Hadithi Animation episode 1

Siielewi halafu katuni hazijaenda shule, na sauti mgogoro.
 
Mwanzo mzuri lakini marekebisho yanahitajika

1. Mbali na sauti kuwa haisikiki, lakini sauti za watoto zinatakiwa ziigizwe kama sauti za watoto, pamoja na matamshi na meneno ya kutumia yawe ya kitoto vile vile

2. Picha na sauti hazijaenda sawa sawa.

3. Katuni zipo too rigid, zimekosa uhai wa kiuhalisia

Ahsante
 
Breezer... Hongera saana kwa kweli unastahili pongezi. Inapendeza, kasoro ambazo nimeona naona ndizo hizo hizo zimetajwa hata ha Gaijin hapo. Sauti, movements alafu kwa kuongezea wiano. Kuna mahala wapo mkekani, wiano wa yule mtoto na yule mama in relation na wawili wengine walio keti hapo kidogo haupo sawa. Otherwise hongear...

Magembe R. Malima nasubiri input yako...
 
mwanzo mzuri ila graphics sio nzuri .. mshughulikie na sauti pia
 
Mwanzo mzuri kama wengine walivyochangia.
Nadhani "body movement" umejitahidi lakini zibanie kidogo kwani zinaonekana kuwa too much. Camera iweke karibu kidogo, yaani, sio lazima kuona full frame ya mwili muda wote, hapo utapunguza hizo body movement kwani frame itakuwa ya ukaribu zaidi.

Subtitles, jaribu rangi nyeupe, na kama unaweza kui'frame text, basi, iwe na mzunguko au kivuli karibia na black.

Ground level ipo "flat" sana, kama software unayotumia unaweza kuweka "mawimbi" hapo itasaidia pia. Texture ipo flat, je hiyo software inaweza kuonyesha "milima na mabonde"/shadows mfano kwenye ground, naona kuna mawe, scene ionyeshe hiyo kidogo (all depends on software though...)

Random assets. Naona matunda yote yameanguka in same direction. weka randomnness kwenye hizo scenes. Miti pia pana repetition ambayo inaonekana.

Mwisho, movement kwenye assets za miti nk, just subtle movement inatosha...

Anxiously waiting for second episode.
 
breezer

Umewahi kuona anime inayoitwa Ponyo (Ponyo by the cliff on the sea)? (kama hujaiona nakushauri uione)

Hii anime imetengezwa kwa mkono lakini movement ya kila kitu huko ina uhalisia wa hali ya juu mno hata kushinda anime zinazotengenezwa na wataalamu kwa kutumia softwares. Michoro 170,000 ilitumika kuonyesha kila movement itokanayo na wahusika na mazingira yao

Ningekushauri utengeneze anime kwa njia hii ya mkono kwanza mpaka ukihitimu ndio uingie kwenye softwares kama hujafanya hivyo bado, na kama umewahi tungependa kuona kazi zako za mkono

Sikushauri hivi kukurudisha enzi za mkoloni au kama adhabu (Najua kwa mkono ni kazi kubwa zaidi) ila kwa sababu walimu wengi wa masomo ambayo unaweza kutumia ama mkono au software hushauri hivyo kwa sababu unapata familiarity na movements, spatial changes,...ambayo itakurahisishia na kuongeza ubora wa kazi yako ukianza kutumia software
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom