Stephen Ngalya Chelu
JF-Expert Member
- Oct 31, 2017
- 7,621
- 16,372
- Thread starter
- #21
MAISHA YANGU NYUMA YA PAZIA JEUSI
SEHEMU YA 07
Ilipoishia….
“ Ingrid, hivi unadhani mimi si mwanadamu? Au unadhani mimi nafurahi kukuona una huzuni kwa ajili yangu? Hata mimi naumia pia, lakini ni bora maumivu haya unayoyapata sasa kuliko hayo ambayo utayapata baadae kwa kuwa na mimi. Umeamua kutangaza kuvunja urafiki wetu kwa jambo hili dogo, sawa. Lakini nakuomba utambue kuwa unanionea, haunitendei haki hata kidogo. Najua hatuwezi acha kuonana kila siku…lakini jaribu kufikiria mimi nitakuwa najisikiaje pale ambapo nitakuwa nakuona? Anyway… nipo tayari kukupa ukweli wangu wote nyuma ya maamuzi yangu siku yoyote ile ambapo utahitaji na kama ratiba yangu itaruhusu. Baada ya hapo unaweza kuendelea na msimamo wako wa kukata mahusiano na ukaribu wetu. Vinginevyo, nita’miss’ vitu vingi kutoka kwako rafiki yangu, Ingrid” sikutaka kumpa nafasi aijibu hoja hii,ilikata simu, nikaizima, nikalala.
Endelea…..
Asubuhi iliyofuata niliamka nikiwa na uchovu kwa kiasi fulani hivi. Nilichoamua kukifanya kwanza ni kufungua simu kisha nilitoka nje ili kufanya mambo mengine kama kuswaki na kuoga. Baada ya kukamilisha yote hayo nilirudi ndani na kukuta simu yangu kwenye kioo ikionyesha kuwa kulikuwa na jumbe mpya tatu za kawaida. Nilizifungua ili kujua ni nini kilikuwa kimeandikwa huko ndani na ni nani aliyekuwa amezituma.
Alikuwa ni Ingrid, ndiyo Ingrid. Msichana ambaye jana usiku alijiapiza kuwa hatowasiliana na mimi kamwe. Jumbe zote zilionyesha kuwa zilitumwa jana usiku. ujumbe wa kwanza ulisema ‘mbona umekata simu sasa’ ujumbe wa pili ulisema ‘barry, ndo umeamua kunizimia simu kabisa sio?’ na ya tatu ilisema ‘ipo siku utalipa kwa maumivu haya unayonisababishia’.
Nilisoma jumbe hizo huku nikiwa natabasamu, yaani mtu aliyekuwa aliyejiapiza kuwa ananichukia sana na pia hatonitafuta tena alikuwa ametuma jumbe tatu mfululizo. Lakini kiuhalisia hiyo ndiyo rangi halisi ya wanawake. Mwanamke anaweza kukwambia ndiyo ilhali akimaanisha hapana au anakwambia hapana ilhali anamaanisha ndiyo, mwanamke anaweza kukukasirikia usoni lakini moyoni anakufurahia au anaweza kuonyesha tabasamu usoni lakini moyoni anakuchukia pasi mfano. Hivyo ndivyo walivyo, kuna nyakati ni ngumu sana kutambua ni nini hasa kinaendelea ndani ya mioyo yao.
Hata hivyo jumbe zake zilinipa nguvu kwa kuwa nilikuwa nimebaki na hatua moja tu ya kukamilisha lengo langu la kumtoa Ingrid katika zone ya yeye kuwa mpenzi wangu na pia aendelee kuwa rafiki yangu. Nilijiona mshindi katika hili.
Japo alikuwa anakuja katika njia niliyokuwa naitaka lakini sikutaka kujibu jumbe zake kwani ule ulikuwa ni mchezo wa hisia na nilipaswa kuucheza kwa umahiri ili nishinde mechi katika dakika za awali kabisa. Nilimaliza kujiandaa kisha nikaenda zangu kazini kama kawaida. Baada ya kufika eneo langu la kazi nilianza kutekeleza majukumu ya kawaida ya kila siku. Ilipofika saa nne na dakika zake hivi niliona simu yangu ikiita…nikaangalia kwenye kioo, alikuwa ni Ingrid. Akili yangu ilivurugika ghafla maana nilijua ni lazima atakuja na malalamiko mengi kabisa. Nilitaka nisiipokee simu yake lakini nikaona kwamba kama nisipopokea nitaongeza matatizo hivyo ni heri niipokee tu.
Nilipokea simu kusikiliza huyu mwanamke alikuwa na mashitaka gani tena.
“hi barry, mzima wewe?” alisema akiwa na furaha hadi nikajiuliza kwani leo imekuwaje. Kwa jinsi tulivyoachana jana usiku sikutarajia kama angekuwa katika hali kama ile.
“mi mzima tu ndugu yangu” nilisema kwa sauti ya kuchangamka ili kwenda naye sawa ilhali kichwani nikiwa bado nawaza ni nini kimemfurahisha yeye asubuhi asubuhi.
“daaah, barry nina furaha sana leo, yaani we acha tu” alisema huku akionyesha ni kweli alikuwa na furaha. Hata mimi nilijikuta natabasamu kama zoba huku nikiwa sijui ni nini kinanifanya nitabasamu.
“hivyo ndo inavyotakiwa, siyo unakaa umenyong’nyea kama unadaiwa madeni, haya nimegee na mimi nifurahi basi rafiki yangu mwenyewe” niliongea kwa bashasha huku nikiongeza kicheko cha kinafki.
“leo matokeo yetu yamatoka, na nimefanya vizuri….yaani hadi siamini” alisema Ingrid akizidi kuidhihirisha furaha yake. Dooh kumbe ni mambo ya shule tena. Mimi shule niliitupaga mkono japokuwa nafsi haikuwa imependa, na nilikuwa natamani sana siku na mimi ningekuwa darasani na nifikie hatua kama yake lakini haikuwezekana.
Munkari ulishuka, japokuwa niliendelea kushikilia kiwango kilekile cha hisia nilichokuwa nacho mwanzo ili ingrid asinigundue kama kuna jambo kwa upande wangu halikuwa sawa. “safi sana ingrid, umepata division ngapi” nilimuuliza.
“one’ alijibu.
“hongera sana aisee, kumbe una miakili mingi hivi! kwa hiyo chuooo kileeeeeee, utakweda kusomea nini madame?”
“mi hata sielewi yaani, ila napenda sana sheria na mambo ya pesa pesa”
“sheria, unataka kuja kumfunga nani, mimi?” nilimtania.
“yaani wewe ndo utakuwa wa kwanza kabisa. Yaani jinsi unavyoninyanyasa mimi na hisia zangu siku nikipata safasi lazima uozee jela nakwambia” aliogea kwa utani lakini iliyokuwa na hisia za maumivu ndani yake.
“aisee, haina shida madame. Hata ukinihukumu kunyongwa mpaka kufa ni sawa tu maana sheria utakuwa nayo mikononi mwako” Nilikubaliana na mtazamo wake. Niliwahi kuambiwa kuwa ukitaka kumaliza migogoro isiyo ya lazima, kubaliana na kile mgomvi wako anakisema juu yako.
“barry, yaani nilianza kukuchukia lakini nimejikuta nashindwa, barry wewe ni mwanaume gani lakini?, unatongozwa na mwanamke unakataa?, na sijui hicho kitu unachotaka kuniambia kitakuwa na matokeo gani kwa upande wangu” aliongea kwa sauti ambayo nilikuwa nimeizoea, sauti ya mahaba yaliyojaa unyonge. Tayari tulikuwa tumesharudi kwenye uwanja wa nyumbani, uwanja uliojaa hisia za upendo na malalamiko.
“Ingrid, mimi nakujali kuliko unavyofikiria, na siku hiyo utajua tu kwa nini huwa nayasema yale ninayoyasema…..”
“si uniambie sasa hivi”
“Sasa hivi ni saa za kazi, pia ni story ndefu kidogo, so inahitaji muda pia”
“kwa hiyo ni lini?”
“nadhani jumapili hii, baada ya kutoka kanisani”
“mmmmh….haya sawa, maana hata kama nikipinga wewe ni kichwa ngumu, huwezi nielewa, sawa tu” wakati anayaongea hayo kuna mteja alifika pale akiwa anahitaji huduma, nikaamua kukatizo mazungumzo . “hapana ingridi, unanielewa vibaya, badae madame..niache nitimize wajibu kwanza” nikakata simu na kuendelea kumhudunia mteja. Niliendelea kufanya kazi yangu kwa moyo wote na ilipofika jioni nikaenda kukabidhi hesabu kwa bosi kama kawaida kisha nikarudi zangu geto. Siku zilizidi kusonga huku nikijaribu kujiweka mbali na Ingrid maana niligundua kuwa kadri nilivyokuwa najiweka karibu naye ndivyo alivyokuwa akipata matumaini ya kuwa huenda mimi na yeye tutakuwa pamoja.
Hatimaye siku ikafika, sikutaka kwenda kanisani. Niliamka asubuhi nikafanya usafi na nikaendelea kujiandalia kifungua kinywa. Nilifanya hayo huku nikiperuzi kwenye mtandao wa jamiiforums. Jamiforums ilikuwa ni sehemu ambayo nilikuwa naitumia kama sehemu ya kuniondolea msongo wa mawazo. Si kwamba nilikuwa naperuzi tu kama mgeni bali nilikuwa mwanachama kabisa, nilikuwa natumia jina la ‘Jiwe la gizani’. Japo sikuwa na muda mrefu sana tangu nijiunge jf lakini nilikuwa nimeanza kuwa maarufu kutokana na nyuzi zangu zenye story zilizojaa ucheshi. Watu wengi walikuwa wakivutiwa nazo. Japo kile nilichokuwa nakiandika hakikuwa na uhalisia katika maisha yangu lakini nilikuwa nafurahi kwa sababu nilichukulia kama sehemu ya burudani kwangu na kwa wasomaji wengine. Wakati naperuzi katika uzi wa picha za vituko, simu yangu iliita. Alikuwa ni ingrid,…nikapokea.
“mambo barry” alinisalimia
“ni gud madame, lete habari..”
“safi, twende kanisani” alisema Ingrid
“leo mimi sijisikii kwenda” ilimjibu
“kwa nini?”
“jana nilichoka sana so nimeamka na uchovu” nilidanganya.
“mh, haya. Kwa hiyo leo nitatembea peke yangu?” aliiuliza kwa sauti yeye deko la kike.
“kaniombee tu madame” sikumjibu swali lake ila nilimwambia hivyo hili ahitimishe maongezi yake.
“unakumbuka leo ndiyo siku uliyoniahidi kuwa utaniambia kwa kina kuhusu ile ishu”
“yeah, nakumbuka vyema kabisa”
“saa ngapi sasa?”
“ukitoka kanisani”
“usije ukaondoka sasa maana wewe akili yako unaijua mwenyewe”
“nani kakwambia tunakuja kuongelea nyumbani? Tunatakiwa kutoka nje ya hapa, mazingira ya hapa si rafiki kabisa”
“mmmmh!..... hivi unadhani kupata ruhusa kutoka kwa baba ni jambo rahisi,?”
“kama ikishindikana basi”
“mmmh una roho mbaya wewe, ok ngoja nitajaribu. Ni wapi huko tutaenda?” aliuliza.
“nadhani itakuwa vizuri kama tutaenda sehemu iliyotulia kama ufukweni hivi”
“kuna fukwe nyingi sana lakini” alisema Ingrid. Nilimtajia ufukwe ambao niliona unafaa kwa kuzingatia umbali kutoka eneo tuliloishi. “mhh..haya, niombee nipate ruhusa” alisema Ingrid. Nikamhakikishia kuwa nitafanya hivyo kisha tukaagana na kukata simu.
Baada ya kukata simu, simu yangu ilinirudisha kwenye ukurasa wa jamiiforums ambao nilikuwa naupitia kabla ya simu ya Ingrid kuingia lakini niliamua kutokuendelea kuperuzi kwa kuwa akili yangu ilitekwa na jambo jingine. Nilifikiria kile ambacho ningeenda kumwambia Ingrid. Nikajikuta mnyonge ghafla. Lilikuwa ni jambo ambalo nilikuwa sipendi kabisa kulisimulia ila nililazimika kutokana na jinsi Ingrid alivyokuwa, alikuwa ni king’aganizi mno. Hivyo kwa wakati huo hiyo ndiyo ilikuwa ndiyo njia pekee ya mimi kujinasua kwake. Niliamini kama angekisikia kisa hicho angenielewa na kuniacha huru.
Hali ya kulifikiria tukio hili ilisababisha nifungue begi na kutoa bahasha ambayo ndiyo ilikuwa ni kielelezo na kumbukumbu pekee niliyokuwa nayo kuhusu tukio lile. Nikaifunngua nikavitoa vilivyokuwamo, nikavitandaza chini sakafuni kisha nikawa naviangalia. Jinsi nilivyokuwa naviangalia ndivyo nilizidi kuchochea hisia za maumivu na majuto ambayo yaliweka kambi ndani yangu kwa muda mrefu. Hisia hizi zilikuja kwa nguvu kubwa kiasi nilishindwa kuyazuia machozi. Kuna msemo kuwa kila mtu ana sehemu ya udhaifu wake, na ule ndiyo ulikuwa udhaifu wangu. Mara zote nilijikuta mnyonge sana mbele ya tukio lile.
Nilifumba macho huku nikiendelea kuyahisi machozi yakiwa yanatiririka taratibu kwenye mashavu yangu. Kisha taratibu nikaanza kuona taswira ya msichana ikiwa katika hali iliyofifia. Kadri muda ilivyozidi kwenda taswira ile ilianza kuonekana dhahiri kiasi cha kuweza kumtambua, alikuwa ni Jennifer. Jennifer alionekana akibubujikwa na machozi zaidi yangu mimi huku akionyesha ishara za kunilalamikia.
“damn, what the f..” niliongea kwa sauti kubwa huku nikirusha mikono. Na kwa kuwa niliongea kwa sauti kubwa sana nilijistukia na nikaamua nisiimalizie sentensi hiyo. Nilikuwa nahema kwa sauti kubwa sana. Nilijifuta machozi huku nikivurudisha vile vitu kwenye bahasha na kisha nikairudishia bahasha kwenye begi.
Niliendelea kuandaa kifungua kinywa huku nikiwa siko sawa kihisia.
Masaa yakasonga, asubuhi ikaondoka kinyonge huku ikiukaribisha mchana. Jua likawaka na joto likazidi kuongezeka. Siku hiyo sikujisikia kabisa kujiandalia chakula cha mchana hivyo nikatoka kwenda kwa mama’ntilie ambaye nilikuwa nakwenda kila mara kama ikitokea siku hiyo sijisikii kupika. Na kwa kuwa muda ulikuwa umeenda hivyo niliamua kuunganisha safari kwamba nikitoka hapo niunganishe moja kwa moja kwenda kwenye eneo la miadi.
Nilipomaliza kula nilichukua usafiri wa umma nikasogea eneo la miadi yangu na Ingrid. Nikashuka nikatembea kwa miguu hadi nilipofika eneo rasmi tulilokubaliana. Muda wote huu nilikuwa nawasiliana na Ingrid kwa njia ujumbe mfupi. Aliniambia kuwa baba yake alimruhusu lakini kwa masharti ya kuwa awe amefika nyumbani kabla ya saa moja usiku. Pia aliniambia kuwa alipata ruhusa hiyo kwa kumdanganya baba yake kuwa anaenda kumtembelea rafiki yake na akanisisitiza kuwa muda uzingatiwe. Nikamhakikishia kuwa mambo yatakuwa sawa.
Nilikaa kumsubiri huku nikiangalia madhari ya ufukwe, niliwatazama watu waliokuja na wapenzi wao kujivinjari. Kuna walikuwa wanacheza michezo ya kimahaba, kuna waliokuwa wamekaa huku wakiongea, ilimradi kila mtu alijaribu kumuonyesha ni kwa jinsi gani anampenda na kumjali mwenzi wake. Lakini kwangu ilikuwa ni kinyume, yaani wakati watu wengine wanawaleta watu wao kuja kuimarisha mapenzi yao, mimi nilikuwa nimemwita Ingrid pale kuja kuliua penzi lake changa alilokuwa nalo juu yangu. Kweli binadamu tunafanana lakini hatupo sawa. Nilitembea huku mikono nikiwa nimeitumbukiza kwenye mifuko ya suruali huku masikio yangu yakiwa yanaburudishwa na sauti za mawimbi ya maji yaliyokuwa yakipiga kwenye ufuo. Bahari iliniburudisha kiasi chake ikizingatiwa kuwa mimi nilikulia maeneo ya kanda ya kati ambako kulikuwa na mazingira ya ukame hivyo kuona eneo kubwa la ardhi lililojazwa maji halikuwa jambo nililoweza kulishuhudia. Macho yangu yalizoea kuona madimbwi na mabwawa madogo madogo.
Ilikuwa na saa tisa na dakika zake hivi wakati Ingrid aliponipigia na kuniambia kuwa alikuwa amefika eneo ambalo tulitakiwa tuonane. Nilimuelekeza mahali ambapo nilikuwepo, dakika kadhaa baadaye alifika mahali nilipokuwepo. Alikuwa amevalia vyema kiasi cha kuongeza mvuto wake ambao nilizoea kuuona kila siku. Alivalia gauni la urefu wa saizi ya magoti lenye rangi nyekundu, rangi inayotafririwa kuwa ni rangi ya upendo japo kua wakati rangi hii huashiria uovu. Hii ni kwa sababu upendo na chuki, vyote kwa pamoja hutembea katika damu. Urefu wa gauni lake ulifanya miguu yake iliyojaa vyema kuonekana dhahiri kabisa, watoto wa mjini huiita miguu ya bia. Miguuni alivalia viatu vyepesi visivyo na visigino virefu vilevyokuwa na rangi nyeusi. Nywele alizisuka kwa mtindo ambao hadi sasa sijawahi kuufahamu, labda ni kwa sababu mimi siyo mfuatiliaji sana wa mambo ya urembo kwa wanawake. Kwa ujumla, Ingrid alikuwa ni mwanamke wa ndoto kwa wanaume wengi. Ingrid alikiwa amekamilika katika mwonekano wake na mitazamo yake.
Alinisalimia, nikapokea salamu yake nikiwa na uso wa furaha sana. Bila kusubiri maongezi zaidi nilimshika mkono na kumpeleka mahali ambapo nilipachagua kwa ajili ya sisi kukaa. Palikuwa ni mbali na bugudha za watu waliokuwa wanaogelea na kufanya mambo mengine ya starehe. Niliamua kufanya matendo ya kirafiki ili kuhakikisha kuwa Ingrid hajisikii vibaya. Tulifika mahali tulipokuwa tunaelekea, tukakaa kwenye mchanga safi wa ufukwe. Ingrid alikaa upande wa wangu wa kushoto akaweka mikono yake juu ya mikono yangu kisha akaegesha kichwa chake kwenye bega langu. Nami nikanyanyua mkono wangu wa kushoto kisha nikauzungusha mabegani mwake kama sehemu ya kumuunga mkono. Sasa tulikuwa ni muungano haswa. Hisia zetu ziliunganika na kutengeneza hisia moja, hisia ya penzi lililojaa mtanziko. Niliamua kuvunja ukimya kabla ya yeye hajafanya hivyo.
“Ingrid” nilimwita
“sema babaa” aliitika huku akiniangalia usoni. Sauti aliyoitumia kutamka hiyo setensi fupi ilinifanya nipoteze kumbukumbu ya kile nilichokuwa nataka kukisema. Nilikaa kimya kwa muda huku nikijaribu kuvuta kumbukumbu ya nini nilitaka kukisema. Baada ya sekunde kadhaa, nilikumbuka na nikaendelea kuongea.
“mara zote umekuwa ukiniona mimi ni mtu nisiyejali hisia zako, ama nakufanyia makusudi kwa kuwa najua kuwa unanipenda mimi sana. Si kweli, leo nataka kukupa kisa kilichonikuta na kufanya niwe mgumu kukubaliana na wewe. Nadhani tukishatoka hapa utakuwa unaelewa ni kwa nini nakuwa mzito sana kukualiana na wewe.” Niliongea huku mkono wangu wa kushoto ukitambaa taratibu katika bega la Ingrid hali iliyofanya Ingrid azidi kutulia.
“barry, nipo hapa kukusikiliza. Lakini nadhani wajua ni jinsi gani ninavyokupenda” aliongea huku akiupapasa mikono yangu.
“najua, najua Ingrid. Ndiyo maana nimekuita hapa ili nikushirikishe jambo hili kubwa sana katika maisha yagu” niliongea huku macho yangu yakiwa yanaangalia mawimbi ya bahari. Niliendelea kuangalia upande wa bahari, nikazidi kuangalia mawimbi yalivyokuwa yakitembea kwa kasi kuja na kurudi. Nilifanya yote haya ili kuvuta kumbukumbu zote za tukio zima ili nisisahau hata tukio moja. Nilipanga kumwambia kila kitu.
Baada ya kuwa na hakika kuwa nilikuwa nakumbuka kila kitu nikaanza kusimulia.
Miaka sita iliyopita..
Itaendelea…..