Hadi Wafe Watanzania wangapi ndio wahusika wawajibike? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hadi Wafe Watanzania wangapi ndio wahusika wawajibike?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MAMMAMIA, Jul 19, 2012.

 1. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #1
  Jul 19, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Bado Watanzania tuna kumbukumbu za MV Bukoba ambapo mamia ya Watanzania walifariki kwa mpigo.
  Ikiwa hiyo ni ya mbali, mwaka jana Septemba 10 Watanzania zaidi ya 200 walikufa wakijiona.
  Tarehe 13 Mei Mwaka huu injni za meli ya Sea Gul zilizima moto ikitokea Pemba kuelekea Unguja.
  Na leo tena, meli ya kampuni hiyo hiyo imezama. Katika ajali zote hizo, wahusika wakuu hasa hawawajibiki.

  Ukiachia ajali za meli, huwa haipiti wiki, kwa wingi mwezi mmoja, tunashuhudia ajali za mabasi ya mikoani ya abiria yakipata ajali na kuuwa makuni ya Watanzani. Hivi serikali yetu tukufu, sikivu, inasubiri wafe abiri wangapi kwa mpigo au mmoja mmoja ndio iwajibike?

  Hatutaki uwajibikaji wa kujiuzulu, kwani hailipi. Hatutaki hata adhabu ya kunyongwa kwa wale wanaosbabishwa haya kwani kuwanyonga wao ni kidogo sana kuliko Watanzania wenzetu wanaokufa katika machinjio ya barabarani na majini. Tunataka suluhisho la kudumu la kuondosha ajali zinazoweza kuzuilika. Tunataka barabara zitengenezwe kwa viwango na sheria za usalama barabarani ziimarishwe. Tunataka kusimamishwa mara moja meli chakavu zinazochukua roho zetu. Tunataka rushwa na maslahi binafsi vikomeshwe. Msituue kwa maslahi yenu binafsi.
   
 2. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #2
  Jul 19, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  SASA HAWA MAOFISA watapata wapi hella za kusomeshea watoto wao USA, UK na International schools?
   
 3. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #3
  Jul 19, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Mtoa mada hadi hapo utakaposikia au kuona baaadhi ya majibu haya(i mean surname)
  -fulan bin karume
  -fulan bin Jakaya
  -fulan bin makinda(kama ana mtoto)
  -fulan bin sumaye
  yaan na wengineo wanaofanana nao
   
 4. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #4
  Jul 19, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Tutaunda tume kushughulikia hili, afu mheshimiwa Mwakyembe atapanda meli hadi zanzibar kujionea mwenyewe,afu serikali imejipanga tatizo kama hili HALITATOKEA TENA!
   
 5. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #5
  Jul 19, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  mungu apishilie mbali lakini huu usemi wa tatizo halitajirudia ni butu na tasa!
   
 6. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #6
  Jul 19, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Kibanga Ampiga MKoloni, Heshima Mkuu,
  Kwa mujibu wa vyombo vya habari, idadi iliyokuwa inatajwa ni hiyo, na ukiangalia taarifa ya Ofisi ya Makamo wa Raisi Zanzibar ilitaja 202. Asante sana kwa kuchangia.


   
 7. Mabagala

  Mabagala JF-Expert Member

  #7
  Jul 19, 2012
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,465
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Usafiri wa zanzibar haumo kwenye muungano wa tanganyika na zanzibar. Yule waziri mhusika kuna kipindi alikuwa kwenye kipindi cha Dakika 45 cha ITV, aliulizwa kuhusu kuzama kwa Spice Islander kama kuna watu wamewajibishwa au yeye alichukua hatua gani. Alisema serikali haiwezi kuwajibika kwa hilo maana si meli ya serikali na wala yeye hiyo ajali haijamgusa moja kwa moja, kama ingemgusa basi angewajibika. Nahisi alisema sawa, nchi hii mpaka wafe watoto wao au familia zao au mwana ukoo wao basi utaona watawajibika na kuwawajibisha wahusika wakuu iwe serikalini ama sehemu nyengine. Subiri rais wa tanzania akiongea atasema anawapongeza vyombo vya usafiri kwa kazi nzuri wanayofanya.
   
 8. JamboJema

  JamboJema JF-Expert Member

  #8
  Jul 19, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,148
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Hivi huyu jamaa anahusika na huko? Nilidhani huko yupo yule jamaa wa CUF aliyegoma kujiuzuru mwaka jana kuwa 'madudu aliyakuta'? Safari hii sijui itakuwaje kwake.
   
Loading...