Hadithi hadithi (zimepotea),tufanyeje ili zirudi kwa watoto zetu?

Perimeter

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
3,178
2,000
Zamani ilikua kila ikifika december tukienda kwa bibi huwa ni raha bin amani maana sio kwa hadithi zile,mtasimuliwa story moja itakuja nyingine,nakumbuka enzi zile wakati dada wa kazi akinilisha chakula bila kunidanganyia HADITHI nlikua sili na ukitaka nile we nipigie Hadithi tu.

Nakumbuka Marehemu BIBI alikua ana hadithi ikiisha hii inakuja ile,tukimwona tu wajukuu woteeeee tunakaa miguunii kusikiliza hadithi,ama kweli ilikua raha ya aina yake.

Lakini zama za sasa sioni hadithi,watoto wakitaka kuskia Alichofanya BABU NYERERE wote utawaona wanashika simu ni Ku google,wakitaka kujua zamani ilikuaje kuhusu babu mkwawa ni mwendo wakushika Tablet na kuperuz,siku hizi hata tukienda kijijini hamna hata ile taste ya u kijiji maana Ma flat TV yamejaaa yani sioni hata kama kutakuja kuwa na kitu HADITHI HADITHI huko mbele tunakoendea.

Hadithi ni simulizi za mababu zetu ambazo zilitokea sisi tukiwa hatupo,lakini saivi ni kama na tulikuepo maana tunajua mpaka Nyerere alifia wapi,tunajua hamna MTI UNAO ONGEA yani saivi no kudanganya mtoto..yani watoto wa saivi ukisema Hadithi hadithi atakuitikia vizuri tuuu ILA ukisema Hapo zamani za kale palitokea mfalme SIMBA yaniii mitoto ilivyo haina adabu utaiskia inakuumbua AAAAAAAAAH BABA SIMBA ANAONGEA TANGU LINI?

ama kwa hakika kuna vitu vinaenda kupotea kwa kizazi hiki ambacho kilikua kizuri sana,SIJUI TUFANYE NINI tuweze rudisha hadhi ya Hadithi hadithi,maana kwa sasa ndo hyooo inapotelea tena.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom