Hadithi: Tabia

Chachasteven

JF-Expert Member
Jul 4, 2014
1,878
1,849
JINA: Tabia.

MWANDISHI: Chiamaro Mokiri.

Umri wake ulikuwa ni miaka 19. Alikuwa hazidi hapo. Labda kama ni chini ya hapo. Na kama ingelikuwa ni kampuni ya bima, basi wangempatia miaka mingine 60 ya kuishi. Ila mimi nilikadiria labda masaa 36, au dakika 36 ndizo alikuwa nazo kama mambo yangeenda ndivyo sivyo. Asili yake ya nywele ilikuwa ni njano na mwenye macho ya bluu, lakini hakuwa Mmarekani. Wasichana wa Marekani wana kitu fulani kwenye mionekano yao, walichorithi kutoka kizazi hadi kizazi, ambacho msichana huyu hakuwa nacho.

Bila shaka wahenga wake walikuwa wamepata kujua heshima na nidhamu. Na huo urithi alikuwa nao kwenye uso na mwendo wake. Macho yake yalionesha hofu. Mwili wake ulikuwa ni mwembamba. Sio ule wembamba ambao unaupata kwa kujua nini cha kula, hapana. Ulikuwa ni ule wembaba anaokuwa nao mtu ambaye wazazi wake wameshindwa kumudu gharama za chakula. Tembea yake ilikuwa ya kulegealegea, huku akionesha uoga ingawa alijikaza sana kuonesha alikuwa anafurahia maisha.

Binti huyu alikuwa ndani ya baa moja jijini New York akinywa bia, huku akisikiliza muziki wa bendi uliokuwa unachezwa na bila shika alikuwa amevutiwa na mpiga gitaa wa bendi hiyo. Hilo halina ubishi. Kitu pekee ambacho kilimuonesha ana hisia fulani za tofauti ilikuwa ni macho yake alipokuwa akimtazama yule mcheza gitaa. Muonekano wake ulionesha ni Mrusi. Na alionesha dalili zote za ukwasi. Alikuwa amekaa peke yake kwenye meza ya ‘VIP’ iliyokuwa karibu na jukwaa. Na alikuwa na mzigo wa pesa ambazo alikuwa anatumia kulipa vinywaji vyake bila kuomba chenchi. Mhudumu aliyekuwa anamhudumia aliufurahua sana usiku huu.

Kulikuwa pia kuna mwanamume mmoja aliyesimama peke yake kwenye kona moja wapo baani humo. Alikuwa anamtolea sana macho mwanamke huyo. Kama mlinzi wake. Alikuwa ni mrefu, mwenye mwili mkubwa akiwa kanyoa kipara. Alikuwa kavaa Tisheti nyeusi na suti nyeusi kwa juu. Huyu mwanamume alikuwa ni sababu moja wapo ya binti yule kuwa anakunywa bia baani mule licha ya umri wake kuwa miaka kumi na tisa tu. Hata hivyo, baa yenyewe haikuwa na mkazo kwenye sheria ya kuzuia watu walio chini ya umri wa kisheria wasinywe bia. Ilikuwa ipo mtaa wa Bleecker, ikiwa imejaa wafanyakazi ambao wengi pia walikuwa ni wanafunzi, kwa maoni yangu. Walikuwa wanajaribu kutafuta pesa ya kukidhi pengine ada za shule.

Nilimtazama yule binti kwa dakika moja tu, halafu nikatazama pembeni. Jina langu ni Jack Reacher, na nimewahi kuwa polisi wa wanajeshi, na ni mtu ambaye nina msimamo kwenye mambo ya wakati uliopita. Hata hivyo nimetoka jeshini kwa muda mrefu na kuingia uraini. Lakini tabia za zamani hazipotei kirahisi. Nilikuwa nimeingia baani hapa kama ninavyoingia sehemu zote – kwa uangalifu na umakini. Ilikuwa ni saa saba na nusu usiku. Nilikuwa nimetokea West Fourth kwa treni na kushukia Six Avenue kabla ya kufika hapa Bleecker na kuanza kutafuta sehemu ya kutulia. Nilikuwa nina hamu ya kusikiliza muziki na nikajikuta hapa.

Niliona watu wamejipanga mstari nje ya baa hii. Kulikuwa pia kuna Mercedes Benz ikiwa imeegeshwa kwa nje na dereva akiwa amesinzia kidogo. Nilisikia muziki unatoka ndani ya jengo la baa hii kwahivyo nikaamua nitaingia. Nilitembea nikalipa $5 na kuruhusuwa kuingia ndani.

Nilipoingia niligundua kuna milango miwili ya kutokea baani humo. Wa kwanza ukiwa ni ule nilioingilia na wa pili ulikuwa upande wa ndani kabisa upande wa korido iloyoelekea chooni. . Bar yenyewe ilikuwa upande wa kushoto, ikiwa na viti, meza na ukumbi wa kucheza muziki. Halafu kwa mbele jukwaa ambapo wanabendi walikuwa wanatumbuizia.

Bendi yenyewe ilionekana kama wamekutana kwa ajali tu. Kila mmoja alikuwa wa aina yake. Mtu wa Bass alikuwa ni mzee mmoja mweusi aliyekuwa amevalia suti na kaushi kwa ndani. Mpiga ngoma alionekana kama mjomba wake. Mwimbaji alikuwa ndiyo kituko. Alionekana mkubwa kuliko mpiga ngoma, ila mdogo kuliko mpiga Bass ingawa kiumbo aliwazidi wote.

Mpiga gitaa alikuwa tofauti sana. Alikuwa kijana mdogo tu. Na alikuwa ni mzungu. Umri wake kati ya miaka 20, na urefu kati ya futi 5 au 6. Alikuwa analichalaza gita lake haswaa.

Muziki ulikuwa mzuri lazima nikiri hilo. Wale jamaa watatu weusi walikuwa wanajua kazi yao, na yule dogo mzungu pia alikuwa anajua wakati gani aguse nyuzi ipi kwenye gitaa lake. Yeye alikuwa amevaa tisheti nyekundu na suruali nyeusi na raba nyeupe. Uso wake ulionesha yuko kikazi muda wote. Hakuwa Mmarekani. Nilimkadiria angekuwa Mrusi, pia.

Nilitumia karibu nusu ya wimbo wao kuikagua baa yenyewe, kuhesabu watu waliokuwemo, na kusoma ishara za mwili za huyu na yule. Tabia za zamani hazipotei kirahisi. Kulikuwa na mabwana wawili wamekaa kwenye meza upande kwa upande huku mikono yao ikiwa chini ya meza. Bila shaka mmoja wao alikuwa anauza kitu fulani, na mwingine alikuwa ni mteja.

Wahudumu wa baa hii pia walikuwa wanamtapeli mmiliki wake kwa kuuza bia zao sana kuliko zile za baani. Walikuwa wanachukua mbili za baa na moja waliokuja nayo wenyewe pembeni. Mimi niliagiza bia moja na kwenda kukaa nayo kwenye kiti kilichokuwa ukutani na ni wakati huu ndipo nilipomuona yule binti akiwa peke yake kwenye meza, na mlinzi akiwa hayupo mbali naye. Nilikadiria pengine ile Mercedes Benz iliyokuwa pale nje ni ya kwao. Lazima alikuwa ni binti wa tajiri mmoja hivi. Sio bilionea. Ila milionea mmoja hivi aliyewekeza mtoto wake asome N.Y.U kwa miaka minne.

Watu wawili tu wenye tofauti kati ya watu 80 waliokuwemo mule ndani. Sio tatizo hata.

Nilikuwa sahihi mpaka nilipoona jamaa fulani hivi wawili wengine.

Walikuwa kama pea. Warefu na weupe. Warusi pia. Walikuwa wapo pamoja. Hakuna shaka kabisa. Inawezekana hawakuwa bora zaidi kuwahi kushuhudiwa na ulimwengu, lakini lazima nikiri hawakuwa wabovu sana pia.

Walikuwa wamekaa kivyao kwenye meza tofauti, lakini macho yao yalikuwa yapo kwa yule binti. Walikuwa na shauku, na nia fulani ingawa kulikuwa na uoga kidogo ndani yao. Nilielewa hali yao. Mimi pia nilikuwa nimeipitia mara nyingi. Kwahivyo nilijua hawa mabwana kuna jambo walikuwa wanataka kufanya.

Kwa akili zangu nilijua, kuna mamilionea wawili walikuwa na ugomvi, na mmoja kati yao alikuwa amemwekea mwanae mlinzi na dereva, na mwingine alikuwa anatuma watu kumteka huyo mwanae. Halafu ingekuja kuombwa hela, mateso na masharti mengine ili mtoto aachiwe.

Biashara! Kwa staili kama ya Moscow.

Lakini sio biashara yenye uhakika wa kufanikiwa sana. Utekaji nyara una kanuni nyingi na mara nyingi huwa unafeli kwa sababu zaidi ya milioni. Na kwa uzoefu wangu, urefu wa uhai wa mtu aliyetekwa nyara ni masaa 36 tu. Baadhi yao huwa wanabahatika wanaachiwa uhai, lakini wengi wao huwa ni kuuliwa tu. Na baadhi hufa kwa mshtuko wa tukio lenyewe.

Pesa za yule binti zilikuwa zinawanasa wahudumu kama ulimi wa kinyonga unavyonasa nzi. Na walipokuja kumhudumia hakuwafukuza. Alikuwa anakunywa chupa moja baada ya nyingine. Na bia ni bia tu. Kwahivyo muda sio mrefu lazima angeenda uwani. Tena sio mara moja. Ni mara nyingi tu. Na korido iliyokuwa inaenda uwani ilikuwa na kiza na ndefu halafu ndiko mlango wa pili wa kutokea nje ulipokuwepo.

Niliendelea kumtazama kupitia mwanga kidogo uliokuwa unamulika huku nikisikiliza mashairi ya muziki wa wale wanabendi. Na sio mimi tu niliyekuwa namwangalia. Wale mabwana wawili walikuwa wanamuangalia. Na mlinzi wake pia alikuwa anamuangalia.

Yule binti yeye alikuwa anamuangalia tu mpiga gitaa. Walikutanisha macho ya na mpiga gitaa akatabasamu kwa aibu na kuinama. Aliporudisha uso tena, alitabasamu tabasamu pana.

Yule binti alinyanyuka. Alijivuta nyuma ya kiti na kuanza kuelekea ilipokuwa korido itakayomuongoza hadi uwani. Mimi pia nilinyanyuka kutoka nilipokuwa nimekaa na kuelekea huko pia. Kwa hatua nilizokuwa napiga nilifika huko wa kwanza. Sauti ya muziki ilikuwa kubwa bado. Choo cha wanawake kilikuwa katikati ya korido. Cha wanaume kilikuwa kwa mbele zaidi. Niliegemea ukuta na kumuangalia yule binti akija nilipokuwa. Alikuwa amevaa viatu vya kisigino kirefu na suruali ya kubana na kila hatua ya mguu aliyonyanyua ilikuwa fupi tu na alitembea kawaida. Alikuwa bado hajalewa. Alikuwa ni Mrusi usisahau. Hawa watu wana vichwa vigumu. Alipofika aliusukuma mlango wa chooni na kuingia ndani.

Sekunde kumi baadae wale wanaume wawili walifika koridoni hapo. Nilihisi pengine watamsubiria atoke chooni kwanza, lakini hawakufanya hivyo. Waliniangalia tu kama vile nilikuwa ukuta wakanipuuza halafu wakaingia ndani ya choo cha wanawake. Mmoja baada ya mwingine. Mlango ukajibamiza nyuma yao. Muziki ukaendelea kulia.

Mimi niliingia baada yao. Na nikuambie tu, kila siku huwa inakuja na jambo geni. Kiukweli nilikuwa sijawahi kuingia kwenye choo chochote cha wanawake. Hii ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza.

Yule binti alikuwa amesimama kuegemea ukuta. Na wale wanaume walikuwa wapo mbele yake wanamtazama. Walikuwa wamenipa migongo.

Nilianza kuongea, “Oya.”

Lakini hawakunisikia. Labda kwa sababu ya kelele za mziki. Hivyo niliamua kuwakamata kwenye viwiko, kila mmoja kwa mkono mmoja. Waligeuka kwa kasi wakiwa tayari kupigana, lakini ghafla wakabadili mawazo. Mimi nina mwili mkubwa na ninadhani ndicho kitu kilichowatisha. Walibaki wamesimama kwa sekunde na kuanza kuondoka. Walifungua mlango na kutoka nje.

Yule binti alibaki ananitazama kwa jicho ambalo nilishindwa kutafsiri maana yake. Tulikaa hivyo bila kuongeleshana na nikaondoka kurudi baani na kumuacha amalize shughuli yake. Nilienda kukaa kwenye meza yangu. Wale jamaa pia walikuwa wamerudi kwenye meza zao. Yule mlinzi alikuwa yupoyupo tu. Macho yake yalikuwa kwenye bendi. Na binti alikuwa bado yupo uwani.

Muziki ulisimama. Au niseme ulifika mwisho. Wale wanaume wawili walisimana na kuelekea tena kule koridoni. Na watu wengine pia walianza kusimama kwaajili ya kuondoka. Nilinyanyuka nikamfuata yule mlinzi na kumgusa begani kumsontea aelewe. Lakini hakuonesha kuelewa, hadi yule dogo aliyekuwa anapiga gitaa aliponyanyuka na yule mlinzi akanyanyuka.

Hapo ndipo nikagundua nilikuwa nimekosea. Kumbe mlinzi alikuwa ni wa yule dogo mpiga gitaa na wala sio yule msichana. Baba yake na huyu kijana alikuwa amempatia dogo wasanii wa kuimba nao kwenye jukwaa na mlinzi pamoja na dereva kwenye gari.

Na maadui wake sio watu wawili, ila watatu. Yule binti na wale wanaume wawili. Mpango makini sana. Wangemsuburi amalize kuimba halafu wamtegeshee chooni kwa mtego wa binti na kumchukua kuondoka naye.

Niliwaacha wafanye mpango wao halafu wakati ambao yule binti alianza kumkumbatia yule dogo na kuwapa muda hawa wanaume wawili waingie bafuni ndipo nikatokea. Nilimpiga mwanaume mmoja kwa nguvu na yule wa pili nilimpiga kwa nguvu zaidi kiasi damu zikanirukia kwenye shati langu kutoka mdomoni mwake. Wale wanaume wawili walianguka chini na yule binti nilimuacha akimbie. Na muda huo ndipo mlinzi wa yule dogo aliingia chooni mule. Nilimuomba anipe shati lake. Sikutaka kutembea na shati lililojaa damu. Lingezuwa mashaka sana.

Halafu nikatoka nje ya ile baa. Kwa kawaida ingetegemewa nipite kulia, ila nilipita kushoto, ambako nilipanda treni ya 6 kutokea Bleecker kwenda Lafayette. Nilipokaa nilianza tena kuchunguza nyuso za watu waliokuwa mule. Nilianza pia kuchunguza mazingira ya mule ndani ya behewa la treni. Tabia za zamani hazipotei kirahisi.

MWISHO.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom