni kama mwanga huu unasema

“Uko sehemu sahihi ama sio sahihi na mtu huyu nimwangalie vizuri”

Alitua Nelson kwa ongea yake ya kuvuta maneno.

Dokta Mtabuzi alikuwa akimtazama kwa makini huku akitikisa kichwa chake kama ishara ya kukubali jambo.

“Mmh!

Kuna kitu kingine juu ya Saa hiyo?”

Aliuliza tena huku macho yake yakionyesha udadisi.

“Ndiyo, hii Saa ni kama Daraja ama ngazi inakupeleka mahari ambako wengine hawawezi kwenda yaani ulipotoka na unakoenda simaanishi mahali hapa namaanisha Wakati”

Dokta Mtabuzi aliruhusu tabasmu lake lionekane wazi na hapo Anitha alishtuka, alijipanga vizuri kwenye kiti chake kama mtu anayefuatilia kisa makini katika Runinga ama kifaa chochote cha kielekroniki.

Tabasamu lile lilimpa picha ya wazi wazi ya mtu anayemfahamu , ninazidi kumpenda sana Nelson ndio maana picha yake inanijia akilini haraka

Alijisemea kimoyo moyo Anitha kisha akaendelea kukazia uangalifu mazungumzo ya Nelson na Dokta Mtabuzi. Dokta Mtabuzi alibonyeza kitufe fulani katika meza yake na mara moja ilisikika sauti ya Kike ikipokea. Vinywaji vitatu Tafadhari ikiwezekana vipande sita vya mkate vitatutosha.

Alibonyeza tena kile kitufe na hiyo ilionekana alikuwa akikata mawasiliano.

Dakika chache zilipita yule mwanamke aliyempokea Anitha alikuja amebeba vitu hivyo katika kifaa cha kubebea na kuwatengea mezani,

“Karibu sana”

Alitamka yule mwanamke na kuondoka bila kuisubiria Asante ya watu wale.

Nelson na Anitha walitazamana kwa huruma na hapo Dokta Mtabuzi aligundua jambo na kuuliza,

“Mmepata kumuona mtu huyu mahali popote?”

Haraka Anitha aliropoka

“Ndie alikuwa akilia kuliko watu wote”

Dokta Mutabuzi huwa hakurupuki kujibu wala kupokea jambo, Hujipa Mda wa kulichakata kwanza. Hivyo alinyanyua kikombe cha chai na kuvuta funda moja , alipokwisha kuweka kikombe chake chini aliuliza

“Kitu gani kilikuwa kikimliza na Mwaka gani?”

Kisha akanyanyua kikombe na kuvuta funda lingine huku macho yake akiyageuza taratibu kuwatazama Nelson na Anitha .

“Tulikuwa miaka Ishirini na tano mbele, ilionyesha ulikuwa umekufa watu wengi walikusanyika ni kama waliandamana juu ya kifo chako, lakini saa yangu ilionyesha mwanga wa Hatari inaonekana kifo chako kitakuwa cha kutengenezwa (kukusudia)

“Alitamka Nelson kwa njia ya huzuni.

Dokta Mtabuzi alinyanyuka na kikombe chake mkononi huku vipande vya mikate vikiwa mkono wa kushoto, na kuwaambia Nelson na Anitha wamfuate wote walifanya kama alivyofanya yeye na Safari ya taratibu isiyoweza kuruhusu tone la chai kudondoka ikionekana Safari hiyo iliwapeleka moja kwa moja mpaka chumba flani kilichokuwa chini ya Hospitali hiyo.

Chumba chenyewe kilikuwa na giza mpaka dokta alipowasha taa ndipo walipoanza kukiona vizuri chumba kile chumba chenyewe kilikuwa kikubwa kila kitu kilipangwa kwa utaratibu. Mlio wa Saa ya ukutani ndio uliosikika. Saa hiyo ilikuwa kubwa zaidi ya Saa walizozizoea ziambwazo ukutani na ilikuwa na mishale mingi ukilinganisha na Saa zingine vifaa mbalimbali vitumiwavyo maabara vilijaa kila meza na Dawa za kila aina zijulikanazo kama Miti shamba zilijaa katika kontaina mbalimbali kulikuwa na mbao tatu za ukutani na ubao wa kwanza ulijaa hesabu za kila aina na hasa hesabu za Wakati na miaka ndizo zilionekana kuwa nyingi.

Ubao wa pili ulijaa haina mbalimbali za Dawa na matumizi yake na upande wa kulia wa ubao huo yaliandikwa Majina ya Watu wa zamani Nelson alijaribu kuyasoma mara kwa mara hata hivyo ni majina mawili tu aliyowahi kuyasikia, kati ya majina hayo mengi ni Jina la Mwanamarindi pamoja na Kaiyula nkuba ndiyo amepata kuyafahamu kwa kutumia masikio yake.

Ubao wa tatu uliandikwa hadi katikati na maneno yake yalisomeka kiurahisi ili yalikuwa magumu kueleweka.

Yalisema: Mtabuzi 1860, Mtabuzi 1960 Mtabuzi 2060.

Hapo akili ya Nelson ilianza kujaa udadisi na moyo wake ukashindwa kuhifadhi udadisi huo akajikuta anauliza,

“Hii Mtabuzi mara tatu inamaanisha nini?”

Dokta Mtabuzi aliweka kikombe chake cha chai juu ya meza na kipande cha mkate juu ya kikombe hicho, kisha alichukua kipande cha chaki na kusimama pale ubaoni na kusema

“Baada ya kujibu swali lako, naomba muulize maswali yoyote mlio nayo kunihusu ama kuhusu Mda”

Aliyua kidogo na kuchukua kipande cha mkate, kisha akakirowanisha na chai iliyokwisha anza kupoa

“Mwaka 2060, kutakuwa na Ugonjwa utakao usumbua ulimwengu na ugonjwa huu chanzo chake ni ongezeko la kemikali katika uso wa Dunia, Viumbe vyote vilivyo hai vitakuwa hatarini , ni jamii ndogo sana itakayonusurika, Dunia itakuwa si sehemu salama tena kwa viumbe wanaotamani kuishi, wala waliorundika vipande vya kutosha vya fedha na dhahabu watakuwa wameviongezea thamani zaidi.

Watakuwa wanajiandaa kuihama sayari hii adimu kwa kuwa itakuwa si adimu tena itakuwa imeharibiwa vya kutosha, Wao watakuwa wamejaribu kujenga makao katika sayari jirani, nitafanyaje kuokoa hiki kizazi kijacho ambacho leo hii hakina udadisi wowote wa usalama wa wakati ujao zaidi ya kujazwa ubunifu wa Matangazo yanayowaambia vuna leo, kula leo, fanya uwezalo leo, maana cha leo ndicho chako, cha jana kimepita na cha kesho kina wenye nacho.

Mimi sio Mtaalamu wa kila jambo ila nimeufahamu Wakati.

Mwaka 1960, ndio mwaka ambao aina ya kibinadamu ilianza kupuuza uasili wa Dunia na vitu vyake, kipande cha Fedha kikawa maalufu kuliko jambo lingine lolote utitiri wa vitu bandia ilimladi vinaingiza vipande vingi vya Fedha vikachukua atamu.

Kufikia hapa tulipo vitu vilivyokusudia kuitegemeza Dunia na Watu wake havina thamani tena vilivyopo vinalenga kusogeza jamii iliyo hai kwa uharaka na wepesi kama zilivyo Dawa za kuongeza kinga ya mwili.

(A R V).

Mwaka 1860 ndio mwaka uliowatoa machozi mengi, Waliojua maana na Thamani ya uasili wa Dunia na vitu vyake.

Damu za Watawala zilipotezwa na kuruhusu kila aliye na kipawa ama nguvu anaweza kuvitumia kuwatawala wengine, ili mradi avune vipande zaidi vya Fedha. Jamii nzima ya asili iliyeyuka na uasili wake.

Kulingana na ugunduzi huu wa Mda nina lengo la mapema la kuwarudisha au kuwaleta mahali pamoja wajadili mstakabadhi wa ulimwengu wa Miaka ya 2060, Mimi Mtabuzi ndiye nitakayekuwa naongoza kikao hiki. Nina imani kubwa mradi wangu huu utaleta matokeo mazuri.

Alimaliza Dokta Mtabuzi, huku Nelson na Anitha wakistaajabu ufafanuzi huo.

“Ulipaswa kuwa Mwalimu”

Anitha alijikuta amewaza kwa sauti, Maneno yaliyomfanya Mtabuzi kucheka kwa sauti kubwa.

“Mimi ni Mwalimu Mwalimu na hiyo ndiyo kazi yangu ya kwanza alitamka Mtabuzi kwa kujigamba.

Kuna swali lolote ambalo bado linaangaisha akili yenu?”

Aliuliza kwa uchangamfu Dokta Mtabuzi.

“Je hakuna madhara yoyote yatokanayo na kwenda na Mda?”

Anitha aliuliza kwa wasiwasi huku akitazamia kukosolewa, maana akili yake ilimwambia kama kungekuwa na madhara basi asingekubali kujiingiza katika utengenezaji huo.

Lakini jambo la ajabu alishangaa kuona Dokta Mtabuzi akimpigia makofi.

“Safi Binti yangu nilikuwa sahihi kukupatia Saa hiyo! Nilikuona toka mwanzo ulivyo na chuki na matatizo kila kitu ulimwenguni kina madhara unahitaji kipimo sahihi, Asali ni Tamu ila ukiizidisha inakuwa chungu, Ndivyo ulivyo Wakati unahitaji hekima ya hali ya juu kwenda katika Mda vivyo hivyo unahitaji hekima zaidi kujaribu kurekebisha Mda, ukifanya kwa hisia unapata maumivu, ukifanya kwa utambuzi unanufaika.

Nitatoa mfano ulio wazi ili mnielewe:

Miaka kadhaa nyuma imepita nikiwa hapa hospitalini kwangu, alikuja Kijana amembeba Binti mgongoni, Binti huyo alibakiza pigo moja tu la moyo, ili uhai wake umtoke kwa kuwa kwakuwa nilijua kwenda na Mda nilirudisha Mda nyuma ili nipate mapigo mia pekee, Ambayo yangenitosha kuiondoa sumu iliyokuwa imesambaa mwilini, Katika pigo la tisini na nane nilikuwa nimefanikiwa kuondoa sumu yote mwilini mwake, Wakati pigo la tisini na tisa likimalizika macho ya Binti huyo yalikuwa yakiliangaza vazi langu hili jeupe (Dokta Mtabuzi alikuwa akilishika shika vazi lake la kidaktari).

Mnaonaje kama ningerudi saa nne nyuma pale ofisini kwa Mkuu wa Shule ili kurekebisha Mambo, huenda nisingekuwa najibu swali hili, mbele ya Vijana wawili wenye fukuto la huba moyoni, hii ndio maana ya kutumia hekima kwenda na Mda.

Lakini pia kuna madhara ya kisaikolojia na kibaiolojia unapokutana na wewe wakati ujao au uliopita ni Dokta Mtabuzi pekee aliyegundua tiba ya jambo hilo, Ndio maana Saa zenu ni tofauti kabisa na Saa zingine, hata za wale wanotembea juu ya Mda (kwenda na Mda).

Rangi hizo mnazoziona zikibadilika ni tiba tosha ya Saikolojia na Baiolojia, ndio maana chama chetu (Taasisi yetu) ya kwenda na Mda inaitafuta mpaka leo hii , ili niwaondolee madhara hayo.

Maelezo hayo ya Dokta Mtabuzi yaliwafanya waduwae kwa Mda, Tukio lililosimuliwa na Dokta lilikuwa halisi Maishani mwao, lilichochea hisia nyingi mioyoni mwao, picha ya Nelson amembeba Anitha iliusisimua sana mwili wa Anitha, na moyo wake ulianza kuwa mlegevu, hisia za kumrukia Nelson na kumkumbatia zilimjia, Lakini kabla hajafanya hivyo Dokta aliuliza.

“Mna jambo lingine vijana wangu?

Ndio Dokta mimi ninalo!

Alitamka Nelson kwa upole,

“Kuna wakati kila kitu kinasimama hakisongi hata tone dogo la maji, ni nini hutokea mahari hapo?

Dokta Mtabuzi alinyanyua kichwa chake na kuitazama ile Saa iliyokuwa ukutani kisha Akageuka kuwatazama,

“Mwanangu kila kitu husonga kwa kufuata kani sumaku, ikiwa Dunia isingezunguka Mda usingesonga na ikiwa isingejizungusha kusingekuwa na majira, hivyo sumaku isingekuwa na maana ulimwenguni, mlango uliofungwa usingefunguliwa na siku ukiona kila kitu kimesimama, ujue mlango wa Mda umefunguliwa na hilo haliwezi kuchukua nusu Dakika machoni pa wengi, Lakini aliyeufungua humchukua Saa za kutosha kuliona tukio hilo, ikiwa hujaelewa Mwanangu , Subiri uingie katika lango hilo.”

Alimaliza kwa kupigia mstari maneno yaliyokuwa kinywani mwake ingawa mstari ulionekana ubaoni.

“Kwani Dokta ni wakati gani unafaa kurekebisha Mda?”

Aliuliza Nelson aliyekuwa amechanganywa na maneno ya Dokta Mtabuzi.

“Mlifaa kuwa katika kikao hiki, na mnafaa kuwa katika kikao kingine muhimu cha kuuokoa Ulimwengu huu, Mda ni mtambuko sana kuna mambo tunahitaji kuyajua zaidi, hatujafikia mwisho wa utafiti wa muda, kuna mambo tunayafurahia ingawa hayakupaswa yawe hivyo ikiwa ungebadili kwa kufuata hisia moyo ya wengi ungeumia, si kila wakati kosa ni lenye madhara wakati mwingine Kosa huchochea ubunifu, hukupatia nafasi ya kutafakari na kuboresha mambo, hukukutanisha na kilichomuhimu kwako na pia huchochea udadisi.

Lazima ufikirie mambo hayo yote kabla ya kulekebisha wakati.

Wote walibaki kuduwaa kwa majibu ya Dokta Mtabuzi walishindwa kuelewa kile alichokuwa akikizungumza, ingawa alikizungumza kwa lugha yao wenyewe, ila walikubaliana kuwa waliitaji Mda ili kukielewa.

Wakati Nelson na Anitha wakiendelea kuyatafakari majibu ya Dokta Mtabuzi, yeye alikuwa ubaoni akikokotoa hesabu zake ambazo, wao hawakuelewa ni hesabu za aina gani.

“Dokta”

Nelson alimkatiza Dokta Mtabuzi baada ya kuita kwa ushupavu, Baada ya Dokta kugeuka na kuwatazama alliuliza.

“Nimesikia ukisema mna Taasisi ya Watu watembeao na Mda, Taasisi hiyo inapatikana wapi? Na ni kwa nini wakutafute labda ulijiengua? Na kama ulijiengua ni nini sababu ya kufanya hivyo?

Wakati Nelson akiuliza maswali yake Dokta Mtabuzi alikuwa amemtazama kwa makini huku akitikisa kichwa chake. Dokta Mtabuzi alinyoosha mkono wake na kuuelekeza kichwani, alianza kukuna kipara chake kilichokuwa kikingaa kama kioo, na alifanya hivyo huku akijiadhari asikichafue kwa chaki.

“Kuna msemo unaosema ukiona Mtu anakutumia kwa faida yako,ujue ipo siku atakutumia kwa faida yake”

Dokta Mtabuzi aliwatazama kama Dakika mbili bila kuongea chochote vile alipomaliza zoezi tena la kukikuna kipara chake, akasema

“Hivyo ndivyo Taasisi zote zilivyo”

Alitua tena na kuwatazama kwa Dakika kama mbili huku akirudia zoezi lake la kukuna kipara chake.

Anitha hakuwa ameelewa chochote Alihisi Lugha iliyokuwa ikizungumzwa hakuwai kuisikia ingawa maneno ya lugha hiyo alikuwa akiyafahamu vizuri .

“Sasa tunafanyaje Dokta usijekupoteza uhai na kuwaumiza watu wote hao?”

Aliuliza Anitha

“Ilikurekebisha Wakati ujao, hakikisha Wakati uliopita umekaa sawa maana wakati huu uliopo ni matokeo ya wakati uliopita na unachokianza Wakati huu hicho ndicho kitakupa wakati ujao.

Bado nawasisitiza kuwa makini na Mda huu. Binti yule niliyemsimulia awali alidhamilia kuiua leo, hakufikiria kamwe madhara ya kesho Viumbe wawili watakao iokoa kesho ya ulimwengu huu wangeishia mikononi mwa Binti yule aliyekuwa ameichukua leo. Maneno yale ya Dokta Mtabuzi yalionekana kuwa magumu sana masikioni mwa Anitha na Nelson hivi kwamba walibaki kumtazama kama Mwalimu anayefundisha hisabati Saa saba mchana katika Darasa la Sanaa.

INAENDELEA....................................................
 
Big up

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
 
nipe link ya story yako niipitie
 
Ni nzuri ofcoz. Ila jitahidi kupata mjuzi wa lugha akuelekeze makosa ya kilugha ujirekebishe nayo, maana yanashusha hadhi ya kazi yako adhwim kabisa.

Ofcoz makosa madogo madogo.
 
Back
Top Bottom