Hadithi Muathirika Wa Ngono

SEHEMU YA 22

“This is the one,” (ndiye huyu sasa) alisema Kenji huku akimtambulisha Bhoke mahali hapo.
Hakujua maisha ya msichana huyo, ni kwamba alikutana naye kwenye ndege tu, alihisi kuwa alikwenda Nairobi kwa biashara zake nyingine kumbe mwenzake alifika hapo kwa ajili ya kujiuza tu.

Kwa jinsi Kenji alivyokuwa na pesa, aliamini hata marafiki zake hao walikuwa na pesa pia hivyo alizitaka, hata kama kungekuwa na uwezekano wa kulala na wote, alikuwa tayari.

Kazi ya Bhoke mahali hapo ilikuwa ni kujishembendua tu, alikuwa akileta mapozi ya kike yaliyowafanya wanaume wote kutamani kuwa naye.

Stori ambayo waliambiwa na Kenji kwamba msichana huyo alikuwa si mchezo faragha ziliwachanganya kupita kawaida na kila mmoja mahali hapo alihitaji kulala naye.

Walikuwa wakinywa pombe, muda mwingi Bhoke alimmiminia pombe Kenji na kumtaka kunywa mfululizo, marafiki zake walikuw wakishangaa kwani halikuonekana jambo la kawaida kwa mwanamke kama huyo kumlazimisha Kenji kunywa pombe nyingi kiasi hicho.

Kichwa cha Bhoke kilifikiria pesa tu, hakukuwa na kitu kingine ambacho kilikuwa kichwani mwake muda huo.

Alihitaji pesa za wanaume wengine mahali hapo na ndiyo maana njia nzuri ambayo aliiona kufaa ilikuwa ni kumlevya Kenji ili apate muda wa kuzungumza na hao wanaume wengine.

Ni ndani ya nusu saa tu, Kenjia alikuwa hoi, alikuwa hajiwezi, kazi yake ilikuwa ni kupiga kelele mfululizo kama mtu aliyechanganyikiwa. Hicho ndicho alichokitaka Bhoke, hivyo akaanza kudili na wanaume hao.

“I prefer sex than eating and drinking...” (napenda sana ngono kuliko kula na kunywa...” aliwaambia wanaume hao maneno yaliyoonekana kuwashtua sana.

“Sure?” (kweli?) aliuliza jamaa mmoja huku akionekana kushtuka.
“Try me...” (nijaribu) alisema Bhoke.
“How much?” (kiasi gani?)
“15000 Kenyan shillings...” (shilingi elfu kumi na tano ya Kenya) alijibu Bhoke, kiasi hicho kwa pesa ya Kitanzania ilikuwa ni zaidi ya laki tatu.
 
SEHEMU YA 23

Kilikuwa kiasi kikubwa lakini kwa jinsi Kenji alivyokuwa amemsifia msichana huyo, hakukuwa na mtu aliyetaka kuona akiondoka pasipo kulala naye.

Mwanaume mmoja miongoni mwa hao watatu waliokuwa mahali hapo akaingiza mkono mfukoni na kutoa pochi iliyokuwa na noti kadhaa na kumpa msichana huyo.

Hapo hotelini kulikuwa na vyumba, akamchukua Bhoke na kuondoka naye huku msichana huyo akichukua namba za simu za wanaume waliobaki na kuwaambia kwamba angewatafuta.

Hapo ndipo walipogundua kwamba Bhoke alikuwa malaya aliyekuwa akijiuza na hakuwa ‘wife material’ kama alivyotamba Kenji alipokuwa akizungumza nao.
Huko chumbani mambo yalikuwa moto, hiyo ilikuwa ni kazi yake, mbali na kuwashwa sana mwili lakini alipenda mno kufanya ngono kuliko kitu chochote kile.

Mwili wake uliathiriwa na matumizi ya ngono, hakuzoea kukaa siku mbili bila kufanya mapenzi. Alipenda ngono zaidi ya mbwa na kila alipokuwa akiifanya, aliifanya kwa nguvu zote kwa kuwa alijua ndiyo kitu pekee kilichokuwa kikimpa pesa za kumfanya aishi.

Mwanaume ambaye alikwenda kulala naye, siku iliyofuata aliwaambia wenzake kwamba Bhoke hakuwa msichana wa kawaida, alitisha kwani kitandani alijua michezo yote kiasi cha kumfanya kuhema kama mbwa.

Huko Nairobi Bhoke alikaa kwa siku kadhaa, akatengeneza milioni tano na kurudi jijini Dar es Salaam ambapo aliendelea kujiuza kama kawaida.
*** “Halo! Upo wapi Johnson?” ilisikika sauti kutoka kwa mwanaume mmoja upande wa pili wa simu.

“Nipo hosteli!” “Naweza kukuona?”
“Sasa hivi?”
“Ndiyo!”
“Haina shida.”

Johnson alikuwa akiongea kwa simu na mwanaume ambaye alimfahamu kabisa. Walizungumza kwa sekunde chache tu na kukata. Harakaharaka akaamka kutoka kitandani, akaelekea bafuni na kuanza kuoga. Kichwa chake kilijiuliza maswali mengi juu ya ile simu aliyokuwa ameipokea.

Ilitoka kwa mwanaume aliyeitwa Fredrich Thuram, alikuwa Mfaransa ambaye aliishi kwa kipindi kirefu nchini Marekani. Alikuwa mmoja wa watu waliokuwa wakipiga pesa nyingi kwa utapeli au madili yoyote ambayo hayakuwa yakikubalika na serikali.
 
SEHEMU YA 24

Alichokuwa akikifanya Thuram ni kuwaandaa vijana na kuwapa dili moja kubwa na kulipiga, lilipofanikiwa, alikuwa akiingiza kiasi kikubwa cha pesa lakini hata vijana wengine ambao aliwatuma kucheza dili hilo akaunti zao za benki zilijaa pesa.

Wakati Johnson alipokuwa amewasili nchini Marekani katika Chuo Kikuu cha Yale aliambiwa kuhusu mwanaume huyo, kama kweli alihitaji kufanikiwa kwa haraka, kuwa na mamilioni ya pesa, kuendesha Lamborghin ilikuwa ni lazima aonane na mwanaume huyo na kumwambia na yeye apewe dili.

Hakuwa mtu wa madili lakini baada ya kuambiwa hivyo na baadhi ya vijana wa hapo, akawa na hamu kubwa ya kukutana na mwanaume huyo. Hakujua angeonana naye vipi na ni kwa jinsi gani angemwambia kwamba alihitaji dili lolote lile.

Aliambiwa kwamba kulikuwa na mabilionea wengi walikuwa wakilizwa na Thuram kwa kuwatumia vijana wake aliopenda kuwaita kwa jina la Nyoka. Vijana hao hawakuwa wakiogopa kitu chochote kile, walicheza madili makubwa na kuchukua pesa nyingi kutoka kwa mabilionea wakubwa.

Miongoni mwa madili waliyokuwa wamecheza ilikuwa ni kuichukua Almasi ya Waridi ambayo ilijulikana kama almasi ghali zaidi duniani kutoka kwa mwanaume aliyejulikana kwa jina moja la Petrov.

Huyo alikuwa Mrusi mwenye pesa, aliyeingiza kiasi kikubwa cha pesa kila siku. Alijishughulisha na biashara ya madini mpaka pale alipofanikiwa kuipata almasi hiyo ambayo ilitoka nchini Liberia.

Baada ya Thuram kupata habari kuhusu almasi hiyo, moyo wake ukashtuka, hakuamini kama mwanaume huyo alifanikiwa kuipata almasi hiyo hivyo akaandaa vijana wake kwa lengo la kutaka kujua ni kwa namna gani angeweza kuipata.

Mchoro ukachorwa, mpango ukafanyika na mwisho wa siku kujua ni kwa namna gani wangeweza kuichukua almasi hiyo ambayo ilikuwa ikilindwa vilivyo katika jengo moja lililokuwa huko Texas nchini Marekani.

Kwa kuwatuma Nyoka, akawapeleka watalaamu wa kompyuta, watu waliokuwa na uwezo wa kupambana na msichana mmoja hatari aliyeitwa Vivian.
 
SEHEMU YA 25

Walikwenda mpaka Texas, walisoma ramani ya nyumba ile, walifuatilia kwa karibu na kuijua vizuri ratiba ya walinzi waliokuwa wakilinda, kwa kutumia utalaamu wa vijana wake wa kompyuta, walidukua kamera, wakazima umeme na kuingia kininja ndani ya nyumba hiyo kubwa.

Humo walikutana na chumba kilichokuwa kimefungwa kwa vault, kwa kumtumia mtu wao wa umeme, akarekebisha kwa kuukata umeme wa ndani kabisa kuachana na ule wa nje, walipoona wameshindwa kabisa, mtu wa kompyuta akaanza kufanya vitu vyake kwa kutumia alama za mikono ya Petrov ambayo aliitumia kufungulia vault hiyo na kuingia ndani.

Waliipata almasi hiyo, walinzi walifungwa katika kibanda kimoja na wao kuondoka nayo. Hiyo ndiyo ilikuwa michezo waliyokuwa wakiicheza, Thuram aliwatumia vijana hao kufanya uhalifu kila kona ambapo aliona angeweza kupata kiasi kikubwa cha pesa.

Alifanikiwa pasipo FBI wala CIA kugundua kitu chochote kile kwani kwenye kila tukio ambapo kulikuwa kukifanyika uhalifu, hakuwepo, kulikuwa na vijana wake tu ambao alikuwa akiwalisha maneno mengi na kuwaambia kwamba hawakutakiwa kutoa siri juu ya kitu chochote kile, nao wakala yamini.

Huyo ndiye ambaye Johnson aliambiwa kwamba kama angeungana naye basi angeweza kupata kiasi kikubwa cha pesa na kuwa tajiri. Alifanikiwa kuonana mara mbili na mwanaume huyo, alizungumza naye, alimwambia ni kwa jinsi gani alitamani sana kuingia kwenye kundi lake la Nyoka.

Mara ya kwanza Thuram hakumwamini, alihisi kama alikuwa ofisa wa CIA ambaye alifika hapo kwa ajili ya kumpeleleza. Alimkatalia na hata alipomwambia tena, alimkatalia pia.

Hilo lilimpa mawazo Johnson, ilikuwa ni lazima aungane na mwanaume huyo. Alipoambiwa kuhusu madili ya pesa nyingi, yalimchanganya na ukiangalia alikuwa Mchaga aliyeijua pesa, kichwa chake kilivurugika zaidi.

Hakuacha kumsumbua mwanaume huyo, alimuomba sana, kwa miezi miwili mfululizo yeye ndiye alikuwa akiongoza kumpigia simu mpaka pale ambapo mwanaume huyo aliamua kuwaita vijana wake na kuongea nao kuhusu Johnson.
 
SEHEMU YA 26

Kila mtu alimpa mawazo yake, kuna wengine ambao walimwambia amuweke kwenye kundi lakini kuna wengine walimwambia hakutakiwa kuingia kwa kuwa walikuwa na wasiwasi naye.

Hilo lilimuingia akilini lakini mwisho wa siku kabisa akapata wazo kwamba kama kweli kijana huyo alitaka kuingia kwenye kundi lake basi ingekuwa ni vizuri ampe kazi moja kubwa, ngumu ambayo wenzake waliishindwa, na kama angeiweza na kupata kile alichokuwa akikitaka, basi angemuingiza moja kwa moja.

“Nitampa kazi ya kumfuatilia Bruce,” alisema Thuram maneno yaliyomshtua kila mtu mahali pale.
“Kazi ya Bruce?” aliuliza kijana mmoja aliyeitwa kwa jina la Tony.
“Ndiyo! Yeye si anataka kazi, sasa subiri nimpe hiyo,” alisema Thuran.

Bruce Carner alikuwa mmoja wa wafungwa waliohukumiwa kifungo cha maisha katika gereza la Shelton Hill lililokuwa pembeni ya Jiji la Washington DC.

Mwanaume huyo alifungwa huko kwa kosa la kufanya mauaji ya polisi waliokuwa wakilinda pesa kiasi cha dola bilioni tano na kwenda kukificha mahali fulani.

Kwenye ishu hiyo hakuwa peke yake, alikuwa na wenzake wawili, Johnny Kelly na mwingine alikuwa Simon Pegg. Yeye ndiye ambaye alionekana na kugundulika, alikimbia na pesa hizo na kwenda kuzificha sehemu.

Huko alipozificha, hakukuwa na mtu aliyejua kwani hata watu hao wawili ambao alishirikiana nao, hakukuwa na mtu yeyote yule ambaye aligundua mahali pesa hizo zilipokuwa.

Hilo liliwaumiza mno watu hao na hata waliposikia Bruce anapelekwa gerezani na kufungwa, huko mtaani walihangaika kutafuta pesa hizo lakini hawakufanikiwa kuzipata kabisa.

Hilo likawapa mawazo tele, likawapa kazi ngumu mno kujua mahali pesa hizo zilipokuwa. Kila walipomtembelea Bruce na kumuuliza kuhusu pesa hizo, mwanaume huyo alisema hakumbuki mahali alipoziweka kwani ni muda mrefu ulikuwa umepita.

Thuram alifanikiwa kulijua dili hilo, kiasi cha dola bilioni tano kilikuwa kikubwa mno, kingemfanya kuishi maisha yake yote kiutajiri, afungue biashara nyingi na kuwa bilionea mkubwa, akataka kujua mahali pesa hizo zilipokwenda kufichwa lakini hakuweza kupata ukweli.
 
SEHEMU YA 27

Aliwatumia vijana wake, walihangaika kumfuatilia Bruce, walimfanya awapende lakini bado kulikuwa na ugumu mkubwa mno wa mwanaume huyo kuwaambia mahali pesa hizo zilipokuwa.

“Au nitumia askari magereza?” Hilo ndilo alilolifanya Thuram, akawalipa askari magereza kiasi kikubwa cha pesa na kuwataka wazungumze na Bruce mpaka awaambie mahali pesa hizo zilipokuwa lakini ilikuwa vigumu kwa mwanaume huyo.

Alipoona ameshindwa, ndipo alipojishauri kwamba kama kulikuwa na kijana aliyeomba sana kuingia kwenye kundi lake, basi ilikuwa ni lazima amtumie kwa kumpa kazi hiyo ili kama atafanikisha, achukue pesa hizo, agawane naye na kuondoka zake.

Hiyo ndiyo ilikuwa sababu ya kumpigia simu Johnson na kuomba kuonana naye. Kijana huyo alijiandaa na kwenda katika Mgahawa wa KFC na kuonana na mwanaume huyo.

Siku hiyo Thuram alimchangamkia mno Johnson kiasi kwamba mpaka akasikia raha, alimwambia wazi kwamba alikubali ombi lake la kuwa mmoja wa vijana wake kwa sharti moja la kupewa kazi ngumu, kama angefanikisha, basi angekuwa mmoja wa vijana wake.
“Kazi gani? Nipo tayari bosi!” alisema Johnson huku akimwangalia mwanaume huyo.

“Kuna ishu ya dola bilioni moja zimefichwa sehemu ninataka ujue ni mahali gani zilipofichwa,” alisema Thuram, hakutaka kumwambia kijana huyo kiasi halisi cha pesa hizo kwani alijua endapo angemwambia ukweli na siku kuzipata, basi angehitaji makato makubwa na ndiyo maana aliamua kumdanganya.

“Zimefichwa wapi?” aliuliza Johnson.
“Hakuna anayejua zaidi ya mtu mmoja tu!” alisema Thuram.
“Nani?”

“Anaitwa Bruce. Huyu mwanaume yupo katika Gereza la Shelton Hill huko Washington DC. Kama utathubutu kwenda na kuzungumza naye, akamwambia mahali pesa zilipo, basi tutafanikiwa kwa kiasi kikubwa kuzipata pesa hizo,” alisema Thuram.

“Umesema dola bilioni moja?” aliuliza Johnson manake kiasi hicho kilishamchanganya.
“Ndiyo!”
“Mmh!” aliguna.
 
SEHEMU YA 28

Kilikuwa kiasi kikubwa mno, alikiweka kiasi hicho kwenye pesa za Kitanzania, kilikuwa ni zaidi ya shilingi trilioni mbili. Kama angezipata pesa hizo ilimaanisha kwamba asingeishi maisha ya kawaida hata siku moja, kilikuwa ni kiasi kikubwa kupita kawaida.

Hakutaka kujiuliza sana, akamwambia Thuram kwamba alikuwa tayari, kama kweli kulikuwa na kiasi hicho cha pesa mahali fulani, na kulikuwa na mwanaume mmoja tu ambaye alitakiwa kumwambia mahali pesa zilipokuwa, hakuwa na tatizo lolote lile.

“Nitafuatilia suala hilo na ninakuhakikishia kwamba nitafanikiwa kujua pesa zilipo,” alisema Johnson.
Hakutaka kubaki mahali hapo, akaondoka zake. Kichwa chake kilichanganyikiwa, hakuwa ameifanya kazi hiyo, hakujua ilikuwa ngumu kiasi gani lakini kichwa chake kilimwambia kwamba angefanikiwa kuzipata pesa hizo.
 
SEHEMU YA 29

Ukiachana na hilo, pia wazo jingine likamjia kichwani. Kama angefanikiwa kujua mahali pesa zilipokuwa, isingekuwa rahisi kumpelekea Thuram pesa hizo, kama angekuwa amezihangaikia yeye mwenyewe, kulikuwa na umuhimu gani kumpelekea mwanaume huyo ambaye wala hakuwa amehangaika kwa lolote lile?

“Yaani nihangaike, nijue pesa zilipo halafu nikamwambie, aje azichukue kirahisi! Hakuna ujinga huo,” alijisemea.
Akaondoka mpaka hosteli, alipofika huko, akatulia kitandani. Siku hiyo hakuwa sawa kabisa, mawazo yake yalikuwa kwenye pesa hizo tu, alitamani sana kuona anafanikiwa kuzichukua na kuondoka nazo akaanze maisha yake kivyake.

Alikaa huko akijifikiria na wazo la mwisho kabisa lililomjia kichwani mwake ni kwenda huko Washington DC, atembelee gereza hilo na kuangalia uwezekano wa kuongea na huyo Bruce ili amwambie mahali alipozificha hizo pesa, kama angekuwa radhi kumwambia katika hilo, basi alikuwa na uhakika wa kuzipata na kutoroka kuelekea nchini Tanzania.

“Cha kwanza ni kwenda huko Washingtona DC. Huu mchezo ni lazima uchezwe, pesa zijulikane zilipokuwa,” alijisemea Johnson, hakutaka kuwa na hofu, aliamini kabisa kwamba angefanikiwa kwenye suala hilo pasipo tatizo lolote lile.

Pale waliposhindwa watu wengine, yeye alitaka kufanikiwa, na kwa sababu dili hilo lilihusu pesa, hakuona kama angeshindwa hata kidogo. Aliamini kwenye dili lolote la pesa, Mchaga hakuwahi kushindwa. |
|
|

Je, nini kitaendelea?
 
SEHEMU YA 30

Bhoke hakuacha kutembea na wanaume mbalimbali, alipenda sna ngono na katika maisha yake hakuamini kama kungekuwa na mwanamke ambaye angeweza kufanikiwa pasipo kutumia mwili wake.

Akili yake ni kama ililemaa, kila alipokuwa akipita na kuwaona wanaume wakiwa vifua wazi au hata eneo la kwenye zipu kutuna kidogo alichanganyikiwa kupita kawaida.

Alijipenda, alijua kuvaa na kila mwanaume ambaye alimuona, alimuita na kuanza kuongea naye.

Alifanya ngono kupitiliza kiasi kwamba mpaka akili yake ilikuwa ikifikiria ngono kila wakati.
Alikuwa na orodha ya matajiri wakubwa jijini Dar es Salaam, matajiri ambao walimpigia simu na kumwambia kwamba walihitaji kufanya naye mapenzi.

Alitumika sehemu nyingi na matajiri hao kiasi cha kumuingizia pesa ambazo kwake aliona kama zilikuwa nyingi kutokana na kazi ndogo aliyokuwa akiifanya.

Baada ya kukaa Dar kwa wiki kadhaa akapokea simu kutoka kwa mtu ambaye hakuwa akimfahamu, mtu huyo alijitambulisha kwa jina la Emmanuel Mambili ambaye alimwambia kwamba alihitaji sana kuonana naye kwa kuwa kulikuwa na kitu alihitaji kuzungumza naye.

Kwanza aligoma lakini mwanaume huyo akamuondoa wasiwasi kwamba hakukuwa na tatizo lolote lile, endapo angekwenda na kufanya hayo mazungumzo, angempa kiasi cha milioni moja na kama wangezungumza na kufikia makubaliano, angempa kiasi cha milioni moja nyingine na kama angempa kazi na kufanikiwa, basi angempa milioni tano.

Bhoke aliposikia hivyo, akachanganyikiwa mno, hakuamini hata kidogo kwamba aliahidiwa pesa nyingi mno ambazo hakuwahi kuzishika tangu azaliwe.

Hakutaka kuchelewa na hakutaka kujiuliza sana mwanaume huyo alihitaji kuzungumza naye kuhusu suala gani, alichokifanya ni kuelekea huko kwa ajili ya mazungumzo hayo.

Ni ndani ya dakika kadhaa akafika nje ya jumba moja kubwa Osterbay ambapo alielekezwa aende,akachukua simu yake na kumpigia mwanaume huyo, akamwambia kwamba alifika mahali hapo kwa ajili ya mazungumzo hayo.
 
SEHEMU YA 31

Haraka sana geti likafunguliwa na gari kuingizwa. Kwa jinsi humo kulivyokuwa, Bhoke alibaki akishangaa, lilikuwa jumba la kifahari na lililokuwa na kila kitu humo.

Alibaki akishangaa kwanza kabla ya kuteremka na kumuona mwanaume mmoja akimfuata na kumpokea.

Akasalimiana naye na kujitambulisha kwamba aliitwa Mambili na yeye ndiye ambaye alimuita kwa lengo la kuzungumza kidogo na kumpa pesa ambazo alimuahidi.

Kwa jinsi mwanaume huyo alivyokuwa ilikuwa ni vigumu sana kugundua kama yeye ndiye alikuwa mmiliki wa jumba hilo kubwa, alionekana mtu wa kawaida sana kumbe upande wa pili alikuwa mwanaume aliyekuwa na pesa nyingi mno.

Hofu haikuwepo moyoni mwake, alitokea kumwamini mno mwanaume huyo kana kwamba alikwishawahi kufahamiana naye kabla. Akaingizwa mpaka sebuleni na kukaa kwenye kochi kubwa lililoyafanya makalio yake yaingie kwa ndani.

Akili yake ilimwambia kwamba Mambili alihitaji kufanya naye mapenzi, alijipanga, alijiweka sawa na alijiahidi kwamba siku hiyo angemuonyeshea staili zote mwanaume huyo, yaani angemfanyia utundu kiasi kwamba angeshangaa yeye mwenyewe.

“Umependeza sana Bhoke,” alisema Mambili huku akimwangalia msichana huyo na kumpa juisi, akaanza kunywa.

Kuambiwa hivyo alizoea, kila mwanaume aliyekuwa akimwangalia ilikuwa ni lazima amwambie kwamba alipendeza, alikuwa mzuri wa sura na maneno mengine mengi tu. Akaitikia kwa kumwambia ahsante kisha mazungumzo mengine kuendelea.

Walizingumza mambo mengi, Bhoke ambaye alikuwa na uwezo wa kumsoma mtu yeyote yule kila aliokuwa akimwangalia mwanaume huyo, hakuona kama alihitaji kulala naye, alionekana kuwa mtu wa kawaida, aliyekuwa akitaka kumwambia maneno ya kawaida tu kitu ambacho kwake hakikumuingia akilini kwa sababu alipenda ngono, kitendo cha kuingia ndani ya nyumba hiyo kilikuwa ni ishara tosha ya kulala na mwanaume huyo.

“Bhoke! Nafurahi sana kuona ukijiamini sana,” alisema mwanaume huyo huku akiwa na tabasamu pana usoni mwake.
“Umejuaje?”

“Unavyoonekana tu. Kwa jinsi ulivyo, ninaamini utakwenda kufanya kazi yetu vizuri kabisa,” alisema mwanaume huyo.
“Kazi yetu?”
“Yaap! Namaanisha mimi na wenzangu!”
 
SEHEMU YA 32

“Akina nani?”
“Hutowajua kwa sasa,” alijibu Mambili.
Bhoke akatulia kwanza, hakutakiwa kuwa na papara ya kuuliza maswali mengi kwani aliamini kazi hiyo ilikuwa na umuhimu mkubwa na ndiyo maana aliahidiwa kiasi kikubwa cha pesa.

Akasubiri aambiwe kwanza kuhusu kazi yenyewe. Mambili akasimama na kuelekea chumbani kwake, baada ya sekunde kadhaa akarudi huku akiwa na bahasha na kumuwekea msichana huyo juu ya meza.

Bhoke akaichukua na kuifungua, humo akakutana na picha kadhaa, zilikuwa za mwanaume mmoja aliyemfahamu vilivyo kabisa, aliitwa Selemani Makame, alikuwa mbunge wa Jimbo la Ubungo kwa kupitia tiketi ya Chama cha Diplomatic.

“Hiyo ndiyo kazi yenyewe,” alisema Mambili huku akimwangalia Bhoke.
Msichana huyo alishangaa, hakujua kazi hiyo ilitakiwa kufanyika vipi, alimwangalia Mambili kwa macho yaliyokuwa na maswali mengi ambayo kwa muda huyo yalihitajika majibu yake haraka sana.

Mambili alielewa hivyo akaanza kumwambia kuhusu kazi yenyewe.

Huo ulikuwa mwaka ambao Tanzania ilitakiwa kufanya uchaguzi mkuu ambao ungewaweka madarakani wabunge wengi na rais. Kulikuwa na upinzani mkubwa kuliko miaka yote, kila kona kulikuwa na mikikimikiki ya watu ambao walitaka kuwa viongozi nchini humo.

Mambili alikuwa mmoja wa wagombea ambao walitakiwa kugombea nafasi ya ubunge wa Ubungo kupitia Chama cha Republic ambacho kilikuwa na upinzani mkubwa na Chama cha Diplomatic.

Mbele yake aliona upinzani mkubwa, Makame aliahidi kwamba ni lazima afanye kila liwezekanalo kuhakikisha anachukua tena ubunge wa jimbo hilo kwa sababu tu aliamini kwamba anapendwa na kila mtu aliyekuwa akimchekea mbele yake.

Kwenye mikutano yake mingi watu walimsifu, walijaa kitu kilichowapa uhakika kwamba ni lazima mwaka huo angechukua tena kiti hicho cha ubunge na kurudi bungeni.

Wakati huo Tanzania ilikuwa ikiongozwa na Chama cha Republic, walikuwa wakihitaji kupata ubunge katika majimbo yote jijini Dar es Salaam na jimbo ambalo lilionekana kuwa gumu lilikuwa ni hilo la Ubunge.
 
SEHEMU YA 33

Chama hicho kilifanya kila liwezekalo kuhakikisha wanalipata jimbo hilo. Walitumia njia nyingi sana kumnyong’onyesha Makame lakini walishindwa kabisa.

Hawakuona kama mwanaume huyo angeweza kurudi nyuma. Baada ya kuona kwamba walitumia nguvu nyingi kutaka kumyumbisha mwanaume huyo ili aonekane si kitu ndipo wakasikia kuhusu mwanamke fulani mrembo aliyekuwa akijiuza, Bhoke.

Walihitaji kumtumia, ni kweli waliwatumia wasichana wengi kwa lengo la kumfuata kimapenzi lakini alishtukia mchezo, hakutaka kabisa kuona akiingia kwenye majaribu kwani aliamini hiyo yote ilikuwa ni mitego iliyosukwa vilivyo hivyo ilikuwa ni lazima apambane kiume.

Wakati yeye akisema kwamba asingeweza kutekwa kiboya, upande wa pili watu waliendelea kuandaa mikakati na ndipo walipoamua kumtumia huyo Bhoke.

Hawakutaka kugundulika, waliwafahamu wanawake, hawakuwa watu wa kuficha siri na ndiyo maana waliamu kumtumia Mambili ili azungumze naye kwa kirefu, kama alihitaji pesa basi angepewa za kutosha lakini mwisho wa siku wafanikiwe kile walichokuwa wakihitaji kutoka kwa msichana huyo.

“Sasa kazi gani inatakiwa kufanyika?” aliuliza Bhoke.

“Tunahitaji kupata picha ukifanya mapenzi na huyu mwanaume,” alisema Mambili huku akimwangalia Bhoke.
“Mh!” aliguna.

“Unaguna nini? Unaogopa?” aliuliza Mambili huku akimwangalia msichana huyo.

Ni kweli aliogopa, kwake, kujiingiz akwenye vita vya kisiasa hakutaka kabisa, alihitaji kuwa na marafiki, hakutaka uadui na mtu yeyote yule na ndiyo maana alikuwa akitumia muda wake mwingi kujinadi kwenye mitandao, ishu ya kuwa na maadui hakutaka kabisa.

Leo, mwanaume aliyekuwa mbele yake alimwambia kwamba ni lazima kazi moja ifanyike kwa malipo makubwa, huyo Makame ilikuwa ni lazima aingizwe katika mtego huo na picha kupatikana ambazo zingetumika kumchafua katika kampeni ambazo zilitarajiwa kufunguliwa baada ya wiki mbili.
“Hii ni kazi ngumu sana!” alijibu msichana huyo.

“Sidhani kama kuna ugumu! Yaani sisi tunataka ulale naye na ujipige picha, ni hilo tu,” alisema mwanaume huyo.
“Pasipo kufanya naye mapenzi ama?”
“Wewe sasa! Ila sisi tunataka tupate picha ukiwa naye chumbani!” alisema Mambili.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom