Hadithi kali Faili namba 25

HADITHI:FAILI NAMBA 25

MWANDISHI:ROBIN MIHO

***********03************

Tulibaki tukitazamana na Harold kwa dakika nzima kabla hajapiga hatua za tahadhari, akakifikia kitanda na kuinama kuchukua faili huku angal bado ananitazama, akiwa kalishika faili akapeleka mkono kiunoni na kuchomoa bastola aina ya Magnum357.

Sikutaka kuwa nyuma, nami nikachomoa bastola yangu nikaikamata barabara nikisubria kuona hatua za bwana huyu, akaitazama bastola yangu na kuangua kicheko kikali hadi akaegemea ukuta, alicheka sana kiasi cha kunifanya nijistukie.

"unatumia bastola ya kuwindia njiwa bwana Jackson"

"una hakika ya kuwindia njiwa hii? " niliuliza huku nikiikoki vizuri Barreta M9

"unataka kufanya nini sasa bwana Jackson" aliuliza baada ya kuona namna nilivyoondoa usalama wa bastola hii.

"nataka niitest kwako kama kweli ni ya kuwindia njiwa"

"hebu acha ujinga wewe" aliongea kwa hamaki huku akipiga hatua kunifuata.

Nilimtazama akipiga hatua za hraka hadi aliponifikia,alikuwa ni mfupi kiasi kwamba alinifikia kidevuni, aliponifikia akarusha bastola yake kitandani kisha akaikamata bastola yangu na kuondo risasi abla hajaitupia kitandani na kunikwida kifuani na kunibamiza ukutani.

"unaharibu shati langu Harold" nililalama, safari hii Harold akaachia konde la mkono wa kulia lililoishia tumboni, nikaona sasa hapa hakuna utani tena, nikakusanya nguvu kwa kasi nikaondoa kabari ile kifuani kwangu kabla sijamsindikiza na teke kali la kifua.

Harold alianguka chini kama gunia la mchele, nikapiga hatua za haraka na kuachia teke kali kuelekea usoni, Harold akaudaka mguu wangu na kuuvuta kwa nguvu bila kutarajia nikakutana na ngumi kali ya kifua iliyonifanya nione kama kwamba pumzi inagoma kutoka nilipiga mwereka wa nguvu.

Nikiwa pale chini, Harold akanisogelea na kunipa mkono, nikamtazama kwa hasira kabla sijaupokea mkono ulie, akanisaidia kuinuka lakini nikiwa nainuka akauachia mkono nikarudi chini bila kupenda, nikajizoazoa kwa hasira nikamfuata kwa kasi.

"Come on Sajini we have to do work" aliongea huku akijiweka mbali nami.

"mpuuzi wewe"

" na wewe mpuuzi pia"aliongea huku sasa akiliweka faili juu ya meza, akavuta kiti na kukaa, akaniangalia nami nikapiga hatua hadi mezani nikavuta kiti na kukaa., akafugua faili ile iliyokuwa na namba 25 iliyoandikwa kwa wino mzito mwekundu.

"faili namba 25" akasoma maandishi meusi yaliyoandikwa katika karatasi ya kwanza ya faili ile, akafunua ukurasa wa pili.

"Mauaji ya waziri mkuu Ipini Mwaijande, waziri wa madini Baraka Kipingu na mfanyabiashara wa madini Remo Kyaruzi" akanitupia macho na kuendelea.

"Tarehe 16 mwezi wa tatu Remo Kyaruzi aliuawa akiwa nyumhani kwake Ilemela kwa kupigwa risasi ya kichwa, kamera za usalama zilibainika kuwa zilizimwa takribani wiki moja kabla na aliamuru zizimwe yeye mwenyewe Remo"

"pia alikuwa na walinzi binafsi wawili waliobadilishana shift za kulinda nyumba yake, mlinzi aliyekuwepo siku ya tukio pia alijeruhiwa ubavuni kwa risasi mpaka sasa yupo hospitali ya Kissesa" alishusha pumzi na kufunua ukurasa wa tatu.

"Uchunguzi wa awali ulibaini ya kwamba siku moja kabla ya mauaji ya Bwana Remo alikuwa amefanya mawasiliano na waziri wa madini mheshimiwa Baraka kipingu ambaye aliuawa wiki moja mbele, tarehe 23 mwezi wa tatu akiwa anatoka nyumhbani kwake Tabata Chang'ombe,

alipigwa risasi ya kichwa yeye na dereva wake, wote walifariki papo hapo mita chache kutoka katika geti la kutokea nyumbani kwake, kamera za usalama pia zilikuwa zimezimwa" akanyamaza na kuniangalia.

"aisee kamera zilikuwa off, polisi waliokuwa zamu kulinda numba yake wanasemaje? "niliuliza

"hakuwa akilindwa na polisi, aliajiri kampuni binafsi ya SGA" alijibu kisha akaendelea,

"siku tatu kabla ya kifo chake alikuwa amefanya mawasiliano na waziri mkuu Ipini Mwaijande alyefariki tarehe saba mwezi huu wa nne, amefariki baada ya figo kushindwa kufanya kazi"

"kikosi cha watu wanne kikiwa chini ya Meja Awadhi Mpekula kimeteuliwa kufanya kazi ya siri kuchunguza wahusika wa mauji ya waziri wa madni bwana Kipingu na mfanyabiashara Mr. kyaruzi,

vilevile uhalali wa kifo cha Mheshiiwa waziri mkuu Ipini". Alimaliza a kulifunga faili lile, akajiegesha kitini akizama kwenye tafakuri nzito.

"uchunguzi wa polisi umeonyesha chochote? Nikauliza

Bila kugeuka wala kujitikisa akajibu "faili ni jeupe, hebu tazama ukurasa wa mwisho"

Nikalitwaa faili ile na kuitazama ukurasa wa mwisho nikajikuta nimechoka zaidi baada ya kubaini kuwa unahitajika uchunguzi mpya pasipo kujali uchunguzi uliokwishafanyika awali, ingawaje nakala ya uchunguzi wa awali iliambatanishwa.

Ukimya wa dakika mbili hivi ulikatishwana mlio wa simu mojawapo kati ya simu zile mbili zilizoachwa na Meja Awadhi, nikajisogeza kitandani kivivu na kuichukua simu ile, mpigaji alisomeka kama EAGLE01.

"anaitwa eagle namba moja"niliongea na kumwangalia Harold.

"pokea"

"halooo"

"code no EAGLE 01 Awadhi mpekula Naongea na code E03 Jackson Makusu"

"ndio nakusikia" niliongea na kuweka loud spika

"natumaini code E02 Harold Mlembuka ananisikia" akaendelea

"Code E04 yupo nje anawasubiri, natumani mmekwishakupitia faili namba ishirini na tano tafadhali kutaneni na code E04 Cliford Sanga haraka iwezekanavyo over" simu ikatoa mlio wa kukatika.

"twende"

Harold alisema huku akikusanya vitu vyake, akaitwaa simu moja iliyosalia,faili akalisundika katika begi lake na kuanza kutoka, sikupoteza muda nami niliwahi kila kilicho changu nikatoka nje, tukaambaa hadi katika maegesho.

Gari nyekundu aina ya Toyota surf iliwasha na kuzima taa sote tukaikazia macho, akashuka mwanaume kipande cha mtu akiwa amenyoa ndevu kwa mtindo wa O, akasemama mbele ya mlango wa gari huku ametukazia macho,

inspekta Harold akapiga hatua kumfuata nami nilifuata nyuma kama mkia.

"code E04" alizungumza

"code E02" aliitikia Harold huku akimpa mkono.

"code E03" nilijitambulisha huku nikimpa mkono.

Code E04 bila kuongea chochote akaingia garini, nasi tukafuatia kujipakia garini, mimi pamoja na code E02 tukajipakia viti vyanyuma hivyo code E4 akiwa dereva alikaa peke yake na siti ya mbele ilibaki wazi, akawasha gari na kuliondoa taratibu tukaingia katika barabara pweke inayotoka katika hoteli hii maarufu.

Hakuna aliyemsemesha mwenzie, tuliingia barabara ya capri point baada ya mwendo wa dakika kadhaa tukakamata barabara ya stesheni moja kwa moja hadi round about ya samaki samaki.

hatimaye tukachukua barabara ya CBA mwendo wa dakika tano ulitufikisha Lumumba relini tukakunja kulia kuifuata barabara ya Lumumba hadi tulipoufikia msikiti wa masijid Raudhwa.

Tukaingia katika nyumba moja kubwa yenye uzio wa matofali nayo ilikosa kitu kimoja tu, Geti.

Code E04 akatoa mfuko mdogo wa nailoni akatupa bila kugeuka.

"simu zenu" tukatazamana na code E02

"simu zetu hata hatujawataarifu familia zetu kama tumefika salama wewe unazitaka simu, najua kabisa mda huu mpenzi wangu atakuwa roho juu"nililalama kwa taharuki.

"yupo salama" alijibu akiwa bado ametulia katika kiti cha dereva.

"yupo salama? Unamjua mchumba wangu wewe? "

"simuuu" alibwata code E04 akionekana kukereka na mabishano yale.

Bila kupenda tukazitoa simu zetu na kuzima kabla hatujazitupia katika kimfuko kile, sasa tulibakiwa na simu tulizopewa na meja Awadhi ama code E01.

code E04 akashuka nasi tukamfuata, tuliambaa katika uwanja wa nyumba ile na kushika ueleke wa nyuma ya jengo lile ambako tulikuta banda kubwa la bati.

Code E04 au Cliford Sanga akalikamata lango la banda lile na kufungua, kulikuwa na grai iliyofunikwa turubai, tukasaidiana kulivua turubai lile, lilikuwani gari ya kazi aina ya Nissan patrol ya rangi ya nyeupe.

tukajipakia na kuondoka kupitia geti la nyuma ya jengo lile pweke, tukatumia barabara ndogo ya mtaa ule hadi tulipotokeza katika mtaa wa Rwegesora, tukaukata mtaa huu hatimaye tukaingia barabara ya Pamba.

Tukaifuata barabara hii hadi tulipofila katika majengo ya Marwa store tukachepuka kuufuata mtaa wa mwembechai.

safari yetu iliishia katika nyumba ndogo ya kisasa, yenye geti jeusi na ukuta mfupi ulionakshiwa kwa rangi nyeupe, akitumia remoti alifungua geti ila akaegesha gari kabla ya kutugeukia na kutuambia.,

"hapa ndipo maskani yetu kwa sasa, mipango yote tutaipanga hapa hadi tutakapoona kuna ulazima wa kuhamia kwingine karibuni" aliongea code E04, tukashuka na kuingia katika nyumba ile, kila mtu alijitupa kochini isipokua code E04 aliyepitiliza hadi jikoni huku akidai njaa inamuuma.

Ilimchukua dakika kumi kutoka jikoni akiwa na sahani iliyosheheni sambusa za nyama, akaitua mezani na kulifuata friji dogo na kutoka na soda mbili aina ya pepsi na juisi moja ya embe, akamkabidhi code E02 soda moja na mimi akanikabidhi soda mojawapo, tukaanza kuzishambulia sambusa zile hadi zilipokwisha.

"haya leteni mipango sasa" Clif alizungumza

"kila mtu amekwishakuliona suala lililopo mbele yetu ni wazi tunahitaji vitendea kazi" aliongezea Harold

"kila kitu kipo humu ndani" alisema clif

"basi nadhani tuanze kulishughulikia sasa" aliongea Harold huku akifungua begi lake na kutoa faili namba ishirini na tano

****************************

KAZI NDIO KWANZA INAANZA TUKUTANE KESHO
 
Mpaka hapa ni super mkuu. Big up . Ila kama naruhusiwa kutoa maoni . Lugha ya kiswahili inafanya hadithi inoge zaidi, mana Kinge kina sheria nyingi.
 
Ipo vizuri
 
Hii ngoma ni mulua kabisa changamoto za humu ni simulizi kufika mwisho
 
  • Thanks
Reactions: ADK
Upo sahihi kabisa, kitu pekee anafhohitaji mwandishi na kuona anaungwa mkono, kupokea ushauri na kuwafahamu wasomaji thru likes
Basi wadau tujitokeze vya kutosha nadhani hatuguarimu chochote kugonga like na kureply kwenye kitu kizuri kama hiki
 
Similar Discussions

16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom