Hadithi: Robinson Kruso na kisiwa chake

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,200
12,692
Hadithi hii ni tafsiri ya kitabu Robinson Crusoe, iliyoandikwa mwaka 1719 na muandishi muingereza, Daniel Defoe, miaka ya sitini ilitafsiriwa kwa kiswahili. Nitaiweka hapa yote, pia unaweza kuisoma bure ndani ya app ya maktaba(by pictuss) iliyopo playstore.
Ni nzuri kuisoma kujikumbusha zamani au kumsomea mwanao.
New Doc 2021-08-16 00 18 55_page-0001gg.jpg
 
SURA YA 1

1629699229584.png


Hapo kale kabla ya kugunduliwa redio palikuwa na mvulana mmoja aliyekuwa akipenda sana kusikiliza hadithi. Yeye alipenda sana namna zote za hadithi lakini zaidi hadithi au visa vya baharini. Jina la mvulana huyo lilikuwa Robinson Kruso, naye aliishi Uingereza, katika mji wa York.

Mtu yeyote alipomuuliza Robinson juu ya kazi atakayoifanya atakapokuwa mkubwa, siku zote alijibu, “Nitakuwa baharia.” Lakini baba yake alipomsikia akisema hivyo, alicheka tu maana alijua kuwa baadaye Robinson atabadili nia yake. Lakini Robinson hakubadili nia yake hata kidogo.

Aliendelea kusikilizahadithi za baharini na alipojua kusoma alisoma vitabu vyovyote alivyoweza kuvipata -si vya hadithi za baharini tu lakini hata vyenye habari za nchi nyingine za mbali. Haikutokea hata mara moja kubadili nia yake ya kusafiri baharini.

Siku moja alipopata makamo alimwambia baba yake, “Nina hakika sasa mimi ni mkubwa wa kutosha kuwa baharia. Je, nikatafute merikebu ya kufanyia kazi?”

Baba yake akacheka, akamjibu, “Mabaharia hufanya kazi ngumu merikebuni mwao.”

Robinson akajibu, “Najua.”

Baba yake akasema, “Tena mara nyingi merikebu hazina raha.”

Kijana akajibu, “Najua hilo pia.”

Baba yake akasema. “Pia kuna dhoruba na maharamia na hatari za kila namna baharini.”

Robinson akajibu, “Ndiyo, baba lakini bado ninanuia kuwa baharia. Maharamia hawatanikamata.”

Baba yake akashikwa na mshangao na kutikisa kichwa na kusema, “Kafikiri tena, labda utabadili nia yako baadaye.”

Robinson akajaribujaribu . Hakukuwa na lolote alilopenda zaidi kuliko kusafiri baharini. Lakini baba yake alizidi kupinga.

1629699278166.png


Robinson alikuwa na rafiki mmoja ambaye baba yake alikuwa na merikebu. Siku moja huyo rafiki yake alimwambia, “Nitasafiri kwenda London katika merikebu ya baba. Utakuja kunisindikiza?”

Robisnon akajibu, “Ndiyo nitakuja. Tena natamani sana kusafiri pamoja nawe.”

Rafiki yake akajibu, “Ndiyo. Njoo tu. Chumba changu kina nafasi ya kututosha sote wawili.”

Basi marafiki hao walipofika bandarini Hull, ilikotia nanga ile merikebu, Robinson aliingia merikebuni atazame kile chumba cha rafiki yake. Alisisimkwa kuwamo ndani ya merikebu badala ya kusoma habari zake tu hata akanuia kukaa humo kabisa.

Akamwambia rafiki yake, “Ndiyo, lazima tutakwenda London pamoja. Nitampelekea habari baba kumjulisha niliko na kwamba nasafiri baharini.”

Rafiki yake akacheka akasema, “Vizuri; nina hakika mimi na wewe tutakuwa na furaha.”

Kweli walikuwa na furaha. Mabaharia wote walikuwa wachangamfu. Baada ya kazi zao mmoja alizoea kupiga fidla yake na wengine wakiimba nyimbo za kibaharia.

1629699307513.png


1629699329513.png



Robinson aliona maisha hayo ni ya ajabu. Kwa muda kila jambo lilikwenda sawa, lakini mara ghafla kukatokea dhoruba. Merikebu ilisukasuka na kwenda mrama . Robinson alishikwa na kizunguzungu na kutapika.

Akajuta na kusema, “kwanini nimekuja humu.”

Basi alilala chumbani mwake akiwa mgonjwa sana. Wale mabaharia wote walishughulika na kazi zao wala hawakupata nafasi ya kumchangamsha.

Kabla merikebu ile haijafika London iliharibika, ikabidi ikae katika bandari moja kwa muda mrefu. Basi Robinson alimuacha yule rafiki yake, naye akaendelea kwenda London kwa njia ya nchi kavu.

1629699374478.png
 
SURA YA 2

Robinson alipofika London tu alisahau alivyotaabika wakati wa ile dhoruba baharini. Mara akatafuta merikebu nyingine. Siku moja alimkuta nahodha aliyekuwa amerudi karibuni kutoka pwani ya Guinea ambayo ni sehemu ya Afrika.

Nahodha yule alimwambia Robinson, “Nitarudi huko hivi karibuni. Je, utapenda kwenda nami ?”

Tukichukua vitu vya kuchezea watoto na shanga kwa watu wazima wa huko, wao watatupa dhahabu, nasi tutatajirika.”

Robinson alijibu, “Naam, tutakwenda pamoja pwani ya Guinea.”

Basi walisafiri katika merikebu ya yule nahodha. Ilipakia bidhaa ya vitu vya kuchezea watoto na shanga. Watu wa huko walivipenda sana vitu hivyo, nao walikuwa na kawaida ya kutafuta dhahabu mitoni na kuibadilisha kwa vitu hivyo,

Robinson na yule nahodha walifanikiwa sana. Robinson alipata dhahabu nyingi ya kumtosha kumfanya awe tajiri, lakini aliona heri aende tena pwani ya Guinea.

1629699551218.png


Lakini safari hii merikebu moja ya maharamia iliwajia ikawateka mabaharia wote pamoja na Robinson. Ikawabidi kuwatumikia maharamia wale. Mkuu wa maharamia wale alimchagua Robinson awe mtumwa wake maalum. Alimpeleka katika nchi yake ambako ilimbidi Robinson kufanya kazi nyingi na kufanya kama alivyoambiwa. Hakuipenda hali hii, basi siku moja alitoroka kwa mashua ndogo ya kuvulia. Alikwenda kwa mashua hii karibu karibu na pwani, alipoona njaa alikwenda nchi kavu na kuchuma matunda. Siku moja alimwua simba kwa bunduki na ngozi yake akajitengenezea tandiko.

1629699584907.png


1629699602751.png


Kisa hiki kilikwisha wakati merikebu moja ya watu wema ilipomchukua. Nahodha wa merikebu hiyo alipoona kwamba Robinson hana fedha, alimsikitikia. Akanunua ile mashua na ngozi ya simba ili Robinson apate fedha ya kutumia atakapofika Brazil, Amerika ya Kusini, ilikokuwa inakwenda ile merikebu.

Robinson akasema, “nitakapofika Brazili tu, sitakwenda tena baharini. Baba yangu aliniambia kuwa yatakuwa maisha ya hatari, na ni kweli. Nitanunua ardhi niwe mkulima.”

Basi hivyo ndivyo Robinson alivyofanya. Alinunua ardhi, akawa mkulimma wa miwa na tumbaku. Kwa muda mrefu alikuwa na furaha. Lakini baadaye alianza kuwa na nia ya kurudi baharini. Mwishowe alimuomba jirani yake amtunzie shamba lake naye akasafiri baharini kuendea Afrika. Hapo ndipo Robinson alipoanza kupatwa na mambo makubwa kupita yote.
 
SURA YA 3

1629699884113.png


Maskini Robinson! Merikebu ile baada ya kusafiri kwa siku chache tu, ilipigwa na dhoruba kubwa kwa ghafla. Ikakwama katika fungu la mchanga na haikuweza kusafiri tena. Basi mabaharia waliingia mashuani kwenda kwenye kisiwa kimoja ambacho waliweza kukiona hakiko mbali.

Upepo ulivuma na mvua kubwa ikanyesha. Mawimbi yalikuwa makubwa sana, na ile mashua ilisukasuka kama jani tu juu ya maji. Mabaharia walijitahidi kupiga makasia yao kwa nguvu zote.

Lakini bahari ilichafuka hata ile mashua ikapinduka. Watu wote waliokuwamo walikufa maji isipokuwa Robinson Kruso tu peke yake, ambaye aliogelea kwa nguvu katika mawimbi yale ya kutisha mpaka mwishowe aliweza kujikokota mpaka ufukoni pa kisiwa kile.

1629699913178.png


Robinson akachoka sana kwa kuogelea.

Alipumzika kwa muda mchangani mpaka akaona kuwa usiku utaingia mara.

Akasema, “sasa nitafute mahali pa kulala pa salama kwa kujihadhari na wanyama mwitu wakali. Mti ule kule utanifaa kwa kulala juu yake, nitaupanda nilale mpaka asubuhi.”

1629699942591.png

1629699964677.png




Basi Robinson aliupanda ule mti akapata mahali pa kulala pazuri penye panda madhubuti. Muda si muda akapata usingizi mzito.

Asubuhi alipoamka, ile dhoruba ilikuwa imekwisha; akashuka chini ya ule mti

Alitweta akasema , “Ah, naona taabu sana! Mti ule si laini kama kitanda chenye tandiko. Tena naona njaa. Nitapata wapi kitu cha kula?”

Mawimbi yalikuwa yakipigapiga mchangani na bahari ilikuwa shwari. Kulikuwa hakuna kiumbe chochote chenye uhai ila mbayuwayu. Mbele kidogo Robinson aliona ile merikebu iliyokuwa imekwama mchangani.

Akasema, “Mna chakula mle merikebuni. Nitaogelea mpaka kule nikaone nitakachoweza kupata.”

Basi akaogelea kwenda merikebuni. Alipokuwa anaogelea alifikiri , “Labda itanibidi kukaa katika kisiwa hiki kwa muda mrefu kabla sijaokolewa. Kwa hiyo, itanibidi nijenge kibanda kiwe ndiyo nyumba yangu. Pia lazima nichukue vyombo vingine kutoka humo.”

Robinson alikuwa na furaha sana alipoona kwamba mbwa wa mle merikebuni alikuwa hai bado. Mbwa yule aliruka kumsalimia Robinson. Robinson alimpapasa kirafiki na kumwambia , “Oh, mbwa mwema. Tutaishi kisiwani pamoja, lakini kwanza na tule chakula.”

1629699999437.png

1629700027236.png




Robinson alitafuta huku na huku na kwa bahati akaona biskuti na nyama. Alikula vitu hivyo na yule mbwa, pia na paka wawili waliokuja pale.

Robinson akacheka, “Ahaa, sasa tumekuwa jamaa nzima. Ninyi paka nitawaita Tim na Tom. Nawe mbwa nitakuita Mbwa. Sasa na tutazame tutakavyovichukua kuvipeleka kule kisiwani.”

1629700060406.png


Alitengeneza chelezo kwa vipande vya mbao, kisha akakishusha baharini. Juu yake akaweka sanduku kubwa lililokuwa na vyombo, bastola na baruti, mifuko, mapipa ya vyakula na tanga. Mwisho alimuweka yule mbwa na wale paka. Chelezo kilipakiwa sana hata kikawa karibu kuzama lakini kilifika pwani salama.

1629700085418.png
 
SURA YA 4

Kwa siku chache zilizofuata, Robinson Kruso alikuwa na kazi nyingi. Lile tanga alilitengeneza hema. Kisha alilisimika karibu na pango penye kijito cha maji. Aliweka chakula chake na baruti ndani ya pango lile ili baruti ikauke. Kisha alitengeneza meza moja na kiti avitumie mle hemani.

Wakati wowote bahari ilipokuwa shwari Robinson alikwenda kwa chelezo chake mpaka merikebuni na kuchukua chochote alichoona kitamfaa.


1629764115240.png



Aliendelea kufanya hivyo mpaka usiku mmoja bahari ilichafuka mno, hata asubuhi yake ile merikebu ilikuwa imevunjikavunjika na hakukua na chochote kilichobakia.

Robinson alitumia wakati mwingi kwa kutengeneza vyema hema lake. Alikuwa na chakula cha kutosha ingawa hakikuwa kizuri. Pia aliweza kupata matunda karibu karibu.
1629764158069.png



Alikuwa na mengi ya kufanya basi wakati ukapita haraka haraka. Ila alikuwa na wasiwasi mmoja; nao ni kwamba atakaa katika kisiwa kile kwa muda gani kabla hajaokolewa….miezi au miaka ?

Akasema, “Afadhali nihesabu siku ili nijue tarehe na siku za jumapili.”

Basi alisimamisha mti mrefu na kila asubuhi alitia alama na kwa kila jumapili alikata alama kubwa zaidi. Mti ule ulikuwa kama kalenda kwake.

1629764188348.png


Kwanza alitumia wakati mwingi akikaa kwa juu ya kilele cha kilima akitumaini kuona merikebu yoyote ikija upande ule. Lakini hatimaye alikata tamaa ya kuokolewa kwa upesi, maana hakukuwa na merikebu iliyoonekana.

Wale paka wawili walitembeatembea kwa furaha mwituni. Humo hamkuwa na wanyama mwitu wakali ila mbuzi, na hao hawakuwadhuru paka. Pengine mbwa alikwenda kuwinda peke yake lakini mara kwa mara alipenda kukaa na Robinson.

1629764212366.png


Siku moja Robinson alimpigia mluzi mbwa akamwambia , “Njoo, leo sitafanya kazi yoyote. Tutapumzika. Wewe na mimi tutatembea kisiwani humu tuone sehemu nyingine zilivyo.”

Basi Robinson alichukua chakula na bunduki, kisha wakaenda zao wakapitia mwituni, ambamo mlikuwa na maua mengi mazuri. Safari moja wakaona kundi la ndege wazuri sana ambao hajapata kuwaona na safari nyingine aliona kundi la kasuku.

Baada ya kutembea huku na huku wakipanda milima na kushuka wakatokea mahali palipokuwa wazi. Mahali hapo palipendeza sana hata Robinson alipopaona tu akakata shauri kuishi hapo.

1629764304154.png


Akasema, “Mbwa, hapa ndipo nitakapojenga kibanda kitakachokuwa nyumba yetu ya shamba. Je, rafiki yangu unapenda shauri hili ?” Mbwa alitikisa

Mkia wake kwa furaha kama vile anajibu, “Nimekubali.”

Robinson akaendelea kusema, “Ndiyo naweza kuwinda mwituni na kuchuma matunda. Tazama, hata mizabibu ipo. Nitaweza kuzikausha ili tuzile wakati wa shida ya matunda.”

Robinson aliona kwamba palikuwa na miti bora ambayo aliweza kuitumia kujengea kibanda chake. Basi siku moja akaanza kukata miti kwa shoka na kazi ya kujenga kibanda ikaanza. Alikata miti mingi ili atengeneze kitanda na viti. Vyote hivyo aliviweka kibandani.

1629764332416.png


Kibanda kilipomalizika Robinson alikionea fahari kwa uzuri wake. Akapanda miti kukizunguka. Hali ya hewa ilikuwa nzuri na ile miti mara ikasitawi. Baada ya muda mfupi tu pakawa na ua madhubuti wa kuweza kumkinga adui yeyote. Robinson alijitengenezea njia ya siri ya kumfaa yeye mwenyewe tu. Kwa hiyo alijiona yu salama.

Akasema, “kwa kuwa nina makazi mawili nitakuwa na raha hata nikikaa hapa kwa muda mrefu. Nitakuja kwenye kibanda kwa mapumziko.”

1629764375088.png
 
SURA YA 5

Siku moja Robinson aliona vichipukizi vya mimea vikiota pale mahali alipokuwa amemwaga punje za mpunga na nafaka alizokuwa ameleta toka merikebuni, na mara mimea ikakua pale.

Akastaajabu sana akasema, “Ama, nitaweza kupanda mpunga na kuchoma mikate kwa nafaka yangu mwenyewe! Nitalima kijishamba mara moja na kupanda mbegu.”

Basi ingawa Robinson alikuwa na vifaa vya kujengea, lakini hakuwa na chombo cha kuchimbulia. Basi alitafuta mti mgumu sana, akatengeneza sepeto. Akalitumia sepeto hilo kuchimbulia ardhi iliyozunguka hema na kibanda chake. Akapanda miti ya matunda, mpunga na nafaka. Mara akawa na bustani nzuri. Alikata miti ili apate nafasi ya kulima mashamba na mara akawa na shamba moja kubwa. Alikamata mbuzi mwitu na kuwafuga. Kwa hiyo siku zote aliweza kupata maziwa na jibini. Aliweka jibini na maziwa hayo katika vyombo alivyovitengeneza kwa udongo wa mfinyanzi na kuvichoma. Robinson Kruso alitengeneza jibini kwa yale maziwa nayo akaitumia kwa kulia mkate uliotengenezwa kwa unga uliosagwa uliotoka shambani mwake.

1629764746311.png

1629764764771.png




Alikamata kasuku mmoja mwituni akamfundisha kusema. Kwa hiyo aliweza kusikia sauti ya kiumbe. Jambo hili lilimtoa upweke Robinson ambaye alikuwa hana mtu yeyote wa kuzungumza naye.

1629764807037.png


Baadaye alikata shauri kutengeneza mtumbwi ili autumie kwenda nchi nyingine ambako kuna watu.

Alikumbuka kwamba katika visa alivyopata kusoma, watu walitengeneza mitumbwi ya magogo. Basi alikata mti mkubwa na akakomba gogo lake. Alitengeneza mashua kubwa ili itoshe kuchukulia vitu vyake vyote kuvuka bahari.

Lakini alipokwisha maliza kutengeneza mashua ilikuwa kubwa mno na nzito hata hakuweza kuifikisha majini. Aliisukuma kwa nguvu zake zote, lakini mashua haikusogea popote.
1629764844304.png



Akasema kwa huzuni, “Ole wangu ! muda wangu wote nimeupoteza bure. Sasa itanibidi nianze mambo yote upya nitengeneze mashua nyingine.”

Safari ya pili alichagua mti mdogo akatengeneza mashua ambayo aliweza kuikokota kwa urahisi. Lakini haikufaa kwa safari ndefu, ilifaa kwa kuvulia samaki tu na kutembelea kando ya pwani.

1629764865969.png


Wakati huo nguo za Robinson zilikuwa kuukuu mno na akatambua kwamba hataweza kuendelea nazo kwa muda mrefu.

Akasema, “Sina budi kupata kivazi. Lakini nitavaa nini. Sina nguo.”

Alitingwa na jambo hilo kwa muda mrefu. Kisha akakumbuka ngozi za mbuzi alizokuwa ameziweka kibandani. Alizitafuta kwa haraka akaziona.

Akasema, “Kama zilikuwa zikiwahifadhi mbuzi kwa jua na mvua , basi hata na mimi zitanifaa.”

Alizitazamatazama, alizichagua zile zilizokuwa bora, kisha akajitengenezea koti na kaptula kwa ngozi hizo, na kofia moja ya kuchekesha. Hivyo, aliweza kukamilisha kivazi chake . Baada ya hayo alitengeneza mwamvuli wa kumhifadhi na jua na mvua , nao aliupenda sana.

1629764909634.png


Robinson alicheka sana alipovaa nguo zake za ngozi ya mbuzi kwa mara ya kwanza.

Alichekelea akasema, “Kama mtu akija kuniokoa sasa, itanibidi kusema upesi, au sivyo atafikiri mimi ni mbuzi, hasa kwa hivi nilivyoota ndevu.” Mbwa naye pia alicheka.

1629764956415.png


Basi
1629765000198.png
pamoja na kibanda, shamba, mashua na nguo zake za ajabu aliishi katika kisiwa kile kwa muda mrefu sana. Baadaye wale marafiki zake, Tim, Tom na mbwa, walikufa mmoja mmoja kwa uzee baada ya kuishi naye kwa furaha sana. Lakini alibakiwa na yule kasuku. Wakati alipokwenda matembezini, kasuku alikaa begani pake.

Siku moja Robinson alikuwa akitembea ufukoni, na mara alisimama akatazama mchangani kwa mshangao. Mbele yake kidogo palikuwa na alama ya unyayo wa mtu. Alama hiyo haikuwa yake

Robinson alitweta akasema, “Kafika hapa mwanadamu mwingine. Huyu ni nani, na hivi sasa yuko wapi?”
 
SURA YA 6

Robisnon Kruso alitazama huku na huku akafikiri labda adui aweza kumrukia, lakini hapakuwa na mtu yeyote isipokuwa yule kasuku wake, ambaye alilia, “Robin, Robin!” Alipokuwa akilia kasuku huyo alisugua mdomo wake penye shavu la Robinson.

Katika siku na majuma yaliyofuata, Robinson wakati wote alikuwa na wasiwasi katika kisiwa chake. Kwa hiyo ilimbidi ajilinde asishambuliwe na adui ghafla.

Siku moja alikuwa kilimani karibu na nyumbani kwake. Alipoangalia pwani aliona mitumbwi ikija kuelekea ufukoni. Alijificha mwituni karibu na ufuko. Mara mitumbwi ikafika ufukoni na wakashuka washenzi wakali sana, nao walikuwa na wafungwa ambao walikuwa wakiwatendea ukatili sana.

Robinson aliwaangalia wakati walipokoka moto mkubwa tayari kwa kula karamu yao na kucheza. Akafikiri, “Sijui alikuwa mmoja wa wale walioacha alama ya unyayo mchangani.”

Kisha alimuona mfungwa mmoja akijitahidi kujifungua kamba alizofungwa. Mtu yule aliruka ghafula akawakimbia washenzi wale wakali kama alivyoweza. Alipokuwa akikimbia hivyo wale washenzi walimtupia mikuki lakini hakusimama na wala haikumpata.

1629863869300.png

1629863894868.png




Robinson akawaza, “Sina budi kumsaidia mtu yule.” Basi alitoka mle mwituni, aliinua bunduki yake akawapiga wale washenzi ambao walikuwa wakimfukuza yule mfungwa. Watu wale walishikwa na hofu sana kwa bunduki ile, wakamwacha yule mfungwa aende zake. Wao wenyewe wakaingia ndani ya mitumbwi yao hali wakitambaa na kukimbia upesi.

1629863920162.png


Yule mtu mweusi aliyekuwa mfungwa wao, alipiga magoti mchangani. Kisha akaibusu miguu ya Robinson kuonyesha kwamba amekubali kuwa mtumwa wake.

1629863953139.png


Robisnon alichekelea akasema, “Njoo simama!” Yule mtu alielewa maana ya maneno ya Robinson ingawa hakufahamu maneno yenyewe. Alisimama akangoja.

Robinson akasema tena. “Njoo.” Naye akaanza kwenda upande ule wa kwenye kibanda, alimpungia mkono na yule mtu akaanza akumfuata.
1629863977083.png



Robinson alikwenda na furaha kwa kumuokoa mtu huyu. Walipokuwa wanakwenda aliwaza, “Atakaa nami na nitamfundisha kusema kiingereza.”

Yule mtu mweusi alikuwa na njaa sana. Tena alikuwa amechoka sana baada ya msukosuko alioupata. Basi Robinson alimpa chakula akamuonyesha mahali pa kulala. Alipoamka Robinson akakata shauri kwamba ni wakati wa kupeana majina.

Akasema . “Mimi Robinson,” huku akijionyeshea kidole, “Robinson.”

Yule mtu mweusi akainamisha kichwa chake . Alijibu polepole, “Robinson, Robinson.”

Kisha yule mtu akajinyoshea kidole kifuani pake akasema maneno fulani ambayo Robinson hakuweza kuyafahamu maana hakujua lugha yenyewe.

Alicheka akasema, “Sitaweza kabisa kusema hivyo. Hebu kwanza – nitakuita kwa jina la siku niliyokupata…Ijumaa.”

Basi jina la mtu yule likawa Ijumaa. Akawa mtumishi na rafiki muaminifu wa Robinson. Kila siku alijifunza maneno machache ya kiingereza mpaka akaweza kuongea na Robinson. Jambo hilo lilimfurahisha sana Robinson, maana alikuwa amekaa kwa muda mrefu bila ya kuwa na mtu wa kuzumngumza naye.

Alimuonyesha Ijumaa jinsi ya kutumia vyombo, na jinsi ya kutunza shamba na wale wanyama.

Siku moja Ijumaa alimwita Robinson , Je, huyu ndege wa ajabu anayezungumza naye nimpe chakula?”

Robinson akajibu, “Ndiyo waweza kumpa huyu kasuku mbegu. Huyu ni mpole. Hatakuuma.”

1629864009669.png


Alipoona kuwa Ijumaa aweza kuaminika kuchukua bunduki, alimfundisha jinsi ya kuitumia ili waweze kwenda kuwinda pamoja.

Kulikuwa na mambo mengine ambayo Ijumaa alimfundisha Robinson. Alimfundisha kutengeneza mtumbwi na mikuki ya kuvulia samaki, na jinsi ya kupanda minazi na kuangua nazi pevu.

1629864044026.png


Wakati walipokwenda kuwinda, Robinson alivaa mavazi yake ya ngozi za mbuzi, lakini maskini Ijumaa hakuwa na chochote cha kuvaa. Mvua iliponyesha, maji yalimwingia katika nywele zake na kutiririka katika ngozi yake. Yeye mwenyewe Ijumaa hakujali. Lakini siku moja Robinson alisema, “Lazima nawe uwe na mavazi kama yangu ya kukuhifadhi na jua na mvua.” Basi wote wawili wakaanza kumtengenezea Ijumaa mavazi ya ngozi ya mbuzi. Yalipokamilika na alipoyavaa, Ijumaa alirukaruka na kucheza kwa furaha.

Akasema kwa kiingereza kibovu, “Mimi kama wewe, bwana.”

1629864069711.png


Ijumaa alitaka kujua habari zote za nchi ya wazungu, na Robinson alimsimulia habari za miji na za merikebu zilizoweza kuvuka bahari kuu. Ijumaa alimwambia habari za watu wa kwao wanaoishi katika kisiwa kingine.

Robinson akastaajabu , akasema kwa nguvu, “Watu weupe! Labda hao ni mabaharia waliovunjikiwa na merikebu. Nitakwenda kuwatazama.
 
SURA YA 7

Robinson akatengeneza mashua moja kubwa ya kutosha kuvuka bahari akaonane na wale watu weupe. Siku moja, kabla mashua hiyo haijamalizikakwisha, Ijumaa alimwendea Robinson mbio akamwambia, “Bwana! Ah, huzuni! Ah vibaya!”

Robinson akamuuliza, “Je, kuna nini Ijumaa? Kumetokea nini?”

Ijumaa akasema akitweta, “Kule !” alionyesha kidole baharini, “Mitumbwi mitatu inakuja.”

Robinson aliwaza, “Je, washenzi wakali wanakuja tena !” Akatoa bunduki zake mbili upesi. Moja akampa Ijumaa, kisha wote wawili wakajificha pwani na kuchungua.

Ile mitumbwi ikakaribia na wale washenzi wakashuka nchi kavu. Robinson aliweza kuona kwamba walikuwa na wafungwa wengine na mmoja alikuwa mzungu. Akapiga kelele, “Ijumaa, njoo, piga.”
1629864213019.png



Robinson na Ijumaa wakapigana na wale washenzi mpaka wakakkimbia na mitumbwi yao, wakimwacha yule mfungwa mzungu na mwingine mtu mweusi wamelala chini na kamba zao na mtumbwi wao mmoja. Ijumaa alifurahi sana kuona kwamba kumbe yule mfungwa mweusi ni baba yake. Basi wote wawili walikuwa na furaha sana. Ijumaa akamwambia baba yake kuwa Robinson alikuwa ni bwana mwema na mkarimu kwake.

1629864240385.png


Baba yake Ijumaa alifurahi sana kumwona Ijumaa katika hali njema na mwenye furaha maana alifikiri alikuwa amekwisha uawa na wale washenzi zamani.

Yule mfungwa mzungu alikuwa ni mhispania, naye akamwambia Robinson kwamba kuna wahispania wengine waliovunjikiwa na merikebu zao huko washenzi walikokuwa wanaishi. Ijumaa alikwisha kumwambia Robinson jambo hilo.

Yule mhispania na Robinson wakafanya shauri la kuwaokoa wale wahispania wengine kutoka katika kile kisiwa cha washenzi wakali na wawalete kwenye kisiwa cha Robinson Kruso. Kwanza iliwabidi kupanda chakula cha kutosha kuwalisha watu wengi zaidi.

Walipokwisha kufanya hivyo yule mhispania na baba yake Ijumaa waliondoka kwa ule mtumbwi, wakiwa na bunduki mbili za Robinson.

Walipokuwa wanaagana yule mhispania alicheka akasema, “Tutarudi baada ya wiki mbili. Tutengenezeeni karamu.”

Wakati ule Robinson hakujua kwamba hatamwona tena yule mhispania, maana lilitokea jambo wasilolitazamia kabla ya kurudi kwao.


1629864267722.png
 
SURA YA NANE

Kama wiki moja hivi tangu kuondoka yule mhispania, Robinson aliona merikebu ikija kuelekea kisiwani kwake. Robinson kwanza alitaka kuwasha moto mkubwa na kupanda juu ya kilima ili awavute waje kule. Lakini baadaye akasita.

Akamwambia Ijumaa, “Lazima tujihadhari, labda ni meli ya maharamia. Kwa hiyo tutajificha tuone ni watu wa namna gani. Inaelekea kama kwamba wanakusudia kushuka hapa.”

1629864432209.png

1629864473091.png




Walijificha mwituni kama kwanza. Wakaona kikundi cha mabaharia wakija pwani, watatu wao walikuwa wamefungwa kamba mikono nyuma. Ilikuwa ajabu sana maana mmoja wa wale watatu alikuwa amevaa mavazi ya kinahodha.
1629864506919.png



Yule nahodha alisema kwa sauti, “Siku moja Mungu atakulipeni kwa uovu huu, enyi watu wabaya.” Lakini wale waliokuwa wakimlinda hawakujali kitu. Waliinua bastola zao na kumhimiza aende upesi ufukoni.

Joto lilikuwa kali mno hata mara baada ya wale mabaharia kufika pwani, walilala chini na usingizi ukawachukua na huku wamewaacha wafungwa wao chini ya miti. Ndipo Robinson na Ijumaa wakatambaa mpaka kwa wale wafungwa. Kwanza wafungwa waliogopa kuona watu wawili wamevaa mavazi ya ngozi za mbuzi na kila mmoja akiwa na bunduki.

Robinson akanong’ona, “Msiogope. Mimi ni mzungu kama nyinyi. Nimekuja kuwasaidieni .”

1629864562576.png


Mtu yule alimwambia Robinson kwamba yeye ni nahodha wa merikebu ile, lakini wale mabaharia walitaka kumtupa yeye na wenziwe wawili pale kisiwani na wao wachague nahodha mwingine wampendaye, waende zao.

Robinson akasema, “Lakini huo ni uasi, si haki kutenda hivyo. Merikebu lazima iwe na nahodha mmoja tu. Tutakufungua kamba wewe na rafiki zako. Na tutakupeni bunduki mpigane na hao waovu.”

Yule nahodha akasema, “Asante sana rafiki yangu. Na kwa msaada wako huu tutakwenda sote nyumbani Uingereza.”

Basi wale mabaharia walipoamka, waliwaona wale wafungwa wao na Robinson wamesimama kiume na bunduki zao. Vita kali ikatokea lakini wale mabaharia wakashindwa.

1629864590812.png


Wakasema, “Tuhurumieni, tuhurumieni! Tunasikitika kwa mambo tuliyotenda , tumetubu.”

Yule nahodha aliwasamehe wengine, lakini akasema wale waliokuwa waovu zaidi lazima wakae pale kisiwani na iwe ndiyo adhabu yao.

1629864618466.png


Robinson akawaambia, “Nitawaelezeni jinsi ya kulima chakula. Nami nitawaachieni vyombo vyangu. Basi mtaishi vema hapa kuliko nilivyoishi mimi nilipokuja hapa kwanza. Na labda siku moja merikebu itakuja kuwaokoa.”

Wale watu walinung’unika, lakini walijua wazi kwamba kama yule nahodha atawarudisha merikebuni mpaka Uingereza, watapata adhabu kali zaidi. Basi waliona heri wafuate yale waliyoambiwa na Robinson.

Yule nahodha akamwambia Robinson kwamba anasikitika hawezi kumngojea yule rafiki yake mhispania na watu wake maana merikebu yake ilikuwa imekwisha chelewa mno.

Robinson akasema, “Nitamwachia barua, naye atafahamu. Yeye atawaangalia watu hawa na kutawala kisiwa hiki.”

Basi Robinson Kruso alimchukua rafiki yake Ijumaa na kasuku wake. Ijumaa aling’ang’ania waende pamoja Uingereza. Baada ya Robinson kufika Uingereza, aliuza shamba lake lililokuwa Brazil na akapata mali ya kutosha. Watoto wadogo wakazoea kwenda nyumbani kwake wakati wa jioni na kumsikiliza akiwasimulia visa vyake vya ajabu.


1629864657004.png

1629864696016.png

1629864735881.png
 
Back
Top Bottom