twasafi
Member
- Oct 12, 2018
- 53
- 67
- Thread starter
- #21
Sehemu ya tatu hii hapo mkimaliza kusoma natamani kuskia maoni yenu mpka hapoSEHEMU YA TATU
Wakiwa wanaendelea na safari afande baraka alikuwa akiendelea kupitia baadhi ya mafaili huku akiangalia huku na kule ndani ya gari ndipo alipo fungua kwenye dashboard na kitu cha kwanza alichoona kwa haraka kilikuwa ni kiboski kidogo kilicho fungwa na matilio ya kung’aa alitaka kujua ni basi alitoa na kuuliza
“Nini hiki”
“Au ndo ulikuwa unataka kumpa veronica hii” aliongezea kabla hata hajajibiwa
“ Iyo ni zawadi nimepewa na mke wang” alimjibu akiwa anamtazama
“alf kwa nini uwaze na nataka kumpa veronica” akaongezea
“Kwani mimi sina macho, mkubwa anaambiwi tazama”
“We unachofikilia hakipo, me mwaminifu”
“ Sawa lakini, macho nayo yanaongea ”
“Chunga usiruhusu watu wakakusoma kilahisi”
“ unamanisha nini.” Afande mwita aliweka kituo na kuuliza baada ya kupewa fumbo ambalo hakulielewa
“ We angalia mbele bana”
“Usije kuniingiza machakani” akaongezea kisha akarudisha zawadi ile pahari alipo ikuta lakini bado alikuwa haamini kama inatoka kwa mke wake na alikuwa anataka sana kujua ina nini ndani.
Afande mwita baada ya kuachwa kwenye fumbo kubwa alikuwa hana budi ya kuendelea kuendesha gari huku waki wapo robo ya safari yao.
Walitembea kilometa nyingi bila kusimama ikafika pahari Afande mwita alikuwa anahitaji kutulia na kutoa haja ndogo pia mda huo afande baraka alikuwa kapitiwa na usingizi, alishuka kwenye gari na kwenda kichaka kilichokuwa pembene ya barabara. Kipindi anatoka kujisaidia aliona watu wakiwa kwenye msululu wakiwa wanavuka barabara aliwatazama kwa mbali na alielekea kwenye gari, aliingia na kuwasha injini na kuondoa gari lakini baada ya kuendesha akiwa kwenye kasi ghafla watu aliona wanavuka barabara kwa mbali walitokea kwa mbele ndipo alipo minya bleki kwa kasi kubwa nusra awagonge mpka afande baraka shituka usingizi
“Mungu wangu nakufa!” alikuwa ni afande baraka baada ya kushituka kwenye usingizi mzito
Afande mwita alikuwa bado katahamaki haelewi nini kimetokea,mikono ikiwa ipo kwenye ushukani akiwa hata haskii afande baraka akimsemesha
“oya kaka” afande mwita alimshutua afande mwita kwa kupiga makofi kumtoa kwenye kitu kama msongo wa mawazo
“Naam”
“kaka utaniua na presha”
“ unajua kuendesha familia, gari inataka kukushinda” akaongezea
Afande mwita hakujibu chochote alichukua chupa ya maji na kunywa alijisahau na kuiweka pembene huku akiwa ajaifunga na kuwasha injini ndipo kichupa kilidondoka na kumwaga maji
“ Ah kaka nini tena”
“ uko sawa kweli?” afande baraka alipata wasiwasi
“ Ndio kaka” aliwasha injini kwa mara nyingine baada ya gari kuwa limezima na kuendelea na safari.
Baada ya kutembea robo tatu ya safari walipita kibao kimoja kilichopo pembene upande wa kulia wa barabrara ambacho kilikuwa na kutu lakini kinaonekana kinasomeka “Gamboshi Kilometa 12”
Walikipita baada ya kama dakika kumi na tano gari lao lilizima injini ndipo walipaki pembene
“Shida nini tena “ Afande mwita alijiuliza
“ Hii gari imeshachoka” Afande baraka alimjibu akiwa anashuka kwenye mwita nae alifwata na kwenda kufungua boneti ya gari kutazama kuna shida gani
Alitazama kwa sekund lakini sababu yeye hakuwa mtaalamu wa magari alirudishia boneti kwanza na kuchukua simu yake mfukoni alipo washa alikuta mnara wa mtandao umebaki mmoja kwenye ndipo alikumbuka alipewa namba za mwenyeji atakae wapokea, aliwahi na kufungua mlango wa gari lakini mda anaangaza aliona karatasi ndogo imeloana na majI
“Aaaah baraka!”
“Nini hiki” akaongezea huku akiwa kaishika karatasi ndo iliyokuwa na namba za simu za mtu atakae wapokea watakapo fika
“We ndo ulimwaga maji” alijibiwa na afande baraka
“ Sa tunafanyaje” aliuliza tena
“Kwani ulikuwa hujasave kwenye simu” Afande baraka aliuliza
“Hapana” Alijibu huku akipitia phonebook yake
“ Tuko karne ya 20 na unashindwa kusave kitu cha msingi kwenye simu unaacha kwenye karatasi”
“Sasa unanambia au unafoka” Afande mwita aliuliza huku akimtazama
“ Hapa cha kufanya ni kutafuta plan b” akaongezea
“Kuna plan b” Afande baraka akauliza
“Haipo ndo naifikiria”
“ Tupo katikati ya poli wewe upo kufikiria plan b”
“Sasa unataka nifanye nini”
“Wewe unawazo gani” Afande mwita aliuliza
“Sina!” Afande baraka alimjibu huku akiendelea kumtazama
Afande mwita aliangaza huku na kule na kweli walikuwa katikati ya poli na mda unaenda hajui afanye, alichukua maamuzi ya kushuka kwenye kichaka kilicho pembene yao na kumwacha afande akiwa kasimama mbele ya gari
“Plan b yako ni kunitelekeza hapa!?” Afande baraka aliuliza huku akimtazama afande mwita akiishiria kwenye machaka, alibaki peke yake akiangalia huku na kule lakini kulikuwa hakuna dalili ya kupata msadaa.
Afande akiwa kichaka alikuwa akitembea bila kujua anaelekea wapi alitembea kwa mwendo wa dakika kumi ndipo alisikia sauti ikitokea nyuma yake na kumwita “Mwita choma Maige” aligeuka kwa kasi na kutoa buduku yake aina ya pisto iliyokuwa kwenye pembene ya kiuno chake. Aliinyoosha kwa mtu huyo alikuwa ni mzee sio chini ya miaka 40 afande mwita alimtazama na kuuliza
“We nani?”
“Weka bunduki chini” mzee huyo alimwambia bila wasiwasi
“Naongea kwa mara ya mwisho sitarudia”
“We nani?” alimwambia huku akiweka bunduki yake tayari kwa kupiga
Mzee huyo aliuliza swali moja ambalo lilimfanya afande baraka arudishe bunduki yake ilipokuwa
“Yuko wapi Veronica”
“ Nimeamwacha hosipitali” alijikuta hakijibu bila kutaka huku akilegeza mikono yake
“Na wewe ni nani yake”
“Mme wake” akaongezea
“Hapana, Boss wake” alijibu akiwa anamtazama kwa makin sana
“Haya basi twende kijijini” Mzee alimwambia huku akimwosha njia kwa mkono
“Kuna askari mwenzangu nilimwacha kwenye gari “
“Naomba tumwende” akaongezea
“Kuna mtu mwingine tofauti na veronica?” mzee aliuliza kwa mshangao ambayo hata Afande mwita hakuelewa. Afande mwita aliongoza njia kwenda kumrudia alipo mwacha afande baraka lakini wakitembea walikutana nae njia kabla hata hawajafika mbali
“Mkuu”
“Ulikuwa umeenda wapi?”afande baraka aliuliza
“Na huyo ni nani”Akaongezea
“Mwenyeji wetu”
“Umempataje”
“Ilo sio swali” Afande mwita alimjibu na kumgeukia yule mzee na kumwambia tunaweza kwenda
Mzee aligeuka kulia kwake na kuongoza njia huku afande mwita na baraka wakifwata.
Ilikuwa ni majira ya saa kumi na moja jioni walitembea kufikia mpaka afande baraka kuhitaji maji ya kunywa aliona maji yakitililika na kuamua kusogea pale alipotaka kutafuta namna aweze kunywa maji mzee alimkataza na kusogea karibu yake alichukua jani dogo na kuchukua tone ya maji yaliyokuwa yakitililika akamwambia ageuke mkono wake afande baraka alifanya ivo alimwekea yale maji juu ya mkono wake ndipo afande baraka alihisi kama kuna moto umedondoka kwenye mkono wake alishutka na kurusha mkono juu, Yule mzee hakuongea mengi aliendelea kuwa ongoza walitembea kwa mda wa masaa mawili walifika gamboshi mida ya saa moja jion cha kushangaza palikuwa kimya hamna kelele wala mtu hata mmoja afande mwita ndoa alikuwa haelewi
“Ndo hapa?” aliuliza akiwa hana wakika na swali lake
“Ndio” mzee alimjibu bila kumtazama huku akiendelea kutembea
“Wanasema huku usiku huwa ni ulaya mbona buza pazuri sasa” Afande baraka alijuliza mwenyewe bila kupata jibu
Walikuwa kitembea huku kila hatua waliyokuwa wakitembea ilikuwa ikisikika, mpaka walipofika kwenye nyumba ndogo pia napo kulikuwa kimya kabisa mzee aliwafungulia mlango palikuwa giza akawaambia waingie walianaglia na kuingia kishingo upande aliwafungia mlango na kuwasha taa kwa nje akawaogaza kwa kuwaambia pumzikeni afande baraka alipo jaribu komeo palikuwa pamefungwa kwa nje
“Huyu mzee vipi”
“Kafunga kwa njee” alijiuliza mwenye huku akimtazama afande mwita akiwa tayari kashasinzia sababu ya uchovu wa kutembea na kuendesha gari na yeye alibakiwa hana njisi na kujilaza na kupumzika kama walivoambiwa na mzee yule nae alielekea kitandani na kupumzika.