Hadithi: Kalume-Kenge, Bibi Tarabushi etc.

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,049
12,417
Hadithi hizi zinapatikana katika kitabu Someni kwa furaha kitabu cha kwanza. Unaweza kuzisoma na nyingine nyingi bure ndani ya Maktaba app(by pictus), Icheki playstore.

Kalume-Kenge




1631330425556.png



Kalume-Kenge alikataa kwenda shule, baba yake akamwambia mbwa: je, mbwa, wataka kumwuma Kalume-Kenge? Hataki kwenda shule.
Mbwa akakataa.
Baba yake akasema kwa fimbo: je, fimbo, hutaki kumpiga mbwa? Yeye hataki kwenda shule.
Fimbo ikakataa.

Baba kaukamata moto, akasema: je, moto, wataka kuichoma fimbo? Kwa maana haitaki kumpiga mbwa, naye hataki kumwuma Kalume-Kenge, naye hataki kwenda shule.
Moto ulikataa.
Baba akasema kwa maji: je, maji, wataka kuzima moto?
Moto hautaki kuchoma fimbo,
Nayo haitaki kumpiga mbwa,
Naye hataki kumwuma Kalume-kenge.
Naye hataki kwenda shule.
Maji yalikataa
Baba kamwendea mbuzi: je, mbuzi, hutaki kunywa maji?
Kwa sababu hayataki kuzima moto.
Nao hautaki kuichoma fimbo,
Nayo haitaki kumpiga mbwa,
Naye hataki kumwuma Kalume-Kenge.
Naye hataki kwenda shule.
Hata mbuzi alikataa.

1631330458191.png



Baba akamwendea sultani.
Je, sultani. Hutaki kumchinja mbuzi?
Amekataa kunywa maji,
Nayo hayataki kuzima moto,
Nao hautaki kuichoma fimbo,
Nayo haitaki kumpiga mbwa,
Naye hataki kumwuma Kalume-Kenge,
Naye hataki kwenda shule.


1631330483359.png



Sultani akakubali.
Akamchinja mbuzi
Naye akanywa maji,
Nayo yakazima moto,
Nao ukaichoma fimbo
Nayo ikampiga mbwa,
Naye akamwuma Kalume-Kenge,
Naye Kalume-Kenge akaenda shule.
 
Hadithi ya Kakakanzi na Bibikuku

Walikuwako watoto wawili, mtu na dada yake. Majina yao Kakakanzi na Bibikuku. Mama yao akawaambia, “Watoto, msiende kutembea mwituni.”

Wakasema, “Hatuendi mama, tunacheza tu.”
Lakini katika mchezo, wakajaribu kumkamata kipepeo. Kipepeo mzuri kabisa akacheza-cheza angani, akaruka-ruka mauani.

Kila akiruka mbele wakamfuata. Polepole kipepeo akaingia mwituni. Na watoto wakamfuata. Hawaoni mwitu, wanaona kipepeo tu. Hawakumbuki maneno ya mama, wanakumbuka kipepeo tu.

Hivi wakaingia mwituni, wakaingia sana. Miti mirefu, na kichaka na giza. Walikuwa wamekwenda mbali mno. Hawamwoni mtu, hawaoni njia. Walikuwa wamepotea.

Bibikuku akaanza kulia machozi. Kakakanzi akasema, “Usilie machozi Bibikuku, tutafika tu.”
Wakaenda mbele, wakaenda wee… mpaka usiku.

1631331272318.png


Wakashikwa na usingizi, wakalala katika majani makavu.

Asubuhi yake wakainuka tena. Wakazidi kutafuta njia. Mara wakaona nyumba ndogo. Wakafurahi kuona nyumba, wakaenda kuiangalia.

Kumbe, ni nyumba ya ajabu; kuta na viambaza vyote vya mkate wa kumimina. Na sukari juu yake. Walikuwa na njaa, walianza kuondoa vipande vya kiambaza, wakala mkate mzuri mno

Walipokuwa wakila mara mlango ukafunguliwa. Akatokea kizee kungwi, mbaya sana, macho yake mabaya kama simba.
Akawaambia watoto, “Kumbe mnakula nyumba yangu. Karibuni ndani nina chakula tayari kwenu.”

1631331295018.png




Wakaingia.

Na walipokuwa ndani yule kizee akamkamata Kakakanzi. Akamfunga ndani ya sanduku yenye kidirisha. Lo! Lo! Kakakanzi sandukuni.
Na Bibikuku ikampasa kufanya kazi nzito. Kazi ya kupasua kuni na kuteka maji na kutwanga.


1631331319801.png



Kila siku kizee yule akapitisha chakula kwa mtoto kwenye dirisha la sanduku. Kila siku kizee kamwambia, “Nyosha mkono niupapase, nione kama umenenepa.”Kwa maana yule kizee kungwi alitaka kumchinja na kumla.

Lakini Bibikuku akafanya hila, akampa kaka yake mfupa wa mbuzi, naye akiambiwa na kizee, “Nyosha mkono niupapase nione kama umenenepa, hutoa mfupa wa mbuzi. Kizee Kungwi macho yake mabaya, haoni vizuri. Akapapasa mfupa, akaona amekonda, na hakutaka kumchinja bado, kwa maana amekonda.

Siku nyingi zikapita, Kakakanzi sandukuni, Bibikuku kazini. Lakini siku moja kizee kungwi akalala usingizi. Hapo Bibikuku akatwaa ufunguo wa sanduku, akaifungua.

Kakakanzi akatoka upesi, wakatoroka wote wawili. Wakarudi nyumbani. Baba yao akawapokea kwa furaha, akasema, “Kumbe, ninyi mlikuwa wapi? Sehemu gani?”

Mama yao akafurahi kabisa, naye akasema, “Ninyi watoto wangu, ni ukaidi kwenda mwituni bila ruhusa? Msifanye mara ya pili”
Wakajibu, “Mara ya pili hatuendi, hatutaki kumwona kizee kungwi.”

1631331356719.png
 
Mtego


1631335314926.png





Kulikuwa na mtego wa panya. Panya wawili wakaja kuuangalia. Wakaona kinofu juu yake, harufu ya kinofu tamu sana.

Mmoja akamwambia mwenzi wake, “Twende kuonja kinofu kile.”

Rafiki yake akajibu, “Nafikiri kitamu, lakini naogopa. Baba kaniambia hivi, ‘Mwanangu, ukiona kinofu kimewekwa peke yake katika kibau kidogo, usikiguse; ni mtego.’”

Panya wa kwanza akasema, “Huu si mtego, naujua mtego mimi. Hapa hakuna hatari yoyote. Twende tule kinofu, kina mafuta… Lo! Sijala nyama tangu siku tano.”

Mwenzi wake akajibu, “Na mimi sikula nyama tangu siku sita, lakini baba kaniambia, ‘Ukiona kinofu kimewekwa peke yake kukupendeza kumbuka ni tego:

Usijaribu kuonja

Usijaribu kugusa

Usikubali kunusa

Kumbuka ni mtego.’”

Panya wa kwanza akasema, “Wewe muoga mno, hakuna hatari. Kama ni mtego mbona hautegi? Je, panya yoyote amenaswa?

Twende kula kinofu kile

Twende polepole kabisa.

Vuta kinofu kwa utaratibu, hakuna hatari.”

Akajibu, “Baba yangu akiniona, je?

Akasema, “Baba yako hayuko. Anajua hakuna hatari. Wewe usiogope namna hii. Ukivute tu kinofu kile.”

Basi panya yule mjinga, asitake mwenyewe kugusa kinofu kile, akakubali kwa ajili ua mwenzi wake. Akakaribia polepole, akatia meno katika kinofu, kumbe….

Kwa ghafula mtego ukafyatuka, panya mjinga akanaswa wa pili akawa salama.
 
Sultani akakubali.
Akamchinja mbuzi
Naye akanywa maji,


Sultani akakubali.

Akamchinja mbuzi

Naye akanywa maji,

Huyo mbuzi amechinjwa alafu akanywa maji????? Mshana Jr njoo utupe elimu hapa
 

Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom